Greataziz

Greataziz Kukubali Kukosolewa na Kujifunza ni Sehemu ya Mabadiliko na Kukua kwa Binadamu
(1)

Ukiwa mwanaume fala fala huweziona k**a unateswa na mapenzi, kiuhalisia asilimia kubwa ya wana wanaoteswa na mepenzi ni ...
21/11/2023

Ukiwa mwanaume fala fala huweziona k**a unateswa na mapenzi, kiuhalisia asilimia kubwa ya wana wanaoteswa na mepenzi ni wale ambao.

1. Hawana kipato + insecurity za kuzidi.

2. Hawajui malengo yao ni nini katika maisha.

The later results to the former

K**a haujui malengo yako lazima ukose kuwa na kipato maana asilimia 90 ya malengo ya mwanaume ni kushika pesa.

Lengo likiwa mafanikio yako maana yake utapambana kupata kipato na hautokuwa na insecurity za ajabu.

K**a hauna malengo basi utapambania huyo mwanamke anaekuliza huku ukimuona ni wa maana kuliko hata maisha yako mwenyewe.

Ukipambania malengo yako, Trust me unapoteza energy ya kubembeleza mwanamke kila siku na hapa ndio unapata ile class ya ma broo tunaoambiwa.

UNADHARAU SANA na UNAJIONA SANA.

ThrowBack 2012 🧵🌍 😂 Sema Muda Umeenda Sana.
16/11/2023

ThrowBack 2012 🧵🌍 😂 Sema Muda Umeenda Sana.

*MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU*1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi ...
06/11/2023

*MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU*

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa K**a somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa K**a somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa K*K, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni k**a kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.
31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

Una Maoni Gani Kuhusu Maboresho Haya, Je Unadhani Yataleta Tija kwenye Elimu Yetu....!?

03/11/2023

LEO NAKUSHUSHIA BAADHI YA BIASHARA UNAZOWEZA KUFANYA KWA MTAJI MDOGO TU.

✒️ BUSINESS PLANS | MONEY MAKER

1. Advertiser Magazine Case Study & Fact Sheet
2. Agrovet Business Guide
3. Bank Agency Factsheet
4. Beef Butchery Guide
5. Boda Boda Info Pack
6. Bookshop Quick Guide
7. Bottled Water Business Guide
8. Building Materials Yard - Dynamics and Case Study
9. Car Wash Business Guide
10. Chapati Wholesale Case Study
11. Chemist Retail Business Guide
12. Chicken Butchery Guide
13. Chips and Chicken Guide
14. Cookie Mania
15. Corn Chips Quick Guide
16. Cosmetics Retail Business Guide
17. Courier Guide
18. Cyber Cafe Guide
19. Daycare Guide
20. Electrical Parts Retail Guide
21. Executive Barber Shop Guide 2018
22. Feasibility of Cooking Oil Filtering Service
23. Fish Supply to Hotels – Nairobi
24. Flower Business In Nairobi
25. FMCG Small Scale Distribution Quick Guide
26. Free Advertiser Magazine Quick Guide and Case Study
27. Fruit and Juice Parlour Guide
28. Gas(LPG) Retail Guide 2018
29. Gift Services Overview
30. Greenhouse Tomato Guide - Prodution & Market
31. Gym Business Guide
32. Hair Salon Plan
33. Handbag Rental Feasibility
34. Ice Lollies Quick Guide
35. Informal Money Lending Guide
36. Innerwear Quick Guide
37. Keg Bar Business Guide
38. Laundry Business Guide
39. Leather - Skin Trade
40. Local Bar Business Guide
41. Milk Distributorship & Industry Overview
42. Mitumba Retail Guide
43. Motorcycle Spare Parts Retail Guide
44. M-pesa Sub Agency Guide
45. Nails Making Guide
46. Non Woven Bags Making Guide
47. Paint Mixing Business Guide
48. Petrol Station (Independent) Guide
49. Plumbing Hardware Business Guide 2018
50. Pork Butchery & Eatery Guide 2018
51. Printing Business Guide 2018
52. Quick Guide To Supermarket Shelf Space
53. Second Hand Novels Guide
54. Sifted Maize Flour Guide
55. Slot Machines Quick Guide
56. Smokies & Eggs Vending Guide
57. Tents & Chair Leasing Business Guide
58. The Cake Packaging
59. Tiles Retail Business Guide
60. Timber Retail Business Guide
61. Wines and Spirits Retail
62. Sacco's and chamas
63. How to start a business from scratch.
64.Most 200 profitable business in Tanzania.
65. Import business in Tanzania
66.Bank agents business

Jaribu Biashara Mojawapo Kati ya Hizi.

