01/01/2025
Mbwembwe za “Chifu” Godlove.
Chifu Godlove Mwakibete wa Mbeya ame “trendi” kwa spidi ya kutisha katika mitandao ya kijamii. K**a kijana mwenye umri mdogo kumiliki mimali yenye thamani kubwa hasa “ndinga” kali, huku akifurahia kupiga nazo picha. Sambamba na kuonekana ameyakumbatia mabulungutu ya “misimbazi” pesa, hivyo kujiita “tajiri”, anaye kula bata hadi kuku wanamuonea wivu hapa mjini.
Katika kula bata kwa Huyu mwamba “chifu” Godlove Mwakibete, yeye “mademu” si sehemu ya starehe anazo zikubali. Tofauti na “matajiri” wengi tunao wajua au au kuwasikia. Kwa lugha rahisi kabisa, ni kwamba mwamba hajihusishi kabisa na maswala ya “ngono” au “kwichikwichi” isipokuwa kujichukulia sheria mkononi. Pisi kali zote za mjini yeye anawaona k**a dada zake tu, yaani hawamshughulishi kwa lolote.
Katika Siku za hivi karibuni ameonekana sana katika mitandao ya kijamii aki“hang” na mtoto wa kiume aitwaye Greyson Kenyenye (6). Huyu ni mtoto aliyekuwa akiishi na mama yake tu anayesemekana ni mfanyabiashara maarufu mjini Dodoma, Bi. Zainab Shaban - al maarufu “Jojo.”
Na kwa taarifa zisizo rasmi ni k**a “chifu” alimuasili huyu kijana Greyson. Hivyo mara kadhaa alikuwa akimtambulisha k**a mwanaye mbele ya jamii na watu wake wa karibu. Uhusiano wa Baba na mtoto baina yao ulishamiri na kustawi sana.
Mama wa Greyson, Bi. Zainab a.k.a Jojo ana mahusiano na Bw. Hamis Mpete wa Ilazo Extension jijini Dodoma ambaye ni Afisa Uvuvi katika Bwawa la Mtera. Usiku wa mkesha wa Krismas kuamkia Desemba 25, 2024, walikuwa wote Pamoja na mtoto Greyson Nyumbani kwa huyo Bw. Hamisi.
Ilipo timia saa 6.00 za usiku, Zainab na Hamis walikubaliana kutoka na Kwenda kufanya “anasa” katika moja ya kumbi za starehe mjini Dodoma. Hivyo walikubaliana kumuomba rakifi yao wa karibu aliyejulikana kwa jina la Kelvin Gilbert. Anaye jishughulisha na kazi ya “Bodaboda” kuja hapo nyumbani kwa Bw. Hamis kukaa na mtoto Greyson mpaka wapenzi hao watakapo rudi.
Msh*tuko Mkubwa.
Wapenzi hao wakiwa katika “hang-over” ya balaa za mkesha walirudi nyumbani Asubuhi, na kukuta Greyson amefariki akiwa peke yake nyumbani.
K**anda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 25, 2024. saa 1:00 asubuhi ambapo Bwana Hamis Mpeta akiwa na mama wa mtoto, Zainab, walibaini kuuawa kwa mtoto huyo.
“Walimkuta mtoto huyo akiwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na shingoni, amekatwa na kitu chenye ncha kali. Katika tukio hilo, mama wa mtoto alimwacha mtoto huyo na dereva wa Bodaboda anayejulikana kwa jina la Kelvin Gilbert. Nyumbani kwa Bwana ake, Hamis Mpeta,” amesema.
Amesema walimuacha mtoto huyo kwa dereva bodaboda saa 6:00 usiku, nyumbani kwa Hamis Mpeta (rafiki wa Zainab) na kwenda matembezini. Hata hivyo, K**anda Katabazi amesema waliporudi saa 1:00 asubuhi, Desemba 25, 2024, walikuta mtoto ameuawa na Kelvin hakuwepo nyumbani.
K**anda Katabazi alisema Kelvin alikuja kujitokeza baadaye na kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo. Kwa sababu aliachiwa mtoto huyo amwangalie ili asiweze kudhurika.
Alipoulizwa ni nani alitoa taarifa ya kuuawa kwa mtoto huyo, K**anda Katabazi amesema mara baada ya kukuta mtoto ameuawa. Mpeta na Zainab waliwasiliana na polisi ambao walifika katika eneo hilo kwa wakati.
“Lakini kipindi hicho, huyu Kelvin hakuwepo na alikuja kujitokeza baadaye na ndipo tulipomshikilia kwa ajili ya mahojiano zaidi. Kwa hiyo, tunao watuhumiwa wawili tunaowashikilia akiwemo mtuhumiwa mwingine,” amesema.
Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, jana, Dk. Makaranga amesema taarifa za tukio hilo ziko chini ya Jeshi la Polisi. Na familia wamelipokea tukio hilo k**a lilivyo k**a jamii nyingine inavyosikia.
“Ni kweli ameuawa kwa kushambuliwa lakini majibu mengi ambayo sisi hatuna yako kwa Jeshi la Polisi. Kwa taarifa za awali nilizozipokea kutoka kwa dada yangu (Zainab) kuwa mtoto wake amefariki. Baada ya dada yangu kuamka asubuhi na kupewa taarifa hizo,” amesema Dk Makaranga.
“Sisi k**a ndugu, kwa kweli ni masikitiko makubwa kwa sababu ni kitendo cha kinyama na kikatili ambacho amefanyiwa mjomba wetu. Na taratibu za nchi yetu zipo na zinaeleweka. Tunaliomba Jeshi la Polisi liendelee kufuatilia kwa haraka tupate angalau kujua nini kilimtokea (Greyson),” amesema.
Dk. Makaranga ameliomba Jeshi la Polisi lihakikishe haki ya mjomba wake aliyeuawa kikatili inapatikana na kuonekana ikitendeka.
Azikwa Dodoma
Dk. Makaranga amesema mtoto huyo amezikwa leo katika makaburi ya Kilimo Kwanza jijini Dodoma na kuhudhuliwa na chifu Godlove. Katika ibada iliyofanyika nyumbani, amesema mtoto huyo atakumbukwa kwa kipaji chake cha kuimba kwaya na tabia ya ucha Mungu.
Amesema merehemu alikuwa akisali katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Area “D” jijini Dodoma.
“Greyson atakumbukwa kwa upendo na ucheshi aliokuwa nao kwa watoto wenzake. Greyson alifariki dunia Desemba 25, 2024 kwa kuchinjwa na kupigwa na kitu kizito kichwani mpaka kuuliwa,” amesema.
“Tunatumai kuwa mwisho wa mwaka familia zote huwa zinajumuika kwa Pamoja. Tujitahidi kuwa waangalifu, kuwadhibiti watoto wetu pamoja na watu wenye mahitaji maalumu,” amesema.
Mchungaji wa Kanisa TAG la Area D. Rehema Pangasi, amesema mtoto huyo alikuwa ni mshirika wa kanisa hilo na alikuwa mwimbaji wa kwaya ya Shekina. Na kwamba alikuwa akifika kila Jumamosi kanisani kwa ajili ya mazoezi.
“Hata Jumamosi hii (Desemba 20, 2024) alikuwa kanisani kwa ajili ya mazoezi ya kwaya. Jumapili alikuwa kanisani anaimba, nilimchukua video kidogo wakati anaimba. Hata sikujua kwanini niliichukua, Mungu anajua yote,” amesema Rehema.
Amesema Jumamosi iliyopita, alivyokwenda katika mazoezi ya kwaya, alimuuliza iwapo amrudishe nyumbani kwao. Lakini alikataa kwa kuwa mama yake alimweleza kuwa atamtumia bodaboda imfuate.
Amewataka watu kumgeukia Mungu kwa kuwa wakiwa na hofu yake, hawatafanya vitendo vya ukatili k**a walivyofanya kwa mtoto huyo.
Amesema wakati wanasherekea sikukuu ya Krismasi kanisani, walimtafuta mtoto lakini hakuwepo na walikuja kupata taarifa baadaye kuwa ameuawa.
Licha ya kwamba hadi sasa haijawekwa wazi baba mzazi wa mtoto huyo ni nani, mwanamitandao, chifu Godlove Mwakibete wa Mbeya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amejitokeza na kueleza yeye ndiye baba wa hiari wa Greyson.
Kupitia ujumbe wake aliombatanisha na picha akiwa na mtoto huyo. Chifu Godlove ameonesha kusikitishwa na kitendo kilichotokea kwa mtoto huyo na kueleza anaacha sheria ichukue mkondo wake.
“Nilikuwa bado siamini k**a binadamu wamegeuka wanyama kiasi cha kupoteza uhai wa mtoto asiye na hatia wala ugomvi na mtu”.
“Limeniumiza na sitoweza kulibeba kwa yeyote aliyehusika hatokuja kuishi kwa amani kwenye hii dunia na ahera. Najua wewe ni malaika huna hata chembe ya ugomvi wala hasira. Tunaicha sheria ichukue mkondo wake wote waliohusika wak**atwe,” ameandika.
Hata hivyo, rafiki wa karibu wa mama yake Greyson. Amesema marehemu alizoeana sana na chifu Godlove Mwakibete na kumuomba kuwa baba yake wa hiari.
www.snapstz.com