LoyalForum TV

LoyalForum TV Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from LoyalForum TV, Iringa.

💯💯💯🌐🏆
11/07/2024

💯💯💯🌐🏆

WABONGO NA MISEMO YAO KATIKA SIRI ZA MAISHA.1. SIRI YA KWANZATengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku...
17/01/2024

WABONGO NA MISEMO YAO KATIKA SIRI ZA MAISHA.

1. SIRI YA KWANZA
Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho ki nguoni mwako!", Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake!

2. SIRI YA PILI
Usimwamini sana rafiki yako, kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako!, K**a hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako halafu boss wako akurushie. Utatamani kufa.

3. SIRI YA TATU
Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1. Majaaliwa, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Yote huna, acha kulala mchana.

4. SIRI YA NNE:
Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja.

5. SIRI YA TANO
Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka!, Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia, ila hujauona.

6. SIRI YA SITA
Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute K**a kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?

7.SIRI YA SABA
Ili ufurahie maisha, jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba!, Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha yako hovyo!

8.SIRI YA NANE
Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Huyajui ya mama yako kwa sababu baba yako alichagua kuyaficha! K**a unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako.

9. SIRI YA TISA
Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure. Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende zake, tena mpe na nauli.

10. SIRI YA KUMI
Hata k**a umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga. Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike

11. SIRI YA KUMI NA MOJA
Haijalishi umri umekwenda kiasi gani k**a una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee ni hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu.

"HAWA NDIO WABONGO NA MISEMO YAO"
Je ina Ukweli au ni ya Uongo?
Je Umejifunza Kitu?
SHARE na wengine nao wajifunze

WELLCOME ♟higher quality low price 📞 0713052836 also on what’s up 🗜Location :Dar Es Salaaam &Mwanza “Time : 24 hrsVisit ...
30/10/2023

WELLCOME
♟higher quality low price 📞 0713052836 also on what’s up
🗜Location :Dar Es Salaaam &Mwanza “
Time : 24 hrs
Visit LoyalForum TV on instagram also on YouTube

UKWELI KUHUSU MOTIVATION and INSPIRATION TALK*_”Sababu ya kumpiga tunayo, Nia ya kumpiga tunayo, Uwezo wa kumpiga tunao,...
21/10/2023

UKWELI KUHUSU MOTIVATION and INSPIRATION TALK*

_”Sababu ya kumpiga tunayo, Nia ya kumpiga tunayo, Uwezo wa kumpiga tunao, nguvu ya kumpiga tunayo hivyoo ni lazima Apigweeeeee!!!”_

Hii ni sehemu ya Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya mwaka 1978 akiongelea uvamizi wa Nduli Idd Amin Dadaa kwa ardhi ya Tanzania, Kagera.

Mwalimu aliongea huku akishangiliwa na kupigiwa makofi na watanganyika wote, tukamuelewa vizuri na kukubali gharama ya kumpiga Nduli mpaka akome.

Kuna watu foolishly wanakejeli “motivation” na “inspiration” talk kusema ni upuuzi na uongo usio fanya kazi, wajinga hawaelewi umuhimu na nafasi yake.

Kila mtu katika wakati mmoja au mwingine anahitaji mahali ambapo atapata motivation na inspiration talk asonge mbele.

MOTIVation ni MCHAKATO wa kumsaidia mtu aone KUSUDI (PURPOSE) la maisha yake, au MOTIVE ya jambo fulani, ili ainuke na kuchukua hatua kufikia MALENGO YAKE hasa pale anapitia changamoto kubwa.

Inspiration, tofauti na motivation, ni mchakato wa kum-STIMUlate mtu, kumtia moyo na kumpa motisha afanye kitu anafahamu na kuelewa kinahitajika kufanyika.

Changamoto ya Motivation na Inspiration ni kuwa “haidumu”, ni k**a nguvu ya soda, inabidi urudi tena na tena kuongeza stimu.

Ni k**a KUOGA, huwezi kusema sitaoga maana kuoga kwenyewe kuna-hitajika kila siku - tutakuona chizi wewe!

Utaoga leo, kesho na kesho kutwa, siku zingine itabidi uoge mara tatu maana umepiga kazi au vita mwili ume-chafuka na kuchoka unahitaji maji ya moto na sabuni!

Ndugu yangu, asikudanyanye mtu, tafuta mazingira na mahali na mtu ambaye ataku-pump na kukupiga stimu ufanye the impossible.

