Taifa Choice

Taifa Choice Online TV For Breaking News, Politics, Sports and Entertainment News.


©2024 Taifa Choice . All Copyright Reserved
(1)

10/08/2024

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa orodha wa waamuzi wa mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii 2024 kati ya...
10/08/2024

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa orodha wa waamuzi wa mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii 2024 kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC kesho ndani ya dimba la Benjamin Mkapa. Arajiga atasaidiwa na Frank Komba na Mohamed Mkono, huku mwamuzi wa akiba akiwa Amina Kyando.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na maafisa ugani na wanaushirika Ikulu...
10/08/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na maafisa ugani na wanaushirika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma, tarehe 10 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waandishi wa Habari kutoka mkoa wa Dodoma...
10/08/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waandishi wa Habari kutoka mkoa wa Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao na maafisa ugani pamoja na wanaushirika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma, tarehe 10 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na maafisa ugani pamoja na wanaushiri...
10/08/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na maafisa ugani pamoja na wanaushirika kabla ya kuanza kwa kikao na maafisa hao Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma, tarehe 10 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia vitalu vya bustani za mazao ya mboga m...
08/08/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia vitalu vya bustani za mazao ya mboga mboga na mavuno yake yaliyotumia mbolea iliyozalishwa nchini. Bustani hiyo imekuwa ni sehemu ya elimu kwa wananchi wanaotembelea viwanja vya Maonesho ya Nane Nane 2024, Nzuguni jijini Dodoma ili kuona faida za matumizi ya mbolea zinazozalishwa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimvisha taji Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bas...
08/08/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimvisha taji Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya zana za kilimo kwa Wizara ya Kilimo ili kuendelea kuhamasisha matumizi bora ya zana za kisasa ili kuongeza tija na uzalishaji nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Bashe amesema Wizara ya Kilimo imeanza kujenga Vituo Jumuishi vya Zana za Kilimo (mechanization Centers) ili kumsaidia mkulima kuweza kupata huduma hiyo kwa urahisi.

Jumla ya trekta 119 za aina ya Swarage zenye horsepower tofauti tofauti zimekabidhiwa, power tiller 800 pamoja na majembe 200 kwa ajili ya maandalizi ya mashamba.

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA MAABARA YA TAIFA YA KILIMO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, M...
08/08/2024

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA MAABARA YA TAIFA YA KILIMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08 Agosti, 2024 ameweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Kilimo ikiwa ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ambapo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho.

Jengo hili lenye maabara 14 ndio litakuwa Maabara ya Rufaa ya Vituo vyote vya Tafiti za Kilimo nchini vilevile ndipo patakuwa Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI ili kuacha kutumia vituo ambavyo vipo Mikoani.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Mradi huo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo amesema pamoja na kuwa na hizo maabara 14 kila maabara itakuwa na ofisi yake vilevile kutakuwa na ofisi 14 za utawala ili kurahisisha utendaji wa kazi katika maabara hizo.

"Baada ya kuwa tumeanza kujenga hili Jengo tutaongea na wenzetu wanaohusika na mji wa Serikali hapa pembeni kuna viwanja viwili vina square meter k**a 60000 ambavyo tumekwisha viomba ili kuweza kuongeza ukubwa wa eneo hili,” ameeleza Waziri Bashe.

Vilevile Mhe. Bashe amesema kukamilika kwa mradi huu kutasaidia suala la uzalishaji wa miche na teknolojia ambapo utekelezaji wake utaanza kwa kujenga maabara ya Bio-Science mwaka huu pamoja na ujenzi wa Vituo vya Horticulture Mkoani Arusha ambapo kutakuwa na Maabara ya Tissue Culture kubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma kushiriki kilele cha Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024.

KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA MAANDALIZI MAZURI YA MAONESHO YA NANE NANE 2024Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses...
06/08/2024

KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA MAANDALIZI MAZURI YA MAONESHO YA NANE NANE 2024

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka ameipongeza Wizara ya kilimo pamoja na Taasisi zake kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane alipotembelea na kujionea Teknolojia mpya za uzalishaji pamoja na Tafiti mbali mbali za Kilimo.

Balozi Dkt. Kusiluka amayasema hayo leo tarehe 6 Agosti, 2024 alipotembelea katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma akiambatana na Katbu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe.

Aidha Katibu Mkuu Kiongozi amewaalika wananchi kuja katika Maonesho hayo kujifunza Teknolojia mbali mbali za kilimo pamoja na mnyororo mzima wa thamani.

Kwa upande mwingine Balozi Dkt. Kasiluka amesema kuwa hivi sasa kilimo ni biashara kubwa na teknolojia zinazotumika ni za kisasa ambapo ametoa wito kwa vijana kujihusisha na usindikaji wa kisasa wa bidhaa za kilimo kwani kilimo kina fursa lukuki.

