Tafuta kumjua MUUMBA WAKO kama vile yeye anavyo kufahamu,
Tafuta ufalme wa MUNGU,
Mjue KRISTO,
Lijue kusudi la kuumbwa kwako,
Omba neema ya kumjua na kumtumikia MUNGU,
Kuna siri kubwa sana katika ilimwengu wa kiroho.
Tafuta kuaminiwa na MUNGU,
Ili uzijue siri izi kwa kadili ya uelewa wako,utayari wako na uhaminifu wako kwake,
Tumia ujana wako vema,
Tumia uzee wako vema,
Maisha yako ya mtukuze MUUMBA wako,
MHUBIRI 11:9
"9 Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni."
***
Tambua kila nafasi unayoipata leo halijirudii tena katika maisha yako, wekeza kwa MUNGU,
Kwa maana mwisho wa mambo yote MUNGU atakuleta hukumuni, ana heri yule mwenye matendo mema, anaheri yule aliyeandikwa katika kitabu cha uzima.
.
UFUNUO 20:13
"13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake."
**
Mwana wa MUNGU,
Umesikia NENO la MUNGU,
Umesoma NENO la MUNGU,
Umeshuhudia mambo makuu ya MUNGU humu duniani,
Umekua wa tofauti tangu kuzaliwa kwako,
Wewe ni mshindi mpaka sasa kama umemkili BWANA YESU kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako,
Shika sana ulicho elewa , ishike sana iyo kweli, shika sana iyo imani. Tunza uaminifu wako kwa MUNGU, tunza sana utii wako kwa MUNGU, ulichofunzwa kitumie, ulichofunzwa kishuhudie kwa mwingine ili naye amjue MUNGU ndivyo unavyojiwekea hazina yako kule mbinguni, hazina isiyo haribika wala kuoza.
Muda umebaki mchache sana maana BWANA asema hatakuja kama vile Mwivi ajapo kukuibia.
***
1 WATHESALONIKE 5:2-3
"2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku."
.
"3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa."
.
MUNGU akupe nguvu ya kutunza ulichonacho,
Omba BWANA YESU akupe kukitunza ulichopata.
Bwana Yesu asifiwe,
Mwana wa MUNGU, Neno linatuelekeza kuchunga sana kauli tuzitoazo kwa maana neno moja linaweza kutupa baraka ama kutupa laana
Kichunge kinywa chako
YAKOBO 3:10
"Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo."
.
Vinywa vyetu vijae baraka, tamka baraka hata kwa walio kukosea ni vema sana kujizuia kuongea kupita kiasi usije ukategwa kwa maneno yako mwenyewe
.
Zaburi 34:13
"Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila."
.
Methali 6:2
2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,