![MFAHAMU JONATHAN IKANGALOMBO A.K.A SPEED MAN KWA UCHACHE. ๐ฐ๐ฐ๐ฐKwa majina ni Jonathan Ikangalombo Kapela,,, Mchezaji huyu ...](https://img4.medioq.com/016/288/122194620110162889.jpg)
16/01/2025
MFAHAMU JONATHAN IKANGALOMBO A.K.A SPEED MAN KWA UCHACHE. ๐ฐ๐ฐ๐ฐ
Kwa majina ni Jonathan Ikangalombo Kapela,,, Mchezaji huyu ambaye ni Raia wa DR Congo alizaliwa tarehe 5 ya mwezi Aprili mwaka 2002 hivyo kwa sasa ana umri wa miaka 23.
Nafasi yake uwanjani ni winga wa kulia lakini pia anao uwezo wa kucheza k**a winga wa kushoto na mshambuliaji wa kati. Jonathan amewahi kuitumikia klabu ya DC Motema Pembe ya huko huko DRC na A.S VITA CLUB aliyojiunga nayo mnamo mwaka 2023.
Jonathan Ikangalombo ametambulishwa saa 6 usiku wa kuamkia leo Alhamisi ya tarehe 16.01.2025 kuwa mchezaji rasmi wa Young Africans Sports Club
Mwananchi umeupokeaje usajili wa winga Jonathan Ikangalombo???