TATIZO = FURSA
ukiijua hiyo hesabu vizuri maisha kwako yatakuwa bam bam
Wasanii wengi kwa kipindi kirefu tumekuwa tunalalamika kuwa tunabaniwa
kwenye MEDIA bila kuelewa kwa kifupi tu ukweli wa mambo. Kwa Uchunguzi nilioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu hivi nimegundua
haya, Watayarishaji au watangazaji wa vipindi kwa siku wanapokea zaidi
ya nyimbo 30 kutoka kwenye studio mbalimbali hapa nchini,
kwao inakuwa
ni vigumu kucheza nyimbo zote kutokana either muda kuwa mdogo wa
vipindi vyao au kuwa na request nyingi za nyimbo ambazo wamekuwa
wanazicheza sana. SULUHISHO LA TATIZO
Baada ya kuliona tatizo nikapata idea ya kuzunguka kwanza Manispaa
zote ILALA, KINONDONI na TEMEKE kuangalia usajili wa vituo vya
bodaboda na bajaj zilizosajiriwa kwenye vituo ambazo pia wameweka
radio ambazo zinatumia flash na memory cards,
Huku nikapata idea ya kuanzisha KITAA RADIO FM ambayo itahusika na
kuwasambazia watu hapa muziki ule ambao ulishindwa kupenya radioni
muziki wa aina yeyote wa Kitanzania ambao mzuri kusikika na watu
wakaupenda. Pili, kwenye upande upande wa video napo nikajiuliza ni mabus mangapi
yaendayo mikoani ambayo ndani hutoa burudani ya movies , music video
nk nikakuta ni zaidi ya mabus 2000 ,ambapo kwa siku kila bus
linasafirisha si chini ya abiria 50
Huku nako nikapata idea ya kuanzisha BODA 2 BODA Television ambayo
itakuwa inatoa burudani ya music videos zile tu zilizokosa kupewa
Airtime kwa namna moja au nyingine