09/12/2024
Kampeni ya msaada wa kisheria ( Mama Samia Legal Campaign ) inatarajiwa kuendelea kutekelezwa, katika Mikoa minne ya Tanzania.
Kampeni hiyo itafanyika kwa siku 10 mfululizo katika kila Mkoa, ambapo Mkoani Iringa itazinduliwa tarehe 10, Desemba, 2024, Mara tarehe 11 Desemba, 2024, Songwe tarehe 12 Desemba 2024, kisha itaendelea Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ester Msambazi, amesema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kuhakikisha kuwa msaada wa kisheria unafika kwa wananchi katika katika kila eneo, na kwamba kampeni hiyo itakuwa endelevu ili kufikia mikoa yote 26 ya Tanzania katika mwaka huu wa fedha 2024/25.
Ester Msambazi ameongeza kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha haki za wananchi zinaheshimiwa na kuwawezesha kupata msaada wa kisheria bila kikwazo.