Dr Ruge Khan

Dr Ruge Khan Tunakusogezea habari zote zinazo make headlines tukidadavua hasa katika Michezo, muziki, sanaa

Karibu tena comrade  wewe ni tunu ya taifa na nguzo muhimu sana, Imani ya vijana wengi ni utaendeleza yale mazuri na mak...
22/10/2023

Karibu tena comrade wewe ni tunu ya taifa na nguzo muhimu sana, Imani ya vijana wengi ni utaendeleza yale mazuri na makubwa zaidi ulokuwa umeyatanabaisha ndani ya dar es salaam sasa yatumikie kitaifa chuni ya mwenyekiti na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh imekupa wigo mpana Sasa kalitumikie taifa kiueledi na kuisimamia ilani ya chama....
Mwenyezi Mungu aendelee kuzisimamia njia zako..... KARIBU SANA🙏

Wao wanasema UNYAMA NI MWINGI
26/07/2023

Wao wanasema UNYAMA NI MWINGI

25/05/2023
“Wanawake wenye makomwe wana asili ya kupenda kudeka, wana wivu sanaa wakiwa kwenye mapenzi na hupenda kususa harakaa. N...
25/05/2023

“Wanawake wenye makomwe wana asili ya kupenda kudeka, wana wivu sanaa wakiwa kwenye mapenzi na hupenda kususa harakaa. Na inapotokea akiumizwa kwenye mapenzi hupenda kulia huku wanajipiga Piga kwenye mwili na kuchana nguo”

Kitaalam hii inaitwaje😆😆😆

  wanasema wako na Jambo laoMwananchi unatarajia kushangilia ushindi ukiwa wapi
13/05/2023

wanasema wako na Jambo lao

Mwananchi unatarajia kushangilia ushindi ukiwa wapi

Home Land
09/09/2022

Home Land

Black is black but truth stands.. we loose together we win together 🦁
17/01/2022

Black is black but truth stands.. we loose together we win together 🦁

Mr president of Manzese Vs Mr president of Wasafi😂
10/12/2019

Mr president of Manzese Vs Mr president of Wasafi😂

JONIJOO & KUSAGANi  Kwenye TV ya wasafi tv Kesho Juma Tano Saa 3 Kamili USIKU 🔥, Jonijooo Uso kwa Uso na Mkurugenzi Mten...
10/12/2019

JONIJOO & KUSAGA

Ni Kwenye TV ya wasafi tv Kesho Juma Tano Saa 3 Kamili USIKU 🔥, Jonijooo Uso kwa Uso na Mkurugenzi Mtendaji wa CLOUDS MEDIA GROUP je ni Kweli anamiliki hisa zake ndani ya Wasafi Media ya Diamondplatnumz...Mengi zaidi kesho jumatano...
POWERED BY : .
MACHO YOTE NI KESHO JUMATANO SAA 3 KAMILI USIKU NDANI YA ..... PIA USIKOSE KUTAZAMA MARUDIO SIKU YA ALHAMIS SAA 6 MCHANA NA ITARUDIWA TENA JUMAPILI SAA 4 USIKU .
Cc :

10/12/2019

Suleiman Matola sasa ni rasimi ndo kocha msaidizi wa Simba SC Tanzania

Ndo kusema kwamba nini labda😲😲
09/12/2019

Ndo kusema kwamba nini labda😲😲

"Kwa upande wangu imekuwa safari fupi kufika hatua hii. Hata hivyo najivunia kusema wazi kwamba ajenda ya mabadiliko bad...
08/12/2019

