Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amepongeza ushirikiano wa mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na wadau wa haki za binadamu kwa kupaza sauti ya pamoja kupinga tukio la utekaji wa mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu hapa nchini, Maria Sarungi ambaye amepatikana akiwa salama ikiwa ni saa kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo.
"Tunashukuru wenzetu wa Kenya Coalition Nairobi na wenzetu wa Kenya Law Society pamoja na Amnesty International, kwa ujumla ni kwamba tayari Mwanaharakati Maria Sarungi amepatikana na yupo salama nyumbani. Na taarifa za awali zinaonyesha kwamba alichukuliwa na watu waliokuwa na gari aina mbili, ambapo moja wapo ni Probox nyeupe na nyingine ni Noah walikuwa wkimfuatilia akiwa katika shughuli zake na aliyeshuhudia ni dereva wa Uber ambaye alikwenda kituo cha polisi, kwa ushirikiano na chama cha mawakili nchini Kenya kwenda kutoa taarifa kwenye vituo vya polisi jijini Nairobi." Amesema Olengurumwa
Hapo awali Olengurumwa aliandika kupitia ukurasa wa kuwa mtandao wa watetezi unafuatilia kwa ukaribu ili kupata taarifa zaidi juu ya utekwaji wa Mwanaharakati Maria Sarungi, aliyetekwa leo Januari 12,2024 majira ya alasiri, jijini Nairobi, nchini Kenya.
Mwanaharakati na Mtetezi wa haki za binadamu hapa Nchini, Maria Sarungi, amepatikana akiwa salama baada ya tukio la utekaji lililotokea Leo majira ya saa tisa na robo alasiri katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza kupitia video, Maria amewashukuru wote walioshiriki kupaza sauti kuhusu tukio hilo ambapo amesema kesho atazungumza kwa Uzuri kuonyesha shukrani zake.
Taarifa za tukio hilo la utekaji zilisambaa mitandaoni baada ya shirika la Amnesty international kutoa taarifa kuwa Mwanaharakati huyo ametekwa na watu watatu wenye silaha wkiwa kwenye gari aina ya Noah Nyeusi.
"Tumekuwa na wapambe wa wagombea ambao wamekosa nidhamu kwa chama (CHADEMA) na wagombea ambao hawawaungi mkono, sasa kwa mujibu wa mwongozo wa taratibu za kuendesha uchaguzi ndani ya chama toleo la mwaka 2012 kifungu cha 2 (3) kinasema 'itakuwa ni marufuku kwa mgombea ama wapambe wake kusambaza taarifa zenye lengo la kukashifu mgombea au kiongozi wa chama'. Sasa pamoja na zuio hilo, tumeshuhudia uwepo wa maneno makali, ya kashfa, matusi ambayo yamekuwa yakitolewa kwa pande zote ambazo zinashiriki katika huu uchaguzi, na isivyo bahati ni kwamba yapo maneno ambayo mengine hayana staha yametumika kwa viongozi wetu na hapa sizungumzii upande mmoja"
Mwanaharakati wa haki za kijamii na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godlisten Malisa akizungumza katika mkutano na wanahabari uliofanyika mkoani Dar es Salaam leo Januari 12, 2025.
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemnyima dhamana Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Dkt. Wilbroad Silaa na kwa kile kinachoelezwa kuwa ni hofu juu ya usalama wake.
Akizungumza baada ya kutoka mahakamani hapo Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Wakili Boniface Mwabukusi amesema kuwa makosa yaliyofanya Dkt. Slaa kukamatwa ni kutoa taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii "alizungumza kwenye mtandao wa X akieleza kuna mawasiliano kati ya Rais(Dkt. Samia Suluhu Hassan) na Mbowe na mawasiliano hayo ni ya kupeana msaada wa kifedha kwa hiyo Jamhuri inasema makosa hayo ni ya uongo na kinyume na kifungu cha 16 cha sheria cha makosa ya mtandao"
Mwabukusi ameeleza kuwa baada ya walipofika mahakamani walikuta Jamhuri imewasilisha kiapo cha kupinga Dkt. Silaa asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake lakini mawakili wa upande wa utetezi hawakuwa wamepewa kiapo hicho hivyo kuhitaji muda wa kukifanyia kiapo ili kuandaa kiapo kinzani.
