02/05/2024
KUOMBA ROHO MTAKATIFU AKUPE MSAADA WAKE HALISI
:yoh 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
:yoh 16:8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu
:matendo 7:54-59
54 Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno.
55 Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu.
56 Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
57 Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja,
58 wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli.
59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.
:luka 2:25-34
25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie k**a ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, k**a ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
33 Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake.
34 Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
:matendo 3:1-9
1 Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.
2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.
3 Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.
4 Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.
5 Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.
6 Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
7 Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
8 Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.
9 Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.
kutana na Yesu ndio mwenye majibu yako,
ishara zitakazo kusaidia kutambua ujapata msaada halisi.
1.kitu kipo pale pale
2.unaendelea kuona jambo lipo palepale.
3.unaweza kupata lkn ukageuka kiroho
zab106:15 aliwapa walichokipata akawakondesha roho zao.
yoh 1:4-5,9-10
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza .
9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
mbinu za shetani ili tusipate msaada halisi
1,kutompokea Yesu na vitu alivyo navyo.
2, kutambua uumbaji na uwepo wake.
3,Adui anafanya tusitafute mashauri ya Bwana
yoh11:4
yoh12:43
4, shetani anatuua,haupitishi vya Mungu katika maisha
yoh15:5
5,kuwaza au kuonesha kuna mambo yanaweza kwenda bila Yesu, mf;elimu.
matendo 7:20-23
wae11:24
6,roho zingine hukaa ndani yetu,ya wengine au mazingira yanayokuzunguka.
matendo 13
kuomba vile anavyotaka Mungu ktk maisha yako,
shida ni vifundo.