Sports kitaa

Sports kitaa Sportskitaa.com: Football News, Live Scores, Results and Transfers

Sportskitaa.com is a purely up-to-date sports and entertainment website.
The East African based website, is professionally run by a seasoned East African sports fans and proudly using Swahili language.

SIMBA SC Yajibu mapigo baada yakuambiwa WALIPE MILLIONI 256/ Hiki ndicho walichoandika
04/01/2025

SIMBA SC Yajibu mapigo baada yakuambiwa WALIPE MILLIONI 256/ Hiki ndicho walichoandika

DIAMOND Achukizwa Na Shabiki Aliyemuita P-DIDY Aongea kwa Uchungu mbele ya MASHABIKI/ nimefanikiwa
04/01/2025

DIAMOND Achukizwa Na Shabiki Aliyemuita P-DIDY Aongea kwa Uchungu mbele ya MASHABIKI/ nimefanikiwa

04/01/2025

🗣️Zinchenko: "Siku moja, Pep alikosoa pasi yangu katika mazoezi. Nikasema: ‘Mr Nilikosa pasi moja tu, unajua?’ Na itikio lake lilikuwa la ajabu. "Oh, sawa, samahani, samahani, Bwana Zinchenko. Pole. Sawa, asante, kila mtu hapa ndani (mazoezini).’
"Mazoezi yalisitishwa kwa sababu nilimjibu. Nilijua niko kwenye matatizo.”
Zinchenko aliwekwa benchi katika mechi yake iliyofuata.
Follow Gazeti la Championi

04/01/2025

Emmanuel Okwi ametimiza miaka 32 juzi kwenye Krismasi.
Ukifanya rejea ndogo utaona Okwi alianza kucheza Ligi Kuu akiwa na miaka 16 na aliingia Bongo akiwa na miaka 17 pekee kucheza Simba SC!
Huenda ni kipaji cha ajabu miaka 16 uwe ligi Kuu! Maana yake hakupoteza sana muda kujisaka mtaani na kwa Sasa akiwa na miaka 32 huenda ndiye mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza ligi Kuu barani Afrika!
Baadhi ya timu alizopita ni pamoja na
2008–2009 SC Villa
2009–2013 Simba SC
2013 Étoile du Sahel
2013 SC Villa
2013–2014 Yanga SC
2014–2015 Simba
2015–2017 SønderjyskE
2017 SC Villa
2017–2019Simba SC
2019–2021 Al Ittihad
2021–2022 Kiyovu Sports
2022–2023 Al-Zawra’a
2023–2024 Erbil SC
2024– Kiyovu Sports
Sijui tunaelewana!? Kuna mchezaji mnaymkumbuka Afrika kacheza ligi Kuu akiwa na miaka 16!?

04/01/2025

BONDIA wa ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo amerusha jiwe kwa wadau wa ngumi kwa kusema kuwa kila anaposimamia maslahi makubwa kwa mabondia wanaonekana kunguru waoga kutaka hela nyingi.
-
Wakati huo huo, ametoa pole kwa familia ya bondia aliyepoteza maisha hivi karibuni akiwa ulingoni Hassan Mgaya akisema ni mara ya tatu wanazika watu kwa vifo vya aina hiyo.
-
Mwakinyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram, amesema “Leo kiasi cha malipo ya sh 60,000 ndio kimekatisha safari ya ndugu yetu…. na wengine wana pigania mpaka magari yaliyotumika. Huu ni ujinga tunapaswa kuwa mifano kwa maslahi ya wengi,”
“Binafsi mimi nasimama na promota wa hilo pambano ya kuwa yeye hana makosa amelipa mabondia kulingana na uwezo wake, wengi wakubwa hawathamini mabondia wadogo,”
-
Ametoa rai na kusema serikali ingetoa macho kupitia ngumi kuhakikisha kunapatikana wadhamini hata kwa mapambano madogo ya mitaani ili mabondia wadogo wanufaike.
“Hili liwe fundisho kwa mabondia wengine na sasa waachane na ngumi za mkali nani, ukifa haufi na unaowafurahisha unakufa peke yako,”alisema.
-
Mgaya alipoteza maisha Desemba 29 mwaka jana katika Hospitali ya Mwananyamala kufuatia kupigwa kwa TKO na mpinzani wake Paulo Elias katika pambano lililofanyika kwenye ukumbi wa Dunia ndogo uliopo Tandale kwa mtogole.
-
Imeandaliwa na Grace Mkojera