Usidanganywe kufanya jambo lolote la kijinga kwa kutumia    ya "Sijali watu wanasema ninaishi maisha yangu" Ndio huwezi ...
14/10/2023

Usidanganywe kufanya jambo lolote la kijinga kwa kutumia ya "Sijali watu wanasema ninaishi maisha yangu" Ndio huwezi kumfurahisha kila mtu na huwezi kuishi maisha yako kufikia viwango vya kila mtu lakini kuwa na sifa nzuri bado ni jambo jema.

Ukiwa Angani, unaona Nyumba ndogo k**a size ya tofali na ukiwa chini kwenye nyumba unaona ndege ndogo k**a size ya njiwa...
10/10/2023

Ukiwa Angani, unaona Nyumba ndogo k**a size ya tofali na ukiwa chini kwenye nyumba unaona ndege ndogo k**a size ya njiwa.

Ndivyo matatizo yalivyo,tatizo linaonekana dogo kwa kadri linavyo kuwa mbali na wewe... likikufikia ndo unaona ukubwa wake halisi.

ELIMU YA MIKOPO BENKIKumekuwa na malalamiko na vilio kwa baadhi ya watumishi kuhusu mikopo wanayopewa na benki. Wengi wa...
30/09/2023

ELIMU YA MIKOPO BENKI

Kumekuwa na malalamiko na vilio kwa baadhi ya watumishi kuhusu mikopo wanayopewa na benki.

Wengi wao wanalaumu mikopo hiyo kuwa ni kandamizi kwao badala ya kuwapa unafuu imegekuka kuwakandamiza na kuyafanya maisha yao kuwa magumu.

Hapa tatizo sio mikopo inayotolewa na benki bali shida ipo kwenye elimu juu ya namna bora ya kukopa.

Kwa kukosa elimu hiyo, mtumishi wa umma unapokwenda kukopa benki afisa mikopo atakupa chaguo (option) ambalo litakuwa na faida zaidi kwa benki.

Mfano,
Mtumishi mwenye mshahara wa
Tsh.700,000/=baada ya makato
(take home)

Kwa mtumishi asiyekuwa na elimu ya mikopo, akifika benki atamuuliza afisa mikopo kwa mshahara wa laki 7 naweza kukopa kiasi gani??

Hapa afisa mikopo atakachoangalia kwanza ni chaguo lipi litaingizia benki faida kubwa zaidi!

Atapiga mahesabu, kuzingatia sheria ya 1/3 ya mshahara ibaki kwa mtumishi , atapata 2/3 ya 700,000/= ni k**a 466,666.67 hivi.

Sasa chukulia hapo muda wa chini uwe miaka mitano.

Atakwambia una uwezo wa kukopa hadi 19M, makatao yote itakuwa sawa na Tsh. 443,000 kwa mwezi.

Mtumishi asiyekuwa na elimu ya mikopo akiangalia mshahara wake anajikuta inabakisha 270,000.
Anamuuliza afisa mikopo nikichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane je?

Anaambiwa ukichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane kila mwezi utakatwa 325,000 na utabakiwa na 375,000/= kila mwezi.

Mtumishi asiye na elimu hii anakubali kuchukuwa 19M kwa miaka nane kwa sababu tu makato ni madogo.

*USICHOKIJUA SASA*

1. Ukichukuwa mkopo wa 19M kwa miaka
mitano marejesho yako ya Tsh 443,000/=
kila mwezi kwa miaka 5 ni sawa na
Tsh. 443,000×12×5= 26,580,000/= na hivyo
mkopo huo utakuwa umeipatia benki faida
ya Tsh 7,580,000.

2 Ukichukuwa kwa 19m kwa miaka nane kwa
marejesho ya Tsh. 325,000/= kila mwezi
utakuwa na jumla ya marejesho
Tsh. 325,000 ×12×8= Tsh.31,200,000/=
hivyo utaipatia benki faida ya 12,200,000.

K**a mkopo huu lengo lake kubwa ikiwa ni kuendeleza ujenzi wa nyumba, kwa hiyo unachukuwa hiyo 19M ndani ya miaka nane anaishia kwenye kufunga linta.

*KUMBE BASI*
Tunalopaswa kulielewa kwa sisi watumishi wa umma ni kuwa
-🖍Mkopo unaozidi miaka miwili na nusu hapo ni
kujiumiza wenyewe.

-🖍Mtumishi wa umma jitahidi ukope kwa
awamu mgawanyiko zenye muda mfupi
mfupi ili upate unafuu na uifurahie ajira yake.

Chukulia hii 19M ambayo mtumishi mwenye take home ya 700,000 ambaye alichagua kukopa kwa miaka nane, njia bora ni kuanza na 9.5M kwa miaka miwili na nusu tu ambapo atatakiwa kulipa 11.5M kwa makato ya 380,000 kwa mwezi. Riba ya miaka miwili na nusu atakuwa around 1,900,000.

Baada ya kuisha miaka miwili na nusu anachukuwa 9.5M nyingine.
Hapo riba ya miaka mitano itakuwa ni 3,800,000 badala 7,600,000 kwa muda ule ule wa miaka mitano.