SILINDE AHAMASISHA MATUMIZI YA ZANA BORA ZA KISASA KWENYE KILIMONaibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema ...
03/08/2024

SILINDE AHAMASISHA MATUMIZI YA ZANA BORA ZA KISASA KWENYE KILIMO

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wizara imedhamiria kuwawezesha Vijana katika Sekta ya Kilimo kwa kuwapatia zana mablimbali ikiwemo matrekta waweze kulima kwa tija.

Mhe. Silinde amesema hayo wakati akikabidhi matrekta 09 kwa wakulima kutoka Kampuni ya PASS Leasing Company Limited katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma leo tarehe 03, Agosti 2024.

"K**a serikali tumejipanga katika kuhakikisha vijana wanapata uelewa kuhusu kilimo na tayari tushatoa maelekezo kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwajili ya vijana ili Taifa letu la Tanzania lijitosheleze na mazao ya kilimo". amesema Silinde

kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PASS Leasing Limited, Rosebud Kurwijila amesema kampuni hiyo imekabidhi vifaa vya kulimia kwa wakulima zikiwemo trekta 9 zenye thamani millioni 401.76 kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma, wilaya ya Kongwa na Chemba.

"Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 2000; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 30 na kuwafikia wanufaika takribani 300 kwa kipindi cha msimu mmoja". amesema Rosebud Kurwijila

Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamasisha matumizi ya zana bora za killmo ikiwa ni pamoja kujenga uwezo wa zana za kilimo na kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa zana wanazotumia katika shughuli zao za kilimo ili kufkkia dhamira ya Serikali kufikia matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030.

PROFESA SHEMDOE ATEMBELEA VIPANDO VYA MAZAO YA KILIMO NANE NANE DODOMAKatibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Rizik...
02/08/2024

PROFESA SHEMDOE ATEMBELEA VIPANDO VYA MAZAO YA KILIMO NANE NANE DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Jabil Shekimweli wakipata maelezo ya vipando vya mazao ya kilimo kutoka kwa waoneshaji mbalimbali waliofika katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 leo Agosti 02, 2024 kwenye Viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Maonesho haya yenye hadhi ya Kimataifa yalizinduliwa Agosti 01, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kuhudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Taasisi mbalimbali za Umma.

02/08/2024

MAONESHO YA NANE NANE 2024 NI TOFAUTI NA NANE NANE ZILIZOTANGULIA

Wananchi mbalimbali waliohudhuria Maonesho ya Nane Nane 2024 katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma wamepongeza maandalizi mazuri ya Maonesho hayo ya Kimataifa ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa jana Agosti 01, 2024 huku yakitarajiwa kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 08, 2024 (88)

"Nimefika hapa kwenye maonesho ya Nane Nane 2024, nimekuta mabadiliko makubwa sana, tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo kwa jitihada zao katika kuwezesha maonesho ya Nane Nane 2024 kuwa hivi, kumejengwa tofauti sana" - Alisema Merkiori Tesha, baada ya kutembeela mabanda mbalimbali viwanja vya 88 Nzuguni Dodoma.

Kwa upande wake, Zaina Mwakijazi, Mkazi wa Makulu Dodoma, yeye amesema Nane Nane ya Mwaka huu imekuwa na maandalizi makubwa zaidi tofauti na miaka iliyopita kwanzia kwenye mazingira lakini pia wafanyabiashara wamejitokeza kwa wingi sana na kuna vitu vingi vizuri.

BASHE: MATREKTA 500, POWER TILLER 800 KUZINDULIWA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE 2024Zaidi ya matrekta 500 na power tiller...
01/08/2024

BASHE: MATREKTA 500, POWER TILLER 800 KUZINDULIWA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE 2024

Zaidi ya matrekta 500 na power tiller 800 zitazinduliwa wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 ikiwa ni sehemu ya matrekta 10,000 yanayotarajiwa kununuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema hayo wakati wa Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho hayo tarehe 1 Agosti ya Nane Nane 2024 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma, katika viwanja vya Nzuguni.

Hatua hiyo ni kujenga uwezo wa zana za kilimo na kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa zana wanazotumia katika shughuli zao za kilimo.

Waziri Bashe amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kufikia matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030.

MAJALIWA AZINDUA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA JIJINI DODOMAWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassin ...
01/08/2024

MAJALIWA AZINDUA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassin Majaliwa (Mb) amewataka Wakulima, Wajasiliamali na Wafanyabiashara kutumia fursa ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo zitakazowawezesha kulima kisasa na kuzalisha zaidi.