04/01/2025

“Hatuna wasiwasi…! Tutamfunga Yanga hapa hapa na mashabiki waje wakiwa wengi…! Tuna uwezo huo na huu ni mchezo mwingine ambao hatuhitaji kupoteza…! Tulisare nyumbani na hatukuwa na furaha…! Tutashinda hapa hapa Dar Es Salaam,” Lamine N’diaye, Kocha wa TP Mazembe kuelekea mchezo vs Yanga SC.
Ripota:

04/01/2025

Ni takribani miaka mitatu imepita tangu Ahmed Ally alipoanza kuitumikia klabu ya Wekundu wa msimbazi Simba k**a Msemaji.
Nini kinakuvutia zaidi kwa Semaji?
😂

04/01/2025

Ngono kati ya Mwanamke na roboti itakuwa ya kawaida zaidi kuliko Wanaume Mwaka Huu 2025. Ni kwa mujibu wa Utafiti Uliochapishwa Na Jarida la The Sun Mwaka 2016
Utafiti huo ulifanywa na Dr lan Pearson ambaye ni mtaalam wa masuala ya utabiri na mambo ya baadaye (futurologist) na alieleza kwamba kutokana na ongezeko la wanawake kutumia midoli kujistarehesha, basi mwaka huu 2025 kustarehe na roboti itakuwa sio jambo la kustaajabisha na kufikia mwaka 2050 binadamu watakuwa wakistarehe zaidi na mashine kuliko binadamu wenzao kutokana na kukua kwa teknolojia ya akili mnemba (Artificial Intelligence) na mashine.
Wanawake watakuwa wanawanyima wanaume wanapotaka kupata hali ya joto na wanaweza kuanza kuzipenda mashine hizo, Kwa Mujibu Wa Ripoti.
✍️: ( )

Aliyekuwa msaidizi wa Kanye West, Lauren Pisciotta, amewasilisha kesi mpya akidai kuwa alileweshwa kwa madawa na kufanyi...
13/10/2024

Aliyekuwa msaidizi wa Kanye West, Lauren Pisciotta, amewasilisha kesi mpya akidai kuwa alileweshwa kwa madawa na kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia alipokuwa kwenye studio na bosi wake wa zamani pamoja na Sean "Diddy" Combs.

Kulingana na malalamiko hayo, Pisciotta anadai kuwa aliwekewa dawa kwenye kinywaji chake ambacho alipewa katika kikao hicho kilichofanyika studio huko Santa Monica.

Kanye West, mwenye umri wa miaka 47, ndiye anayetuhumiwa kuagiza kinywaji hicho, ingawa Combs, 54, ambaye pia alihudhuria kikao hicho, hajatajwa kwa makosa yoyote.

Lauren Pisciotta anadai baada ya kunywa kinywaji hicho, alihisi kutojitambua vizuri na kushindwa kudhibiti mwili wake.

Siku iliyofuata, alijikuta akiwa na hali mbaya na aibu kubwa, lakini hakuwa na ufahamu kamili wa kilichotokea. Anasema aligundua baadaye kwamba aliweza kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia baada ya Kanye West kukiri kuwa walikuwa "wamefanya kitu" usiku huo.

Madai haya ni sehemu ya kesi iliyowasilishwa Juni 2024 ambapo Lauren Pisciotta anamtuhumu Kanye West kwa unyanyasaji wa kijinsia na kuachishwa kazi kinyume n utaratibu.

Wanasheria wa Ye wamekanusha madai hayo na kudai kuwa Pisciotta alikuwa anajaribu kumdharirisha Kanye baada ya kuachishwa kazi.

