Taifa Digital Forum

Taifa Digital Forum Tunahusika na Uzalishaji wa Habari na Makala zinazohusu mstakabali wa Serikali ya Tanzania na Wananchi wake | Kufanya Mahojiano na watu mashuhuri.
(12)

02/08/2024

DIWANI WA MAGOLE KILOSA AWAITA WANAWAKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Diwani wa tarafa ya Magole wilaya ya Kilosa Bi Raheli Elia Kazimoto amemshukuru Rais Samia kwa niaba ya wanawake wa Kilosa kwa kutembelea wilaya yao pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara, vituo vya afya na elimu.

Sambamba na hilo ametoa wito kwa wanawake wote wa Tanzania kumuunga mkono Rais Samia kwa mengi makubwa aliyoyafanya licha ya watu wengi kutokuwa na imani na utendaji wa wanawake hasa katika masuala ya uongozi. Amesema,

"Wakina mama wote Tanzania hii mnaonisikiliza
tumuunge mkono mama Samia Suluhu Hassan ni mwanamke katika wanawake amefanya mambo mengi kwenye nchi hii mpaka tunakosa namna ya kusema"

02/08/2024

WAFUGAJI WAMFAGILIA RAIS SAMIA KWA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Jamii ya wafugaji wa wilaya ya Kilosa imempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo kwa muda imekuwa ikiwatesa wakulima na wafugaji hasa katika wilaya ya Kilosa ambapo mara kwa mara wafugaji na wakulima walikuwa wakishambuliana kufuatia kugombania ardhi.

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji wengine wakati ziara ya Rais ilipofika wilaya ya Kilosa mwananchi Shaka Stoni ambaye ni mfugaji amesema,

"Kwa niaba ya kilosa na wafugaji wote niseme sisi wafugaji tunamfurahia mama kwa kuwa tangu alipokaa kwenye kiti hatujawahi kuona ugomvi kabisa na bei ya mifugo imeongezeka sisi k**a wafugaji tunampenda sana na tunataka aendelee kwa sababu mama ndio chaguo letu".

02/08/2024

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa na nia ya dhati ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na ndiyo sababu ya yeye kuboresha kituo cha afya ambacho hakikuwa na miundombinu za kutosha kuwahudumia wananchi wa Gairo.

"Hospitali hii imekamilika kwa kiasi kikubwa kwa sababu huduma za upasuaji kwa ajili ya kuna mama wajawazito zinapatikana hapa, watu hawatakwenda tena Morogoro Mjini au Dodoma kwa ajili ya kupata huduma za upasuaji" Ameeleza Ummy Mwalimu.

Aidha Waziri Ummy amesema kwamba hospitali hiyo ina huduma za kisasa za mionzi katika hospitali hiyo akisema kuwa kwa mkoa mzima wa Morogoro hakukuwa na Digital X- Ray hata moja lakini kwa sasa mkoa una digital x- Ray nane ikiwamo iliyofungwa kwenye hospitali hiyo.

Licha ya hatua zinazozidi kupigwa, Waziri Ummy amesema kuwa bado kuna changamoto ya wananchi kujiunga na mifumo ya bima za afya ambayo imesababisha gharama kubwa kwa wananchi kupata huduma ya afya na kuwaomba Wanagairo na Watanzania kwa ujumla kujiunga na bima ya afya.

06/07/2024

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi nchini Dkt Denis Mchunguzi ameeleza kwa undani zaidi tukio la aliyekuwa mbunge wa Iringa mjini na kada maarufu wa CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa kuamia CCM.

30/06/2024

MAMIA WAJITOKEZA KUPATA MSAADA WA KISHERIA UBUNGO; RAIS SAMIA AMPONGEZWA

Mamia ya Wananchi wa Wilaya ya Ubungo waliojitokeza kupata huduma ya msaada wa kisheria iliyotolewa na Shirika la Citizen Foundation kwa kushirikiana na Mama Samia legal Aid Campaign; wamempongeza Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwepo wa kampeni hiyo kwani imekuwa msaada mkubwa hasa kwa Wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawikili kwenye utatuzi wa changamoto za kisheria zinazowakabili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika Viwanja vya Bakheresa Manzese, Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo tarehe 29 Juni 2024; Wananchi hao wamesema “tunashukuru Serikali na Viongozi wote kwa kutusaidia kutupa msaada wa kisheria sisi tumeridhika na huduma, tumepata mwongozo mzuri wa kufuatilia madai yetu na tumepata imani na Serikali yetu’’.

