17/01/2026
Habari Bongo Source,
Kwa majina ninaitwa Siraji Nuru Athuman, natokea Mkoa wa Kagera. Kwa sasa ninasoma katika Chuo cha Mahadi Omaan kilichopo Mkoa wa Tabora.
Naomba unisamehe kwa kukusumbua kupitia ujumbe huu. Nimeandika kwa unyenyekevu nikiomba msaada wako wa shilingi elfu thelathini na tano (35,000) kwa ajili ya nauli ya kurejea chuoni.
Wenzangu tayari wameshaondoka kuelekea chuoni, ila mimi bado nipo kutokana na kukosa nauli. Kwa sasa hali yangu ni ngumu sana, sina msaada wa karibu kwani mimi ni mtoto yatima, sina baba wala mama.
Naomba msaada wako kwa moyo wa huruma, endapo itakuwa ndani ya uwezo wako. Mungu akubariki sana kwa kunisikiliza na kunisaidia.
Wako mnyenyekevu,
Mawasiliano yake ya kumchangia jina liatoka -: Siraji Athuman namba yake ni 📞 0681 739 980