Focus Digito Tv

Focus Digito Tv One of the Best Online TV Conveying Content and Adding Value for the Public Interest.

Wanaogopa Kufukuzwa kazi ndio maana wanaenda Kazini Kila siku. 😁🫴
16/01/2025

Wanaogopa Kufukuzwa kazi ndio maana wanaenda Kazini Kila siku. 😁🫴


Fursa zipo Dodoma, kutoboa ni wewe na Akili Yako. πŸ˜πŸ€—πŸ«΄
16/01/2025

Fursa zipo Dodoma, kutoboa ni wewe na Akili Yako. πŸ˜πŸ€—πŸ«΄



Mzazi Kagoma Kulipia Hela ya School Bus kasema atamleta Mwenyewe mgongoni, ni Sehemu ya mazoezi pia k**a ushauri wa Prof...
16/01/2025

Mzazi Kagoma Kulipia Hela ya School Bus kasema atamleta Mwenyewe mgongoni, ni Sehemu ya mazoezi pia k**a ushauri wa Profesa Janabi wa kutembea kufanya mazoezi. 😁🫴


Mkuu wa wilaya ya Iringa, Kheri James, amezitaka Taasisi zote za umma zinazofanya shughuli zake ndani ya Wilaya ya Iring...
15/01/2025

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Kheri James, amezitaka Taasisi zote za umma zinazofanya shughuli zake ndani ya Wilaya ya Iringa kuwekeza kikamilifu katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi ili kujenga ustawi na kuchochea maendeleo huku akizitaka taasisi zote wilayani humo kufanya shughuli zake kwa kuzingatia Utawala wa Sheria, Haki, Usawa, Umoja na mshik**ano.

DC Kheri James ametoa maelekezo hayo Januari 15, 2025 katika kikao kazi kilichojumuisha viongozi wa Taasisi za Umma, Idara za Serikali zinazofanya shughuli zake wilayani Iringa, Kamati ya Ulinzi na usalama, pamoja na Maafisa Tarafa wa Tarafa zote za wilaya ya Iringa. Kikao ambacho kimefanyika katika Ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iringa kwalengo la kujipanga na kuwa na uelewa wa pamoja.

Akizungumza katika kikao hicho, DC Kheri James ameeleza kuwa, Serikali imezijengea uwezo taasisi zake kwa kuajiri watu mahiri, kuweka vitendea kazi na mipango mizuri, lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa Wananchi. Hivyo ni wajibu wa kila Taasisi kujipanga kuhakikisha huduma bora ndio kipaumbele chao.

Pamoja na mambo mengine, DC Kheri James amewahimiza wakuu hao wa Taasisi kuhakikisha Mipango na maamuzi yao yanazingatia hali na maslahi ya umma ili umma uweze kuona tija ya uwepo wa Taasisi hizo.

"Dhamira ya Serikali katika wilaya ya Iringa ni kuona Wananchi wana sikilizwa, wanahudumiwa na kufikiwa na huduma zote za msingi kwa ubora na kwa wakati" - Amesema DC Kheri James.

Kupitia kikao hicho pia, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewapongeza watumishi wote wa umma wilayani humo kwa kazi kubwa na nzuri wanazofanya na amewatakia heri ya Mwaka mpya.

πŸ€΅β€β™‚οΈ .kheri_james


Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Joachim Nying'o, katika picha ya pamoja na Mwanafunzi wa Kwanza Kuripoti katika Shule Mpya ya ...
15/01/2025

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Joachim Nying'o, katika picha ya pamoja na Mwanafunzi wa Kwanza Kuripoti katika Shule Mpya ya Sekondari ya Wasichana Lugalo na Mkuu wa Kwanza wa Shule hiyo.

Shule Mpya ya Sekondari ya Wasichana Lugalo ipo Kijiji cha Mbigili Kata ya Lugalo Wilayani ya Kilolo Mkoani Iringa.

Kutoka kwenye Uzinduzi wa Siku ya Upandaji Miti Mkoani Iringa Kuunga Mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutunza na kuhifadhi Mazingira.