Mwisho usikope kwa kufuata mkumbo.
Weka mipango yako kwa awamu ili kuweza kuitekeleza bila maumivu makali

HII ELIMU NI MKOMBOZI WA WATUMISHI
TAFADHALI SHARE NA WENGINE WANUFAIKE

Don’t Be Scared To Start Over, You Might like Your New Story Better.
04/09/2023

Don’t Be Scared To Start Over, You Might like Your New Story Better.

Don’t Be Scared To Start Over, You Might Like Your New Story Better
03/09/2023

Don’t Be Scared To Start Over, You Might Like Your New Story Better

See how far you've come? Be proud of yoursef. If nothing else, one day, you can look at someone straight in the eyes and...
13/07/2023

See how far you've come? Be proud of yoursef. If nothing else, one day, you can look at someone straight in the eyes and say:

"But I lived through it and it made me Who I Am Today 🙏🏾

SOMA KISA HIKI KISHA UTUAMBIE UMEJIFUNZA JAMBO GANI KUBWA.Siku moja alikuja Mzungu kijijini akasema ananunua ngedere mmo...
03/07/2023

SOMA KISA HIKI KISHA UTUAMBIE UMEJIFUNZA JAMBO GANI KUBWA.

Siku moja alikuja Mzungu kijijini akasema ananunua ngedere mmoja kwa 2000, basi wawindaji baadhi wakaleta ngedere.

Wiki iliofuata akapandisha bei ikawa 10,000 kwa ngedere wawindaji wote pale kijijini wakaingia porini kusaka ngedere wakaleta, yule bwana akawanunua akaenda zake

Yule bwana akarudi week nyingine akatangaza bei ni 50,000 wanaume wote na wawindaji kijiji wakaingia porini wakaleta ngedere akawanunua akaenda zake😂.

Baada ya siku 3 akarudi bei ni 100,000 wananchi wote sasa mpaka watoto wakaingia porini kusaka ngedere waje kumuuzia mzungu😂

Cha kustaajabisha wakakuta ngedere waliokua wanapatikana kirahisi tu hawapatikani tena mle maporini, wakapata wachache tu ..watu wakafurahi wakamuuzia yule bwana hao wachache.

Mzungu akawanunua kwa 100,000 akaenda zake😂.

Baada ya siku kadhaa mzungu akarudi na bei ya 200,000 kwa kila ngedere.. wananchi porini saka sana ngedere wasione hata mmoja, wote walishaisha wamemuuzia mzungu😂.

Watu wakarudi jioni mikono mitupu wakiwa na mawazo sana watapata wapi ngedere wengine wa kumuuzia mzungu.

Kidogo wanaskia kuna mtu ananunua mashamba na nyumba kwa bei nzuri wakaona ngoja tumuuzie huyu mashamba na izi nyumba ili tukanunue ngedere tuje tumuuzie mzungu tupate hela tutanunuaga mashamba na nyumba nyingine😂.

Katika kujadili wakaskia kuna mzee kijiji cha pili apo ana z**i la ngedere wengi sana anawauza kila ngedere 100,000, wanakijiji wakauza nyumba na mali zao ili wakanunue wale ngedere kwa yule mzee waje huku wamuuzie mzungu😂.

Basi wakauza mashamba na wengine nyumba zao wakaenda kwa yule mzee kununua ngedere, wakawanunua wale ngedere wotee😂😂.

Kurudi kule kijijini na wale ngedere wakauze wakakuta yule mzungu hayupo😂😂, kuuliza vizuri wanaambiwa mzungu alisharudi kwao siku ile wamemaliza kununua ngedere kwa yule mzee wa kijiji cha pili 😂😂.

Shughuli ikawa wana ngedere mikononi ambao hawawezi kuwafanyia kitu tena maana mteja kashaondoka..😂, na kuna wengine hawana mashamba wala nyumba sababu waliziuza ili wanunue ngedere😂😂.

Kumbe yule mzee kule kijiji cha pili alichonga deal na yule mzungu amhifadhie wale ngedere wake aliokua anawanunua kule alafu atampa 10% ya Udalali Akifanikisha Kuwahadaa wananchi😂😂😂

Baada ya mwezi mzungu akarudi anataka kuanzisha shamba kubwa pale pale kijijini😂, watu wakashangaa atapata wapi wasijue pia yule mtu alienunua mashamba na nyumba zao nae pia alitumwa na yule mzungu nae kala 10% (Hawa Ndio Madalali Wakubwa Nchini) 😂😂.

Wakajikuta pale kijijini wenye nyumba na mashamba wamebaki wachache sana wengi wao hawana nyumba, wala mashamba wana ngedere tu😂😂.

