Msasa Online

Msasa Online Matangazo Piga Simu +255758379300
(1)

MSASA ONLINE
Ni kiwanda cha habari kinacho tumia ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia kwa kutoa habari, michezo, burudani, na elimu kidijitali kwa wafuasi wake na jamii inayo zungumza kiswahili duniani kote karibu.

 ZELENSKIY ATAKA WANAJESHI WA NJE KUPELEKWA KUMSAIDIA HUKU AKITAKA VITA KUMALIZWA HARAKA KIDIPLOMASIA.Na VENANCE JOHNRai...
10/12/2024


ZELENSKIY ATAKA WANAJESHI WA NJE KUPELEKWA KUMSAIDIA HUKU AKITAKA VITA KUMALIZWA HARAKA KIDIPLOMASIA.

Na VENANCE JOHN

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy leo amesema anataka vita kati ya nchi yake na jirani yake Urusi kumalizika haraka iwezekanavyo kwa njia za kidiplomasia

"Ukraine inataka vita hivi viishe zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Bila shaka, azimio la kidiplomasia lingeokoa maisha zaidi. Tunalitafuta," Zelenskiy amewaambia waandishi wa habari mjini hii leo.

Matamshi hayo yamekuja katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na kiongozi wa upinzani wa Ujerumani Friedrich Merz yakiwa ni mazungmzo ya hivi punde zaidi kuashiria ongezeko la uwazi wa Ukraine katika mazungumzo ya vita.

"Unaweza tu kutumia nguvu ikiwa Ukraine ina nguvu. Ukraine yenye nguvu kabla ya diplomasia yoyote ina maana Ukraine yenye nguvu kwenye uwanja wa vita," amesema, akimaanisha kwamba Ukraine inahitaji msaada wa kijeshi ili kuwa na nguvu.

Vita kati ya majirani hawa vimedumu kwa miezi 33 sasa na Rais Zelenskiy ameibua wazo kuwa wanajeshi wa kigeni wanatakiwa kutumwa nchini mwake ili kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO kwa ajili ya kupambana na Urusi.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ambaye amesema anataka kumaliza vita haraka, jana alitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na mazungumzo ya kumaliza vita hivyo alivyoviita "wazimu", baada ya kukutana na rais Zelenskiy na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Paris.

Zelenskiy amesema kwamba aliwaambia viongozi hao wawili kwamba haamini kuwa rais Putin kweli anataka kumaliza vita hivyo na kwamba rais wa Urusi inahitajika kulazimishwa.

09/12/2024


WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Wananchi katika kata ya Kibaoni iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuanza kutekeleza mpango wa matumizi bora ya Ardhi ikiwa ni kupanga kupima na kumilikisha Ardhi.

Haya yamesemwa leo tarehe 09 Desemba 2024 katika Sherehe za maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika Kiwilaya katika Chuo cha Mizengo Pinda Tawi la Chuo cha Sayansi ya Kilimo (SUA) na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Jimbi la Kavuu Mhe. Geophrey Mizengo Pinda ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo.

Awali katika hotuba yake ya Ufunguzi wa sherehe hizo Mhe. Naibu Waziri Geophrey Pinda amesema kuwa Ardhi haiongezeki isipokuwa idadi ya watu hivyo watumie ili kulingana na mpango wa matumizi ya Ardhi husika.

Wizara ya Ardhi inatekeleza miradi kadhaa kwa ajili ya utambuzi wa maeneo mbalimbali mathalani kupitia Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (K*K) ikiwa ni juhudi za kuunga maono ya Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 UWEKEZAJI SEKTA YA NISHATI TANZANIA KUNUFAISHA NCHI WANACHAMA EAPP – MHE.KAPINGANaibu Waziri Nishati, Mhe. Judidhi Kapi...
09/12/2024


UWEKEZAJI SEKTA YA NISHATI TANZANIA KUNUFAISHA NCHI WANACHAMA EAPP – MHE.KAPINGA

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judidhi Kapinga amesema uwekezaji uliofanyika kwenye Sekta ya nishati nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu itazinufaisha Nchi Wanachama wa Umoja wa Mashariki mwa Afrika (EAPP) katika biashara ya kuuziana na kununua umeme.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Desemba 09, 2024 Mombasa nchini Kenya katika mkutano uliowakutanisha nchi wanachama wa EAPP na wadau mbalimbali katika sekta ndogo ya umeme.