Tukutane YouTube ya Focus Digito TV.


Kutoka kwenye Uzinduzi wa Siku ya Upandaji Miti Mkoani Iringa Kuunga Mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz...
15/01/2025

Kutoka kwenye Uzinduzi wa Siku ya Upandaji Miti Mkoani Iringa Kuunga Mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutunza na kuhifadhi Mazingira.

Januari 15, 2025 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo Wilayani Kilolo.

Tukutane YouTube ya Focus Digito TV.

Serikali ya Mkoa wa Iringa imepanga kupanda jumla ya miti Milioni 42 ndani mwaka 2025 k**a sehemu ya kuunga mkono juhudi...
15/01/2025

Serikali ya Mkoa wa Iringa imepanga kupanda jumla ya miti Milioni 42 ndani mwaka 2025 k**a sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imedhamiria kuwekeza nguvu kubwa kwenye utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kuhamisha upandaji miti ili kudhibiti mabadiriko ya tabia ya Nchi na kulinda vyanzo vya Maji na Mazingira kwa maslahi ya Wananchi.

Hayo yameelezwa Januari 15, 2025 kwenye zoezi maalumu la uzinduzi rasmi wa Siku ya upandaji wa miti lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lugalo iliyopo Kata ya Lugalo Kijiji cha Mbigili katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

Akizindua rasmi zoezi la upandaji miti katika mkoa wa Iringa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Joachim Nyingo, amewahamasisha wananchi mkoani humo kuunga Mkono zoezi hilo Kwa kutoa Ushirikiano wa kutosha kufanikisha lengo huku akiwataka waelewe kuwa misitu ni Uchumi, ni Siasa, misitu ni Maendeleo ya Jamii na Kwa kifupi misitu ni Uhai.

"Rai yangu na Ombi langu Kwa sisi sote, hii miti iliyotolewa na kupandwa itunzwe vizuri na ilete tofauti katika Mazingira, ili tuoneshe kuwa siku ya upandaji miti imekuwa na manufaa na hiyo miti inaonekana" - Amesema DC Joachim Nying'o.



Exclusive na Fredrick Siwale  MwanaHabari Mkongwe, afunguka mengi, Uandishi wa habari ulivyokuwa hapo zawani, mabadiriko...
14/01/2025

Exclusive na Fredrick Siwale MwanaHabari Mkongwe, afunguka mengi, Uandishi wa habari ulivyokuwa hapo zawani, mabadiriko ya sasa na changamoto zake, agusia mwiba wa maafisa habari na wanahabari wanaoteuliwa kushika nafasi za uongozi.
πŸ‘‡

Exclusive na Fredrick Siwale MwanaHabari Mkongwe, afunguka mengi, Uandishi wa habari ulivyokuwa hapo zawani, mabadiriko ya sasa na changamoto zake, agusia m...

Kaa Tayari Kumtazama na kumsikiliza MwanaHabari Mkongwe, Fredrick Siwale, akifunguka mengi. πŸ“‘ 🎀 Focus Digito TV Kupitia ...
14/01/2025

Kaa Tayari Kumtazama na kumsikiliza MwanaHabari Mkongwe, Fredrick Siwale, akifunguka mengi.

πŸ“‘ 🎀 Focus Digito TV

Kupitia YouTube, Instagram, TikTok

"Samia scholarship ni ufadhili wa masomo Kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa kidato cha sita am...
14/01/2025

"Samia scholarship ni ufadhili wa masomo Kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa kidato cha sita ambapo ulianzishwa mwaka 2022 huku lengo kuu ikiwa ni kuwasaida wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi, Hisabati, Tehama na Tiba huku kigezo kimoja wapo chakupata mkopo huo kikiwa ni GPA 3.8 na endapo usipofikia kiwango cha ufaulu wa GPA 3.8 automatically unaondolewa kwenye ufadhili wa masomo ya Samia Scholarship na unapelekwa kwenye mfumo wa bodi ya mkopo" - Ameeleza Prof Adolf Mkenda - Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia.