"Kwa upande wangu imekuwa safari fupi kufika hatua hii. Hata hivyo najivunia kusema wazi kwamba ajenda ya mabadiliko bado inaendelea na tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa klabu ya soka ya Simba inapiga hatua kubwa zaidi kisoka."- CEO Senzo.
"Nina uhakika kwamba waanzilishi wa klabu hii wanafurahia kuona klabu inafanya mageuzi muhimu ambayo yataisaidia kuifikisha hatua ya juu zaidi na kuhakikisha kuwa Simba inakuwa moja ya timu bora katika soka la barani Afrika."- CEO Senzo.
"Siku chache ambazo nimekuwepo nchini zimenifungua macho na nafurahi kwamba nimekuta gari moshi likiwa tayari safarini na mimi nimekuwa mwongozaji. Soka ni kitu cha pekee katika kila nchi na kila bara, nina hakika pia ndivyo ilivyo hapa Tanzania."- CEO Senzo.
"Tegemeeni mageuzi kadhaa ndani ya uongozi. Mageuzi haya yamelenga katika kuisuka klabu katika mtazamo mpya wa kitaalamu. Nimeazimia kusimamia uwazi na uongozi jumuishi na wa kitaalamu katika mtindo wangu wa uongozi."- CEO Senzo.
"Yafuatayo ni maeneo muhimu ambayo nimedhamiria kuyaimarisha nikiwa k**a CEO. (1) Marekebisho ya muundo wa ndani wa Uongozi, tunahitaji kuwa na muundo huru na wa kitaalamu wa uongozi wa kuiendesha klabu hii."- CEO Senzo.
"(2) Mabadiliko ya kisoka, hii itahusu usajili wa wachezaji na benchi la ufundi. (3) Ukuzaji wa Simba k**a brandi ya mauzo ndani ya EA na sehemu zingine za Afrika. Tunahitaji kuitangaza Simba duniani kwa kufanya matangazo kwa juhudi kubwa."- CEO Senzo.
"(3) Usimamizi wa mali za klabu zilizopo. (4) Maendeleo ya vitengo mbalimbali vya biashara. Upanuzi wa vyanzo vyote vya mapato na kubuni njia zingine za kuingiza mapato nje ya kutegemea wahisani na makusanyo ya uwanjani."- CEO Senzo.
"(5) Kuwafanya mashabiki kuwa wateja. Simba ni klabu yenye mashabiki wengi. Tunahitaji kubuni miradi itakayoifaidisha klabu, mashabiki na wanachama wetu kwa kuhakikisha kuwa uhusiano baina yao na klabu unakuwa zaidi na kufikia kuwa wateja wa klabu"- CEO Senzo.

"Wiki hii, tunaleta kocha mpya, kocha mwenye kiwango kinachostahili kufundisha mabingwa wa nchi hii. Sasa tunaleta kifaa...
08/12/2019

"Wiki hii, tunaleta kocha mpya, kocha mwenye kiwango kinachostahili kufundisha mabingwa wa nchi hii. Sasa tunaleta kifaa. Mtatangaziwa rasmi, ni nani, na anatoka nchi gani."- Mo Dewji.
"Baada ya kusema hayo napenda kuishukuru Bodi ya Wakurugenzi ninayofanya nayo kazi. Hawa ni watu makini na wananisaidia sana katika kutimiza wajibu wangu, k**a mwenyekiti wao na mwekezaji ndani ya klabu hii."- Mo Dewji.
"Kipekee, niishukuru kwa dhati serikali yetu chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, hakika serikali hii inatupa kila ushirikiano tunaohitaji k**a klabu. Nimshukuru Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa."- Mo Dewji.
"Nisema kitu kuhusu mgeni rasmi wetu wa leo, Naibu Spika. Amedhihirisha Usimba wake wa kindakindaki. Alfajiri ya leo alikuwa anaongoza msafara wa wabunge wenzike kwenda Uganda, lakini amehairisha safari hiyo muhimu baada ya kupokea mwaliko wetu."- Mo Dewji.

"Leo nianze na neno moja kubwa na lenye maana pana sana, Alhamdulillah! Shukrani za dhati ziende kwa Mungu wetu Mtukufu ...
08/12/2019