“Uzalishaji wa umeme awali ulikuwa kwa kiasi kikubwa ukitegemea gesi, lakini baada ya ujenzi wa mradi mkubwa wa Julius Nyerere ambao kwa sasa unazalisha takribani megawati 1,175 tumekuwa tukitumia zaidi nishati ya maji kuzalisha umeme." Amesema Mhe. Kapinga

Ameongeza kuwa, Tanzania inazingatia suala la uzalishaji wa umeme kwa nishati mchanganyiko (energy mix) na kutoa wito kwa Nchi wanachama EAPP kuwekeza zaidi katika nishati jadidifu ambazo ni nishati safi.

Kuhusu usambazaji wa umeme Vijijini, Mhe. Kapinga ameeleza kuwa Tanzania ina mkakati wa kuhakikisha Vijiji vyote 12,318 vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo 2025 na kuongeza kuwa tayari zaidi ya asilimia 99 ya vijiji vimeshafikiwa na nishati hiyo.

Kapinga ameeleza kuwa, Tanzania inatarajia kujiunga na mfumo wa kuuziana na kununua umeme wa Kusini mwa Afirka (Southern African Power Pool).

Amesisitiza kuwa, kwa Tanzania kuwa na miunganiko ya umeme ni muhimu na ndio maana k**a inaungana na nchi tofauti tofauti katika biashara ya umeme ili kuufanya mfumo wa gridi kuwa imara.

Kapinga amesisitiza kuwa Nchi nyingine za Afrika zitanufaika na sekta ya nishati kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanyika nchini kwa uwepo wa umeme wa uhakika.

Kwa upande wa Wadau wa Maendeleo, Mhe. Kapinga ameeleza kuwa Tanzania inathamini mchango wao katika sekta sekta ya nishati na kuongeza kuwa kwa kiasi kikubwa miradi inatekelezwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

 DC BABATI ATOA AGIZO TAASISI AMBAZO HAZIJASHIRIKI SHEREHE ZA UHURU KUTOA MAELEZO YA KINA KWA MAANDISHI......Na VENANCE ...
09/12/2024


DC BABATI ATOA AGIZO TAASISI AMBAZO HAZIJASHIRIKI SHEREHE ZA UHURU KUTOA MAELEZO YA KINA KWA MAANDISHI......

Na VENANCE JOHN

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, ameonesha kutoridhishwa na baadhi ya taasisi kutokushiriki sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania, zilizofanyika leo Desemba 9,2024.

Katika hotuba yake akifungua mdahalo maalumu kuhusu uhuru, Kaganda ameeleza kuwa kitendo cha taasisi hizo kutoonekana katika sherehe hizo ni dhihirisho la ukosefu wa uzalendo na kushindwa kutambua umuhimu wa siku hiyo adhimu kwa Taifa.

“Sherehe za Uhuru siyo tu siku ya kumbukumbu, bali ni fursa ya kuonyesha mshik**ano wetu k**a Taifa, kutohudhuria ni sawa na kudharau historia ya nchi yetu na juhudi za waasisi wa uuhuru" amesema Kaganda

Akizungumza kwa msisitizo, Kaganda ameagiza taasisi zote ambazo hazijahudhuria sherehe hizo kuwasilisha maelezo ya maandishi yakieleza sababu za kutokushiriki.

“Tunahitaji kujua sababu za kushindwa kwenu kufika, ninaomba mdahalo huu urudiwe wakihusishwa Vijana, Wanafunzi na taasisi zote" amesisitiza DC Kaganda.

Kaganda amesema ni muhimu kw tukio hilo kuhudhuriwa na taasisi zote ili kuhakikisha kila taasisi inawajibika ipasavyo na kutoa mchango wake katika matukio ya kitaifa yanayojenga mshik**ano na heshima kwa nchi.

 UPINZANI GHANA WAPATA USHINDI WA KIHISTORIA, ALIYESHINDWA ASEMA HATAKUWA MPINZANI WA KUVURUGA.....Na VENANCE JOHNRais w...
09/12/2024


UPINZANI GHANA WAPATA USHINDI WA KIHISTORIA, ALIYESHINDWA ASEMA HATAKUWA MPINZANI WA KUVURUGA.....

