19/12/2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufuatia Uteuzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wake Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Samuli kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
Aidha katika hatua hiyo Rais Samia amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.