Dkt. Slaa alikamatwa usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2025.
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini (PDPC) imetoa onyo kali kwa taasisi binafsi na za umma ambazo bado hazijajisajili, licha ya agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa tume hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Mkilia, amesema agizo hilo lilikuwa ni kuhakikisha taasisi zote za umma na binafsi zinasajiliwa kabla ya Desemba 31, 2024.
Dkt. Mkilia amesisitiza kuwa kutokuzingatia matakwa hayo kunahatarisha juhudi za Serikali katika kusimamia usalama wa taarifa binafsi za wananchi.
Aidha, amesema tume imebaini idadi kubwa ya taasisi ambazo hazijaanza kabisa zoezi la kujisajili, huku taasisi chache zikiwa bado hazijakamilisha usajili.
Hata hivyo, tume hiyo imetangaza kuongeza muda wa mwisho wa usajili hadi tarehe 30 Aprili mwaka huu. Taasisi zitakazo shindwa kujisajili ndani ya muda huo zitachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Tunaona watu ambao walishaondoka CHADEMA huko miaka ya nyuma kama akina Dkt Wilbroad Slaa ambao walikimbia CHADEMA wakaenda Chama cha Mapinduzi wakapewa na zawadi ya ubalozi, eti leo naye amekuwa ndiye mpiga debe mkubwa wa Makamu Mwenyekiti wangu kutaka awepe Mwenyekiti wa chama na kubeza na kutweza watu na wengine wa vyama vingine vya upinzani"-
Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA na mgombea wa nafasi hiyo 2025, akizungumza kupitia Clouds Tv.
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt Tulia Ackson amejitokea kumsomesha mpaka ukomo mtoto Yohana Japhet mweye umri wa miaka 14, mwanafuzi wa darasa la saba shule ya Msingi Nsongwe, kata ya Ilomba Jiji mbeya, baada ya kumkuta akiponda mawe ili kuweza kupata mahitaji yake huku akiishi katika mazingira magumu.
Yohana anayeishi na Bibi yake Mlezi Katika Kata ya Ilomba ,Mtaa wa Ituha Mbeya Mjini, anasoma Darasa la Saba kweye shule ya msingi Msogwi hapo awali alikuwa akifanya Kazi ya Kuponda Kokoto Ili apate Fedha Kwaajili ya kununua Mahitaji Mbalimbali ya Shule na Chakula kwa ajili ya familia licha ya kuishi na bibi yake mlezi anayefaya shughuli za kilimo.
Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini CCM amemtembelea Kijana huyo na Kuahidi Kumsomesha hadi atakapofikia ukomo wa Masomo huku akimsaidia Bibi yake Chakula (Mchele Kilo 40) na Mavazi (Nguo na Blanket).
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Chama Cha ACT- Wazalendo, Abdul Nondo ametaka vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi wa matukio ya utekaji kwa haraka na kutoa majibu ili kudhibiti vitendo hivyo katika jamii.
Nondo amesema hayo leo Januari 09,2025 akizungumza mbele ya waandsishi wa habari kufuatia tukio la utekwaji alilofanyiwa mwishoni mwa mwaka 2024.
Nondo amesema Jeshi la polisi lilichukua maelezo ya tukio hilo tangu akiwa hospitali lakini mpaka sasa hakuna taarifa ya yoyote juu ya uchunguzi huo, ikiwa ni pamoja na matukio mengine ya utekaji yaliyotokea 2024 ambapo baadhi ya waliotekwa hawajulikani walipo mpaka sasa akiwepo Deusdedith Soka na wenzake.
VIDEO: Kiongozi wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo Abudul Nondo, amesema bado ana hofu ya usalama wake baada ya tukio la kutekwa lilitokea mwishoni mwa mwaka 2024 kwani watekaji walimtishia kumuua endapo atazungumza kuhusu tukio hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 09,2025, Abdul Nondo ameelezea mkasa wa namna alivyotekwa ikiwa ni tukio la mara ya pili kwani aliwahi kutekwa mwaka 2018 akiwa Dar es salaam na kupatikana Mkoani Iringa.