Mzungu akachukua mashamba yake aliyoyanunua kwa mtaji wa fedha za ngedere kutoka kwa wananchi akafungua kampuni akatangaza ajira 🤗

Mwishoe wananchi wengi waliishia kuwa watumwa kwenye yale yaliokua mashamba yao wao wenyewe na pia wakaanza kupanga kwenye wale wenye nyumba wachache ambao hawakuziuza kwa bei kali sana😂😂.

Kule mzungu anawapa mshara kiduchu huku analima na kupata faida kubwa huku wananchi wenzao wanawapandishia kodi kila uchwao😂.

FUNZO KUBWA KWENYE KISA HIKI.
Kwenye mambo haya ya uwekezaji na wawekezaji kutoka nchi za nje, baadhi yetu wapo k**a yule mzee wa kijiji cha pili (Madalali) aliehifadhi ngedere akala 10%😂.

Wapo waliotumwa na mzungu kununua mashamba wakala 10% (Madalali) 😂

Wapo waliosambaza habari kuwa kuna mzee kijiji cha pili ana z**i la ngedere ambao anawauza nao walilipwa ujira wa kusambaza habari chafu😂.
Wapo waliowapandishia wenzao kodi na wengi wao wakaishia kuwa watumwa kwenye ardhi yao wenyewe😂.
Tujiangalie tujitathmin tunasimama wapi!!

PICHA HAINA UHUSIANO NA KISA HIKI.

🎬Picha kutoka Maktaba.

utatoa nini
18/09/2022

utatoa nini

07/06/2022

People who can’t find peace will try to destroy yours.

Happy birthday to my sweet little Nailah! You fill my heart with so much love, and each day I tell myself how very bless...
10/02/2022

Happy birthday to my sweet little Nailah! You fill my heart with so much love, and each day I tell myself how very blessed I am to have a daughter like you!
I want you to know that no matter what happens in life, you will always be my little girl and I will love you forever.
Big kisses to you on your birthday today!

Hebu tupate funzo kidogo Jana jioni nilipata mwaliko nyumbani kwa rafiki yangu mmoja ambae pia ni kapteni wa JWTZ kikosi...
16/01/2022

Hebu tupate funzo kidogo

Jana jioni nilipata mwaliko nyumbani kwa rafiki yangu mmoja ambae pia ni kapteni wa JWTZ kikosi cha anga (Air Transport Station) hapo Majumba sita.

Baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya huku Kitunda, akanijuza anahitaji nimpe namba ya shemeji yangu flani.
Nikataka kujua anaitaka ya nini?
Bila kusitasita, akanijuza kwamba anauza nyumba yake iliyopo maeneo ya Kivule ili wagawane malipo na mkewe!!

Nikashtuka sana, zaidi ya nilivyoshanga.....!

Nikamuuliza kivipi ilhali mnaishi pamoja kwa ndoa halali ya kikristo?

Akanijibu "Tumetengana tangu mwezi November!!"
Hili jibu likanipa kizunguzungu haswaa, yaani zaidi ya kushtuka na kushangaa awali sasa nikapata kizunguzungu.

Awali nikahisi labda ananitania na kwamba tayari pombe ilikuwa inaanza kufanya brain changes zake (maana hawa wajeda wakilewa hawaishagi kufanya vituko vya kuchekesha) lakini akasisitiza kabisa kwamba hatanii wala hafanyi mzaha bali yupo seriously!!

Nikataka kujua ipoje hadi kufikia hatua ya kutengana (huku nikihisi labda kutokuonekana kwa mkewe, alikuwa likizo huko kijijini maana mkewe uyo ni mwalimu wa sekondari flani ya kata).

Akaanza kunisimulia sasa.

Kwamba, mapema mwezi Oktoba 2017, alipata job part time na Knight Support Security Kwa ishu flani za kiintelijensia ya kijeshi na wakamwahidi kumpa Tsh 6M k**a malipo kwa ajili ya kazi iyo, na Tsh 250,000 kwa ajili ya allowances za usafiri wa hapa na pale, chakula na vocha.

Baada ya mapatano hayo, akamjuza mkewe k**a sehemu ya wajibu wake ili ajue kwamba atakuwa anachelewa kurudi nyumbani kwasababu akitoka kazini, atakuwa anaenda huko KSS HQ na maeneo kadhaa kwa mujibu wa hitaji la iyo kazi.

Akanambia kwamba, siku 3 kabla ya kuimaliza iyo kazi akakaa na mkewe ili wapange jinsi ya kuitumia kwa maendeleo ya familia yao (wana watoto watatu).

Basi bwana, katika mjadala huo, mkewe akataka wafungue saluni kubwa ya kupamba wadada ikiwa na uuzaji wa vipodozi, nguo, viatu na mambo kadhaa ya wadada.
YEYE AKAMPINGA kwa hoja kwamba iyo biashara kwasasa ni ngumu sana na haina faida ya haraka haraka, ivyo ni bora wakaongeze vyumba kwenye nyumba yao nyingine (hii anayotaka kuiuza sasa) kisha waongeze idadi ya wapangaji.
MKEWE NAYE AKAKATAA.

