06/01/2026
HISTORIA YA DR JOHN THORBURN WILLIAMSON NA MGODI WAKE WA ALMASI MWADUI 3.
Aliamua kuuita mgodi wake jina la Mwadui jina la mtemi aliyemkaribisha, alikuwa anaitwa Ng'wadubhi. Jina la Ng'wadubhi lilimshinda kulitamka ndipo akaita
Mwadui.
Alipoona amekusanya almasi za kutosha ndipo. alipoenda kuuza kwenye soko la dunia na kuja
na mitambo ya kisasa. Alifanya utafiti na kugundua kuwa Mwadui ilikuwa na mkandawa "kimberlite "wenye hifadhi nyingi ya almasi. Ikiwa na ukubwa wa hakari 146, mkanda huu ni wa pili kwa ukubwa Duniani baada ya ule wa Mgodi wa Camafuca uliopo Angola.
Dr. Williamson mwaka 1946 alie kuchumbia katika familia ya kifalme huko Wingereza akitaka kumuoa Princess Margaret, akaambiwa huwezi kuoa kwenye familia yetu wewe ni masikini. Akajaribu kuwashawishi kuwa yeye ni tajiri anamilili mgodi wa almasi huko Tanganyika lakini akatoswa.
Alitoa zawadi ya Almasi yenye rangi ya PINK yenye uzito wa kareti 54.5 kwenye harusi ya Princess Elizabeth na Prince Philip mwaka 1947. Unaambiwa almasi hiyo ipo mpaka leo kwenye jumba la kifalme la Uingereza imewekwa pambo kwenye kofia ya Malkia, ilishachongwa ikabaki kareti 23.6. Mwaka1948 akafunga mkataba na serikali ya kikoloni ya Waingereza wa miaka 100 ( yaani 1948-2048. )
MAISHA NDANI YA MJI WA MWADUI.
Dr. Williamson akautengeneza mji mdogo wa Mwadui na kuwa moja kati ya miji bora sana kusini mwa jangwa la Sahara (MwaduiTownship). Kufikia mwaka 1947, Dr Williamson alikuwa amejenga nyumba bora za wafanyakazi, hospital ya kisasa, shule za msingi tatu, mbili za wafanyakazi wa kiafrika na moja ya wafanyakazi wa kizungu ambayo ndio ilikuwa moja ya "English Medium School" ya kwanza Tanganyika. Akajenga chuo cha Ufundi wa aina zote ndani ya mgodi kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi, chuo cha
kilimo na shule ya upili.
Huko kwao waliita "School Near The Equator". Ilikuwa shule bora na ya kisasa. Dr Williamson akajenga uwanja wa ndege wa kisasa ndani ya mgodi mwaka 1948 akanunua ndege mbili za mwanzo aina ya Dakota DC3 na Cessna 180 wakati huo hata serikali ya Kikoloni ya Muingereza ikiwa haina wazo la ndege, wakati serikali ya Tanganyika ikiwa haina uhakika wa
uwanja wandege kupokea ndege kubwa aina ya Dakota DC4.
Dr Williamson alikuwa tayari na uwanja huo, ambapo wageni toka London Uingereza, ndege zilitua Malta, Khartoum-Sudani na baadae Nairobi (Wakati huo ukiitwa Embakasi Airport) na baadae kuchukuliwa na ndege moja kwa. moja mpaka Mwadui Shinyanga, ambapo Serikali ya Kikolonii likuwa na afisa mmoja wa uhamiaji. Dr Williamson alijenga kanisa na msikiti bora na wakisasa kwa ajili ya wafanyakazi
wake.
Wakatihuo, usafiri pekee wa watumishi wa serikali ya Kikoloni ilikuwa ni meli maarufu ya"The Braimer Castro" iliyokuwa inatoka Ulaya mpaka Mombasa. Yeye Dr Williamson na wafanyakazialioajili walikuwa wanapanda ndege kupitia Embakasi na baadae Mwadui. Williamson akajenga "Power House" yenye uwezo wa kuzalisha 900kw kwa mitambo ya diesel
na 750kw kwa Gas Turbine na hivyo kuwa na umeme wa uhakika kuliko hata mji wa Dar Es Salaam.
Dr Williamson alijenga "SailingClub", yaani Club inayoning'inia katika bwawa alilichimba eneo la Songwa. Hii ndio ilikuwa Club pekee inayoning'inia Kusini mwa Jangwa la Sahara. May 2 mwaka 1955, Gazeti Kongwela "The Cairns Post" (Est.1882) liliandika juu ya uwepo wa bwawa la Songwa, Mwadui-Shinyanga, Tanganyika. Gazeti hilo la Australia lilielezea bwawa la Songwa k**a moja kati ya "Artificial dam" kubwa zaidi duniani, lenye uwezo wa kuchukua "two thousands million gallons of water". Mradi ambao hata serikali ya mkoloni iliushangaa.
Notes;
Hiyo picha ni Dr. Williamson akiwa na Kijana Bundala wakiwa katika harakati za kuitafuta almasi.
ITAENDELEA
Credit: Njile Nkuba Sitta