08/12/2024
Star Wa Muziki Africa SIMBA 🦁 Amemjibu Mchekeshaji Wa Kenya Ambaye Amedai Kuwa Wasanii Wa Kenya Kila Siku Wamekuwa Hawapewi Thamani Kwenye Shows Zao.
“My Brother Eric, Mafanikio hayaji kwa kuwawekea chuki Wengine, bali yanakuja kwa kuongeza juhudi kisha Mungu nae atakubariki... Wewe ni Moja ya Mano zuri kwenye hili, Ulishakuja zaidi ya Mara 10 Tanzania kufanya shows as the Headliner na sikuzote Ulipokewa kwa Upendo, hukuwahi kusikia Standup Comedians wakikuletea chuki ama kuskia Wakisema “Wanaonewa” wala Campaign za “We want 75% Tanzanian Comedians “...WalijiAssess wakaona nini wafanye ili nao kufanikiwa, wakaweka Bidii, Zikaanzishwa ChekaTu, Watu Baki na Platforms Mbalimbali za Standup Comedy ambazo zikazalisha Standup Comedians Wengi, na leo hii nao wananufaika na kazi zao... Juzi tu alikuja Bien Tanzania na Watu wamempokea kwa Upendo na Kufanya kazi na Wasanii Mbalimbali...Afrika Mashariki ni Nchi zinazoishi kwa Upendo na Ushirikiano, jitahidi kuhamasisha Upendo na Ushirikiano na kuweka bidii, instead ya kuwafunza wasanii watuwekee chuki maana sio solution ya Kufanikiwa” - Diamond Platnumz
Hii Baada Ya Sakata La Tamasha La Furaha City Huko Nairobi Jana Ambao Wasanii Wa Kenya Walidai Wasanii Tz Wanapendelewa Zaidi .
✍️: ( )