01/02/2024
Hello π,
Leo tarehe 1/2/2024 tunazindua rasmi vitabu vyetu vinne vilivyochapishwa na Wiki e-Books Publishers.
1/4. GOGU NA MAGOGU: VITA VYA WAKATI WA MWISHO.
Baada ya kutokea vita ya kwanza ya dunia (1914-1918) na ile ya pili ya (1939-1945), wanazuoni na wasomi mbalimbali wamekua wakihofia kutokea tena kwa vita ya tatu vya dunia hii ni kutokana na maendeleo ya uchumi,sayansi na teknolojia baina ya mataifa makubwa na yenye nguvu.
Wanatheolojia na wasomi wa biblia wamekua wakishuku juu ya unabii wa sura za 38 & 39 za kitabu cha Ezekieli zinazoelezea vita ya "GOGU NA MAGOGU" k**a moja ya ishara ya kutokea vita vya tatu vya dunia kwa kuzingatia uhasama ulipo baina ya mataifa makubwa k**a, Marekani na Mataifa ya Ulaya dhidi ya Urusi na China, China dhidi ya Taiwan na Hong Kong, Korea Kusini dhidi ya Korea Kaskazini,Urusi dhidi ya Ukraine , India na Pakistan na zaidi Israeli dhidi ya Palestina na mataifa ya kiarabu.
Lakini hata hivyo hakuna hata vita moja iliyoweza kuthibitisha unabii huo wa Gogu na Magogu na bado kuna maswali magumu ,Je Gogu ni nani na nchi ya Magogu ni ipi? Roshi, Mesheki na Tubali ni nchi zipi katika dunia ya leo? Vita hio itapiganwa lini na nini itakuwa sababu ya vita hivyo?
Maswali hayo na mengineyo yanajibiwa na kitabu cha GOGU NA MAGOGU: VITA VYA WAKATI WA MWISHO kinachopatikana katika maktaba yetu ya Wiki e-Books Publishers.
Jina la kitabu: GOGU NA MAGOGU: VITA VYA WAKATI WA MWISHO ,
Mwandishi: WIKLIF PHINUS TUARIRA ,
Idadi ya kurasa za kitabu: 21,
Bei: Tsh 2999/-,
Wachapishaji: Wiki e-Books Publishers,
Aina ya kitabu: Nakala laini,
Mawasiliano: 0621 142591,
Barua pepe:
[email protected],
Kwa huduma za uchapishaji: [email protected].
__________________________________________________
2/4. HEKIMA ZA MFALME SULEMANI.
Katika maisha ya mwanadamu hapa duniani chini ya jua kila mmoja wetu amekuwa akihangaika kwa nguvu zake zote, kwa moyo wake wote, kwa akili zake zote na kwa roho yake yote kuhakikisha kuwa anapambana kupata maisha bora kwa ustawi wake na familia yake.
Lakini k**a inavyofahamika kuwa pambano lolote lina kanuni, kanuni hizo zisipofuatwa mpambanaji hawezi kupata ushindi ama kupata kile anachokihitaji.
Si jambo geni kwamba tunapomba ushauri kwa wazee wenye mvi za busara juu ya namna gani ya kuishi vyema na kupata mafanikio wamekuwa wakituasa mambo mengi lakini jambo kuu wanalotushauri hasa ni kuishi kwa HEKIMA, lakini je HEKIMA nini?, inapatikanaje?, iko wapi?, nawezaje kuitumia kwenye maisha yangu ya kibiashara, elimu, familia nk?. Maswali yoye hayo na mengineyo ya mfano wa hayo yamejibiwa katika kitabu cha HEKIMA ZA MFALME SULEMANI kinachopatikana katika maktaba yetu ya Wiki e-Books Publishers.
