SERIKALI YAJIPANGA KUKABILIANA NA TAARIFA POTOFU KUELEKEA UCHAGUZI
RAIS SAMIA: VIONGOZI KANUSHENI TAARIFAPOTOFU ZINAPOSAMBAZWA MITANDAONI
Kuku wa mapambo anayeuzwa Shilingi milioni moja
Ukweli kuhusu video ya utekaji watoto Dar es Salaam
Sio Kweli: Gen Z wachoma moto ndege ya Rais wa kenya
Ufuatiliaji na uchunguzi uliofanywa na Nukta Fakti umebaini kuwa hakuna ndege yoyote ya Rais wa Kenya aina ya Jet iliyochomwa moto.
Kwa msaada wa Google Reverse Image, imebainika kuwa picha na video hizo zinaonyesha eneo la Uhuru Park, katikati ya mji wa Nairobi, hivyo sio eneo ambalo kuna kiwanja cha ndege ambapo ndege inaweza kutua bali ni eneo la mapumziko.
Pia, ndege hiyo ambayo ipo katika eneo la Uhuru Park ni ndege chakavu aina ya Boeing 737 ambayo imegeuzwa kuwa mgahawa.
Picha za Google za Agosti 30, 2022, zinaonyesha ndege hiyo ikiwa katika eneo hilo.
Historia ya Uhuru Park
Bustani ya Uhuru Park ilitangazwa rasmi na kufunguliwa kwa umma na Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta, tarehe 23 Mei 1969 kama ishara ya uhuru wa nchi.
Aidha, ni makazi ya mnara wa wapigania uhuru wa Mau-Mau unaoheshimu waathiriwa wa mateso wakati wa enzi ya ukoloni.
Tofauti ya Ndege
Ndege ya Rais wa Kenya ni tofauti kabisa na ile inayoonekana kwenye video. Ndege ya Rais wa Kenya ina rangi nyeupe yenye maandishi ya "Republic of Kenya" (Jamhuri ya Kenya).
Hii inaweza kuthibitishwa kwa video mbalimbali za ndegehiyo, ikiwemo zile za mwaka 2019 na 2023.
Habari za zamani
Pia, kuna habari za picha ya ndege hiyo hiyo iliyosambaa mwaka 2012 ikisema kuwa ndege ya rais wa Kenya imetua kwa dharura.
Habari hiyo ilifanyiwa uthibitisho na PesaCheck na kubainika kuwa sio tukio la kweli.
Kwa hivyo, madai ya kuchomwa kwa ndege ya rais wa Kenya ni ya uongo na yamebainishwa kama uzushi.
Gen Z ni kina nani?
Gen Z inasimama badala ya maneno Generation Z au Zoomer. Ambapo inarejea kuanzia kizazi kilichofuata baada ya millennia, na kinajumuisha watu waliyozaliwa kati ya mwaka 1995 na 2010.
Debunked: Kenyan MP’s did not eat in the bush following bill protest
Makundi yote hayapaswi kuachwa nyuma katika vita dhidi ya Uviko-19.
Kwa kiasi gani tumewashirikisha watu wenye ulemavu katika utoaji wa chanjo ya Uviko-19?
#VumbuaUkweli
Kama bado hujapata chanjo ya Uviko-19 mpaka sasa, ujumbe wako huu hapa 👇👇
#VumbuaUkweli
Fanya haya Jumapili ya leo kuepuka mtego wa habari za uzushi hasa zinazohusiana na Uviko-19.
#VumbuaUkweli
Kifahamu kirusi kipya cha Uviko-19 kinachoitesa dunia kwa sasa.
#VumbuaUkweli