Na VENANCE JOHN

Rais wa zamani wa Ghana, John Drahami Mahama ameshinda uchaguzi na tayari mgombea wa chama tawala amekiri kushindwa hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa na tume ya uchaguzi. Bawumia alitangaza kuwa Waghana walitaka mabadiliko.

Tume ya uchaguzi ya Ghana bado haijatoa matokeo rasmi, lakini Mahamudu Bawumia, ambaye ni makamu wa Rais na mgombea kupitia chama tawala cha New Patriotic, amekiri kushindwa.

"Mabibi na mabwana, tumekubali kushindwa k**a mwanademokrasia mkamilifu angefanya. Lakini hatujaachana na vita vya kubadilisha Ghana na kupanua fursa kwa makundi yote ya jamii yetu. Hatutakuwa upinzani wa kuvuruga".

Kushindwa kwake kumemaliza miaka nane madarakani kwa chama cha NPP chini ya Rais Nana Akufo-Addo, ambaye muhula wake wa mwisho ulikumbwa na msukosuko mbaya zaidi wa kiuchumi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mgombea wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress, John Drahami Mahama, ametarajiwa kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi. Mahama aliwahi kuwa rais wa Ghana kutoka 2012 hadi 2017.

Tume ya uchaguzi imesema huenda matokeo rasmi yakatangazwa kufikia siku ya Jumanne.

 JAY-Z ASHTAKIWA KWA KESI YA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 13.Na  VENANCE  JOHNMwanamuziki nguli nchini Marekani Jay-Z amefu...
09/12/2024


JAY-Z ASHTAKIWA KWA KESI YA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 13.

Na VENANCE JOHN

Mwanamuziki nguli nchini Marekani Jay-Z amefunguliwa kesi ya ubakaji dhidi ya mtoto wa miaka 13 mwaka 2000.

Kesi hiyo iliyorekebishwa iliyowasilishwa katika mahak**a ya shirikisho siku hapo jana Jumapili inadai kwamba msanii huyo maarufu wa rap alimbaka msichana wa miaka 13 pamoja na Sean Diddy Combs maarufu k**a P Diddy wakati wa tafrija mwaka 2000.

Jay-Z hata hivyo amekanusha madai hayo kwenye mitandao ya kijamii na kukashifu kesi hiyo, akiitaja kuwa ni sehemu ya jaribio la uwongo. Mpaka sasa wanasheria wa Jay-Z hawajasema lolote.

Kesi hiyo iliwasilishwa mwezi Oktoba katika Wilaya ya Kusini ya New York na wakati huo haikumtaja Jay-Z k**a mshtakiwa, ingawa kesi iliyorekebishwa inasema kwamba Jay-Z alitambuliwa k**a mtu mashuhuri kwenye malalamiko ya awali.

  RAIS WA KOREA KUSINI YOON SUK YEOL APIGWA MARUFUKU KUSAFARI NJE YA NCHI.....Na VENANCE JOHNRais wa Korea Kusini Yoon S...
09/12/2024


RAIS WA KOREA KUSINI YOON SUK YEOL APIGWA MARUFUKU KUSAFARI NJE YA NCHI.....

Na VENANCE JOHN

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amepigwa marufuku kuondoka nchini humo kutokana na jaribio lililoshindwa la kuweka sheria za kijeshi.

Kauli hiyo imetolewa na afisa wa wizara ya sheria leo Jumatatu, huku kukiwa na miito ya kumtaka ajiuzulu ikionesha kuwa mzozo wa kisiasa katika nchi hiyo unazidi kuongezeka.

Oh Dong-woon, mkuu wa Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi kwa Viongozi wa Vyeo vya Juu, amesema amemzuia rais Yoon Suk Yeol kusafiri nje ya nchi.

Oh Dong-woon, amesema kauli hiyo alipoulizwa katika kikao cha bunge baada ya kuulizwa ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya rais.

Naye afisa wa wizara ya sheria, Bae Sang-up, ameiambia k**ati ya bunge kuwa amri ya marufuku ya kusafiri imetekelezwa.