Amesema hayo leo tarehe 1 Agosti, 2024 alipofungua Maonesho hayo ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na ushirikiano mzuri wa Sekta ya Kilimo; na Sekta ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha washiriki wanajifunza teknolojia za kisasa na mbinu mbalimbali za kuinua kiuchumi shughuli za kilimo. Ameeleza kuwa wakulima pia watajifunza matumizi ya zana bora za kilimo, matumizi ya mbegu bora na upimaji wa afya ya udongo ili kuwa na kilimo kwa uhakika na si kwa kubahatisha.

Maonesho ya Nane Nane 2024 yanafanyika katika Kanda saba nchini ambazo ni Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale; Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere; Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye Viwanja vya Ngongo; Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika Viwanja vya Nyamhongolo; Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi; Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye Viwanja vya Themi; na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye Viwanja vya Fatma Mwasa.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".

WAZIRI MKUU AKIFUNGUA MAONESHO YA NANENANE DODOMA.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa  Ma...
01/08/2024

WAZIRI MKUU AKIFUNGUA MAONESHO YA NANENANE DODOMA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa leo Agosti 01, 2024 anafungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma,

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

NANE NANE RASMI KUANZA KESHO KATIKA KANDA ZOTE SABA NCHINIWaziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), leo tarehe 31 July,...
01/08/2024

NANE NANE RASMI KUANZA KESHO KATIKA KANDA ZOTE SABA NCHINI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), leo tarehe 31 July, 2024 amekagua Uwanja wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 na kuelekeza kuwa ni tayari kuanza rasmi tarehe 1 Agosti 2024 katika Kanda zote saba nchi nzima.

Waziri Bashe amesema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya ufunguzi tarehe 1 Agosti 2024, ambapo Maonesho hayo yanafanyika Kitaifa jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Bashe amewakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika Maonesho hayo katika Kanda zote ili kuweza kujifunza teknolojia mbalimbali zitazowanufaisha wakulima na wazalisha wa bidhaa za kilimo.

Maonesho ya Nane Nane 2024 yatakuwa katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale; Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere; Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye Viwanja vya Ngongo; Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika Viwanja vya Nyamhongolo; Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi; Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye Viwanja vya Themi; na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye Viwanja vya Fatma Mwasa.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".

Mhe. Bashe aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli; Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Prof. Riziki Shemdoe; Menejimenti za Wizara ya Kilimo; na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Singida.

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Мкара katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ...
31/07/2024

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Мкара katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 31 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Bia...
29/07/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) akizungumza kabla ya kufungua Mkutano wa 15 wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam 29 Julai, 2024.

Taarifa kwa Umma kuhusu uapisho wa Mbunge Mteule Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb)
24/07/2024

Taarifa kwa Umma kuhusu uapisho wa Mbunge Mteule Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofan...
24/07/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 24 Julai, 2024.

Chuo cha Viwanda vya Misitu kimeanzisha kozi fupi ya biashara ya hewa kaboni  ambayo imelenga kuifanya nchi kunufaika na...
24/07/2024

Chuo cha Viwanda vya Misitu kimeanzisha kozi fupi ya biashara ya hewa kaboni ambayo imelenga kuifanya nchi kunufaika na zao hilo jipya la misitu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi (FITI), Dkt. Zakaria Lupala amesema asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania ni hifadhi za misitu hivyo kuwa na fursa kubwa ya biashara ya hewa kaboni kwenye soko la kimataifa, lakini jamii haina ujuzi wa kunufaika na fursa ya biashara hiyo yenye mtazamo wa kuhifadhi mazingira.

Amesema pamoja na nchi kuwa na utajiri wa misitu, bado fursa ya biashara ya hewa ukaa haijatumika ipasavyo hatua ambayo imefanya Chuo hicho kuanzisha kozi fupi katika sekta hiyo.

Naye Afisa Misitu Mkuu kutoka Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Emmanuel Msoffe ametoa rai kwa watanzania kutumia fursa ya Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi kuwapeleka vijana wao kupata mafunzo ili waweze kupata ajira na kipato katika kuendeleza maisha yao ya kila siku.

NCHI 45 KUSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE 2024Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. Nyase...
23/07/2024

NCHI 45 KUSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE 2024

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu amewaomba Watanzania wanaoshughulika na kilimo kwenye mnyororo mzima wa thamani wasikose nafasi ya kushiriki katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 kwa sababu ni mwelekeo wa kukuza uchumi na kupanua mtandao mzima wa uzalishaji.

Bw. Nyasebwa ameeleza hayo leo Julai 22, 2024 wakati akihojiwa na Vyombo vya Habari, jijini Dodoma na kuongeza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alishaielekeza Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa Maonesho haya yanakuwa ya taswira ya Kimataifa ambapo kwa mwaka huu yatafanyika katika Kanda Saba, huku Dodoma kufanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni.

