East Africa Radio

East Africa Radio Official EastAfricaRadio page. Listen live @ www.eastafricaradio.com

  Sheikh Maulid Hussein Sombi, Kiongozi wa Jamii ya Waislamu wa Kishia mkoa wa Arusha, amepongeza juhudi za Serikali na ...
11/01/2025

Sheikh Maulid Hussein Sombi, Kiongozi wa Jamii ya Waislamu wa Kishia mkoa wa Arusha, amepongeza juhudi za Serikali na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza Jumamosi, Januari 11, 2025, katika hafla maalumu ya uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia kwa viongozi wa dini ya Kiislam jijini Arusha, Sheikh Maulid amewasihi wadau kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati hiyo.

Amesema matumizi ya majiko ya gesi na nishati ya umeme ni hatua muhimu kwa jamii, hasa kuelekea Mwezi Mtukufu wa Shaaban na Ramadhan. “Mwezi wa funga unakaribia, tunahitaji futari zipikwe kwa wakati na mapochopocho yawe mengi kwa ajili ya waumini,” amesema Sheikh Maulid huku akitoa wito kwa TANESCO na wadau wengine waongeze jitihada za kutoa elimu kuhusu teknolojia hizo mpya.

Aidha, Sheikh Maulid ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuhamasisha maendeleo ya jamii.

“Tunamuombea Dua mama Samia Suluhu Hassan, Mungu amjalie hekima na busara ili aendelee kutuongoza kwa wema na busara,” amesema.

Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) chini ya uratibu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi za dini, na wadau wa nishati safi nchini.

  Afisa Nishati Mkuu kutoka Wizara ya Nishati, M***a Abbas, ameweka wazi athari kubwa za matumizi ya nishati isiyo safi ...
11/01/2025

Afisa Nishati Mkuu kutoka Wizara ya Nishati, M***a Abbas, ameweka wazi athari kubwa za matumizi ya nishati isiyo safi kwa Watanzania na dunia kwa ujumla, huku akisisitiza umuhimu wa elimu na rasilimali ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Takribani 82% ya Watanzania hutegemea tungamo taka k**a kuni na mkaa kwa kupikia, hali inayochangia madhara makubwa ya kiafya, kimazingira, na kijamii.

M***a ameyasema hayo siku ya Jumamosi, Januari 11, 2025 katika Hafla Maalumu ya Uhamasishaji na Kutoa Elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Viongozi wa Dini ya Kiislam Jijini Arusha inayofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Januari 11, 2025, chini ya uratibu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

Ameeleza kuwa watu takriban bilioni 2. 3 duniani bado hawajafanikiwa kutumia nishati safi ya kupikia huku chini Jangwa la Sahara kwa Afrika wakiwa watu milioni 990.

"Takribani watu milioni 3 dunia nzima huwa wanafariki kwa magonjwa ya hewa ambayo yanatokana na matumizi ya nishati isiyo safi, vilevile katika watu hao milioni 3, takribani 60% huwa ni wanawake na watoto, na kwa Afrika pekee takribani watu laki 4 mpaka 7 hufariki kutokana na madhara yanayosababishwa na nishati isiyo safi, na kwa Tanzania takribani watu elfu thelathini na tatu (33000) hufariki kila mwaka kutokana na matatizo hayo", ameeleza Musa.

Ameeleza kuwa Wizara ya Nishati ina Sera ya Nishati ya mwaka 2015 ambayo imeweka bayana kwamba Tanzania inatakiwa kutoka kwenye matumizi ya kuni na mkaa kwenda kwenye matumizi ya kisasa ya kutumia nishati safi. Aidha ameeleza kuwa sera hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuwezesha utekelezaji wa matumizi ya nishati safi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa serikali za mitaa jijini Arusha, Wajumbe wa Jumuiya ya Maridhiano, viongozi kutoka Wizara ya Nishati, watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Masheikh kutoka taasisi mbalimbali za dini ya Kiislamu na wadau mbalimbali wa nishati safi nchini.

  Watanzania wengi wamekuwa wakihofia kutumia umeme k**a nishati ya kupikia kwa kudhani kuwa gharama zake ni kubwa. Hata...
11/01/2025

Watanzania wengi wamekuwa wakihofia kutumia umeme k**a nishati ya kupikia kwa kudhani kuwa gharama zake ni kubwa. Hata hivyo, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza kuwa umeme si tu nishati rahisi na salama bali pia ni suluhisho endelevu kwa changamoto za kupikia nchini.

Hayo yameelezwa na Carol Makundi, Afisa Mwandamizi wa TANESCO siku ya Jumamosi, Januari 11, 2025 katika Hafla Maalumu ya Uhamasishaji na Kutoa Elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Viongozi wa Dini ya Kiislam Jijini Arusha inayofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Januari 11, 2025, chini ya uratibu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

Makundi, amesema matumizi ya umeme katika kupikia yanaweza kusaidia kupunguza gharama za maisha, kulinda mazingira, na kuboresha afya za wananchi.

Makundi ametoa mfano wa gharama zinazotumika kupika nusu kilo ya maharage kwa nishati tofauti, akibainisha kuwa matumizi ya umeme yanaweza kushusha gharama hiyo hadi Tsh 200 pekee, ikilinganishwa na Tsh 1,200 kwa mkaa, Tsh 800 kwa LPG, na Tsh 600 kwa mafuta ya taa.

Amesema kuwa kupikia kwa umeme si tu nafuu bali pia kuna mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uzalishaji wa kaboni na kuimarisha ustawi wa jamii kwa ujumla.

Katika hafla hiyo, TANESCO imeeleza mikakati yake ya kukuza matumizi ya nishati safi nchini, ikiwemo kutoa elimu kwa watumiaji wa kawaida, viongozi wa dini, na wadau wengine kuhusu faida za kupikia kwa umeme. Shirika hilo limekuwa likifanya tafiti kubaini vifaa bora vya kupikia vinavyotumia umeme kidogo ili kupunguza gharama za awali kwa watumiaji, huku likishirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati katika kusukuma mbele ajenda ya nishati safi.

Hafla hiyo, iliyoandaliwa chini ya uratibu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, imehudhuriwa na viongozi wa serikali za mitaa, Masheikh kutoka taasisi mbalimbali za Kiislamu, na wadau wa nishati safi.

11/01/2025

Kwa Mujibu wa Mchungaji Niva Mbaga anasema SIMBA inapewa nafasi ya kushinda kombe la Shirikisho CAFCC.

Unamuona Mnyama akibeba kombe hilo?

Hii ni ya na muda huu.

11/01/2025

🗣UCHAMBUZI WA MECHI YA BRAVOS VS SIMBA.

Hii ni ya na muda huu.

11/01/2025

MSIMAMO WA MCHUNGAJI WA SIMBA NIVA MBAGA MCHEZO WA AL HILAL VS YANGA.

Isikilize ya na muda huu.

11/01/2025

KOCHA IBENGE ASHIKILIA HATMA YA YANGA ROBO FAINALI👇

Shabiki wa Yanga SC Jof Master akizungumzia mchezo wao na Al Hilal ya Sudan.

Address

Mikocheni Light Industrial Area
Dar Es Salaam
0255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when East Africa Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to East Africa Radio:

Videos

Share