07/01/2025
Rais wa shirikiho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Walace Karia ambaye pia ni Rais wa shirikisho hilo ukanda wa nchi za Mashariki na kati mwa Afrika anatarajiwa kuongoza Mkutano Mkuu wa kanda hiyo ya CECAFA unaotarajiwa kufanyika kwa Hoteli ya Raddisson Blu nchini Sudan Kusini.
Mkutano Mkuu usio na uchaguzi wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) utafanyika Januari 22, 2025 huko Juba, Sudan Kusini.
Auka John Gecheo, Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA ametangaza leo kuwa Mkutano huo umehamishwa kutoka Januari 25, 2025 katika Hoteli ya Raddison Blu mjini Juba.
Mkutano huo pia utajadili mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mashindano ya CECAFA kwa 2024 na kalenda ya 2025-2026.
CECAFA chini ya uongozi wa Wallace Karia k**a Rais ana wajumbe 12; Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Eritrea, Somalia, Djibouti, Ethiopia, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan na Zanzibar.
Sponsored By