Ni Ibada ya Uzinduzi ugawaji miche katika bustani ya miti Ofisi kuu KKKT DIRA.
January 14,2025
Elct Dira
#followers
Baada ya taarifa tuliyokuletea awali Sasa Sikiliza Walichosema kwenye Sauti hii
Ibada ya Jubilee ya mwaka mmoja Dayosisi ya Mufindi
Neno na Askofu wa Dayosisi ya kusini Njombe Dkt George Fihavango.
KIONGOZI BORA ANZIA KWENYE NGAZI ZA MITAA!
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Kheri James, amewataka Wenyeviti wa Mitaa wa Manispaa ya Iringa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani, usawa, na uwajibikaji vinazingatiwa wanapohudumia wananchi.
Akizungumza katika kikao maalum na Wenyeviti hao, Mheshimiwa James alisisitiza umuhimu wa kuongoza kwa nidhamu na kujitolea kuleta ustawi wa jamii kwa kutoa huduma bora.
Kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake kilihusisha Wenyeviti waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Mheshimiwa James aliwapongeza kwa kuaminiwa na wananchi na kuwasihi kutumia nafasi hiyo kwa kuimarisha maendeleo ya maeneo yao kwa maslahi ya wananchi wote.
Aliwaambia viongozi hao kuwa uwajibikaji ni nguzo muhimu ya uongozi, huku akiwahimiza kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi. “Ni jukumu lenu kuwa sehemu ya suluhisho, si sehemu ya matatizo,” alisisitiza Mhe.James.
Wenyeviti walioshiriki kikao hicho walionyesha dhamira yao ya dhati ya kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kuleta maendeleo chanya. Walisisitiza kuwa wako tayari kusimamia kwa haki na kuhakikisha wanatoa mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi.
Mheshimiwa James alihitimisha kwa kuwaasa viongozi hao kushirikiana kwa karibu na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha maeneo yao yanastawi na wananchi wanapata huduma wanazostahili. "Pamoja tunaweza kuleta mabadiliko makubwa," alisema.
#Radio Furaha Fm
#UongoziBora
#MaendeleoKwaWote
#IringaYetu
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Heri James amepongeza hatua ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuimarisha mahusiano na wafanyabiashara kwa njia ya vikao na mikutano ya mara kwa mara.
Mh. James amesema hayo katika mkutano wa wadau wa biashara uliofanyika mkoani Iringa na kuongeza kuwa mkutano huo ni fursa kwa wafanyabiashara wote kueleza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.
Kwa upande wao wafanyabiashara akiwemo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bw.Peter Felix na Bi.Lightness Chengula wamesema kuwa kitendo cha wao kukaa pamoja kinaondoa uadui baina yao na maofisa wa TRA.
Naye Meneja wa TRA mkoa wa Iringa Bw. Aziz Rajab anewakaribisha wananchi wote kuendelea kuhudhuria mikutano hiyo inayotarajiwa kufanyika kila siku ya Alhamisi ikilenga kutoa elimu juu ya mabadiliko ya sheria kwa mlipa kodi na kushughulikia kero za wafanyabiashara.
#furahaupdates #elctheadquarter #TRA #elct_iringa #begakwabega
Marafiki wa Dayosisi ya Iringa kutoka Marekani (BEGA KWA BEGA) wametoa Pikipiki aina ya KINGLION kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma katika Usharika wa Balali ikiwa ni sehemu ya msaada kwa watumishi wa Usharika huo.
Mchungaji wa Usharika wa Balali Bw. Ofed Kisoma amewashukuru wote waliochangia ununuzi wa chombo hicho na kusema kuwa usafiri huo utamwezesha kufikia maeneo ya mbali kwa wakati.
Awali, akizungumza wakati wa makabidhiano, Mtunza Hazina wa Dayosisi ya Iringa CPA. Hezron Nziku amesema kuwa chombo hicho ni muhimu katika kueneza Injili ya Yesu Kristo.
Ameongeza kuwa msaada huo ni matunda ya mahusiano mema kati ya Dayosisi ya Iringa na marafiki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo marafiki hao wanatarajia kufanya ziara katika Usharika wa Balali na sharika nyingine ili kuangalia utekelezaji wa miradi wanayoifadhiri.
#Begakwabega#ELCT#
Kiongozi wa mbio za mwenge Komred Godfrey Mnzava ameutaka uongozi wa shule ya Sekondari ya wasichana Ifunda kuweka mifumo ya uvunaji wa maji ili kupunguza adha katika shule ya wasichana Ifunda.
Hayo ameyasema leo wakati akizindua bweni la wasichana wa shule hiyo na kuutaka uongozi wa shule kufuata maelekezo hayo ili kuwarahisishia wanafunzi wa kike kupata huduma za maji kwa urahisi.
Akizungumzia upatikanaji wa maji Mnzava amesema maji ni muhimu hususani kwa watoto wa kike katika kurahisisha ufanyaji wa shughuli mbalimbali na afya kwa ujumla.
#furahaupdates
MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA IRINGA MHE. RITTA KABATI AHOJI MPANGO WA SERIKALI KUSAMBAZA UMEME KATIKA VIJIJI AMBAVYO HAVIJAFIKIWA NA HUDUMA HIYO.
#furahaupdates
YALIYOJIRI BUNGENI LEO ALHAMISI.....
#furahaupdates
MHE. RITTA KABATI AOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA KUELEKEA KWENYE VIVUTIO VYA UTALII.
Mhe. Dkt. Ritta Kabati, Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Iringa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amebainisha hayo wakati anachangia hoja ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii leo Jumatatu Bungeni jijini Dodoma ambako vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa Fedha wa 2024/2025 vinaendelea.
Endelea kufuarahia vipindi vyetu kupitia masafa ya 96.7 MHz na Mtandaoni duniani kote kwa kubofya hapa >>> furaha.listen2myshow.com
#furahaupdates #RadioFuraha #elct_iringa #wizarayayamaliasilinautalii #iringa #ruahanationalpark #iringabomani #isimilamuseums #tanapa #bungetv
#furahaupdates
MBUNGE RITTA KABATI AKERWA NA UBOVU WA BARABARA YA KUTOKA KILOLO-KISING'A-MKARANGA-MLAFU-ILULA.
Mhe. Ritta Kabati, Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Iringa ameonesha hisia zake leo Alhamisi bungeni jijini Dodoma wakati anachangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa Fedha wa 2024/2025.
#rittakabati #elct_iringa #bungetz #tamisemi #tanroads #tarura