"Leo nianze na neno moja kubwa na lenye maana pana sana, Alhamdulillah! Shukrani za dhati ziende kwa Mungu wetu Mtukufu kwa hapa tulipo! Hakika hizi ndio ndoto zetu wanasimba wote, kuifikisha klabu yetu kwenye kilele cha mafanikio."- Mo Dewji.
"Jana Jumamosi yalitimia kule Bunju, na leo tupo hapa na wanachama wenzangu kujadili mustakabali wa klabu yetu, tena kwa amani na utulivu mkubwa, hizi ndio ndoto zetu."- Mo Dewji.
"Mnafahamu kwa sasa mchakato wa kubadilisha muundo wa klabu yetu umekamilika kwa asilimia zaidi ya 90, na yamebaki mambo machache muhimu ili sasa Simba iwe kampuni kamili, itakayoendeshwa vile Wanasimba mlivyotaka."- Mo Dewji.
"Jana tumeshawaonyesha uwanja wetu wa mazoezi ambapo kutakuwa na viwanja vizuri na vya kisasa, cha nyasi bandia na majani asilia, pamoja na viwanja hivyo tumejenga chumba cha kubadilishia nguo chenye ubora na fensi ya kulizunguka eneo la viwanja."- Mo Dewji.
"Hii ni awamu ya kwanza, yanayokuja pale Bunju Complex yatafurahisha nchi na Wanasimba wote, katika suala la miundombinu ya Bunju niwahakikishie wanachama wenzangu mambo yatakuwa bul bul"- Mo Dewji.
"Awamu ya pili ya ujenzi wa Bunju Complex, kujenga hosteli yenye vyumba vya kulala, gym, ofisi za benchi la ufundi, jiko na kantini ya chakula, nutritional center, chumba maalum cha kitaalam kwa uchambuzi wa mechi zetu na mazoezi, pamoja na technical room."- Mo Dewji.
"Mradi huu unatarajiwa kuwa na thamani ya Tsh. Bilioni 2.5 na kwa kuanzia k**a mwanachama na Mwenyekiti wa Bodi nitachangia kiasi cha Tsh. milioni 500. Wanasimba wanahamu yakuchangia ujenzi na upanuzi wa Bunju Complex."- Mo Dewji.
"Kiasi kilichobaki tutafanya fundrising ili kupata fedha inayotakiwa, bila shaka tutafanikiwa ili kwenye msimu wa 2021/22 tuwe kwenye hostel zetu. Kazi yangu ni kuhakikisha wachezaji wanapata mazingira bora na mishahara mizuri ili waweze kufocus na kushinda"- Mo Dewji.

“Uongozi k**a huu ndio tunataka Wanasimba, mimi ni kiongozi wa wote hivyo nawambia na timu zingine huu ni mfano wa kuigw...
08/12/2019

“Uongozi k**a huu ndio tunataka Wanasimba, mimi ni kiongozi wa wote hivyo nawambia na timu zingine huu ni mfano wa kuigwa na wengine”- Dkt. Tulia.
“Nimeona jana mambo mazito kabisa. Nimefurahi kusikia katika moja ya mipango kuanzisha Simba Academy, hili sio muhimh kwa Simba bali hata kwa nchi. Nawapongeza sana viongozi kuona umuhimu wa kusaidia vijana wadogo”- Dkt. Tulia.
“Sisi k**a mashabiki lazima tusiwe wa kwanza kuwakatisha tamaa viongozi wetu, tusiwe wa kwanza kuwasema vibaya, tuwaunge mkono katika kuipeleka timu yetu next level”- Dkt. Tulia.
“Mimi ni sehemu ya wabunge, na wabunge wengi ni Simba, yupo kule Mhe. Spika, yupo pia Mhe. Waziri Mkuu niwambie tu kule wengi ni Simba”- Dkt. Tulia.

"Siridhishwi hata tone na nidhamu ya baadhi ya wachezaji wetu nje ya uwanja. Nimekuwa mnyonge kuona uwekezaji tuliouweka...
08/12/2019

"Siridhishwi hata tone na nidhamu ya baadhi ya wachezaji wetu nje ya uwanja. Nimekuwa mnyonge kuona uwekezaji tuliouweka kwao, baadhi yao, huutumia k**a fimbo ya kutuchapia."- Mo Dewji.
"Niwaambie wachezaji wote, Simba ni klabu kubwa kweli kweli, tena kubwa hasa, na hakuna shaka ni namba moja Afrika Mashariki, bodi ninayoiongoza mimi haitavumilia mchezaji yoyote asiyejua thamani ya Simba. Kuonyana onyana sasa imetosha."- Mo Dewji.
"Sisi tunawalipa vizuri mno, na wao wana wajibu wa kutulipa matokeo na furaha. Na ili furaha iwepo, lazima nidhamu isimamiwe kikamilifu, na katika hili hatutanii. Hatutajali ukubwa wa jina la mchezaji yoyote."- Mo Dewji.
"Nidhamu kwetu ni muhimu k**a tunataka tufikie malengo tuliyokusudia. Na haya ndio yaliyotufanya bodi tuchukue maamuzi magumu kwa kocha wetu. Timu imeshindwa kufikia malengo, kisha nidhamu hakuna, alafu tuvumilie?"- Mo Dewji.
"Simba lazima tuamue kuteseka na moja katika mambo haya mawili, (1) tuzoee uchungu na maumivu ya nidhamu au (2) maumivu ya matokeo mabaya. K**a mpenzi wa Simba, siwezi"- Mo Dewji.
"Mtaniwia radhi kidogo nimekuwa mkali ila nidhamu kwangu ndio kila kitu. Hata mimi mwenyewe naishi kwa nidhamu, na ndio siri ya mafanikio yangu, na naamini watu wote waliofanikiwa, na taasisi zote zilizofanikiwa msingi wake mkuu ni nidhamu ya kazi."- Mo Dewji.
"Klabu yetu imeimarisha sana timu zake za vijana na wanawake, na sasa sisi ni miongoni mwa klabu chache Tanzania zenye timu imara za vijana chini ya miaka 20, na ile ya miaka 17, na tuna timu nzuri ya wanawake, na tunazidi kuziimarisha."- Mo Dewji.
"Na katika msimu huu wa ligi, tutahakikisha tunachukua tena ubingwa ili tuje kuweka rekodi nyingine kwenye klabu bigwa Afrika. Nawahakikishia wanachama wenzangu kujikwaa si kuanguka, hatutarudia makosa! Insha’Allah, Mungu atutangulie."- Mo Dewji.