Mmoja wa Wananchi hao Masoud Athuman Salum mkazi wa Kibamba CCM amesisitiza “Kwa kweli kupitia zoezi hili huyu Rais wetu Mama Samia amefanya la maana sana, unajua mtu unaweza ukanyimwa haki yako hivi hivi kwa sababu kuna watu wengine maskini hawana uwezo wa kuweka Wakili wa kijitegemea, Mama amekuja na mfumo mzuri na sisi tunamuombea kwa Mungu azidi kumjalia azidi kutujadili zaidi sisi wanyonge’’.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hassan Bomboko amesema migogoro mingi inaanzia kwenye ngazi ya familia, kijamii na hata ngazi ya Serikali za Mitaa na kwa kuwa mingi imejikita kwenye mambo ya kisheria ni lazima Wananchi wapatiwe misaada ya aina hiyo.

Amesema katika Wilaya hiyo zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na ameelekeza waratibu kumpatia idadi ya kero zilizosikilizwa ili aweze kutengeneza kazi data ambayo itamsaidia kuongeza nguvu ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi hao siku ya Alhamisi ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kwamba siku hiyo huwa anasikiliza na kutatua kero za Wananchi.

Kwa upande wake Wakili Menegati John Nyamoronga amesema kwa msaada wa Kampeni ya Mama Samia Legal Aid zoezi hilo limeenda vizuri kwani Wananchi wengi wamejitokeza na wamepata msaada wa kisheria huku akitoa wito kwa Wananchi wa Wilaya nyingine kuchangamkia fursa hiyo pale ambapo watapata taarifa za uwepo wa kampeni hiyo kwenye maeneo yao.

30/06/2024

✨️MHE. MPINA ASIFUKUZWE CCM ... Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na uchumi nchini Dkt Denis Muchunguzi ameongea na mwandishi wetu na kuiomba Chama cha Mapinduzi kutokumpa adhabu tena Mbunge Luhaga Mpina kwa yale aliyoyasema Bungeni kuhusu Serikali.

Inatajwa kuwa tuhuma zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania...
24/06/2024

Inatajwa kuwa tuhuma zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata ni za kughushi, na zinazolenga kumchonganisha kiongozi huyo na mamlaka ya uteuzi ili aondolewe kwenye nafasi hiyo, na kutoa mianya kwa 'genge' la wakwepa kodi, wala rushwa na wote wasiolitakia mema Taifa 'kuchomeka' mtu wao

Tumekuwa tukishuhudia mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa TRA chini ya Kidata imekuwa 'mwiba' mchungu kwa wafanyabiashara nchini kwa kile kinachotajwa kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikitoa makadirio ya kodi yasiyoendana na uhalisia, ubabe na kutosikiliza hoja za wafanyabiashara ambao kimsingi ni walipa kodi wakubwa nchini, hilo likienda sambamba na ujumbe unaoshinikiza kiongozi huyo ajiuzulu au aondolewe ili apatikane mtu mwingine anayetajwa kuwa atakuwa rafiki kushughulikia matatizo ya wafanyabiashara nchini

Hata hivyo taarifa za ndani na za kuaminika kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo serikalini zinadai kuwa Kidata amekuwa kinara wa kusimamia sheria zinazotungwa na Bunge, kutocheka na wazembe, wakwepa kodi na wala rushwa kwa namna yoyote ile jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikisha kuziba mianya ya wajanja wajanja waliokuwa wanatumia 'kichaka' cha TRA kufanya 'uhuni' usiolisaidia Taifa kwa muda mrefu

Takwimu za haraka zinaonesha kuwa TRA chini ya Kidata imekuwa ikipaisha ukusanyaji wa mapato kila uchwao jambo ambalo ni jema kwa Taifa, mfano mwezi Desemba 2023 pekee TRA ilivunja rekodi ya makusanyo ya serikali hadi kufikia shilingi trilioni 3.05 ambayo ni sawa na asilimia 103 ya lengo la msingi lililokuwa limewekwa