TOKA HARAKA mahali ambapo unapigwa negative inspiration - futa urafiki na namba za watu wanao kuvunja moyo na kuku-katisha tamaa kwenye mitikasi ya ndoto zako.

Maisha ni safari yenye changamoto nyingi, zipo siku za ups na zipo siku za downs - jifunze wapi upashe moto nafsi yako ukiwa down na pia ukiwa up tafuta namna ya kuwa inspire wengine walio down.

Amani iwe kwako na familia yako yote!


umeipenda?Share wengine

HAKUNA AJUAYE KESHO,KESHO  NI FUMBO KUBWA  SANA!Soma stori hii ya kweli…VILE Mungu hatumuoni na kesho ilivyo fumbo, haku...
30/09/2023

HAKUNA AJUAYE KESHO,KESHO NI FUMBO KUBWA SANA!

Soma stori hii ya kweli…

VILE Mungu hatumuoni na kesho ilivyo fumbo, hakuna darasa la unyenyekevu kupita hilo. Vishindo vya nini ikiwa Mungu hujamuona na hajakuhakikishia chochote kuhusu kesho?

Dunia tangu kuanza kwake mpaka leo, kila elimu imeshafundishwa. Tazama unakanyaga wapi, angalia unayemkanyaga. Kesho ikifika usije shindwa kuinua uso kwa aibu.

Mwaka 1990, rapa na prodyuza tajiri, P Diddy, akiwa amekimbia umande Chuo Kikuu cha Howard katika mwaka wake wa kwanza, alienda kupiga deiwaka kwenye studio za Uptown Records. CEO wa Uptown alikuwa mtu mzima Andre Harrell.

Diddy alikuwa na bidii. Alifanya kazi na wakongwe, Mary J Blige, Jodeci, Heavy D na alimshawishi Notorious BIG asaini Uptown. Mara, Harrell akaanza kumuona Diddy anatishia utawala wake, wasanii walimkubali kuliko yeye CEO. Halafu Diddy hakuwa mwajiriwa, deiwaka tu!

Harrell akaona Diddy anataka kujifanya fahari kwenye z**i lake, na mafahari wawili hawakai z**i moja. Harrell akamtimua Diddy. Baada ya kufukuzwa, Diddy alijikusanya kwa mwaka mzima, akaanzisha kampuni yake ya Bad Boy Entertainment, ikamiliki lebo ya Bad Boy Records. Akamtwaa Notorious BIG.

Uptown baada ya Diddy ikayumba, wakali Mary J na Jodeci wakahamia lebo ya Death Row. Harrell akaenda kuajiriwa Motown. Ubosi wa Uptown akamwachia Heavy D. Mambo yakawa hovyo, Uptown ikauzwa kwa kampuni ya Universal Music Group.

Achana na hisia za kuwepo wawangaji na warogaji, matokeo ya kila siku kwenye maisha ni uchawi tosha! Diddy alifukuzwa na Harrell Uptown mwaka 1993. Ilipita miaka 20, Diddy alimwajiri Harrell.

Yes, mwaka 2013, Diddy alianzisha kampuni ya Revolt Media & TV LLC, inayomiliki mtandao wa televisheni za muziki, Revolt TV. Harrell akateuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Revolt TV, Diddy akawa mwenyekiti.

Harrell angejua kesho ingekuwa hivi unadhani angemtimua Diddy Uptown? Ishi leo kwa unyenyekevu hata mbele ya walio chini yako. Kazini kwako, ndugu zako nyumbani hata wafanyakazi wa ndani. Usikanyage watu aisee! Hujui kesho kuna nini. Maana kesho imekaa kichawi sana.
Umeipenda?
Share na wengine

UNAAMBIWA HAYA NDIYO MAKOSA SABA (7) MABAYA WANAYOFANYA BAADHI YA SINGLE LADIES WAKIWA KATIKA MAHUSIANO.1. Unapotembelea...
26/08/2023

UNAAMBIWA HAYA NDIYO MAKOSA SABA (7) MABAYA WANAYOFANYA BAADHI YA SINGLE LADIES WAKIWA KATIKA MAHUSIANO.

1. Unapotembelea nyumba ya mwanaume, usichukue vitu bila ridhaa yake au ruhusa yake, haijalishi ni kidogo kiasi gani, au uko karibu naye kiasi gani, huko ni kuiba na kuamini wanaume ni wasikivu sana na hawajali ...

