Sufian Mzimbiri

Sufian Mzimbiri page yetu ni maalum kwa habari na mafundisho mbalimbali yanayo husu Uislamu

Napenda Visa Vya Mitume Na
Maswahaba Alayhim Salaam
Ukurasa Rasmi Wa Al-faqeer
Sufian Muhammad Mzimbiri
The Official page for El-Faqeer
Sufian Muhammad Mzimbiri
الصفحة الرسمية للفقير سفيان محمد مزمبر

🎉 Just completed level 3 and I'm so excited to continue growing as a creator on Facebook!
04/01/2025

🎉 Just completed level 3 and I'm so excited to continue growing as a creator on Facebook!

04/01/2025

Hakuja patapo kukuona Ewe Mtume Wa Allah Lakini Tunakupenda

لم نراك يا رسـول الله لكننا نحبك ﷺ.🩵.

ألا بذكرِ الله تطمئنُ القلوب󱢏
04/01/2025

ألا بذكرِ الله تطمئنُ القلوب󱢏

‏{ أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ }.🖤
04/01/2025

‏{ أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ }.🖤

04/01/2025

من أسباب زيادة الرزق كثرة الصلاة على النبي󱢏

With Facebook for Creators – I'm on a streak! I've been a top fan for 3 months in a row. 🎉
04/01/2025

With Facebook for Creators – I'm on a streak! I've been a top fan for 3 months in a row. 🎉

Jambo tusilopenda waume kutoka kwa wake zetu ni SAUTI ya Juu, Mke hakikisha unashusha sauti yako pindi ukiwa uko na mume...
04/01/2025

Jambo tusilopenda waume kutoka kwa wake zetu ni SAUTI ya Juu,

Mke hakikisha unashusha sauti yako pindi ukiwa uko na mume wako au ukiwa unazungumza na watoto wako ilhali mimeo yupo, wanaume wote hatupendi mke mwenye sauti kubwa, na asili ya mke ni kuwa na sauti ndogo, mke kuzungumza kwa sauti ya juu huko ni kujaribu kumtikisa mumeo jambo ambalo ni hatari mno

03/01/2025
FAMILIA YA MTUME (S.A.W)Mtume ametokana katika ukoo wa Ibn Hashimu. Na ukoo huu umeitwa kwa jina hili kutokana na kurith...
03/01/2025

FAMILIA YA MTUME (S.A.W)

Mtume ametokana katika ukoo wa Ibn Hashimu. Na ukoo huu umeitwa kwa jina hili kutokana na kurithi jina hili kutoka kwa mzee wao Hashim Ibn Abd Manaf. Hapa tutaona kwa ufupi.

1. Hashim:
Huyu alikuwa ni katika wazee wanaoheshimika sana katika kabila la kikuraishi Maka enzi hizo. Pia ndie ambaye alikuwa na jukumu la kuwapa chakula na maji mahujaji wote. Mzee huyu alitambulika pia kwa kuwa tajiri na mtu mkweli na muwazi. Pia alijulikana kuwa ndiye mzee wa kwanza kuwalisha mahujaji mkate uliochanganywa na mhuzi.

Jina lake halisi ni Amr na ameitwa Hashim kutokana na kitendo chake cha kutengeneza mikate kwa mahujaji. Pia ndie ambaye alianzisha safari mbili za makuraishi wakatika wa kipupwe na kiangazi jerea Quran suat Quraysh. Pia imeripotiwa kuwa aliwahi kwenda Syria k**a mfanya biashara. Alipokuwa Madina alimuoa Salma mtoto wa Amr kutoka kabila la Bani ‘Adi bin An-Najjar. Alikaa pamoja na mkewake Madina kwa muda kisha akaelekea tena Syria wakati ho alimwacha mkewe akiwa ana ujauzito.

Mzee Hashim alikfariki 497 B.K nchini Palestina katika mji uitwao Ghazza. Bada ya kifo cha mzee huyu mke wake alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa ‘Abdul-Muttalib na lilijulikana kwa jina la utani k**a Shaiba. Alipewa jina hili kwa sababu alizaliwa akiwa na nywele nyeupa yaani mvi kwenye kichwa chake. Mke wake alimchukuwa Mtoto ‘Abdul-Muttalib na kumpeleka kwenye nyumba ya baba yake Madina. Kuzaliwa kwa kijana ‘Abdu-Muttalib hakukujulikana na yeyote katika familia ya Hashim.