Yoon ameomba radhi kwa jaribio hilo lililoshindikana kukamilika na kusema kuwa anaachia hatima yake ya kisiasa na kisheria kwa chama chake tawala cha People Power (PPP) lakini hatajiuzulu.

Leo, wizara ya ulinzi imesema rais Yoon bado ni Amiri jeshi mkuu kwa mjibu wa sheria, ingawa upinzani unaokua kati ya maafisa wakuu wa kijeshi dhidi ya rais umesababisha kutiliwa shaka kushikilia mamlaka hiyo.

 ETHIOPIA YAKAA SAA SITA GIZANI NCHI NZIMA BAADA YA HITILAFU YA UMEME....Na VENANCE  JOHNHitilafu ya umeme iliyotokea nc...
09/12/2024


ETHIOPIA YAKAA SAA SITA GIZANI NCHI NZIMA BAADA YA HITILAFU YA UMEME....

Na VENANCE JOHN

Hitilafu ya umeme iliyotokea nchini Ethiopia, ambayo ilianza majira ya saa kumi na mbili jioni saa za nchini humo siku ya Jumamosi, ilishughulikiwa kikamilifu saa nne usiku.
Taarifa hiyo ilitolewa na mamlaka ya nishati ya umeme ya Ethiopia.

Mamlaka hiyo imesema kuwa umeme ulirejeshwa taratibu kufuatia takribani saa sita za usumbufu uliosababishwa na kuyumba kwa mfumo.

Kukatika kwa umeme kuliathiri nyumba, biashara, na miundombinu muhimu, na kusababisha hasara kwa baadhi ya biashara.

Tukio k**a hilo la kukatika umeme karibu nchi nzima lilitokea mwezi Machi mwaka huu 2024, kwa kukatika umeme kwa saa tano kuliingiza sehemu kubwa ya nchi gizani.

Mpaka sasa sababu ya kukatika kwa umeme haijawekwa wazi, na hivyo kuibua wasiwasi unaoendelea kuhusu kutegemewa kwa gridi ya umeme ya Ethiopia.

  RAIS WA SYRIA BASHAR AL-ASSAD NA FAMILIA YAKE WAPEWA HIFADHI URUSI BAADA YA KUPINDULIWA NA WAASI...Na  VENANCE  JOHNAl...
09/12/2024


RAIS WA SYRIA BASHAR AL-ASSAD NA FAMILIA YAKE WAPEWA HIFADHI URUSI BAADA YA KUPINDULIWA NA WAASI...

Na VENANCE JOHN

Aliyekuwa rais wa Syria Bashar al-Assad na familia yake yuko mjini Moscow nchini Urusi kwa hifadhi ya kupinduliwa na kundi la waasi.

Hayo yameelezwa Jumapili usiku na Ikulu ya Urusi Kremlin, iliyosisitiza kuwa makubaliano yamefikiwa ili kuhakikisha usalama wa kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria.

Awali Urusi ilikuwa imesema kuwa kambi zake ziko katika tahadhari kubwa lakini hakukuwa na kitisho dhidi yao kwa sasa.

Assad ameikimbia nchi baada ya waasi kuchukua udhibiti wa mji mkuu Damascus huku akitoa maagizo ya kukabidhiana madaraka kwa amani.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ni lazima Assad awajibishwe kwa vitendo vya mauaji na mateso kwa mamia ya maelfu ya Wasyria. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo litafanya mkutano wa dharura na wa faragha ili kuijadili hali inayoendelea nchini Syria.

Baada ya mapinduzi, waasi nchini humo wametangaza marufuku ya watu kutembea nje usiku hadi saa kumi na moja asubuhi. Tangazo hilo limejiri baada ya waasi hao kuchukua udhibiti wa mji mkuu Damascus na kuuangusha utawala wa Bashar al Assad.

 ALIYEKUWA WAZIRI WA ULINZI KOREA KUSINI AKAMATWA Na   VENANCE  JOHNPolisi nchini Korea Kusini wamemkata aliyekuwa wazir...
09/12/2024


ALIYEKUWA WAZIRI WA ULINZI KOREA KUSINI AKAMATWA

Na VENANCE JOHN

Polisi nchini Korea Kusini wamemkata aliyekuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Bw. Kim Yong-hyun, huku uchunguzi wa madai ya uhaini ukiendelea.