Jina la kitabu: HEKIMA ZA MFALME SULEMANI,
Mwandishi: WIKLIF PHINUS TUARIRA ,
Idadi ya kurasa za kitabu: 52,
Bei: Tsh 4490/-,
Wachapishaji: Wiki e-Books Publishers,
Aina ya kitabu: Nakala laini,
Mawasiliano: 0621 142591,
Barua pepe:
[email protected],
Kwa huduma za uchapishaji: [email protected].
__________________________________________________
3/4. ZABURI: VIPINDI VITATU VYA MAISHA YA MWANADAMU .
Maisha ni k**a misimu minne (kiangazi, vuli, masika, kipupwe) inayorudia. Bila kujali upendeleo kwa mtu yeyote, kila msimu huja wakati wake na kutoa nafasi kwa msimu unaofuata k**a vile mawazo katika akili ya mwanadamu ambapo kukoma kwa moja kunafuatiwa mara moja na kuibuka kwa lingine. Wakati wa baridi, asili hujifunga; katika vuli, hutoa; katika majira ya joto, huenea; na katika chemchemi huchanua. Misimu ambayo hatupendi inaonekana kudumu kwa muda mrefu. Maua huchipua katika chemchemi na mvua hunyesha katika msimu wa masika na vuli. Joto hupungua wakati wa baridi na zebaki hupanda wakati wa majira ya joto-k**a vile uhai unaoathiriwa na pumzi yako.
Vipo vipindi vitatu ambavyo kila mwanadamu huvipitia katika wakati wake ,hivi vipindi havikwepeki na hujirudirudia ili kutimizia maana halisi ya maisha. Je vipindi hivi ni vipi? Nini cha kufanya ili kukabiliana na vipindi hivi?
Maswali hayo na mengineyo yanajibiwa na kitabu cha ZABURI: VIPINDI VITATU VYA MAISHA YA MWANADAMU kinachopatikana katika maktaba yetu ya Wiki e-Books Publishers.
Jina la kitabu: ZABURI: VIPINDI VITATU VYA MAISHA YA MWANADAMU,
Mwandishi: WIKLIF PHINUS TUARIRA ,
Idadi ya kurasa za kitabu: ,
Bei: Tsh 3650/-,
Wachapishaji: Wiki e-Books Publishers,
Aina ya kitabu: Nakala laini,
Mawasiliano: 0621 142591,
Barua pepe:
[email protected],
Kwa huduma za uchapishaji: [email protected].
__________________________________________________
4/4. USIZINI.
Tangu enzi za kale dhambi imekuwa na matokeo hasi kwa mwanadamu, lakini ipo dhambi moja ambayo imeacha maumivu yasiyofutika, laana, mikosi na majuto miongoni mwa watu nayo si nyingine bali ni ZINAA.
Leo hii ndoa nyingi zinavunjika bila kukosa sababu, maendeleo binafsi yamekuwa magumu kila linalofanyika halifanikiwi, watoto wanazaliwa na wanakua wakirithi tabia chafu, hayo yote na mengineyo yasiyofahamika kwa macho na akili za kibinadamu kwa asilimia nyingi yanasababishwa na ZINAA.
Kupitia kitabu cha USIZINI kinachopatikana katika maktaba ya mtandaoni ya Wiki e-Books Publishers utajifunza athari za zinaa katika mwili na zaidi katika ulimwengu wa roho, katika maisha binafsi, kiukoo na kijamii lakini pia njia za kuepuka zinaa, kuvunja maagano yaliyowekwa baada ya kufanya zinaa na toba iletayo ondoleo la dhambi ya uzinzi.
Jina la kitabu: USIZINI ,
Mwandishi: WIKLIF PHINUS TUARIRA ,
Idadi ya kurasa za kitabu: 63,
Bei: Tsh 5250/-,
Wachapishaji: Wiki e-Books Publishers,
Aina ya kitabu: Nakala laini,
Mawasiliano: 0621 142591,
Barua pepe:
[email protected],
Kwa huduma za uchapishaji: [email protected].
Jipatie nakala yako sasaβΊοΈπ€
"Mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka " Danieli 9:2