🚨 Luis Jose Miquissone toka ajiunge na UD Songo akitokea Simba Sc Amekuwa na kiwango bora sanaa kwenye ligi kuu ya Msumb...
13/10/2024

🚨 Luis Jose Miquissone toka ajiunge na UD Songo akitokea Simba Sc Amekuwa na kiwango bora sanaa kwenye ligi kuu ya Msumbiji 🇲🇿.

Takwimu zake ⤵️

🏟Mechi 6
⚽️Magoli 4
🏆Ameshinda tuzo 3 za Mchezaji bora wa Mechi

“Oktoba 19 Usije siku hiyo ukiwa mnyonge , ukija siku hiyo usiwe na mashaka wala usiwe na wasiwasi , safari hii tuna kik...
13/10/2024

“Oktoba 19 Usije siku hiyo ukiwa mnyonge , ukija siku hiyo usiwe na mashaka wala usiwe na wasiwasi , safari hii tuna kikosi bora sana, tuna kikosi kizuri sana na kwa mapenzi yake mungu tutaenda kutakata Oktoba 19 njoo kifua mbele mwana simba.”-Ahmed Ally

Unaambiwa Jamaa Mali Zake Zote Kawaandikisha Mama Yake Pamoja Na Watoto Wake Yeye Alichonacho Ni Mafuta Tu😀
13/10/2024

Unaambiwa Jamaa Mali Zake Zote Kawaandikisha Mama Yake Pamoja Na Watoto Wake Yeye Alichonacho Ni Mafuta Tu😀

09/10/2024

“Sio rahisi kuwa MVP kwenye Ligi ya Tanzania kwakuwa kuna Wachezaji wengi wazuri k**a Stephen Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Feisal Salum ila nitapambana”

- Jean Charles Ahoua, Mchezaji wa SIMBA SC.

Saboso Gin Jr.

Trent ni Liverpool na Liverpool ni Trent.Hizo zingine ni kelele tu 😂 no way ataondoka Anfield huyu kijana
07/10/2024

Trent ni Liverpool na Liverpool ni Trent.

Hizo zingine ni kelele tu 😂 no way ataondoka Anfield huyu kijana

Jude Bellingham amemfanyia Surprise rafiki yake kipenzi Trent Alexander-Anord katika siku yake ya kuzaliwa kwa kumuandal...
07/10/2024

Jude Bellingham amemfanyia Surprise rafiki yake kipenzi Trent Alexander-Anord katika siku yake ya kuzaliwa kwa kumuandalia picha hiyo.

FOLLOW US.

07/10/2024

Shabiki wa Yanga Sc, Mzee Amir Hussein anaamini timu ya Wananchi itafika hatua ya fainali bila tabu, Mzee Amir amasema kwamba "Yanga tupo vizuri na hatuogopi timu yeyote katika kundi"

Yanga amepangwa katika kundi A, ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kundi linalo jumuisha Tp Mazembe, Al Hilal na MC Alger.
Je, ni kweli Simba imepangiwa timu dhaifu?

Saboso Gin Jr.

07/10/2024

Mama mzazi wa , Janice Combs amevunja ukimya matatizo yanayomkabili mtoto wake akisema hana hatia sababu Diddy hajafikia hatua ya kufanya unyama huo kwa watu wanaomtuhumu.

Mama Diddy amemtetea mwanae kupitia barua ya wazi inayoeleza yanayoendelea kwa Diddy ni uongo na uchochezi kwa wanaotaka faida ya fedha.

"Mwanangu sio mnyama wanamchoresha kuwa hivyo, ni mzaha na kucheka maisha ya mwanangu yakiporomoka mbele ya macho yetu ni jambo ambalo siwezi kusahau kamwe".

"Inasikitisha kuona ulimwengu ukigeuka dhidi ya mwanangu juu ya uwongo na maoni potofu bila kusikia upande wake. Uongo huu unaotupwa huchochewa na wale wanaotafuta faida ya kifedha na sio haki" - Maeleozo ya Mama Diddy

Mpaka sasa Diddy anatuhumiwa makosa 120 ya madai ya unyanyasaji wa kingono.

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sports kitaa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sports kitaa:

Videos

Share

Category