Nondo ameweka wazi kuwa ana hofu kubwa juu ya maisha yake kwani watekaji walimtishia kumuua, na changamoto kubwa anayoiona ni vyombo vya usalama kutokufuatilia kwa karibu masuala ya usalama wa raia hususani yanayohusu vitendo vya utekaji, kwani mpaka sasa baadhi ya matukio hayo hayajachukuliiwa hatua ikiwepo tukio la Ali Kibao na tukio la Edger Mwakabela (Sativa).
Jana Januari 3,2024 Jeshi la Polisi Tanzania lilitoa taarifa ya kuwa linamsaka Kijana mmoja ambaye amejirekodi video na kuisambaza mtandaoni akitangaza kuwa anamuuza Mtoto aliyembeba kwa shilingi milioni moja na laki sita.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi ilinukuliwa ikieleza yafuatayo “Jeshi la Polisi linamtafuta kwa kuendesha msako Nchi nzima Mtu ambaye anaonekana ametengeneza picha mjongeo (video clip) akitangaza kuwa anamuuza Mtoto aliyembeba kwa shilingi milioni moja na laki sita, msako huo utahakikisha anakamatwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata”
“Aidha, Jeshi la Polisi linalaani kitendo hicho cha kikatili na kilicho kinyume na sheria, pia linatoa wito kwa Wananchi kuendelea kufichua vitendo kama hivyo, kuvilaani na kuvikemea kwani vinaweza kusababisha madhara kwa Watoto ili hatua zichukuliwe kabla madhara hayajatokea” - imeeleza taarifa ya Polisi.
Hata hivyo asubuhi ya leo Kijana huyo amechapisha video kwenye ukurasa wake wa Tiktok akisema nia yake haikuwa kumuuza Mtoto huyo bali alikua akitengeneza tu maudhui ya mtandaoni na ameamua asubuhi hii kwenda kituo cha polisi sengerema baada ya kupokea taarifa kuwa anatafutwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera ametembelea Gereza la Ruanda lililoko Jijini Mbeya na Kuzungumza na wafungwa waliopo Kwenye Gereza hilo ikiwa ni Pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na wafungwa hao, RC Homera amewaasa wafungwa kuhakikisha wanajifunza ujuzi mbalimbali wawapo hapo ili watakapopata ridhaa ya kurudi uraiani wautumie kuendesha maisha yao na kuwa walimu wa wengine.
Awali Wakieleza Maombi yao kwa RC Homera wamemuomba awahimize Viongozi wa Serikali kufika gerezani hapo kuwatembelea kwakuwa kufika Kwao wao hupata faraja kuu na kuamini kuwa serikali iko pamoja nao.
"Tunakushukuru sana kwa kuja Mkuu wa Mkoa Mimi nimefika hapa 2015 sijawahi kuona Kiongozi Mkubwa anakuja kututembelea, ujio wako tuna imani kuwa liko tumaini kubwa mbele yetu" amesema mmoja wa Wafungwa.
Mbali na hayo wafungwa pia wamemuomba RC Homera kuwasaidia kumleta Dkt: Tulia Ackson spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Mbeya Mjini kadharika Mganga Mkuu wa Mkoa.
"Mh: tusaidie kumuomba Rais wa mabunge Duniani na Spika Dkt: Tulia Ackson aje atutembelee maana yule ndio Mbunge wetu hata kama hatutokei hapa lakini tayari tuko kwenye Ardhi yake aje atuone"
"Pia Mganga mkuu wa mkoa tunamuomba aje atuone maana tunayo mengi ya kuzungumza naye hasa kuhusu magonjwa mbalimbali yanayotusibu"
Baada ya kusikiliza changamoto hizo Mkuu wa Mkoa ameahidi kuyatendea kazi kwa haraka hasa kuwaleta Viongozi wote sawasawa na maombi yao.
Lakini pia ametoa Kiasi Cha Shilingi Milioni Moja kwaajili ya Kununua Chakula (nyama) Msaada ambao umeambatana na magodoro yaliyotolewa na Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Mbeya Yasin Ngonyani kwa Kushirikiana na mfanyabiashara Achimwene.
"Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama. Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”
Amezungumza Tundu Antipas Lissu, Makamu Mwenyekiti Wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, ambaye pia ni mgombea Nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, akitoa salamu zake za Mwaka mpya leo Januari Mosi,2025.