Itakumbukwa kuwa Alphayo Kidata wakati anateuliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo aliikuta TRA imetoka kukusanya kati ya shilingi bilioni 700 hadi 800 kwa mwezi kwa kipindi cha 2016/2017 lakini katika hali ambayo haikutarajiwa kwa muda mfupi tu akiwa ofisini aliiongoza TRA kukusanya kati ya shilingi trilioni 1.2 hadi 1.5 kwa mwezi, takwimu ambazo hazikuwahi kufikiwa na Makamishna wote waliowahi kupita kwenye mamlaka hiyo

Ikiwa sasa wastani wa TRA kukusanya kodi kwa mwezi unafikia trilioni 2, ndipo tuhuma nzito dhidi yake zinaibuliwa miongoni mwake ni pamoja na 'mgomo feki' ulioitishwa na wafanyabishara ambao kiuhasia hadi sasa haijafahamika ni nani aliyeratibu mgomo huo baada ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, uongozi wa soko la kimataifa la Kariakoo Dar es Salaam, Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) na wadau wengine kukana kuutambua mgomo huo

Ukipitia mitandao mbalimbali ya kijamii utashuhudia baadhi ya wadau/ watumiaji wa mitandao hiyo wengine wakihoji chanzo cha kuibuka kwa tuhuma hizo, lakini pia kuhoji nani aliyepo nyuma ya pazia ya njama hizi zenye nia mbaya dhidi ya mtu ambaye amekuwa akipaisha makusanyo ya mapato ya serikali kila uchwao tena kwa kusimamia sheria na kutocheka na 'wahuni'?, lakini kubwa kuliko yote haya yanaibuka kwa maslahi ya nani?

Ziko taarifa zisizo rasmi zinazodai kuwa 'genge' linaloratibu njama za kumng'oa Kidata TRA ndilo hilohilo lilifanikisha kumng'oa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM (Chama cha Mapinduzi) ambaye kwa sasa ni Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo.

VISHOKA TRA JANGA KUBWA KWA WAFANYABIASHARA KARIAKOO.  Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeombwa kutafuta mbinu bora ya ku...
07/06/2024

VISHOKA TRA JANGA KUBWA KWA WAFANYABIASHARA KARIAKOO.
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeombwa kutafuta mbinu bora ya kufanya zoezi la ukaguzi wa risiti za bidhaa za machine za kielektoniki EFD katika soko la kariakoo kwani mbinu wanayotumia sasa ya kuvizia imesababisha kutapakaa kwa vishoka na wafanyabiashara kujikuta wanatapeliwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari wamesema TRA iangalie namna ya kuwashirikisha wafanyabiashara pindi wanapoleta timu mpya ya wakaguzi na wakusanya kodi kwani mbinu wanayotumia sasa ya kuvamia na kutumia nguvu sio njia nzuri kwani imepelekea kuibuka kwa vishoka wanaojifanya maafisa wa TRA kupita katika maduka na kuwabugudhi wafanyabiashara na kuwatapeli pesa.

30/05/2024

Wakazi wa Ipala mtaa wa Azimio Mkoani Dodoma wamemtaka Mkurugenzi wa Halimashauri ya jiji la Dodoma kuwarudishia ardhi yao huku wakiomba Mhe. Rais Samia Suluhu Hassana kuwasaidia kupata ardhi yao.

"Sisi ni Wapiga Kura wako tunatambuwa kuwa wewe ni muumini wa haki na Mageuzi nasi tunahitaji msaada wako"

27/05/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amesema kuwa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kitafanyika jijini Dodoma tarehe 05 Juni, 2024. “Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame’.

27/05/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amesema maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2024 yatakuwa na shughuli mbalimbali ikiwamo kongamano Kubwa la Kitaifa pamoja na shughuli za usafi katika maeneo tofauti nchi nzima.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum Doroth Gwajima akiongea na wananchi wa Njombe ka...
26/05/2024

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum Doroth Gwajima akiongea na wananchi wa Njombe katika siku kumi za MAMA SAMIA LEGAL AID, katika Hotuba yake amesisitiza na kuwataka Wanaume kuacha kubaki nyuma Kwani hiyo Wizara sio ya wanawake tu hata wanaume

"Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria na haki ...
26/05/2024

"Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria na haki kwa raia" Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na wananchi wa Njombe katika uzinduzi wa siku kumi za msaada wa kisheria wa Mama Samia Njombe.

HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI LEO MEI 31, 2023.
31/05/2023

HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI LEO MEI 31, 2023.

Rais Mhe.  afanya M A B A D I L I K O  ya Wakuu wa Mikoa🙏
15/05/2023

Rais Mhe. afanya M A B A D I L I K O ya Wakuu wa Mikoa

🙏

SERIKALI YA AWAMU YA SITAINAENDELEA KUWAINUA WANANCHIKWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:
09/05/2023

SERIKALI YA AWAMU YA SITA
INAENDELEA KUWAINUA WANANCHI
KWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:





SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAENDELEA KUWAINUA WANANCHI KWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:
09/05/2023

SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAENDELEA KUWAINUA WANANCHI KWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:

Maagizo ya Rais Mhe.  kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
06/05/2023

Maagizo ya Rais Mhe. kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

The President of the United Republic of Tanzania 🇹🇿 H.E Samia Suluhu Hassan  chairing the Cabinet meeting at Chamwino St...
03/05/2023

The President of the United Republic of Tanzania 🇹🇿 H.E Samia Suluhu Hassan chairing the Cabinet meeting at Chamwino State House in Dodoma Capital City today May 3rd, 2023.

 inatoa Pongezi za dhati kwa  (Afisa Habari wa ldara ya Habari-MAELEZO) kwa kuibuka Mfanyakazi Bora wa jumla wa Kitaifa ...
02/05/2023

inatoa Pongezi za dhati kwa (Afisa Habari wa ldara ya Habari-MAELEZO) kwa kuibuka Mfanyakazi Bora wa jumla wa Kitaifa Serikalini, na kutunukiwa zawadi katika Sherehe za Kitaifa za Mei Mosi. 🙏

Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN  ameipongeza Klabu ya  kwa uwakilishi mzuri baada ya kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shir...
02/05/2023

Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN ameipongeza Klabu ya kwa uwakilishi mzuri baada ya kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Wizara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni  imewasimamisha kazi Watumishi saba (07) kufuatia hitilafu ya kukatika kwa umeme w...
01/05/2023

Wizara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni imewasimamisha kazi Watumishi saba (07) kufuatia hitilafu ya kukatika kwa umeme wakati wa mchezo wa na katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

 ❤️  for the 6th phase Government under the Presidency of H.E
27/04/2023

❤️ for the 6th phase Government under the Presidency of H.E

03/12/2022

Kada wa CCM Dr. Dennis Muchunguzi amekemea Video fupi iliyosambaa mitandaoni ikidaiwa kumdhalilisha mwanachama wa CCM

Vice-President Dr. Philip Mpango has directed RCs to supervise the countrywide campaign of planting water friendly trees...
17/11/2022

Vice-President Dr. Philip Mpango has directed RCs to supervise the countrywide campaign of planting water friendly trees along water sources, while ordering people who have built houses on mountainous sources of water to immediately vacate in order to protect the area.

An aide-de-camp (A de C) is a personal assistant or secretary to a person of high rank, usually a senior military, polic...
15/11/2022

An aide-de-camp (A de C) is a personal assistant or secretary to a person of high rank, usually a senior military, police or government officer to a member of a royal family or a head of state.

09/11/2022

"Wakati naingia madarakani kwanza, hakuna Chuo cha Urais, nilivyoingia ilibidi nijifunze kwanza miezi sita mizima najifunza tu hii kazi inafanywaje, lakini sasa hivi naijua " - Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar.

Watu 19 wamethibitika kufariki dunia katika ajali ya ndege inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Precision,  iliyotokea m...
06/11/2022

Watu 19 wamethibitika kufariki dunia katika ajali ya ndege inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Precision, iliyotokea mapema hii leo mkoani Kagera.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Dar es kwenda Bukoba mkoani Kagera, na ilipata ajali hiyo ikiwa na watu 43 ndani.

03/11/2022

Rais Samia alivyopokelewa China.

02/11/2022

Alimwandikia meseji Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN na kujibiwa haya.

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taifa Digital Forum posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Taifa Digital Forum:

Videos

Share

Nearby media companies


Other Media/News Companies in Dodoma

Show All

You may also like