"TUMA NA YA KUTOLEA" ni kauli inayokuja kichwani kwa vijana wa sasa
"TUMA NA YA KUTOLEA" ni kauli inayokuja kichwani kwa vijana wa sasa
Mstaafu wa kazi ya udereva baada ya miaka 30 ya kazi
Serikali imewataka wamiliki wa shule binafsi kuzingatia usalama wa wanafunzi kwa kufanya matengenezo katika vyombo vya usafiri na kuzingatia uwepo wa wasaidizi kwa watoto pindi wanapokuwa barabarani kutoka au kwenda shuleni hali.
itakayosaidi kuwaepusha na vitendo vya ukatili au kupata madhara pindi dharura zinapojitokeza.
Zoezi hilo limefanyika jijini Dodoma ambapo Uongozi wa Halmashauri ya jiji hilo kutoka idara ya ustawi wa jamii ukiongozana na askari wa usalama barabarani umeingia barabarani kugagua usalama wa magari ya kubebea wanafunzi.
Ndoa za mkeka, ni jambo linalosikika kwenye jamii ambayo ni hatua ya wazazi kuwaozesha kilazima vijana wao waliokutwa wakijihusisha na uhusiano wa kimapenzi, ambapo baadhi ya wakazi wa Dodoma wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu utekelezwaji wa jambo hilo.
Ungana naye Abutwalibu Makame akujuze undani wa tafakuli hii.
Waziri wa Madini ANTHONY MAVUNDE kwa niaba ya Serikali amekabidhi gari la wangonjwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. ALPHONCE CHANDIKA ni katika hatua za serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.
Serikali imekabidhi gari hilo katika hospitali ya Benjamini mkapa jijini Dodoma ili kurahisisha huduma za afya kwa wagonjwa ambalo litahusika zaidi kuwafikia wananchi wa maeneo ya pembezoni ambayo awali yalikuwa hayafikiki kirahisi kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara.
@bmhdodoma @anthonymavunde
Mwanamke mmoja jina limehifadhiwa, mwenye umri Miaka 45, amekutwa ameuwawa katika Mtaa wa Mazengo Kata ya Chang'ombe Jijini Dodoma huku chanzo cha Kifo chake kikisadikiwa kuwa ni kufanyiwa udhalilishaji wa kijinsia na watu wasio julikana usiku wa kuamkia leo.
KWA KILA HALI TUTAHAKIKISHA TUNAKUFIKIA
#tbcdodomaupdates