Ameongeza kuwa wadau mbalimbali watashiriki ambap vijana na wanawake wanahamasishwa kuonesha namna gani wanazalisha, wanapata mitaji kwani kilimo kinalipa na ni biashara.

“Kwenye Nane Nane kutakuwa na ushindanishaji wa wakulima kuona teknolojia, mbinu, ujuzi na maarifa katika kilimo chao. Kutakuwa na vigezo ambapo wakulima wanatembelewa kuona wamefanya nini, uwekaji wa kumbukumbu za uzalishaji, namna anavyopata faida, namna anavyo tafuta masoko. Tuzo na zawadi zitakazotolewa kwa washindi zitaongeza ari ya wakulima wengi kuendelea kuboresha kilimo chao,” ameeleza Bw. Nyasebwa Chimagu.

Imeelezwa kuwa maandalizi ya mabanda yanaendelea, lakini pia teknolojia mbalimbali za uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na mifugo vinaendelea kupangwa.

Naye Bi. Upendo Mndeme, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Huduma za Ugani amesema hadi sasa nchi 45 zimeonesha nia ya kushiriki maonesho chini ya uratibu wa pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili wageni wapate huduma stahiki. Amesema wageni wengine wamejisajili kwa ajili ya kupata maeneo ya kuonesha bidhaa na teknolojia.

“Wananchi wetu wana fursa ya kupata teknolojia kutoka kwa wenzetu na sisi waratibu tutapata kitu kipya kutoka kwa wenzetu kwa ajili ya kuboresha Maonesho haya ili yaweze kuleta tija kwa wakulima,” amesema Bi. Upendo.

Bi. Upendo amesema kuwa viwanja vya Nane Nane kila baada ya maonesho ya kila mwaka vitabaki kuwa Vituo Mahiri vya Kuhaurisha Teknolojia na Serikali imeanza ukarabati wa kuviendeleza viwe vya Kimataifa ili wakulima waendelee kujifunza teknolojia mpya za kilimo.

HUDUMA KWA WATEJA WA KILIMO KUTINGA NANE NANE 2024 Wateja na wadau mbalimbali wa kilimo wanakaribishwa kupata huduma kwa...
18/07/2024

HUDUMA KWA WATEJA WA KILIMO KUTINGA NANE NANE 2024

Wateja na wadau mbalimbali wa kilimo wanakaribishwa kupata huduma kwa wateja inayotolewa na Wizara ya Kilimo ambapo timu yake itatinga katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024.

Bw. Zacharia Gadiye, Mratibu Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara ya Kilimo ameeleza kuwa “Wizara imejipanga kuhakikisha taarifa za sekta zitapatikana ili kuwezesha wakulima na wadau kupata elimu ya kilimo cha kisasa, teknolojia katika kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao.”

Amezungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari tarehe 17 Julai 2024 katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa pamoja na uwepo wa wataalam wa ugani katika ngazi za vijiji na kata, Wizara ya kilimo imefanya juhudi za kuimarisha mawasiliano kati ya mkulima na wataalam kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call Center). Huduma hizo zinapatikana kwa kupiga simu namba 0733 800200 au 0800 110810.

Maonesho ya Nane Nane 2024 yatafanyika Kitaifa Mkoani Dodoma katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma kuanzia tarehe 1 Agosti hadi 08 Agosti 2024. Aidha, huduma hiyo itapatikana pia kwa mawasiliano ya simu kwa wateja wa ndani au nje ya nchi.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Ashura Katunzi, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa...
22/06/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Ashura Katunzi, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kabla ya uteuzi huu Dkt. Katunzi alikuwa Afisa udhibiti Ubora wa Shirika hilo na sasa anachukua nafasi ya Dkt. Athuman Yusuf Ngenya ambaye amemaliza muda wake.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza Tarehe rasmi ya Ufunguzi na Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFC...
22/06/2024

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza Tarehe rasmi ya Ufunguzi na Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025 Itayakofanyikia nchini Morocco..

Mechi Ya Ufunguzi itachezwa Tarehe 21/12/2025 na mechi ya Fainali itachezwa Tarehe 18/01/2026.

Uongozi wa klabu y Simba SC Tanzania  umetangaza kuwa hautaendelea kuwa na mchezaji Saido Ntibazonkiza baada ya mkataba ...
18/06/2024

Uongozi wa klabu y Simba SC Tanzania umetangaza kuwa hautaendelea kuwa na mchezaji Saido Ntibazonkiza baada ya mkataba wake kumalizika.

Kutoka ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Sulu...
18/06/2024

Kutoka ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua kongamano la maendeleo ya sekta ya habari na kikao kazi cha maafisa habari wa serikali leo Juni 18, 2024.

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taifa Choice posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Nearby media companies


Other News & Media Websites in Dodoma

Show All