"Walivyoniachia ilikuwa usiku, nakumbuka waliniteka kati ya saa 9 alasiri na walivyoniachia, waliniambia nisiongee na ye...
13/01/2025

"Walivyoniachia ilikuwa usiku, nakumbuka waliniteka kati ya saa 9 alasiri na walivyoniachia, waliniambia nisiongee na yeyote na nisiseme chochote"

"Ninachokumbuka, walitaka simu yangu na walikuwa wanazunguka nami huku wakisema wanamsubiri bosi wao. Nikawauliza, 'Kumbe mna bosi?' Walikasirika kwa kuhisi nimeanza kujua mipango yao," - amesema Maria Sarungi.


Maria Sarungi ambaye ni mwanaharakati na mhariri wa kujitegemea amedai kuwa watu waliomteka Nchini Kenya walimuachia baa...
13/01/2025

Maria Sarungi ambaye ni mwanaharakati na mhariri wa kujitegemea amedai kuwa watu waliomteka Nchini Kenya walimuachia baada ya vyombo vya habari na taasisi mbalimbali za kimataifa kupaza sauti.

"Nawashukuru vyombo vya habari kwa kupaza sauti, na watu, wanasiasa mbalimbali kwa kupaza sauti, pia nawashukuru mabalozi na Serikali za Umoja wa Ulaya na wanaharakati mbalimbali. Maana sauti zao ziliwafanya watekaji wasite kuendelea na mipango yao," amesema Maria Sarungi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Nairobi Nchini Kenya baada ya kuachiwa na watekaji tukio lililotokea Januari 12, 2025.

Kupitia Ukurasa wake wa X, Maria Sarungi amewashukuru wote waliomuombea na kupiga Kelele zilizosaidia mpaka Sasa yeye kuwa Salama.

"Asanteni wapendwa Kwa maombi, kelele na Yote. Thank you for the Prayers and the noise, I have limited access right now but I'm grateful,.... Ni Mungu tu" - Ameandika Maria.


Akikupigia Simu akaanza Kukuita Tajiri, Mtego huoπŸ€—πŸ«΄
12/01/2025

Akikupigia Simu akaanza Kukuita Tajiri, Mtego huoπŸ€—πŸ«΄


Habari kuhusu nyumba pekee iliyonusurika na moto katika Ufukwe wa Malibu, Los Angeles nchini Marekani, ilizua gumzo duni...
12/01/2025

Habari kuhusu nyumba pekee iliyonusurika na moto katika Ufukwe wa Malibu, Los Angeles nchini Marekani, ilizua gumzo duniani kote, kila mtu akiongea lake.

Mmiliki wa nyumba hiyo yenye thamani ya Dola milioni 9 za Kimarekani (sawa na takribani shilingi Bilioni 22.5 za Kitanzania), David Milton Steiner (64) ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Johns Hopkins ya Sera ya Elimu na profesa wa elimu katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ameeleza sababu za nyumba yake kusalimika.

Bilionea huyo anayeishi Texas nchini Marekani, akiwa ni baba wa watoto watatu, amesema wakati anaijenga nyumba hiyo, alizingatia uimara na ubora wa kila kitu akitaka iwe na uwezo wa kuhimili matetemeko yanayotokea mara kwa mara.

"Ilibuniwa kustahimili matetemeko ya ardhi na ina ujenzi imara sana. Kuta zake ni za mawe, zege na saruji na paa lake lilitengenezwa kwa mfumo wa kuzuia lisishike moto.

"Nguzo za msingi pia zilichimbiwa futi 50 kwenda chini ili kuhimili hata mawimbi makali ya maji ya bahari," alisema na kuongeza kuwa alitaka iwe sehemu salama ya kukimbilia iwapo kutatokea tetemeko"

"Kiukweli sikufikiria kabisa kwamba hata baada ya miaka milioni moja, moto unaweza kuja kusababisha uharibifu kwenye ufukwe wa Bahari ya Pacific," - Amesema Steiner kwenye mahojiano na Gazeti la The New York Post Januari, 2025.