Hatua ya kuk**atwa kwa kiongozi huyo ni kutokana na jukumu lake katika sheria ya kijeshi iliyotangazwa na Rais Yoon Suk Yeol, ambaye amenusurika kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye Bungeni.

Licha ya rais kuponea chupuchupu kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye bungeni, bado hata hivyo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Bw. Lee Jae-myung, amesema chama hicho kitajaribu kwa mara nyingine tena tarehe 14 mwezi Desemba kumuondoa madarakani rais Yoon Suk Yeol.

Hata hivyo mzozo wa kisiasa nchini humo unaendelea kutokota kwani kuna ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinazoeleza kuwa waziri wa mambo ya ndani Lee Sang Min, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Yoon Suk Yeol, amejiuzulu.

 TOYOTA FESTIVAL RUVUMA MAGARI ZAIDI YA 5000 KUSHIRIKI....Zaidi ya magari 5,000  aina ya Toyota yatashiriki kwenye Tamas...
08/12/2024


TOYOTA FESTIVAL RUVUMA MAGARI ZAIDI YA 5000 KUSHIRIKI....

Zaidi ya magari 5,000 aina ya Toyota yatashiriki kwenye Tamasha kubwa la Utalii mkoani Ruvuma (Ruvuma Toyota Festive) litakalofanyika tarehe 25 Juni 2025.
Aidha Tamasha hili linatarajia kuwakutanisha watu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na nje ya Nchi.
Maandamano ya Magari aina ya Toyota yataanzia katika Manispaa ya Songea na kumalizika katika mji mdogo wa Mbambabay wilaya ya Nyasa ambalo linalenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Peres Magiri wakati anazindua Toyota Networking Cocktail kwenye ukumbi wa kanisa Anglikana mjini Songea.

 JANA NA LEO WAPI AFADHALI?NI FULL TIME  CS CONSTANTINE 2 - 1 SIMBA SC
08/12/2024


JANA NA LEO WAPI AFADHALI?
NI FULL TIME
CS CONSTANTINE 2 - 1 SIMBA SC

  RAIS SAMIA AFANYA TEUZI MBALIMBALI...Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua, Gerson Msigwa kuwa Katibu Mk...
08/12/2024

RAIS SAMIA AFANYA TEUZI MBALIMBALI...

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua, Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Msigwa licha ya kuwa Katibu Mkuu ameongezewa jukumu la Usemaji Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.

Teuzi ni k**a ifuatavyo
(1) Mhe. Rais Dkt. Samia amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;

(ii) Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari;

(iii) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria;

(iv) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira);

(v) Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi:
(vi) Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;

(vii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

(viii) Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;

(ix) Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu);

(x) Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;

(xi) Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.

Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;

(xii) Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  DIVA AMPA WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA MAUA YAKE..Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi Wasafi FM  ameandika ujumbe huu ikiwa...
08/12/2024


DIVA AMPA WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA MAUA YAKE..

Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi Wasafi FM ameandika ujumbe huu ikiwa ni kumpa maua yake Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa

"Mheshimiwa Waziri Mkuu Babangu Mejisikia tu kukusifu, nataka kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa kazi yako ngumu na kujitolea kwa ajili ya nchi yetu. Tunathamini juhudi zako katika kuboresha maisha ya wananchi na kuleta maendeleo. Tafadhali endelea na kazi hii nzuri."

Follow kwa habari za uhakika saa 24.

 YANGA WAME.....MALIZIA  FULL TIME   MC ALGER 2 - 0 YANGA SC
07/12/2024


YANGA WAME.....MALIZIA
FULL TIME
MC ALGER 2 - 0 YANGA SC

 MCHEZO UNAENDELEA DK 75' MC ALGER 1 - 0 YANGA SC
07/12/2024


MCHEZO UNAENDELEA DK 75'
MC ALGER 1 - 0 YANGA SC

 HALF TIME  MC ALGER 0 - 0 YANGA SC
07/12/2024


HALF TIME
MC ALGER 0 - 0 YANGA SC

Address

Mbezi Louis
Dar Es Salaam
0000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Msasa Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share