Kile wanamaanisha wanaposema....
Adui unayemmudu, usimuachie Mungu. Dili naye
Nilisema kwamba CAF kuna kitu wanakiona kwa soka letu na kuna kitu WANAKIFANYA kwenye soka letu. Kuna wengi mlielewa. Na kuna wengi mlijitahidi kutoelewa. Pengine mkiangakia mambo kama haya, mnaweza kuanza kutumia vichwa vyenu vizuri na mkaelewa.
Sema mimi haikunipa shida maana kuna nyakati najua kuwa #UsipoelewaNdioUmeelewa
Nilipoandika kuwa kuna kitu CAF wanakiona kwa soka la Tanzania na kuna kitu wanafanya katika soka la Tanzania, kuna watu naamini walijitahidi sana kutokuelewa. Nadhani kwa matukio kama haya, baadhi huenda wakirudia ile post wataanza kuelewa.
#UsipoelewaNdioUmeelewa
MGONGANO WA MASLAHI KATI YA DEREVA NA MWAJIRI WAKE (TAJIRI): UTATA MTUPU
*TAJIRI*: Nataka usichelewesha abiria njiani bila sababu za msingi. Usilale lale barabarani. Hakikisha pia unazingatia usalama sitaki hasara.
*DEREVA*: Posho sh. Ngapi?
*TAJIRI*: Mie nalipa 40,000 kwenda, 40, 000 kurudi. Mchana utakula hotelini.
*DEREVA*: Sawa bosi. Wala usijali gari itakaa mbele. Saidia kunisafishia njia tu
*TAJIRI*: Sawa hakuna tatizo. Au aisee hilo mie sihusiki jiongeze mwenyewe. Posho yako utaikuta kwa Agent.
Hadi hapo dereva hajaulizia mkataba bado.
Anaenda safari, baada ya mwezi hivi:
*DEREVA*: Maslahi madogo sana, tochi nyingi barabarani, mkataba wenyewe hakuna . Huyu tajiri ananinyonya sana. Hebu serikali iingilie kati.
*ZINGATIA*: Licha ya kusema haya maneno, hamchukii mwajiri wake bali anaichukia serikali. Akikutana na mwajiri wake dereva ni mnyenyekevu kweli kweli. Na kila siku anahakikisha anakaa mbele. Yupo tayari kumchomekea dereva mwenzake ikiwemo kumsababishia ajali kwa faida ya mwajiri.
*MASHABIKI STENDI:*. Miluzi mingii, na chereko. Nakuona nakuona kidume kiboko yao, baba lao. Leo naona umeikata basi XYZ dah jamaa hata hawaamini aisee. Wee jamaa huna huruma kabisa. Umewaacha wenzio saa nzima?
*DEREVA:* Anatabasamu na bashasha tele. Bichwa hilo.
Ghafla amekuwa maarufu kwenye hiyo njia, hadi abiria wanauliza leo suka ni nani? Kapiteni mwenyewe maridaaadi.
Kesho tena anaamsha anaenda safari anarudi. Licha ya kuwa ana malalamiko lakini anamfanyia bosi wake kazi vizuri sana. Yupo tayari kupigana na yeyote ili mradi tu kalinda maslahi ya bosi wake. Hataki bosi wake asemwe.
*AJALI*: Baada ya muda, bahati mbaya anapata ajali, gari inaharibika. Tajiri anaenda Polisi anamaliza taraibu za ukaguzi wa gari analipeleka gereji, anampa dereva mwingine. Huyu dereva wa awali anaugulia maumivu hospitali au yupo benchi tu.
*DEREVA:* Dah! Matajiri hawana utu kabisa. Yaani mie nimemzalishia kweli kweli. Siku zote naweka gari mbele kama tai, leo hii yeye wa kuniacha m
Siku chache tu baada ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majakiwa kulitangazia taifa kuwa ni ruksa mabasi kufanya safari masaa 24, madereva wetu wameanza kutuonjesha namna gani mambo yatakuwa huko barabarani. Angalia kwa makini hiyo video, jiulize ingekuwa usiku, nq huyo dereva wa lory awe haoni vyema ukingo wa barabara na akaamua akae site yake, nini kngetokea?