Darajani 1905

Darajani 1905 Darajani 1905 ni ukurasa unaokuletea habari za Chelsea kwa lugha ya kiswahili.
(31)

Darajani 1905 ni ukurasa unaokuletea habari kwa ufupi kuhusu kinachoendelea klabuni Chelsea na wachezaji wake.

"Sababu iliyotufanya tumlete Jadon Sancho ni kwasababu tuliona atatusaidia. Jambo pekee analotakiwa kufanya ni kuendelea...
09/12/2024

"Sababu iliyotufanya tumlete Jadon Sancho ni kwasababu tuliona atatusaidia. Jambo pekee analotakiwa kufanya ni kuendelea hivi alivyo kwasasa. Hawezi kuondolewa kwenye kikosi labda hiyo siku aww hachezi."
- amesema kocha Enzo Maresca

Cole Palmer ndiye mchezaji wa kwanza ndani ya msimu huu wa ligi kuu Uingereza kutengeneza nafasi za kufunga 40.
09/12/2024

Cole Palmer ndiye mchezaji wa kwanza ndani ya msimu huu wa ligi kuu Uingereza kutengeneza nafasi za kufunga 40.

"Huu ni mtazamo mpana sana, ni k**a kuitazama klabu ya soka kwa namna tofauti ambayo hakuna mtu amewai kuifanya hapo kab...
09/12/2024

"Huu ni mtazamo mpana sana, ni k**a kuitazama klabu ya soka kwa namna tofauti ambayo hakuna mtu amewai kuifanya hapo kabla. Litakuwa jambo la kufurahisha sana k**a tunavyojua kwenye ligi kuu Uingereza, endapo mtu akija k**a Pep Guardiola au Alex Ferguson kisha akafanya kitu kwa ubora na kikafanya kazi basi wengine wote wanaanza kuiga. Litakuwa jambo la kusisimua sana kwa miaka kadhaa ijayo ambapo ndiyo watu wengi wataanza kuiga mbinu za Chelsea."
- amesema mchambuzi wa soka, Robbie Earle

Kwa mujibu wa taarifa, Chelsea inaweza kupokea paundi milioni 60 k**a dau la kushiriki michuano ya FIFA Club World Cup. ...
09/12/2024

Kwa mujibu wa taarifa, Chelsea inaweza kupokea paundi milioni 60 k**a dau la kushiriki michuano ya FIFA Club World Cup. Fedha hiyo ni sehemu ya mkataba ambao FIFA wamepanga kuusaini na kampuni ya televisheni ya Dazn ambayo inataka kurusha matangazo ya michuano hiyo itakayoanza majira ya kiangazi mwaka 2025.

Chelsea na Man city ndiyo timu pekee kutoka Uingereza kushiriki michuano hiyo itakayozikutanisha timu shiriki 32 kuanzia hatua ya makundi.

"Ninakubaliana kabisa na mwendelezo wa Chelsea chini ya Enzo Maresca. Amekuwa na wingi wa wachezaji wenye vipaji lakini ...
09/12/2024

"Ninakubaliana kabisa na mwendelezo wa Chelsea chini ya Enzo Maresca. Amekuwa na wingi wa wachezaji wenye vipaji lakini amewaleta pamoja na kuwafanya wacheze k**a timu yenye utambulisho wake unaojulikana na mpango unaoonekana."

"Wasiwasi wangu upo kwenye safu ya ulinzi pamoja na kipa Robert Sanchez, lakini tofauti na hao kuna wachezaji wengi wenye vipaji na uwezo mkubwa kwa hivyo kuifanya Chelsea iwe moja kati ya timu zinazowania ubingwa wakati mwanzoni niliwaza watapata tabu kuwania walau nafasi nne za juu."
- amesema mchambuzi wa soka, Phil McNulty

Taarifa zilizopo zinasema Todd Boehly yupo kwenye mpango wa kulinunua moja kati ya magazeti kongwe nchini Uingereza, The...
09/12/2024

Taarifa zilizopo zinasema Todd Boehly yupo kwenye mpango wa kulinunua moja kati ya magazeti kongwe nchini Uingereza, The Telegraph ambalo linafanya kazi kwa zaidi ya miaka 160.

Nyota kinda wa Chelsea, Esrevao Willian ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini Brazil kwa tuzo zinazodhamini...
09/12/2024

Nyota kinda wa Chelsea, Esrevao Willian ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini Brazil kwa tuzo zinazodhaminiwa na ESPN. Estevao Willian ameshinda tuzo hiyo yenye heshima kubwa nchini Brazil huku akiweka rekodi ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kushinda tuzo hiyo zilizoanzishwa mwaka 1973. Estevao kwasasa ana miaka 17.

