Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kimesema kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za udhalilishaji ikiwemo ubakaji na ulawiti nchini hali inayozua maswali mengi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TAWJA, Jaji Barke Sehel amesema kinachoshangaza zaidi ni uwepo wa matukio hayo kwenye mikoa ambayo zamani haikuwa na historia ya matukio hayo.
Imeandaliwa na Esterbella Malisa
Mhariri @moseskwindi
Naibu Waziri wa Maji, Mhandishi Kundo Mathew amemuagiza mkandarasi anaetekeleza mradi wa maji wa miji 28 katika wilaya za Muheza, Korogwe, Pangani na Handeni, kuhakikisha anatekeleza maagizo ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aliyemtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili kutumiza adhma ya kuwapatia wananchi maji.
Mhandisi Kundo ametoa maagizo hayo alipotembelea wilayani Korogwe kukagua mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 171 na kusema bado hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wake.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
Je ukiwatembelea ndugu wakati wa sikukuu, unatakiwa kubeba kitu chochote au uende kama ulivyo?
Haya ni baadhi ya maoni ya wadau juu ya swali hilo, Je wewe unasemaje?
✍ Julliana James
Mhariri | Claud Mshana
#AzamTVUpdates #UTV108
Wajasiriamali mkoani Simiyu wamesema sasa wanauhakika wa kufanya biashara zao bila kusumbuliwa, baada ya kuanza kupata vitambulisho vitakavyowawezesha kufanya biashara zao kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amegawa vitambulisho zaidi ya 2100 kwa wajasiriamali wa mkoa huo, ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawaji wa vitambulisho hivyo.
✍ Rehema Evance
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua tukio la utoaji wa Tuzo za Utalii Nchini ambazo zinaratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Tuzo hizo zinatajwa kuwa na lengo la kutambua mchango wa watu na taasisi ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kupaisha sekta ya utalii Tanzania.
✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
Azam Media Limited imepokea zawadi ya mlipakodi kwa mwaka 2024, ikiwa ni sehemu ya wadau wa kodi nchini kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Paul Walalaze amekabidhi zawadi hiyo leo Desemba 20, 2024 Makao Makuu ya Azam Media na kuhimiza walipa kodi nchini kuendelea kulipa kodi kwa hiari.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
Wizara ya Katiba na Sheria imetoa elimu ya utawala bora na masuala ya kisheria kwa viongozi wa serikali za mitaa na kamati za usalama, ili kuwawezesha kutoa huduma bora na za haki kwa wananchi, ikilenga kupunguza malalamiko ya wananchi na kuboresha ufanisi wa serikali katika utendaji kazi wake.
✍ Joyce Lyanda
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
Mtaalamu wa Masuala ya Fedha Chilwa Kiliaki ameeleza sababu zinazosababisha Dola ‘kushuka’ na Shilingi ‘kupanda’ nchini.
Amesema kuwa miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na uuzaji wa mazao nje ya nchi, uboreshaji wa miundo mbinu, matokeo ya filamu ya ‘The Royal Tour’ na nyinginezo.
Msikilize…….
✍ Alpha Jenipher
Mhariri | Moseskwindi
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewatahadharisha watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kujiepusha na rushwa kwani imekuwa chanzo cha anguko la taasisi nyingi za umma.
Ulega ametoa onyo hilo wakati akizungumza na menejimenti ya TEMESA baada ya kupokea ripoti ya fedha zilizotolewa na serikali na kutumika katika maboresho ya vivuko na ujenzi wa vivuko vipya.
“Serikali imedhamiria kuifanya TEMESA kuwa taasisi namba moja na kimbilio la wote katika utengenezaji wa magari ya Serikali na binafsi hivyo tunatakiwa kupiga vita sana vitendo vya ubabaishaji na rushwa. Huu ndiyo ugonjwa unaoharibu taasisi nyingi na kwa kweli tunahitaji kutumia uwezo wetu wote kupambana na jambo hili," amesema.
Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza baina ya Waziri Ulega na viongozi wa TEMESA tangu ateuliwe kuwa waziri wa wizara hiyo mwezi huu.
Imeandaliwa na Ezekiel Kamwaga
Mhariri @moseskwindi
Maisha ni kupambana. Ndivyo unavyoweza kusema ukimzungumzia Jane Mgune, mwanamke aliyeanza kufundisha chekechea lakini sasa anaishi katika ndoto zake kwa kumiliki shule mkoani Shinyanga.
#azamnewsazamnews
Mhariri| @official_jennifersumi
Mapitio ya #Magazeti ya leo Desemba 20, 2024 ya kwenye #MorningTrumpet ya #UTV108
#AzamTVUpdates
Wadau wa elimu nchini wamekuwa na maoni tofauti mara baada ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoa waraka kwenda kwa walimu nchini, ukiwaeleza kufundisha kwa kutumia Ramani ya Tanzania inayoonesha kuwa mpaka wa Ziwa Nyasa umepita katikati ya Ziwa na siyo mwanzo wa ziwa upande wa Tanzania kama nchi ya Malawi inavyoeleza na kuitumia ramani hiyo kufundishia.
#azamnewsazamnews
Mhariri| @official_jennifersumi