Ikabidi wakubaliane kutokukubaliana na kila mmoja akaondoka na hasira zake.

Siku ambayo alikuwa anapewa malipo yake, akamjuza mkewe ili ajue kwamba atarudi na mapesa ayo 6M.

Baada ya kutoka kule KSS alipopewa yale mapesa, hakuona haja ya kuwa na hofu kwasababu ya taaluma yake ya uofisa wa jeshi.
Akaziweka kwenye begi dogo la kijeshi la mgongoni kisha akapanda gari yake na kuondoka.

Wakati yupo njiani, dada yake akampigia simu apitie kwake Kinyerezi, akaona apitie tu.

Pale kwa dada yake, wakati wanaongea wakawa wanakunywa pombe (dada yake anamiliki Pub hapo hapo mbele kidogo ya nyumba yake na mumewe), ilipofika saa 4hivi usiku, akajihisi ameanza kulewa, ivyo akamwita dada yake ndani na kumjuza kwamba anazo 6M na anaomba abaki nazo ili hata k**a kutatokea mushkeri huko njiani, basi pesa ziwe salama apo kwake.

Akatoa pesa zote na kumkabidhi dada yake, lakini begi akaondoka nalo.

Alipofika nyumbani akamkuta mkewe haeleweki heleweki na kwakuwa alikuwa kalewa, hakujali. Akaingia chumbani na kulala huku lile begi ambalo awali alibebea zile 6M alizoziacha kwa dada yake, likiwa kabatini.

Muda mfupi mkewe akaingia chumbani na kuanza kumpa bia zaidi hadi akalewa ingawa sio sana kabisa kisha uyo mkewe akamjuza kuwa mtoto wao anaumwa (wengine wawili wanasoma primary boarding) ivyo ataenda kulala nae. Akamjibu kilevi levi "OK" lakini baadae kidogo alishangaa, tangu lini huo utaratibu wa kulala na mtoto umeanza na mara kadhaa anaumwa lakini haikuwa ivyo?

Akapuuzia na kuamua kulala.

Akazidi kunijuza kwamba, majira ya saa 8 hivi usiku akahisi kuna watu au vitu vinanyata kuelekea chumba kalala (akanisisitizia kwamba hisia za kijeshi zilimjuza ivyo).

Akaisogeza karibu bastora yake na kuchomoa magazini ili asiweze kujeruhi mtu bali aitumie k**a tishio kwa uyo anayekuja kwa kunyata. Kisha akabana nyuma ya mlango.

Gafla wakaingia vijana wa4 wakiwa na mapanga, na yeye nae gafla akawasha taa na kuwanyooshea Ile bastora ambayo haikuwa na risasi.

Lakini haikuwa k**a alivyotarajia, wale vijana wakamvamia na kuanza kumkata kwa panga huku yeye akikinga kwa mikono ili wasimjeruhi kichwani wala usoni, anasema baada ya k**a dakika 15 hivi huku kukiwa na kurupushani kubwa kiasi cha baadhi ya vitu kuanguka, akafanyikiwa kuwadhibiti wawili (anadai aliwapiga nyuma ya shingo na kupoteza fahamu) ila wawili wakakimbia.

Haraka akapiga simu kikosini ili kuomba msaada wa kuwahishwa hospitali. Gari likaja na wanajeshi kadhaa wakiwemo MP na kuanza kufanya uchunguzi wa awali kisha kuondoka na wale vijana wawili ambao hadi muda huo walikuwa bado wamepoteza fahamu.

Anasema, kitu cha ajabu kabisa ni kwamba mkewe hakushtuka kutoka usingizini wala hakutoa msaada wowote ilhali kulikuwa na pilika pilika kubwa baada ya wanajeshi wenzake kufika hapo kwake (anaishi nyumba yake binafsi).

Wiki 1 baadae akapewa ripoti kwamba mkewe ndie alikuwa master planner na engineer wa huo mpango.

Akanambia hakushtuka wala kushangaa bali aliunganisha matukio ya siku ya tukio na hali aliyomkuta nayo mkewe, jinsi "alivyokimbia kulala pamoja" na kitendo chake cha kumuongezea bia zaidi ilhali mkewe hapendi yeye anywe pombe kupita kiasi.

Akaomba kikosini iyo kesi aimalize kifamilia (ingawa wakuu wake walimgomea lakini baadae walimkubalia na kumjuza kuwa hao vijana ni waendesha bodaboda hapo hapo Kitunda na waliahidiwa kulipa Tsh 1M kwa kazi iyo ikiwa na maana wangegawana 250,000 kila mmoja).

Akanambia baada ya kukubaliwa, ndipo alipomjuza mkewe kwamba *_ndoa imekufa rasmi k**a yeye alivyowakodi vijana waje kumuua kisha wampore ile pesa ambayo hata ivyo hakurudi nayo bali aliicha kwa dada yake kwakuwa alikuwa keshaanza kulewa.