Nenda tena kaiangalie penati ya Cole Palmer, iangalie mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu alafu ukimaliza njoo ha...
09/12/2024

Nenda tena kaiangalie penati ya Cole Palmer, iangalie mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu alafu ukimaliza njoo hapa uniambie mchezaji gani wa Chelsea aliingia kwenye box wakati Palmer anapiga penati, k**a umeangalia vizuri hakuna, kwanini? kwasababu hakuna anayetegemea kwamba kipa ataokoa au mpira kugonga mwamba ndiyo maana wachezaji wote hakuna aliyejisumbua kuingia kwenye box.

"Arsenal, Man city na Liverpool hawawezi kuteleza k**a alivyoteleza Marc Cucurella. Tukiwa wakweli sisi bado hatupo taya...
09/12/2024

"Arsenal, Man city na Liverpool hawawezi kuteleza k**a alivyoteleza Marc Cucurella. Tukiwa wakweli sisi bado hatupo tayari kushindania ubingwa, tupo mbali sana ukitulinganisha na hizo timu. Tunawekeza akili yetu kujijenga kila siku ili tuwe bora zaidi."
- amesema kocha Enzo Maresca

Tangu Mungu alipoumba dunia na kujaza vitu vingi ndani yake, hakuna mwanadamu yeyote aliyepiga penati nyingi mfululizo b...
09/12/2024

Tangu Mungu alipoumba dunia na kujaza vitu vingi ndani yake, hakuna mwanadamu yeyote aliyepiga penati nyingi mfululizo bila kukosa kwenye ligi kuu Uingereza kumzidi Cole Palmer. Penati 12, magoli 12.

"Kuna mtu asiyependa panenka?"- amejibu Cole Palmer alipoulizwa k**a anafikiri k**a mashabiki wameipenda penati yake ya ...
09/12/2024

"Kuna mtu asiyependa panenka?"
- amejibu Cole Palmer alipoulizwa k**a anafikiri k**a mashabiki wameipenda penati yake ya pili

Msimamo wa ligi kuu Uingereza;1. Liverpool - alama 352. Chelsea - alama 313.4.5. we shuka tu6.7.8. endelea kushuka9.10. ...
09/12/2024

Msimamo wa ligi kuu Uingereza;
1. Liverpool - alama 35
2. Chelsea - alama 31
3.
4.
5. we shuka tu
6.
7.
8. endelea kushuka
9.
10. usichoke, ndiyo maisha
11.
12.
13. Mdomooo mdomoooo - alama 19

Hongera umewapata🤣🤣🤣

"Yale makosa mawili yaliyofanyika mwanzoni yalikuwa mabaya lakini hatukuwa na muda wa kufanya chochote. Tottenham hawaku...
09/12/2024

"Yale makosa mawili yaliyofanyika mwanzoni yalikuwa mabaya lakini hatukuwa na muda wa kufanya chochote. Tottenham hawakutengeneza nafasi nyingi za kufunga zaidi ya yale makosa. Morali ya timh kwasasa ipo juu sana na tunataka kuendelea hivihivi kuwa kwenye upande wa kushinda."

"Mashabiki wamepitia kipindi kigumu sana kwa miaka miwili kabla sijaja hapa, na msimu uliopita pia ulikuwa mgumu. Lakini nina furaha kuwaona wanatabasamu na kufurahi hiyo ndiyo sababu inayotufanya tucheze soka."
- amesema Cole Palmer

Ngoja tukumbushane kitu kwanza!Ipo hivi, mchezo wa soka unachezwa kwa dakika 90 na kila timu ina wachezaji 11 maana yake...
09/12/2024

Ngoja tukumbushane kitu kwanza!
Ipo hivi, mchezo wa soka unachezwa kwa dakika 90 na kila timu ina wachezaji 11 maana yake uwanjani kuna kuwa na wachezaji 22 ambao wote wanacheza soka kwa dakika 90.

Hii maana yake kila mchezaji anatakiwa kucheza soka kwa dakika 4, yani kati ya dakika 90 kila mchezaji anatakiwa kucheza soka kwa dakika 4 huku dakika zilizobaki, yani dakika 86 akicheza soka bila kuwa na mpira.

Hapo tupo sawa?

Yani tunaweza kusema kila mchezaji akiingia uwanjani anapewa mpira anauchezea kwa dakika 4 kisha anampasia mwenzake.

Hii inamaanisha nini?

