ITV Tanzania

ITV Tanzania ITV- Independent Television Limited (ITV) associate company of IPP Limited. Tel:+255 22 2775914/6
E-mail:[email protected]

Tanzania · http://www.ippmedia.com
(276)

ITV-Independent Television Ltd,
Mikocheni Light Industrial Area
P.O.Box 4374, Dar Es Salaam,
Tanzania.

11/02/2025

🔴HABARI ZA SAA, SAA SABA NA DAKIKA 55, FEBRUARI 11, 2025

11/02/2025

HABARI ZA SAA, SAA SITA NA DAKIKA 55, FEBRUARI 11, 2025

 : Hali ilionekana kuwa tulivu Jumatatu kwa siku ya pili huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya v...
11/02/2025

: Hali ilionekana kuwa tulivu Jumatatu kwa siku ya pili huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya viongozi wa SADC na Jumuia ya Afrika Mashariki kutoa wito wa sitisho la mapigamo kutokana na hofu kuwa mapigano yanaweza kuchochea mzozo mkubwa.

Wanafunzi katika mji wa Bukavu walirejea shuleni, k**a alivyoshuhudia mwandishi wa AFP, baada ya shule kufungwa katika mji huo siku ya Ijumaa wakati wakazi walipoanza kukimbia na maduka kufungwa kwa kohofia mashambulizi ya wapiganaji wa M23.

Waasi wa M23 ambao inasemekana wanaungwa mkono na Rwanda, katika miezi ya hivi karibuni waliteka maeneo kadhaa katika eneo hilo la mashariki mwa Congo lenye utajiri wa madini.

Mapigano yaliua maelfu ya watu na kusababisha idadi kubwa ya watu kutoroka makazi yao.

Hali kwenye uwanja wa mapigano ilikuwa shwari Jumatatu mchana baada ya mapigano makali kutokea Jumamosi kwenye umbali wa kilomita 60 kutoka Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.

Waasi wa M23 walianza kusonga mbele kuelekea Kivu Kusini mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na Rwanda.

.

11/02/2025

HABARI ZA SAA, SAA TANO NA DAKIKA 55, FEBRUARI 11, 2025

11/02/2025

: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, amesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Chama kitaendelea kushika dola kutokana na wingi wa kura za wananchi na si mtutu wa bunduki.

Wasira aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Busega, mkoani Simiyu alipokuwa akielekea jijini Mwanza.

“Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, CCM tutashinda maana hakuna wa kupambana na sisi. Lengo letu ni kushika dola na dola hatuishiki kwa bunduki bali tunaishika kwa kura zinazopigwa na wana CCM na wasio wana CCM,” amesema Wasira.

11/02/2025

🔴HABARI ZA SAA, SAA NNE NA DAKIKA 55, FEBRUARI 11, 2025

11/02/2025

Katika Ripoti Maalum Jumatano hii.

 : Takriban watu 54 wamefariki dunia baada ya basi kuanguka kutoka kwenye daraja nje kidogo ya Jiji la Guatemala nchini ...
11/02/2025

: Takriban watu 54 wamefariki dunia baada ya basi kuanguka kutoka kwenye daraja nje kidogo ya Jiji la Guatemala nchini Guatemala, wazima moto walisema.

Basi hilo, lililokuwa likielekea mji mkuu kutoka idara ya El Progreso lilikuwa na abiria 75, na lilianguka chini ya bonde lenye urefu wa mita kadhaa na kutumbukia kwenye mfereji wa maji taka, kulingana na idara ya zima moto ya eneo hilo.

Miongoni mwa waliofariki ni watoto wadogo.

Miili ya wengi kati ya 54 waliofariki, akiwemo dereva wa basi, iko katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda karibu na eneo la ajali, wazima moto walisema.

.

11/02/2025

“..suala la ajali linaumiza Watanzania wengi na kupunguza nguvukazi na nitoe wito sasa kwa Kamanda wa Usalama Barabarani kusimamia sheria na madereva wote pia kuhakikisha wanasimamia sheria za usalama barabarani na kuzifuata…tusikubali kupanda pikipiki zaidi ya mmoja kila mmoja achukue hatua..” Naibu Waziri Mambo ya Ndani - Daniel Sillo.

.

 :KUANZIA SAA TISA ALASIRI. :Tabia ya baadhi ya watu kuropoka hovyo. Je, ni tatizo la kisaikolojia au ni tabia?
11/02/2025

:KUANZIA SAA TISA ALASIRI.

:Tabia ya baadhi ya watu kuropoka hovyo. Je, ni tatizo la kisaikolojia au ni tabia?

11/02/2025

🔴HABARI ZA SAA, SAA TATU NA DAKIKA 55, FEBRUARI 11, 2025

 : Netanyahu aliwasili na timu yake ya Mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika mash...
11/02/2025

: Netanyahu aliwasili na timu yake ya Mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika mashtaka ya mwaka 2019 ya kesi tatu zinazohusisha zawadi kutoka kwa marafiki Mamilionea, pamoja na madai ya kutafuta hisani kutoka kwa matajiri wa Vyombo vya Habari kwa kubadilishana na fursa bora ya utangazaji.

Netanyahu amekana mashtaka yote, ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Israel kushtakiwa kwa uhalifu.

Wakati huohuo, ujumbe wa Israel uliokuwa Doha nchini Qatar mwisho wa wiki iliyopita, kwa mazungumzo ya awamu ya pili ya amani kwa Gaza unarejea kutoka nchini humo. Haya yamesemwa leo na msemaji wa Netanyahu bila ya kutoa maelezo zaidi.

digitalupdates

11/02/2025

🔴KUMEKUCHA KISHINDO: UBUNIFU WA KUTUMIA SHANGA.. FEBRUARI 11, 2025

 : Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele jana Februari 10,2025 ametembelea na ...
11/02/2025

: Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele jana Februari 10,2025 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki, katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe vijijini Mkoani Tanga.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza sambamba kuanzia Februari 13 hadi 19,2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

11/02/2025

: Madereva wanaovunja sheria kwa kupita kwenye barabara ya Mabasi yaendayo kasi wamenaswa safari hii, wanachokifanya ni kinyume na sheria na kinahatarisha usalama wao.

11/02/2025

🔴HABARI ZA SAA, SAA MBILI NA DAKIKA 55, FEBRUARI 11, 2025

11/02/2025

🔴KUMEKUCHA MICHEZO: FEBRUARI 11, 2025

 : “Magonjwa yasiyoambukiza kuendelea kugharimu Bajeti kubwa ya Afya. Je, elimu endelevu inatolewa kudhibiti tatizo hili...
11/02/2025

: “Magonjwa yasiyoambukiza kuendelea kugharimu Bajeti kubwa ya Afya. Je, elimu endelevu inatolewa kudhibiti tatizo hili?”

Address

Mikocheni
Dar Es Salaam
14111

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ITV Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to ITV Tanzania:

Videos

Share