Hashim alikufa akiwa na watoto wanne; Asad, Abu Saifi, Nadla na ‘Abdul-Muttalib. Pia alikuwa na watoto wak**e watano ambao ni; Ash-Shifa, Khalida, Da’ifa, Ruqyah na Jannah.

2. Abdul-Muttalib:
Baada ya kifo cha Hashim, kazi ya kulisha mahujaji alipewa ndugu yake Al-Muttalib bin ‘Abd Munaf ambaye alifahamika kwa kuwa na sifa ya ukarim, uwazi na ukweli. Sasa wakati ambao ‘Abdul-Muttalib alipofikia umri wa ujana mzee Al-Muttalib alizipata habari juu ya kuwepo kwa mtoto wa kaka yake Hashimu huko Madina. Hivyo akafunga safari ili akamchukuwe mtoto wa ndugu yake. Basi pindi alipomuona tu machozi yalimtoka na kudondoka kupitia kwenye mashavu yake. Alimkumbatia na kumpandisha kwenye ngamia wake. Lakini kijana alikataa kwenda madina mpaka apate ruhusa kutoka kwa mama yake.

Basi mzee Al-Mutalib akaenda kwa mama yake kijana na kuomba aruhusiwe aondoke nae kuelekea Makkah. Lakini mama nae akakataa kumruhusu kijana wake kuondoka. Lakini mzee Al-Muttalib akatumia maneno ya ushawishi kwa kumwambia kuwa “mtoto wako anakwenda Makka kushika madaraka ya baba yake pia kwa ajili ya kuitumikia Al-kaba (nyumba tukufu ya Allah). Kwa maneno haya mama alikubali kumruhusu mwanae.

Zee al-Muttalib alipofika Makka na kijana wake watu wakadhani kuwa yule ni mtumwa wake, lakini akawaambia kuwa “huyu ni mwanangu, ni mtoto wa kaka yangu Hashim” Kijana Abdul-Muttalib akapelekwa nyumbani kwa baba yake mzee Al-Muttalib, na aliishi pale mpaka mzee Al-Muttalib alipofariki katika sehemu iitwayo Bardman huko Yemen, basi hapo madaraka yote alipewa Abdul-Muttalib. Alifahamika kwa utawala wake ulio mzuri na upendo kwa watu wa Makkah. Alikuwa ndiye kiongozi katika mambo ya kusimamia Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba.

1. Wakati mzee Al-Muttalib alipofariki, Nawfal alichukuwa madaraka kimaguvu kutoka kwa Abdul-Muttalib. Hivyo Abdul-Muttalib akaomba msaada kwa maquraish wakakataa kumsaidia, akaamuwa aombe msaada kwa mjomba wake Abu Sa‘d bin ‘Adi kutoka katika kabila la Bani A-Najjar ambaye alikubali kumsaidia hivyo akaja maka akiwa na wanajeshi wapanda farasi 80. Alipofika akaenda kwa Nawfal na akawashuhudishia wazee wa kiqurayshi kuwa k**a Nawfal hatarudisha madaraka kwa mpwa wake basi atamkata kwa upanga. Baada ya hapo akaenda nyumbani kwa mpwa wake na akakaa hapo kwa muda wa siu tatu. Alifanya ibada ya Umrah kisha akarudi Madinah.

Baadae Nawfal akaingia makubaliano ya kusaidiana kati ya ukoo wake na ukoo wa Bani ‘Abd Shams bin ‘Abd Munaf, makubaliano ya kusaidiana dhidi ya kuwapinga bani Hashim (yaani ukoo wa Abdul-Muttalib). Wakati kabila la Khuzaa lilipoona ukoo wa Bani An-Najjar wanawasaidia bani Hashim nao wakaingia makubaliano na ukoo wa Bani Hashim dhidi ya kumpinga Nawfal na Kundi lake. Kaika wakati wa utawala wa mzee Abdul-Muttalib alishuhudia matukio makuu mawili ambayo ni kuchimbwa kisima cha zamzam pamoja na kuangamizwa kwa jeshi la tembo.

Kwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Basi akachimba na ndipo akakuta chini ya kisima vitu ambavyo vilifukiwa pamoja na kisima. Walofukia vitu hivi ni watu kutoka kabila la Jurhum. Hawa pindi walipolazimika kuondoka Maka walikifukia kisima cha zamzam na kufukia baadhi ya vitu vya thamani k**a mapanga, nguo za vita, na dhahabu. Baada ya hapo mlango wa alka’aba ukatengenezwa kwa hii dhahabu waloipata. Na unyweshwaji wa maji ya zamzam kwa mahujaji ukarudi upya.

Basi kisima cha zamzam kilipoanza kutoa maji, watu kutoka kabila la quraysh walitaka kufanya makubaliano juu ya maji yale lakini Abdul Al-Muttalib alikataa kwa kudai kuwa Allah amempa mamlaka yeye tu. Basi wakakubaliana wakamuulize kuhani kutoka ukoo wa Bani Sa’ad juu ya swala hili. Basi Allah akawaonesha alama za ukweli juu ya madai ya Abdul Al-Muttalib. Baada ya hapo mzee Abdul Al-Muttalib kwa shukran yake kwa Allah akaapa kumtoa kafara mtoto wake kwa Mwenyezi Mungu.

Tukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka’aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)

Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.

Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San’a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.

Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.

Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo.

Mzee Abdul Al-Muttalib alikuwa na watoto wa kiume kumi ambao ni Al-Harith, Az-Zubair, Abu Talib, ‘Abdullah, Hamzah, Abu Lahab, Ghidaq, Maqwam, Safar na Al-‘Abbas. Pia alikuwa na watoto wa k**e sita ambao ni Umm Al-Hakim, Barrah, ‘Atikah, Safiya, Arwa NA Umaima.

3. Abdallah: huyu ndiye baba wa Mtume Muhammad (s.a.w). mama yake aliitwa Fatimah mtoto wa ‘Amr bin ‘A’idh bin Imran bin Makhzum bin Yaqdha bin Murra. Abdallah alikuwa ndiye mtoto mtanashati zaidi kuliko watoto wote wa mzee Abdul-Muttalib alikuwa mcheshi zaidi na alipendwa zaidi kuliko watoto wote wa Mzee Abdul-Al-Muttalib.na huyu ndiye mtoto ambaye mishale ya kafara ya ahadi aloiweka mzee Abdul al-Muttalib ilimuangukia.

Pindi watoto wake mzee Abdul al-Muttalib walipofikia balehe aliwaita na kuwaambia kiapo cha siri alichokiweka juu wa kutoa kafara ya mtoto wake kwa mungu wao Hubal. Basi majina ya watoto yakaandikwa kwenye mishale ya kuangalizia utabiri na jina la Abdallah ndilo likatokelezea kuwa ndie aliyechagulia kutolewa kafara. Kwa kuwa huyu ndiye Mtoto anayependwa zaidi na mzee Abdul al-Muttalib hivyo akashauriwa kubadilisha na ngamia. Baada ya kuangalizi ni ngamia wangapi wanafaa ngamia miamoja ndio wakaonekana wanafaha badala ya kuchinjwa kwa Abdallah. Mtume (s.a.w) alikuwa akisema “mimi ni mtoto wa wachinjwa wawili” yaani ismail mtoto wa Mtume Ibrahimu na Abdallah mtoto wa Abdul al-Muttalib.

Addallah alifariki baada ya mke wake kupata uja uzito kwa muda wa miezi miwili. Wanazuoni wa historia wanatueleza kuwa alifariki akiwa na umri wa miaka 18 na hakuacha chochote katika urithi. Abdallah alifariki Madina alipokuwa anarudi kutoka kwenye safari za kibiashara kutokea Sham baada ya kupatwa na ugonjwa wa ghafla na alizikwa Madina upande wa ujombani kwake.

