20/12/2024
*UONGOZI WA WANA AZ HAR WAFUNGUA MFUKO WA DHARURA ( EMEGENCE FUND)*
Uongozi wa Umoja wa wahitimu wa Al-Azhar tawi la Tanzania chini ya Mwenyekiti wake Dr. Hussein Muhammad Afifu, unapenda kuwatangzia wana Azhar kuwa baada ya kutambua Umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na kusaidiana baina yetu wakati wa maradhi na vifo, na baada ya kupokea maoni mengi kutoka kwa wana Azhar na wadau mbalimbali kuhusu namna bora ya kusaidiana wakati wa changamoto hizo, Uongozi umeonelea ni vizuri kuweka utaratibu rasmi wa kukusanya michango ili kumsaidia mmoja wetu pale anapopatwa na Changamoto ya maradhi au kupatwa na umauti.
Katika kuliendea hilo, Uogozi umeandaa utaratibu rasmi wa kuwaleta wana Azhar pamoja ambao watakao kuwa tayari kushirikiana kwa hali na mali endapo mmoja wetu akipatwa na tatizo la maradhi au kifo na kuhitaji msaada wetu.
Kwa muktadha huo, Uongozi umeanzisha mfuko maalumu wa dharura (Emergency Fund) kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo, ambapo umeandaa fomu ya kujiunga na mfuko kwa wale watakao kuwa tayari kufuata kanuni na taratibu za mfuko huo.
Aidha mfuko huo utajumuisha wana Az har pamoja na wadau wengine wa Azhar Tanzania amabo tumekuwa tukishirikiana nao katika mambo mbalimbali (watakuwa ni wanachama waheshima katika mfuko).
Fomu ya kujiunga na mfuko itagharimu shilingi elfu kumi tu (10,000), ambapo shilingi elfu tano (5,000) itatumika kuchapisha fomu na shilinghi elfu tano (5,000) kuandaa kitambulisho cha uwanachama
Fomu hiyo itapatikana ofisi za wana Azhar tawi la Tanzania, zilizopo Mtaa wa livingstone na Omari Londo, Gerezani, Kariakoo, Dar es Salaam (Nyumba namba 12), kuanzia tarehe 20 Desemba 2024, na mfuko unatajia kuanza rasmi kupokea michango ya wanachama ya kila mwezi kuanzia Januari mosi 2025.
Aidha kopi laini (soft copy) za fomu zitapatikana kwa njia ya mtandao ambapo muombaji akihitaji atarushiwa na kisha kuijaza na kuirejesha ofisi ili kukalisha taratibu za kiidara.
NB: 1. Muombaji atakaporejesha fomu aambatanishe na picha mbili za passport size.
2. Muombaji atakaporejesha fomu atapatiwa waraka wa miongozo unaofafanua namna ya kuchangia mfuko,matumizi ya fedha za mfuko, haki na wajibu wa Mwanachama wa mfuko, ukomo wa Mwanachama na kadhalika.
3. ili kuhakikisha usalama wa michango ya wanachama uongozi utaanzisha akaunti kwenye kampuni ya mawasiliano ya Vodacom (M-Koba) kwa ajili ya kuhifadhi michango ya wanachama kwa usalama na uwazi Zaidi.
Kwa mawasiliano piga namba zifuatazo:-
- Katibu Mkuu: 0784553414
- Mweka Hazina: 0656590995
Imetolewa na Uongozi
Tarehe 20/Desemba 2024.