Akanambia anataka kuuza iyo nyumba kisha pesa yote ampe uyo mwanamke kwasababu ameshajua kuwa anashida ya pesa na sio ndoa.

*****************
Nimeitafakari sana hii kitu na kuona leo niwasimulie ili angalau tupate picha jinsi roho ya tamaa inavyoweza kuingia hata kwa wanandoa kiasi cha kutaka kuuawana ili mmoja apate pesa.

Nawatakia baraka za Bwana huku tukitafakari wa pamoja kisa hiki cha kweli kilichomkuta rafiki yangu huyu ambae k**a asingekuwa mwanajeshi, angeshakuwa amelala mauti kwa tamaa ya mke wake.

28/12/2021
MemoryChelsea welcomed Arsenal to Stamford Bridge for a Premier League game in October 1999.Prior to that game, Chelsea ...
20/12/2021

Memory
Chelsea welcomed Arsenal to Stamford Bridge for a Premier League game in October 1999.

Prior to that game, Chelsea had won six of their opening nine matches, including a 5-0 victory over Sir Alex Ferguson's treble winners, and were yet to concede a goal at home.

They looked likely to continue their home run without conceding, as they were leading 2-0 in over 70 minutes, with goals by Tore Andre Flo and Dan Petrescu.

However, Kanu Nwankwo scored a hattrick in the 75th, 83rd and 90th minute to secure an astonishing comeback win for the Gunners.

Marc Overmars provided assist for Kanu's first and second goal while the third goal was an incredible solo effort by the Nigerian, which resulted in the famous "Kan-U Believe It" commentary line by Martin Tyler.

Kanu was named Africa Footballer of the Year for the second time that year and scored 16 goals across all competitions that season.

Imagine you were born in 1900.When you're 14World War I beginsand ends at 18 years oldwith 22 million dead.Shortly after...
19/12/2021

Imagine you were born in 1900.

When you're 14
World War I begins
and ends at 18 years old
with 22 million dead.

Shortly after, a global pandemic
Flu called 'Spanish' ",
kills 50 million people.
You come out alive and free
You are 20 years old.

Then, at 29, you survive the global economic crisis that started with the collapse of the New York Stock Exchange, causing Inflation, Unemployment, and Hunger.

At 33, the n***s come to power.
You turn 39 when World War II starts and ends at 45 During the Holocaust (Holocaust), 6 million Jews die.
There will be over 60 million deaths in total.

When you're 52, the Korean War begins.

At age 64, the Vietnam War begins and ends at age 75

A boy born in 1985 thinks his grandparents have no idea how difficult life is, but they have survived several wars and disasters.

A boy born in 1995 and now 25 years old thinks it's the end of the world when his Amazon package takes over three days to arrive or when he doesn't get more than 15 likes for their photo posted on Facebook or Instagram. ....

In 2020, many of us live comfortably, have access to different sources of home entertainment, and often have more than we need.

None of this existed before.
But we survived far more disastrous circumstances and never lost the joy of living.

We should be grateful
Michael Crown


When they fail to bring youdown they influence others to hate you 😢💞🙏. (Wanaposhindwa kukushushachini wanashawishi wengi...
14/12/2021

When they fail to bring you
down they influence others to hate you 😢💞🙏.
(Wanaposhindwa kukushusha
chini wanashawishi wengine wakuchukie...)

Chasing after the wrong thing will always leave you disappointed, and disappointed opens the door for depression.

Lord protect me from what’s being planned behind my back!
02/12/2021

Lord protect me from what’s being planned behind my back!

10/11/2021
Mwandishi maarufu na mshauri wa mambo ya kifedha Howard Ruff aliwahi kusema kuwa...“ It wasn’t raining when Noah built t...
08/11/2021

Mwandishi maarufu na mshauri wa mambo ya kifedha Howard Ruff aliwahi kusema kuwa...

“ It wasn’t raining when Noah built the ark”

(Wakati Nuhu Anajenga Safina Mvua haikuwa inanyesha).

Msemo huu una maana kubwa sana kwa kila anayetaka mafanikio.

Tabia ya watu wengi sana ni kuanza kujiandaa pale wanapoziona fursa ama zinapowakaribia.

Ukiwa wa namna hii utajikuta kila siku unachelewa.

Wakati sahihi wa kujenga safina ni wakati ambako hakuna mvua.

Usisubiri usikie kuna kupandishwa cheo ndio uanze kutafuta kuongeza elimu.

Usisubiri uambiwe kuna mchongo ndio uanze kutafuta ujuzi.

Jiulize sasa hivi unahitaji nini?

Na anza kufanyia kazi ili fursa yako inapokuja ikukute ukiwa tayari.