2. K**a una ahadi ya kukutana na mwanamume, usiende huko na rafiki/marafiki zako bila ridhaa yake au ruhusa ya mwanaume. Au rafiki yako aanze kuagiza bila ridhaa yake, huenda hayuko tayari kwa ajili ya nyie wawili na isitoshe baadhi ya wanawake wamepoteza wanaume wao kutokana na tabia hii...

3. Acha kumwambia mwanaume kiasi fulani cha pesa ukifika akupe, mitazamo ya namna hiyo ni kwa makahaba na inaweza hata kukupotezea mume wako mtarajiwa, maana mwanaume atafikiri hivyo ndivyo ulivyo. unafanya mikataba na wanaume tofauti...

4. Wanawake tafadhali acheni kuchunguza chunguza simu au mawasiliano ya mpenzi wako... Wanaume ni watu wasiopenda kufuatiliwa fuatiliwa.. K**a anakupenda,anakupenda tu...

5. Usiingie kwenye maisha ya mwanaume na kuanza kuleta matatizo kati ya familia ya mwanaume na marafiki zake, tumia hekima, tumia busara na uwe na hekima. Pindi marafiki zake wakikuchukia,hautakuwa salama hata uwe mrembo kiasi gani.

6. Tafadhali ACHA kumtembelea mwanamume ukiwa hujabeba chochote. Binti, hata k**a ni mkate, nunua na uende kutembelea, inaonyesha kuwa una busara na unawajibika. Huwezi kwenda mikono mitupu, tumia ubongo wako.

7. Kaa chini na mtu wako mjadili naye biashara au mipango na ajenda za baadaye. Kuweni na mipango ya kuanzia miaka 20 mbeleni.. Be more resourceful... Wadada wengi hawajali hili, wanasema am catching cruise and vibes kwa kula supu ya pilipili na nauli ya usafiri ndio maana mnaishia kuchezewa bure.

Je ni Kweli?
Umeipenda?
SHARE na wengine

✍️

Mumeo Akishapata Pesa Tu anaanza Kuona Hizi ndiyo PISI za hadhi yake.Mwanamke Ilinde Ndoa Yako Kwa Maombi.
25/08/2023

Mumeo Akishapata Pesa Tu anaanza Kuona Hizi ndiyo PISI za hadhi yake.

Mwanamke Ilinde Ndoa Yako Kwa Maombi.

SOMA HII UJIFUNZE KITU:Kuna mambo 3 maishani yanayoweza kumuangamiza mtu:* Hasira* Chuki* MajivunoKuna mambo 3 maishani ...
25/08/2023

SOMA HII UJIFUNZE KITU:

Kuna mambo 3 maishani yanayoweza kumuangamiza mtu:

* Hasira

* Chuki

* Majivuno

Kuna mambo 3 maishani unayotakiwa usiyakose:

* Imani

* Upendo

* Tumaini

Kuna mambo 3 maishani yenye thamani zaidi:

* Uvumilivu

* Uaminifu

* Urafiki

Kuna mambo 3 maishani yanayomtengeneza mtu:

* Heshima

* Juhudi

* Ubora

Ninamuomba Mungu akupe mambo 3 maishani mwako:

* Akubariki

* Akuongoze

* Daima akulinde

Umeipenda?SHARE na wengine

Beautiful ❤️ Painting
25/08/2023

Beautiful ❤️ Painting

25/08/2023

Hakuna Mwekezaji ambae hakuwa na ubahili k**a Yusuph Manji.

💥Amewahi kununua magodoro kwajili kunyonya maji yaliyojaa uwanja wa Uhuru ili tu Yanga icheze.

💥Amewai kuwalipia mashabiki wa Yanga mara kadhaa ili mashabiki wajae uwanjani kwa lengo la kuwapa wachezaji moral.

💥 Alikuwa anasajili mchezaji yeyote pendekezwa kwa kocha.

💥Alishawai kufanikisha kumsajili Kevn Yondani kutoka Simba kwa kumwekea pesa nyingi mezani na kumwambia unasaini aula?

Lakini Viongozi wakalewa pesa wakasahau hata kuomba kujenga uwanja wa Mazoezi ama kweli upele humwota asiye na kucha.😎

Aina ya kwanza ya VITA atakayokutana nayo mkombozi wa familia ni kukabiliana na UCHUNGU wa ndani unaotokana na utegemezi...
25/08/2023

Aina ya kwanza ya VITA atakayokutana nayo mkombozi wa familia ni kukabiliana na UCHUNGU wa ndani unaotokana na utegemezi wa ndugu wengi wasio na shukrani.

