EBONY Digital

EBONY Digital The best Swahili Radio Station from the Southern Highlands of Tanzania. Frequency; Iringa 88.1, Njombe 91.9, Mbeya & Songwe 94.5, Dar es Salaam 106.9

Frequency; Iringa 87.8, Mbeya 94.7, Dar 106.9, Njombe 88.2, Songea 102.2 MHz

TUJUZE KUMEKUCHAJE ASUBUHI YA LEO?
11/02/2025

TUJUZE KUMEKUCHAJE ASUBUHI YA LEO?





Bus la timu ya Dodoma Jiji FC lilipata ajali katika eneo la kati ya Nangurukuru na Somanga, wakati likielekea Ruangwa, L...
10/02/2025

Bus la timu ya Dodoma Jiji FC lilipata ajali katika eneo la kati ya Nangurukuru na Somanga, wakati likielekea Ruangwa, Lindi, baada ya mchezo dhidi ya Namungo FC. Katika ajali hiyo, wachezaji kadhaa walijeruhiwa.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya NBC uliofanyika Februari 9, 2025, Namungo FC walitoka nyuma na kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC.
YOUTUBE.COM

Timu ya Dodoma Jiji FC ilicheza vizuri katika kipindi cha kwanza, lakini Namungo FC walijitahidi kurudi katika mchezo na kufanikiwa kusawazisha na baadaye kuongoza.

Hata hivyo, habari za ajali ya basi la timu zimeleta huzuni kwa mashabiki na wapenzi wa soka nchini. Kwa sasa, wachezaji waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu, na timu inaendelea na maandalizi ya michezo ijayo.




Wakulima wa Mazao ya Misitu, Chakula na Biashara vikiwemo Vikundi vya Kijamii, Vyama vya Ushirika wa Msingi (AMCOS), Vya...
10/02/2025

Wakulima wa Mazao ya Misitu, Chakula na Biashara vikiwemo Vikundi vya Kijamii, Vyama vya Ushirika wa Msingi (AMCOS), Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) na Vikundi vya
Kuweka na Kukopa (VICOBA), katika Mikoa ya Nyanda za Juu, wametakiwa kulitumia vyema

Jukwaa NMB Kijiji Day ili kuharakisha ukuaji wao kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Frank Mganga, wakati wa NMB Kijiji Day iliyofanyika wikiendi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Image, Kata ya Kidegembya ikiwakusanya wananchi wa kata za Kidegembya na Katembwe, kushiriki semina na Bonanza la Michezo.

Kupitia shughuli hiyo Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Wogofya Mfalamagoha, aliyeambatana na mameneja

wa Matawi ya NMB Njombe, Mafinga, Makambako, Makete na Wanging’ombe, alisema katika kufanikisha lengo la kufikisha masuluhisho ya kifedha vijijini, benki hiyo imejipanga kuwafikia wananchi kupitia mawakala




10/02/2025

Je, Somo La Kodi Liingizwe Kwenye Mitaala Mashuleni!?







10/02/2025

AZAM YAANGUKIA PUA

Magazeti Leo Februari 10,2025





10/02/2025

Magazeti Leo Februari 10,2025






10/02/2025

UBINGWA TANZANIA NI WA YAGA NA SIMBA. Uchambuzi wa magazeti Leo





TUAMBIE ASUBUHI HII KUNA HALI GANI YA HEWA?
10/02/2025

TUAMBIE ASUBUHI HII KUNA HALI GANI YA HEWA?





Kutoka Katika Hekima na Maarifa Tuambie Ni Nini Kilicho Anzisha Uadui Kati Ya Shetani Na Mwanadamu?
09/02/2025

Kutoka Katika Hekima na Maarifa Tuambie Ni Nini Kilicho Anzisha Uadui Kati Ya Shetani Na Mwanadamu?




Kutoka Madhabauni Na .winnie
09/02/2025

Kutoka Madhabauni Na .winnie



Usikose kufuatilia mahojiano na  kupitia Tunda La Roho Ya Ebony Fm kuanzia Saa 12:00 Asubuhi mpaka Saa 04:00 Asubuhi.   ...
09/02/2025

Usikose kufuatilia mahojiano na kupitia Tunda La Roho Ya Ebony Fm kuanzia Saa 12:00 Asubuhi mpaka Saa 04:00 Asubuhi.




Wizara ya afya nchini Tanzania imekanusha taarifa za uwepo uhaba wa dawa za kufubaza  makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV) ...
08/02/2025

Wizara ya afya nchini Tanzania imekanusha taarifa za uwepo uhaba wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV) na kusema dawa hizo zipo za kutosha na haziuzwi.





Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Jux amefunga ndoa na mpenzi wake mfanyabiashara kutokaNigeria Priscilia jana Februari ...
08/02/2025

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Jux amefunga ndoa na mpenzi wake mfanyabiashara kutoka
Nigeria Priscilia jana Februari 7,2025.

Ndoa hiyo imehudhuliwa na watu wachache wakiwemo ndugu wa karibu pamoja na wasanii k**a vile Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Abba, Marioo, Ommy Dimpoz na wengine.

Familia ya Princila iliwasili nchini Tanzania tangu Februari 6 kwa ajili ya harusi hiyo akiwemo mama yake ambaye ni muigizaji mkubwa huko Nchini Nigeria lakini pia na ndugu zake wengine.

Mahusiano ya wawili hao yalianza mapema Agosti 2024 huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandano ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.

Ikumbukwe kabla ya Jux kuwa kwenye mahusiano na Priscilla, alikuwa na Karen Bujulu.

Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam. Na hii inakuwa ndoa ya kwanza kwa wapenzi hao wawili.





07/02/2025

Jambo Beats Yawaogesha Mafundi Cherehani Wote Wenye Tabia Za Hovyo…






07/02/2025

asimulia sakata lake na fundi wake kwenye kaoge,tuambie kwenye comment fundi wako amewahi kukufanyia nini!?




Mwanahabari mkongwe Afrika Mashariki, Leonard Mambo Mbotela aliyejulikana kwa kipindi chake maarufu cha Je, Huu Ni Uungw...
07/02/2025

Mwanahabari mkongwe Afrika Mashariki, Leonard Mambo Mbotela aliyejulikana kwa kipindi chake maarufu cha Je, Huu Ni Uungwana? amefariki dunia.

Familia ya marehemu Mambo Mbotela imesema alikuwa mgonjwa kwa muda kabla ya kuaga dunia hii leo Ijumaa saa 9:30 asubuhi.

Mambo Mbotela alizaliwa mwaka 1940 huko Freretown, Mombasa nchini Kenya.

Alisoma shule ya msingi ya Freretown kati ya 1948 na 1953 halafu akaenda Buxton shule ya kati Mombasa kuanzia 1954 hadi 1958. Alihudhuria shule ya sekondari ya Kitui High School kuanzia 1959 hadi 1963.

Alipata nafasi ya kuingia katika ukufunzi wa Sauti ya Kenya akishirikiana na Simon Ndesanjo katika kipindi ‘Hodi hodi mitaani’.

Mwaka 1964 aliajiriwa k**a mtangazaji wa huduma ya Kiswahili. Mambo Mbotela alianzisha kipindi chake cha ‘Salamu za vijana’ na pia akasoma taarifa za habari za huduma ya Kiswahili.

Mwaka 1966 alianzisha ‘Je, huu ni ungwana?’
Alijulikana zaidi k**a mtangazaji wa soka kuanzia mwaka 1967.

Kati ya vipindi vyake vilivyopendwa ni Uhalifu Haulipi, Ongea Lugha Sanifu na Waliosifika.

Wakati wa uasi wa mwaka 1982 (jaribio la kijeshi kuipindua serikali ya rais Moi) Mbotela alilazimishwa kusoma habari za waasi kwa sababu sauti yake ilijulikana kote nchini humo.

Katika maisha yake ya kazi alikuwa pia mhusika wa huduma ya “Presidential Press Service” chini ya Rais Moi kwa miaka saba.

Alirudi Kituo cha Utangazaji cha KBC akastaafu mwaka 1997 akiwa na cheo cha mwangalizi mkuu wa vipindi vya redio.

Hata baada ya kustaafu ameendelea kusikika redioni akisoma habari na kipindi chake “Je Huu ni Ungwana?”.

Mambo Mbotela ameacha mke, Alice Mwikali na watoto watatu, Aida, Jimmy na George Mbotela.



Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa  kwa juhudi, bidii, na mchango wake mkubwa wakati akiwa nasi hapa  na EbonyFm.Umea...
07/02/2025

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kwa juhudi, bidii, na mchango wake mkubwa wakati akiwa nasi hapa na EbonyFm.

Umeacha alama isiyofutika, na mchango wako utaendelea kuonekana katika mafanikio yetu.

Tunakutakia kila la heri katika safari yako mpya! Daima unakaribishwa.



07/02/2025

Ametekeleza..!?





Address

Uhindini
Iringa
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EBONY Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to EBONY Digital:

Videos

Share

Category