Sufian Mzimbiri

HISTORIA YA MTUME MUHAMMAD (SAW)🟢NASABA YA MTUME (S.A.W)Wanazuoni katika fani ya historia wamegawanya nasaba ya Mtume ka...
03/01/2025

HISTORIA YA MTUME MUHAMMAD (SAW)

🟢NASABA YA MTUME (S.A.W)
Wanazuoni katika fani ya historia wamegawanya nasaba ya Mtume katiak makundi matatu. Kundi la kwanza ndilo linakubaliwa na kuwa ni usahihi kwa makubaliano ya wanazuoni wote na hili ni kundi linaloiangalia nasaba ya Mtume kutoka tangu kwa baba yake mpaka kufika kwa Mzee ‘Adnan. Kundi la pili lina shaka kwani hakuna makubaliano ya ujumla juu ya baadhi ya watu. Na kundi hili ni lile linaloangalia nasaba ya Mtume kutokea kwa mzee Adnan mpaka kufika kwa Mtume Ibrahimu (a.s). kundi la tatu lina shaka juu ya ukweli wake. Na hili ni lile kundi linaloangalia nasaba ya Mtume kutoka kwa Mtume Ibrahimu mpaka kufika kwa Mtume Adam (a.s).

1. Kundi la kwanza: Muhammad bin ‘Abdullah bin ‘Abdul-Muttalib (ambaye aliitwa Shaiba) bin Hashim, (aliitwa ‘Amr) bin ‘Abd Manaf (aliitwa Al-Mugheera) bin Qusai (pia aliitwa Zaid) bin Kilab bin Murra bin Ka‘b bin Lo’i bin Ghalib bin Fahr (ambaye aliitwa Quraish na kutoka kwa huyo ndipo tunapata kabila la Quraysh) bin Malik bin An-Nadr (pia aliitwa Qais) bin Kinana bin Khuzaiman bin Mudrikah (pia aliitwa ‘Amir) bin Elias bin Mudar bin Nizar bin Ma‘ad bin ‘Adnan.

1. Kundi la pili: ‘Adnan bin Add bin Humaisi‘ bin Salaman bin Aws bin Buz bin Qamwal bin Obai bin ‘Awwam bin Nashid bin Haza bin Bildas bin Yadlaf bin Tabikh bin Jahim bin Nahish bin Makhi bin Aid bin ‘Abqar bin ‘Ubaid bin Ad-Da‘a bin Hamdan bin Sanbir bin Yathrabi bin Yahzin bin Yalhan bin Ar‘awi bin Aid bin Deshan bin Aisar bin Afnad bin Aiham bin Muksar bin Nahith bin Zarih bin Sami bin Mazzi bin ‘Awda bin Aram bin Qaidar bin Ishmael mtoto wa Abraham (amani iwe juu yao).

1. Kundi la tatu: kuanzia kwa Nabii Ibrahim (amani iwe juu yake) , Ibn Tarih (Azar) bin Nahur bin Saru‘ bin Ra‘u bin Falikh bin Abir bin Shalikh bin Arfakhshad bin Sam bin Noah (amani iwe juu yake) , bin Lamik bin Mutwashlack bin Akhnukh [who was said to be Prophet Idris (Enoch) (amani iwe juu yake) bin Yarid bin Mahla’il bin Qabin Anusha bin Sh*th bin Adam (amani iwe juu yake)

Sufian Mzimbiri

03/01/2025

TUMEMALIZA HISTORIA YA MTUME ADAM MPAKA MTUME ISSA A.S TUTAMALIZIA MTUME MUHAMMAD(S.A.W)

03/01/2025


إِنَّ اللَّهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ۝٥٦

MAFUNZO YATOKANAYO NA HISTORIA YA NABII ISSA/YESU A.SKutokana na Historia ya Nabii Isa(a.s) tunajifunza yafuatayo:(i) Mt...
03/01/2025

MAFUNZO YATOKANAYO NA HISTORIA YA NABII ISSA/YESU A.S

Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a.s) tunajifunza yafuatayo:

(i) Mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ataitwa kwa ubini wa Baba yake na si vinginevyo na mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ataitwa kwa ubini wa Mama yake.

(ii) Waumini wanaharakati hawanabudi kumuomba Allah(s.w) awape watoto wema watakaofanya jitihada za makusudi za kuutawalisha Uislamu katika jamii.

(iii) Tuwalee na kuwaelimisha watoto elimu ya mwongozo na mazingira (elimu juu ya fani mbali mbali) si kwa kutaraji maslahi ya dunia bali kwa ajili ya kusimamisha ukhalifa katika ardhi.

(iv) Wanaharakati wanaposingiziwa au kupakaziwa maovu wasitengeneze majukwaa ya kujitetea na kujisafisha bali wash*takie kwa Allah(s.w) na kumuomba awasafishe na kuwatakasa hapa hapa duniani.