Inawezekana umejenga maana yako nyingine kichwani tofauti na hii maana yangu!
Kwangu hii naona inamaanisha kwenye soka unatakiwa kucheza muda mwingi ukiwa hauna mpira kuliko muda mwingi ukiwa na mpira.

Yani namna utakavyocheza ukiwa hauna mpira ndiyo kutaamua kocha akupange au usugue benchi

Kwa wale waliowai kucheza soka, ulishawai kucheza mshambuliaji wa kati kisha kocha akakwambia ukimuona namba 10 au winga wako anakuja na mpira, wewe sogea pembeni yani hakikisha unakimbia k**a kwenye box basi uende upande tofauti?

K**a yeye anakuja kulia wewe nenda kushoto, k**a anakuja kushoto wewe nenda kulia, hiyo ulishakutana nayo?

Inawezekana kuna sababu nyingi lakini sababu moja kubwa ni kuchukua attention ya mabeki wakufate wewe kukukaba wakati huo wanaacha nafasi ya winga au namba 10 wako kuingia kwenye box kiwepesi na beki akisema akuache amkabe winga au namba 10 basi ndiyo hapo namba 10 au winga wako atakupasia mpira na wewe ukafunge goli.

Nimeeleweka kweli?

Kwahiyo kule kukimbia sehemu tofauti na winga wako au namba 10 pale ndiyo tunasema umecheza soka ukiwa hauna mpira. Yani kitendo ulichokifanya wewe ambaye hauna mpira kimeleta faida kubwa kwa huyu mwenye mpira kufanya maamuzi sahihi.

Wale wachezaji, mlishawai kuambiwa na kocha kwamba mchezaji mwenzako akipata mpira, fungua, tafuta open space alafu kaa hapo, mnakumbuka ile? Sasa ile ndiyo kucheza soka ukiwa hauna mpira.

Olivier Giroud alicheza mechi zote za Ufaransa kwenye Kombe la Dunia na hakufunga goli lakini alikuwa bora sana kwenye kucheza soka akiwa hana mpira na kuwafanya akina Mbappe na Griezman kuwa bora.

Wino umeisha!

"Iwe Chelsea wanataka au hawataki, ushindi wao dhidi ya Tottenham unawafanya wawe kwenye mbio za kushinda taji la ligi k...
09/12/2024

"Iwe Chelsea wanataka au hawataki, ushindi wao dhidi ya Tottenham unawafanya wawe kwenye mbio za kushinda taji la ligi kuu Uingereza."
- amesema mchambuzi wa soka, Nigel Reo-Coker

Sema ndiyo vile tu sababu tumeshinda, lakini ukuta wa Badiashile na Colwill haupo vizuri wala nini, ni ngumu sana kuwach...
09/12/2024

Sema ndiyo vile tu sababu tumeshinda, lakini ukuta wa Badiashile na Colwill haupo vizuri wala nini, ni ngumu sana kuwachezesha miguu ya kushoto wacheze katikati (mabeki wa kati au viungo wa kati) huwa wanapata tabu sana na ndicho kilichotokea jana. Na ukiangalia mipira mingi Sanchez alikuwa hampi Badiashile sababu upande aliokuwepo ni ngumu sana mguu wa kushoto kuwa huru na mpira. Watu wengi hawasemi sababu tumeshinda.

"Tunaeeza kuona wakati akiwa anatoka uwanjani ni k**a alikuwa analia. Ni jambo lenye hisia nyingi. Mimi binafsi nimefura...
09/12/2024

"Tunaeeza kuona wakati akiwa anatoka uwanjani ni k**a alikuwa analia. Ni jambo lenye hisia nyingi. Mimi binafsi nimefurahishwa sana. Ninataka kuona jambo k**a lile, hautakiwi kufurahi unapotoka uwanjani, anataka kufunga magoli, anataka kuisaidia timu na nimependa sana nilivyoona ameumia kwa kufanyiwa mabadiliko."
- amesema mchezaji wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel

Mkataba unasena, endapo Chelsea ikimaliza kwenye nafasi 16 za juu kwenye msimamo wa ligi kuu basi Chelsea itaamua yenyew...
09/12/2024

Mkataba unasena, endapo Chelsea ikimaliza kwenye nafasi 16 za juu kwenye msimamo wa ligi kuu basi Chelsea itaamua yenyewe imsajili Jadon Sancho au iachane naye. Endapo itachagua kumsajili basi itatakiwa kuilipa Man utd dau la paundi milioni 25. Chelsea ndiyo itafanya maamuzi.

Address

Kahama

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Darajani 1905 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Darajani 1905:

Videos

Share


Other Media/News Companies in Kahama

Show All