K**a tulivyoona kwenye part 3 kuwa mkombozi wa familia huwa anapata nafasi ya kuinuliwa na Mungu na kupewa uwezo wa kuwasaidia wengine.

Kinachotokea ni kuwa, wakati yeye mwenyewe bado hajaweza hata kujiimarisha, huwa anajikuta katika wajibu na majukumu ya kuwasaidia ndugu zake wengi wenye shida mbalimbali.

Kwa sababu wakombozi wengi huwa wanawekewa huruma kwenye mioyo yao, mara nyingi hujinyima na kujitoa ili kusaidia wengine.

Wengi hujikuta wanafanya zaidi ya kawaida, yaani wanapitiliza kabisa. Matokeo yake, wanaweza kusababisha wao wenyewe washindwe kufanya baadhi ya vitu au hata kuwatesa na kutoeleweka na familia zao (watoto na wenza wao) kwa sababu ya kujitoa sana kusaidia ndugu.

Kinachogeuza haya yote kuwa ni vita ni pale ambapo baada ya kufanya yote hayo, unaishia KULAUMIWA na KUSEMWA VIBAYA na ndugu walewale uliowasaidia ambao HAWANA SHUKRANI kabisa.

Hii hali imewasababishia wakombozi wengi wa familia kuishi maisha ya kuwa na UCHUNGU na HUZUNI katika MIOYO YAO.

Kwa sababu hii, wakombozi wengi wa familia wameamua KUSUSIA au KUJITENGA kabisa na ndugu zao.

Wengi wameumizwa kwa sababu wameona kuwa pamoja na JUHUDI ZOTE walizofanya hakuna mtu aliyejali.

Unachotakiwa kujua ni kuwa, MUNGU akikupa nafasi ya kuwa mkombozi kwenye familia yako itaambatana na lawama zisizoisha na wakati mwingine kutokushukuriwa kwa juhudi zako.

Kwenye aina ya pili ya vita, tutaona aina ya majanga ambavyo huwa yanamwandama mkombozi wa familia na jinsi ya kukabiliana nayo ili yasikatishe uhai wake.

Share na mwingine ili ajifunze zaidi.

HIVI NDIVYO VIGEZO VISIVYO NA MSINGI VINAVYONYIMA WADADA WENGI BAHATI YA KUOLEWA • Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagu...
24/08/2023

HIVI NDIVYO VIGEZO VISIVYO NA MSINGI VINAVYONYIMA WADADA WENGI BAHATI YA KUOLEWA

• Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe.

• Binti unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome, sijui awe na kazi nzuri, awe na upendo wa kweli, na mambo mengi k**a hayo.

Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa.

Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi.

Kuna msemo usemao, “ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu” na mwingine ufananao na huo unaosema “mchagua n**i hupata koroma”.

MANENO UNAYOJITAMKIA.
• Vijana wengi wamekuwa na desturi ya kujisemea maneno ya laana bila kujua yana madhara gani katika maisha yao k**a (Wanaume wote ni wale wale, sijui siku hizi Hakuna waoji, mara Wanaume wote ni waongo, baba mmoja na mama mmoja.

Kinywa chako kina uwezo wa kuumba. Kila neno baya au zuri unalojitamkia ndivyo litakuwa kwako.

• K**a Unasema Wanaume wote ni waongo basi usishangae Kila mwanaume atakayekuja kwako akiwa muongo. K**a Unasema sina shida ya kuolewa basi miaka 30 itakukuta ukiwa nyumbani kwa baba yako. Chunga kinywa Chako.

MAAGANO ULIYOWEKA HUKO NYUMA.•
K**a kuna mtu mliahidiana kuwa mtaona halafu kwa sababu zisizo na msingi ukamuacha, basi hii inaweza ikawa ni moja ya sababu ya kukufungia baraka yako ya ndoa.

• K**a kuna mtu ana nung’unika kwa ajili yako, k**a kuna mtu ana lia kwa ajili yako huu unaweza ukawa mwiba kwako usiifikie ndoa au ukaifikia lakini isiwe salama.

• K**a kuna watu ulishindwa kutimiza ahadi uliyowaahidi unatakiwa kutubu dhambi hiyo na kutengeneza nao kwa kuwaomba msamaha ili usiwe na vifungo vinavyokuzuia.