Kuna watu wanadhani muda ambao hawana kitu cha kufanya basi ni muda wa kulala siku nzima...
..kuzurura ama kuangalia movie tu n.k

Ukijigundua uko kwenye kipindi kinachoonekana k**a hauna cha kufanya, kumbuka ni muda wa kujiandaa Mungu amekupa.

Usiutumie vibaya, kwa sababu kuna fursa iko njiani itakuja baada ya hapo.
Ikukute ukiwa tayari.

Je, wewe Unajiandaa au Unapoteza muda?

They killed ur name privately but God is about to honor ur name publicly!
22/10/2021

They killed ur name privately but God is about to honor ur name publicly!

NI KAZI KWELI KWELI USIPITE SOMA HAPA NI MUHIMU SANA.MWANAUME ANAHITAJI:1. Kupikiwa2. Unyumba3. Kupumzika4. UvumilivuMWA...
14/04/2020

NI KAZI KWELI KWELI USIPITE SOMA HAPA NI MUHIMU SANA.
MWANAUME ANAHITAJI:
1. Kupikiwa
2. Unyumba
3. Kupumzika
4. Uvumilivu

MWANAMKE ANAHITAJI MWANAUME WAKE UWE:-
1. Mpenzi
2. Rafiki
3. Mshikaji
4. Kaka
5. Baba
6. Mwalimu
7. Bosi
8. Mpiganaji
9. Askari
10. Mlinzi
11. Mpishi
12. Fundi umeme
13. Fundi bomba
14. Mchungaji
15. Mzee wa kanisa
16. Shehe
17. Daktari
18. Mpambaji
19. Mwana mitindo
20. Modo
21. Mnyanyua vyuma
22. Fundi magari
23. Mwanasheria
24. Mhasibu
25. Fundi seremala
26. Mcheshi
27. Mwanamuziki
28. Muigizaji
29. Shamba boi
30. Fundi ujenzi
31. Msafi
32. Unajali
33. Mzazi
34. Mlezi
35. Mvumilivu
36. Mjanja
37. Mpole
38. Mkarimu
39. Msikivu
40. Mtunza siri
41. Mkweli
42. Kiongozi
43. Tajiri
44. Mpangaji
45. Mwana Michezo
46. Mtundu
47. Tegemeo
48. Jasiri
49. Mthubutu
50. Shupavu
51. Mwerevu
52. Muungwana

HAPO HAPO UNATAKIWA:-
53. Uwe Fundi kitandani.
54. Uwe unamtoa outing.
55. Uwe unampa pesa za kutosha.
56. Usimsumbue sumbue.
57. Usiangalie wanawake wengine.

HALAFU KUNA:-
58. Kumnunulia vizawadi zawadi hapa na pale.
59. Kumsifia alivyoumbika.
60. Kumsifia alivyopendeza.
61. Kumfungulia mlango, kumshikia pochi.

PIA USISAHAU:-
62. Siku yake ya kuzaliwa.
63. Kumbukumbu ya ndoa.
64. Siku ya valentine.

MUHIMU SANA, KUWA MAKINI:-
65. Jifunze kutoulizia chenji ukimpa pesa ya shopping.
66. Usipende kubishana nae kila kitu.

*MATATIZO YA AFRICA YATAZIDI KUONGEZEKA HASA BAADA YA UJIO MPYA WA URUSI NA CHINA. TUJIFUNZE KWENYE HILI LA COVID-19* Tu...
12/04/2020

*MATATIZO YA AFRICA YATAZIDI KUONGEZEKA HASA BAADA YA UJIO MPYA WA URUSI NA CHINA. TUJIFUNZE KWENYE HILI LA COVID-19*

Tukiangalia historia ya anguko la shirikisho la SOVIET UNION/USSR na kipindi cha mwisho wa vita baridi miaka ya 1989. Kulitokea nguvu kubwa ya ukuwaji wa kiuchumi kutokea mataifa ya magharibi na Marekani.

Mashirika ya fedha k**a IMF na World bank walitoa mikopo ya masharti yaliyoelekeza haki za binadamu, utawala bora na demokrasia kwa watawala wa Africa.

Hatua hii ilikuwa k**a wimbi la kukua kwa democrasia na utawala bora kwa Africa hasa kwa nchi zilizotaka mikopo hiyo. Afrika ilianza kidogo kidogo kuondokana na watawala madictotar na kuruhusu democrasia, utawala bora na haki za binadamu, ukiangalia nchi k**a Kenya, South Africa nk ziliguswa na nguvu za world bank na IMF, historia inatuambia hivyo. Kwa mashart haya ya IFM na World bank kwa kiasi kikubwa na kwa hatua yaliifanya Afrika kupiga hatua za kidemokrasia na mambo mengine yaliyohusu jamii, mfano afya, elimu na miundo mbinu.