- Allah(s.w) anawaasa waumini wasijali matusi na fitina za wanafiki na makafiri, bali waendelee kutenda inavyostahiki.

Na sema (uwaambie): “Tendeni mambo (mazuri) Mwenyezi Mungu atayaona mambo yenu hayo na Mtume wake na Waislamu. Na mtarudishwa kwa Mjuzi wa siri na dhahiri; naye atakwambieni (yote) mliyokuwa mkiyatenda.” (9:105)

(v) Msingi wa mafundisho ya Uislamu ni Tawhiid. Yaani tunatakiwa tuufundishe Uislamu kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah na kwa lengo la kumuabudu Allah(s.w) katika kila kipengele cha maisha ya binafsi na jamii na kusimamisha Ukhalifa katika jamii – Hii ndio njia sahihi ya kufundisha Uislamu.

(vi) Ukitafakari vizuri utagundua kuwa maumbile yote ya Allah (s.w)yaliyotuzunguka pamoja na nafsi zetu ni miujiza.
Hivyo kuletewa muujiza maalumu, haitakuwa ni sababu ya kumfanya mtu amuamini Allah(s.w) ipasavyo k**a atashindwa kutafakari maumbile mbali mbali yaliyomzunguka.

(vii) K**a mbinu ya kulingania Uislamu katika jamii hatunabudi kuunda kundi la harakati litakalokuwa tayari kuufundisha Uislamu kwa usahihi wake, kuamrisha mema na kukataza maovu – Qur’an (3:104).

(viii) Nyakati zote wapinzani wakuu wa kusimama kwa Uislamu katika jamii ni washika dau (Al-Malaau) wa Dola za kitwaaghuut.

(ix) Tunapoamua kujiingiza kwenye harakati za kuhuisha na kusimamamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kujiegemeza (kutawakali) kwa Allah(s.w) na kuomba msaada wake na kutegemea ulinzi wake.

(x) Mwanaharakati muda wote anatakiwa awe tayari kukabili au kukabiliwa na misukosuko au kufa kwa ajili ya Allah(s.w),Mtume wake na kusimamisha Dini yake.

Sufian Mzimbiri

JE YESU NI MTOTO WA MUNGU?Mwenyezi Mungu si kiumbe. Yeye ndiye Muumba wa kila kitu kilicho na kisicho na uhai. Kuzaa ni ...
03/01/2025

JE YESU NI MTOTO WA MUNGU?

Mwenyezi Mungu si kiumbe. Yeye ndiye Muumba wa kila kitu kilicho na kisicho na uhai. Kuzaa ni sifa za viumbe vya Mwenyezi Mungu, hivyo Mungu si baba mzazi wa Yesu wala si baba wa mwanadamu yeyote. Qur,an tukufu inatuamrisha:

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu aliye mmoja (tu). Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuhitajiwa na viumbe. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Na wala hafanani na yeyote(112:1-4)

Ama katika Biblia, neno Baba limetumika kuonesha sifa ya ulezi wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake, hivyo, Mwenyezi Mungu kuitwa Baba haimaanishi kuwa kamzaa Yesu au binadamu yeyote miongoni mwetu. Na ndiyo maana akasema:

Wala msimwite mtu baba duniani, Maana Baba yenu ni mmoja aliye wa mbinguni, wala msiitwe viongozi;maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo(Mathayo 23:9-10)Na katika maandiko mengine ya Biblia, Yesu amenukuliwa akisema: Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni; Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, hapa duniani k**a mbinguni (Mathayo 6:9-10)

Kwa maana hii, Mwenyezi Mungu ni Baba wa watu wote, si baba wa Yesu tu. Ni Baba yetu, ila si kwamba katuzaa, bali ulezi wake wa kutujaalia riziki za kila aina na kutupatia elimu na teknolojia ya kuweza kuzitumia neema na riziki hizo. Hivyo Isa(a.s) si mwana wa Mungu wa kuzaa, bali ni kiumbe wake aliyemuumba kwa neno la ‘Kuwa’, likawa k**a alivyo muumba Adamu.

Bila shaka mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni k**a Adamu; alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia “Kuwa”, akawa.(3:59)

Sufian Mzimbiri

Address

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Dar Es Salaam
00100

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sufian Mzimbiri posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sufian Mzimbiri:

Videos

Share