![DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VVU BADO ZIPO NA HAZIUZWI - SERIKALISerikali kupitia Wizara ya Afya imetolea ufafanuzi juu ya...](https://img4.medioq.com/367/694/1215174773676941.jpg)
08/02/2025
DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VVU BADO ZIPO NA HAZIUZWI - SERIKALI
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetolea ufafanuzi juu ya uvumi unaosambaa mitandaoni na mitaani kuhusu kuadimika kwa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI ARVS kwa kusema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu hilo kwani dawa hizo zipo za kutosha na wala haziuzwi.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Februari 08, 2025, imeelezwa kuwa Watanzania wapuuze taarifa zisizo za kweli kuhusu upatikanaji wa dawa hizo.
Uvumi wa kuadimika kwa dawa hizo, ulianza kufuatia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa Nchi yake itajiondoa kuchangia shirika la afya Ulimwenguni WHO na kusitisha misaada mingine ambayo Marekani imekuwa ikitoa kwa Mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania kupitia mashirika kadhaa ya Marekani.