UJIO mpya wa China na RUSIA unairudisha Afrika miaka 50 nyuma, haya mataifa mawili ya Asia na Ulaya yamekuja na ajenda ya mikopo isiyokuwa na mashart hasa upande wa haki za binadamu, utawala bora na demokrasia. Kwa hali hii ni watawala wa Africa hawataelekea world bank au IMF kwenye masharti, wengi wataelekea kwa wachina na Rusia ambao wameamua kuja kwa mfumo unaopendwa na watawala wetu. Tumeona wakiwaita watawala kule Beijing na Moscow.

Leo hii Mchina anatuletea vifaa vya kukabiliana na COVID-19 akiviita MSAADA huku media zake zote zikiwa zinaonyesha live ni vipi China inavyo isaidia Africa lakini hawafanyi live coverage pale wanapo wabagua waafrika tena kwenye kipindi hiki ambacho dunia inaongea lugha moja. Inakuwaje umbague mwa afrika unayeishi naye China alafu ukamsaidie aliyeko Afrika!

Pamoja na kwamba gonjwa hili kwa mara ya kwanza lilianzia China pale WUHAN mwishoni mwa 2019 na kuathiri kubwa ya wachina wenyewe, Afrika iliungana na wachina na pamoja tulisema ZHONG GUO JIA YOU/ ikiwa na maana ya kuwatia moyo na nguvu wa China tukiakini ni ndugu na marafiki.

Pamoja na hali ile bado nchi zetu hazikufunga mipaka yetu na wachina, wengine walikimbilia kwetu, wengine tunaishi nao kwa muda mrefu tena bila VISA au resident permit na hata wengine kufanya inter marriage na dada au kaka zetu. Ila wao wanasema China ni kwa ajili ya wachina wakati mwingine wanasema bora wakaribishe watu weupe na siyo mtu mweusi. Ubaguzi wa wachina kwa mwa afrika nchini China ni mkubwa na wa kutisha.

Kinachotokea leo, wachina wanafukuza wa afrika na kuwalaza nje, hawataki walale katika majumba yao, hawataki waingie ktk restaurant zao wala mahotelini mwao wanaamini kuwa mtu mweusi ndiye ana import Corona. Matangazo yamewekwa milangoni mwao yakiwataka wa afrika waondoke. Unafukuzwa kwa usimamizi wa polisi, hapa serikali ya China inajitetea kwa lipi kuwa haihusiki! Madness and madness.

Leo wanakuja na pambio kuwa wanaofukuzwa ni wale wasio kuwa na VISA au resident permit. Hivi hali ya sasa ya dunia unapata wapi nguvu ya kufuatilia VISA za wageni huku unajua kuna lockdown na maofsini, hospital kwao hawataki kuona mtu mweusi. Wakajifunze kwa mjerumani.

Toka awali wachina wamekuwa wabaguzi wakubwa sana kwa mtu mweusi hasa anayetoka Afrika, wanatauita wachafu, wakaorofi, hatuna maana nk. kila jina baya mchina anampatia mwa afrika. Ukweli ni kwamba wachina ni wachafu wakorofi, wababaishaji na wa hovyo kutuliko sisi. Kuna siku nitaeleza kwa nini bara la Afrika wanaliita FEI ZHOU/非洲。

Si kwa wanafunzi, wafanyabiashara au wakazi wa kiafrika walioko China wote wanabaguliwa. Ukienda vyuoni, kuna ubaguzi wa kila namna, Mfano swala la mahusiano ya binti wa kichina na mvulana mweusi ni k**a sumu vyuoni! wachina hawataki kuona wala kusikia haya mahusiano, unaweza kuwa deported, wa afrika wamewawa na hata kufungwa kwa kosa la kuwa na mahusiano na mabinti wa kichina. Wao kwetu wamezaa k**a kuku.

Ndg zangu watu weusi, kuna haja ya kubadirisha mtizamo na mawazo yetu katika kujenga nchi zetu hata k**a itachukua muda mrefu lakini tutafika na tutafanikiwa kuliko kutegemea hawa watu weupe na yellow! Mtegemea cha nduguye hufa maskini.
Naungana na viongozi wenye mitizamo ya kujenga nchi zetu kwa mikono yetu na kwa kutumia rasilimali zetu. Je Afrika tutaweza kujitegemea na kuachana na hawa watu?

Address

Dodoma
41104

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Greataziz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Maisha Ni Safari

Amigos Uthubutu Unakuja Pale Unaporuhusu Wazo Linalokuumiza Kichwa Likuumize Na Mikono Kulitimiza. Pindi Unapoanza Kuona Thamani Yako Utagundua Ni Vigumu Sana Kuendelea Kukaa Na Wasio Jithamini. MUNGU Akikupa Utajiri Wa Mali, Jitahidi Kuwa Maskini Wa Roho Waone Wasio Na Mali Kuwa Bado Binaadamu Wa Thamani Wewe Haukuzaliwa Navyo.

#BusaraZaMtaani #hekima #hekimayamtaani #busara #greataziz1 #greataziz