30/09/2023
ELIMU YA MIKOPO BENKI
Kumekuwa na malalamiko na vilio kwa baadhi ya watumishi kuhusu mikopo wanayopewa na benki.
Wengi wao wanalaumu mikopo hiyo kuwa ni kandamizi kwao badala ya kuwapa unafuu imegekuka kuwakandamiza na kuyafanya maisha yao kuwa magumu.
Hapa tatizo sio mikopo inayotolewa na benki bali shida ipo kwenye elimu juu ya namna bora ya kukopa.
Kwa kukosa elimu hiyo, mtumishi wa umma unapokwenda kukopa benki afisa mikopo atakupa chaguo (option) ambalo litakuwa na faida zaidi kwa benki.
Mfano,
Mtumishi mwenye mshahara wa
Tsh.700,000/=baada ya makato
(take home)
Kwa mtumishi asiyekuwa na elimu ya mikopo, akifika benki atamuuliza afisa mikopo kwa mshahara wa laki 7 naweza kukopa kiasi gani??
Hapa afisa mikopo atakachoangalia kwanza ni chaguo lipi litaingizia benki faida kubwa zaidi!
Atapiga mahesabu, kuzingatia sheria ya 1/3 ya mshahara ibaki kwa mtumishi , atapata 2/3 ya 700,000/= ni k**a 466,666.67 hivi.
Sasa chukulia hapo muda wa chini uwe miaka mitano.
Atakwambia una uwezo wa kukopa hadi 19M, makatao yote itakuwa sawa na Tsh. 443,000 kwa mwezi.
Mtumishi asiyekuwa na elimu ya mikopo akiangalia mshahara wake anajikuta inabakisha 270,000.
Anamuuliza afisa mikopo nikichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane je?
Anaambiwa ukichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane kila mwezi utakatwa 325,000 na utabakiwa na 375,000/= kila mwezi.
Mtumishi asiye na elimu hii anakubali kuchukuwa 19M kwa miaka nane kwa sababu tu makato ni madogo.
*USICHOKIJUA SASA*
1. Ukichukuwa mkopo wa 19M kwa miaka
mitano marejesho yako ya Tsh 443,000/=
kila mwezi kwa miaka 5 ni sawa na
Tsh. 443,000×12×5= 26,580,000/= na hivyo
mkopo huo utakuwa umeipatia benki faida
ya Tsh 7,580,000.
2 Ukichukuwa kwa 19m kwa miaka nane kwa
marejesho ya Tsh. 325,000/= kila mwezi
utakuwa na jumla ya marejesho
Tsh. 325,000 ×12×8= Tsh.31,200,000/=
hivyo utaipatia benki faida ya 12,200,000.
K**a mkopo huu lengo lake kubwa ikiwa ni kuendeleza ujenzi wa nyumba, kwa hiyo unachukuwa hiyo 19M ndani ya miaka nane anaishia kwenye kufunga linta.
*KUMBE BASI*
Tunalopaswa kulielewa kwa sisi watumishi wa umma ni kuwa
-🖍Mkopo unaozidi miaka miwili na nusu hapo ni
kujiumiza wenyewe.
-🖍Mtumishi wa umma jitahidi ukope kwa
awamu mgawanyiko zenye muda mfupi
mfupi ili upate unafuu na uifurahie ajira yake.
Chukulia hii 19M ambayo mtumishi mwenye take home ya 700,000 ambaye alichagua kukopa kwa miaka nane, njia bora ni kuanza na 9.5M kwa miaka miwili na nusu tu ambapo atatakiwa kulipa 11.5M kwa makato ya 380,000 kwa mwezi. Riba ya miaka miwili na nusu atakuwa around 1,900,000.
Baada ya kuisha miaka miwili na nusu anachukuwa 9.5M nyingine.
Hapo riba ya miaka mitano itakuwa ni 3,800,000 badala 7,600,000 kwa muda ule ule wa miaka mitano.
Mwisho usikope kwa kufuata mkumbo.
Weka mipango yako kwa awamu ili kuweza kuitekeleza bila maumivu makali
HII ELIMU NI MKOMBOZI WA WATUMISHI
TAFADHALI SHARE NA WENGINE WANUFAIKE