"Tupo mahali pazuri ambapo mishahara na posho mbalimbali vinatolewa kwa wakati. Wachezaji wetu wanalipwa vizuri ikilinga...
08/12/2019

"Tupo mahali pazuri ambapo mishahara na posho mbalimbali vinatolewa kwa wakati. Wachezaji wetu wanalipwa vizuri ikilinganishwa na klabu k**a Azam na Yanga ambao ni wapinzani wetu wakubwa. Kiwango cha pesa kinachotumika katika usajili na masuala mengine ni kikubwa pia."- CEO Senzo
Haya ni moja kati ya maendeleo muhimu barani Afrika, na klabu chache zinaweza kumudu hatua hii."- CEO Senzo.
"Simba ni timu kubwa katika soka la Afrika. Ni jukumu letu sote, hasa kwa wachezaji kufanya vizuri ndani ya uwanja na kuifanya iendelee kutambulika k**a klabu kubwa."- CEO Senzo.
"Wanachama wakati huu tunafanya mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji, mchakato wa uhakiki wa wanachama wetu, uanzishaji wa matawi wa kibiashara, tuvumiliane na kushirikiana, na tutafanya mchakato huu kwa kasi ya kawaida ili msije kuachwa nyuma."- CEO Senzo.
"Usajili wa wachezaji utafanyika kwa namna tofauti. Tutatoa mikataba mirefu kwa wachezaji kwa kuzingatia utaratibu wa kitaalamu, k**a unataka kucheza hatua ya nusu fainali ya unahitaji kikosi kitakachoweza kukaa pamoja kwa miaka 3-4. "- CEO Senzo.
"Tunahitaji pia kutazama kwa kina muundo wetu wa ukuzaji vipaji kuhakikisha kuwa tunatoa wachezaji wetu wenyewe k**a ilivyokuwa hapo awali. Tunahitaji kufuata njia hiyo."- CEO Senzo.
"Tuna mchezo muhimu na watani wa jadi mwezi Januari. Napenda kuwahakikishia kuwa maandalizi na mambo yote ya mchezo huo yapo tayari. Wachezaji watakuwa kambini na tangazo la nani atakuwa kocha mkuu mpya na benchi la ufundi litatoka rasmi Jumatano ijayo."- CEO Senzo.
"Ningependa kuchukua maneno machache kutoka kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, anasema: “Ili kuwepo na maendeleo ya kweli, watu wanapaswa kushirikishwa.” Julius Kambarage Nyerere, kutoka kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo mwaka 1973.- CEO Senzo.

Messi ndio Baba Lao. Orodha ya 10 bora: Lionel MessiVirgil van DijkCristiano RonaldoSadio ManeMo SalahKylian MbappeAliss...
02/12/2019

Messi ndio Baba Lao.
Orodha ya 10 bora:
Lionel Messi
Virgil van Dijk
Cristiano Ronaldo
Sadio Mane
Mo Salah
Kylian Mbappe
Alisson
Robert Lewandowski
Bernardo Silva
Riyad Mahrez

Address

Dar Es Salaam
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr Ruge Khan posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dr Ruge Khan:

Videos

Share

Category