30/03/2023
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula amewaagiza Wakurugenzi
wote wa Mamlaka za Serikali za mitaa kupima, kulinda na kusimamia
maeneo yote ya umma na maeneo ya wazi ili kuondokana na mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo.
Agizo hilo amelitoa Machi 29 jijini Dodoma kwenye mkutano Mkuu wa Nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji ambapo alisema kumejitokeza utaratibu mbaya na usiovumilika, wa kuvamia maeneo ya wazi, maeneo ya umma pamoja na maeneo hatarishi na kuyabadilisha kuwa ya matumizi mengine hasa makazi.
Amesema Maeneo hatari kimazingira pamoja na maeneo ya wazi, yakiwemo maeneo maalum kwa matumizi ya baadaye (land bank), yanapaswa kupimwa na kulindwa dhidi ya wavamizi.
Alisema ili tuwe na miji nadhifu na iliyopangwa vyema katika nchi yetu hakuna budi kuanza kusimamia upangaji wa miji midogo na vitovu
vya vijiji vyetu.
"Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2022 inaonyesha kuwa miji
inakuwa kwa asilimia 4.8 na taarifa tulizonazo tuna jumla ya miji midogo
inayochipukia 4,310 nchini ambayo isiposimamiwa ipasavyo itakuwa miji
holela ya baadae," Alisema
"Kwa kutambua umuhimu wa miji hiyo na uwepo wa kasi ndogo ya upangaji wa vijiji nchini, Wizara imeandaa mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini ili kuwezesha jamii yetu kuanza kupanga maeneo yao kuanzia vijijini," alisema Waziri Mabula
Aidha alitoa maelekezo kwa Bodi ya Usajili Wataalam wa Mipango Miji na wanataaluma wote kuweka mkazo Zaidi katika namna ya kuzuia miji yetu midogo na vijiji kuwa makazi holela ya baadae kwa kusimamia na kuelimisha jamii matumizi ya mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini.
Pia alisema Serikali itaendelea na jukumu lake la kuimarisha
mahusiano ya kitaasisi ili kuimarisha maendeleo ya miji pamoja na kupata
fedha kwa ajili ya kupanga na kusimamia miji.
Hata hivyo aliekeza kuwa gharama za kuweza kumudu kupanga, kupima na kumilikisha maeneo yote nchini ni kubwa, Ninaelekeza Mamlaka za Upangaji nchini kutenga fedha kutokana na mapato ya ndani ya kila
mwaka, kwa ajili ya kazi ya kupanga, kupima, kumilikisha, kuendeleza
na kusimamia miji katika maeneo yao.
Akiongelea suala la Mabadiliko ya tabia nchi Waziri Mabula alisema suala la Mabadiliko ya tabia nchi ni suala muhimu sana kwa sasa katika sayansi ya usanifu wa miji duniani kote.
"Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika miji yetu tunatarajia mchango mkubwa sana wa Wataalamu wa Mipango miji katika kuweka mifumo wezeshi kwa ajili ya
kukabiliana na majanga mbalimbali kuanzia katika usanifu wa mipango
kabambe ya Miji na mipango kina ya usimamizi wa uendelezaji wa Miji," alisema Waziri Mabula
Aliekeza katika suala la kuhimili janga la mafuriko mijini inahitajika, siyo tu
kuimarisha uwekaji wa miundombinu k**a mifereji ya maji ya mvua, bali pia
kuweka miundombinu ya kijani k**a vile maeneo chepechepe, maeneo ya
Bafa (Buffer zones), mabwawa ya kuzuiamaji ya mvua (detention ponds)
pamoja na maeneo ya kuwezesha maji kuzama ardhini (porous pavements)
ili kupunguza kasi na madhara ya mafuriko.
"Napenda nisisitize kuwa Maafisa Mipango miji mmepewa jukumu kubwa sana la kuongoza mwonekano wa miji yetu na vijiji kupitia taaluma mliyonayo. Ni matumaini yangu jukumu hilo mtalibeba kikamilifu na kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku na kuzingatia kikamilifu matumizi ya takwimu mbalimbali za Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya majengo na takwimu nyingine kwa ajili ya kuwezesha utendaji kazi wenu kikamilifu," alisema
"Naelekeza bodi ya Usajili Wataalam wa Mipangomiji kuongeza kasi na kuboresha mifumo itakayowezesha upimaji wa utendaji kazi wa kampuni na wataalam katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku," alisema Waziri Mabula
Watumishi na kampuni zitakazofanya
vizuri katika upangaji mwone namna ya kuwapatia motisha na kujenga
ushindani mzuri katika upangaji na usimamizi wa miji ili kuwa na miji salama, Jumuishi, stahimilivu na endelevu.
Pia Alisema Kwamba moja ya mahitaji makubwa katika upangaji wa miji endelevu na himilivu ni pamoja na upatikanajiwa takwimu sahihi zinazoendena na wakati. Ni wazi kwamba umuhimu wa takwimu hizi unajitokeza wakati wa kutoa maamuzi katika kipindi cha upangaji wa miji.
Ni muhimu kujua idadi ya watu katika eneo la upangaji ili kujua ni mahitaji gani ya kijamii yanahitajika katika eneo hilo, kwa mfano idadi ya shule za msingi, shule za awali, zahanati, vituo vya Afya, maeneo ya kuchezea watoto Kwa kuwa sensa ya watu na makazi imefanyika Agosti, 2022 ni vyema sasa takwimu hizo zitumike katika upangaji mipango ya uendelezaji miji.
Aidha, takwimu za umri, jinsi, idadi ya nyumba, idadi ya wakazi katika nyumba nk, zinatumiwa na wataalam wetu wa Mipangomiji katika kupanga mahitaji muhimu ya kijamii miongoni mwa rika mbalimbali, ikiwemo makazi ya wazee, mahitaji ya shule za awali, shule za Msingi, Sekondari, mahitaji ya wenye ulemavu Takwimu na taarifa hizo zote zinapatikana kutoka katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
"Miji ni eneo mojawapo katika kuleta maendeleo ya nchi kupitia uwekezaji wa aina mbalimbali, ingawaje inaendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha miji yetu kutokutoa
mchango uliotegemewa katika kuimarisha uchumi, kuongeza uhimilivu, na kuwa endelevu," alisema
Na kuongeza "Mijiyetu inaukuaji wa mtawanyiko ambao unaongeza gharama za kuweka miundombinu k**a ya maji,umeme, barabara nk, pamoja na gharama zakufuata mahitaji muhimu. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 tuna jumla ya majengo 14,348.372kati ya hayo asilimia 0.5pekee ndio majengo ya ghorofa," alisema.
Alitoa rai kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Miji, Manispaa na Majijikupanga miji na kuifanya kuwa ya kiushindani kibiashara,kitalii, na kimazingiraili iweze kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, na kuwamiji salama na mahali pazuri kwa kuishi na kufanya kazi.
Aidha, aliekeza wataalam wa mipangomiji nchini kusimamia kikamilifu utekelezwaji wa mipango kabambe iliyoandaliwa katika maeneo yenu na mipangokina ili kuwa na
uendelezaji wa mji unaozingatia mipangomiji.
" Ninyi wataalam wa mipangomiji mnapaswa kuwa na wivu na taaluma yenu na msiruhusu kuharibika kwa miji machoni mwenu," alisema waziri Mabula