Akielezea jinsi alivyopata taarifa, Steiner amesema yeye na familia yake hawaishi ndani ya nyumba hiyo na kwamba siku ya tukio, alikuwa nyumbani kwake, Texas.

Fundi mmoja aliyekuwa akifuatilia habari za moto kwenye runinga, alimtumia video ikionesha nyumba zote zilizopo jirani na nyumba yake zinawaka moto na akamwambia anahisi na yake pia itaungua.

Steiner anaeleza kuwa alipoiona video hiyo, hata yeye mwenyewe alikata tamaa akiamini nyumba yake itateketea lakini saa chache baadaye, anaeleza kuwa alianza kupigiwa simu nyingi na watu waliokuwa wanamueleza kuwa nyumba yake inaoneshwa kwenye vyombo vya habari.

Anasema alipofuatilia, ndipo alipogundua kwamba kumbe nyumba yake ilikuwa haijaguswa na moto hata kidogo na ndiyo maana ilikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari.

"Ni muujiza! Miujiza haiachi kutokea," alisema Steiner.



"Wengi wanaosema niondoke wanadai umri wangu ni mkubwa hivyo ninapaswa kupumzika, kitu ambacho sio kweli, umri sio kigez...
12/01/2025

"Wengi wanaosema niondoke wanadai umri wangu ni mkubwa hivyo ninapaswa kupumzika, kitu ambacho sio kweli, umri sio kigezo cha mtu kuachia nafasi bali mpimeni mtu kwa matendo yake yaani vitu anavyofanya ndani ya Chama"

"Mimi na Tundu Lissu tumetofautiana miaka mitano tu, hii inamaanisha miaka mitano ijayo Lissu atakuwa na umri wangu wa sasa. Je! mtasema na yeye aondoke kwa sababu ana umri mkubwa? Mimi nawaomba angalia yale ambayo ninayafanya na sio umri wangu. Kuna vijana wana umri wa miaka 30 lakini matendo yao ni ya hovyo sana" - Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Mdau wa Maendeleo Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Aidan Mlawa, amewataka vijana nchini kuyaenzi na Mapinduzi ya Zanzibar...
12/01/2025

Mdau wa Maendeleo Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Aidan Mlawa, amewataka vijana nchini kuyaenzi na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo yaliwakomboa wananchi wa visiwa hivyo katika nyanja mbalimbali za maendeleo huku akisisitiza umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango wa Mapinduzi hayo ambayo uadhimishwa Kila ifikapo Januari 12 Kila mwaka katika historia na maendeleo ya Zanzibar.

"Ndugu Wananchi wenzangu, nitumie fursa hii kuwatakia nyote Kheri na Yote mema katika Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar"

"niwahimize Wananchi wenzangu hasa vijana wa kizazi cha leo kuona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango wa Mapinduzi ya Zanzibar, kuendelea kuyalinda Mapinduzi hayo kwa kuzitunza tunu za amani, umoja na mshik**ano uliopo kati ya Tanzania Bara na Visiwani na kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 61 ya Kazi njema zilizofanywa na Serikali ya Zanzibar Kwa Kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" - Ameeleza Mlawa.

Sambamba na hayo, Mlawa ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Watanzania kuendelea kuchangia pato la Taifa kwa Kulipa Kodi ili kuendelea Kuunga mkono Jitihada Za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu na huduma za kijamii zinazochochea ukuaji wa kiuchumi na kuleta Maendeleo Kwa Wananchi wa hali zote Nchini.



Kwanini lakini! πŸ€—πŸ«΄ πŸ«‚
11/01/2025

Kwanini lakini! πŸ€—πŸ«΄ πŸ«‚


πŸ˜ŽπŸ˜πŸ™Œ
11/01/2025

πŸ˜ŽπŸ˜πŸ™Œ


Address

Iringa
51108

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Focus Digito Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Category