11/01/2024
, π§ππ»
:: Ni muda wa kuandaa mashamba sasa ::
Hakikisha umepata mbegu poa na elimu ya kutosha kutoka Buzwagi Poa. Tumekufikia sasa, Agiza kokote uliko. Mbegu ya Ua Moja, Na yenye uzani wa zaidi ya Gram 1000 kwa ua moja lenye kukupatia zaidi ya Net Gram 200 ya mbegu pekee baada ya kupukuchua.
Zina mafuta mengi na zinakomaa kwa miezi 3 tu.
KULIMA MSIMU WA MVUA ZA AWALI FAIDA NA HASARA ZAKE.
Msimu mzuri wa kulima ni kipindi cha mvua chache. Hii ikiwa ni kipindi cha mwanzo wa msimu wa mvua, hususani mwezi wa 9 na 10 ambapo utavuna mwezi wa 12 na 1.
FAIDA ZA KULIMA KIPINDI HIKI π§ππ»
1. Mvua huwa chache kipindi alizeti ikiwa changa, (haipendi mvua nyingi kipindi ikiwa changa), na mvua huwa nyingi kipindi ikiwa imebeba maua (maana ikibeba ua huhitaji mbua za kutosha ili iweze kukomaa na kupakia mafuta ya kutosha).
2. Ni kipindi cha bei nzuri maana alizeti huiva kipindi cha sikukuu za Krimasi na Pasaka, ambapo mafuta yanakuwa na bei ya juu, na soko halina alizeti ya kutosha.
HASARA YA KULIMA KIPINDI HIKI.
1. Alizeti hukomaa kipindi cha mvua nyingi na upepo mkali. Hivyo kwa kuwa alizeti ni dhaifu katika hali ya upepo, maua mengi huanguka shambani na kuoza kabla hayajavunwa.
2. Kukosa jua la kukaushia maua. Hii husababisha alizeti kupata uvundo na mbagu kuharibika.
Utatuzi wa matatizo haya: TUPIGIE / WHATSAPP +255-746-031110
KULIMA MSIMU WA MWISHO WA MVUA, FAIDA NA HASARA ZAKE
Kwa wale wanaopenda kulima mwishoni mwa msimu wa mvua. kipindi kizuri ni mwezi wa 2 na 3, na mavuno yake ni kuanzia mwezi wa 6 hadi wa 7 zikisha kauka.
FAIDA ZA KULIMA KIPINDI HIKI: π§ππ»
1. Alizeti huiva kipindi cha jua, hivyo kupata muda wa kutosha kukausha alizeti yako. Hasara za uvundo huepukika kiurahisi. Uvundo husababisha mafuta kuwa machungu na yenye harufu mbaya.
2. Aridhi hupatikana kwa bei poa hususani kwa wale wanaokodi mashamba, pia kwa wale wenye mashamba, ni rahisi kupanda baada ya kuvuna mazao mengine.
HASARA ZA KIPINDI HIKI.
1. Alizeti hukomaa kipindi mavuno ni mengi na bei huwa chini sana. Hivyo humlazimu mkulima kuchelewa kuuza ili kusubili bei, na hatimaye kuingi gharama ya kutunza stoo na kupoteza mzunguko wa fedha kwa wakati.
2. Ndege hushambulia alizeti kwa urahisi pindi zinapokauka sana, hii hupelekea mavuno kupungua na kupata faida kidogo, ama hasara kabisa.
3. Mvua huwa bado nyingi kipindi alizeti ikiwa changa, na mvua huwa chache kipindi ua linapokomaa na kuhitaji maji yakutosha, hivyo miche hudumaa na mavuno hupungua.
π§ππ» KWA SEMINA ZAIDI NA ZAIDI, USISITE KUTUPIGIA, NA KUFIKA KIWANDANI PIA KWA MAJIFUNZO ZAIDI YA KILIMO BIASHARA.
π§ππ» KUMBUKA, KUSHINDWA KUPANGA, NI KUPANGA KUSHINDWA (FAILURE TO PLAN, IS PLANING TO FAIL)
π§ππ» NAWATAKIA KILIMO NA MAVUNO MEMA.
Kwa huduma ya kukamuliwa mbegu zako, na kupata mafuta bora na safi, BUZWAGI POA, Ndiyo habari ya mujini.
SIMU/WHATSAPP
+255-746-031110
π§ππ» π§ππ» π§ππ»