N:B Hizi ni tabia za baadhi ya wasichana au wadada tu hivyo siyo wote wana tabia hizo!!

Umeipenda?SHARE na wengine itafuata ya wanaume nao

23/08/2023

* .*

1⃣: *Epuka Mabishano*:

✍🏼```Mara nyingi hasira hupandishwa na mabishano baina ya mtu na mtu/watu. Njia kubwa na rahisi ya kuepuka kupandwa na hasira, ni kwa kuepuka kubishana na mtu au watu, hasa wale wanao onekana wagumu kuelewa. Penda kuepuka kujibizana au kumjibu mtu kwa ukali.```

2⃣: *Penda kujishusha*:

✍🏼```Unapogundua umemkwaza mwenzako, na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu na yenye ukali, basi penda kujishusha na kuzungumza kwa utaratibu, au kuomba radhi. Hii husaidia kumshusha hasira mwenzio, kushuka kwa hasira kwa mwenzio husaidia kushusha yako pia.```

3⃣: *Jifunze kuwa na matumizi mazuri ya kinywa*:

✍🏼```Mara nyingi kinachompandisha mtu hasira huwa ni kauli chafu. Jifunze kuwa na kauli njema itakusaidia kuepuka migogoro ambayo itakufanya upandwe na hasira au umpandishe mwenzio hasira. Hasa kauli zenye kujaa matusi, kejeli, au dharau hupandisha mtu hasira. Na sauti yenye ukali, kukoroma, au ukaripiaji, humpandisha mtu hasira.```

4⃣: *Penda kudharau watu*:

✍🏼```Dharau tunayo izungumzia hapa sio ile dharau ya kumbinulia mtu mdomo, wala kumshusha na kumpandisha macho. Hapana, kudharau means "Humpi mtu attention anayoitaka ili kugombana na wewe " Ukiona mtu anakutusi, analeta kejeli, au hata kuleta shari. Njia pekee ya kumuepuka ni kwa kumdharau k**a mtu asiye na akili, aliyekosa heshima na maadili. Hivyo hujibizani nae, wala kumpa attention anayoitaka.```

5⃣: *Penda kuheshimu upeo wa mtu*:

✍🏼```Binadamu tumetofautiana upeo wetu wa kutafakari, kuelewa, na kujibu jambo, hivyo sio kila wakati mtu atakujibu au kufikiria k**a ulivyotaka akuelewe. Ukiona umemuambia mtu kitu halafu akakujibu hovyo, basi chukulia k**a ndipo uwezo wake kufikiri ulipoishia. K**a unaweza kumrekebisha basi tumia lugha safi, na sauti iliyojaa upole, na umueleweshe kwa hoja zilizo jaa hekima na busara. Kumjibu hovyo pia huweza kuleta mtafaruku kati yenu.```

6⃣: *Jifunze kuishi na watu:*

✍🏼```Binadamu tumetofautiana historia zetu, kuen

Navyozidi kukutana na Watu na kujua tabia zao ndio nagundua Mama yangu kafanya kazi nzuri sana kunilea wallah! Dunia ina...
27/01/2023

Navyozidi kukutana na Watu na kujua tabia zao ndio nagundua Mama yangu kafanya kazi nzuri sana kunilea wallah! Dunia ina watu wana tabu mbayaaa... Watu hawaogopi hata Mungu hee!

Amini usiamini wakati wa shida rafiki anaweza kuwa mzuri kuliko ndugu wa tumbo moja wakati wa shida ndio utamjua rafiki ...
27/01/2023

Amini usiamini wakati wa shida
rafiki anaweza kuwa mzuri kuliko ndugu wa tumbo moja wakati wa shida ndio utamjua rafiki wa kweli huwezi kumjua rafiki wa kweli k**a ujapata tatizo na uwezi kujua rafiki wa kweli k**a aupo kwenye shida rafiki wa kweli ni yule anayekujali ukiwa na shida rafiki wa kweli ni yule anayekujali na kubeba tatizo lako k**a la kwake uyo ndiyo rafiki wa kweli hivyo yani

12/09/2022
29/04/2022
10/04/2022

#

30/03/2022
24/03/2022

__________________________________________________Follow me on Instagram :mwlrobinson Facebookpage :nkigarobinson ...

20/03/2022
19/03/2022

Address

Iringa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LoyalForum TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to LoyalForum TV:

Videos

Share


Other Iringa media companies

Show All

You may also like