Clouds TV

Clouds TV Kituo namba moja cha burudani kwa vijana kikisogeza kila taarifa ya entertainment mbele yako na kuhakikisha hupitwi na yanayojiri ndani na nje ya nchi.
(1)

Drop Comment yako hapa!  Ataisoma LIVE Kwenye show tamu ya Tv The Spark📺🔥Ikumbatie
19/09/2024

Drop Comment yako hapa! Ataisoma LIVE Kwenye show tamu ya Tv The Spark📺🔥

Ikumbatie

PUBLIC NOTICE: REQUEST FOR EXPRESSION OF INTEREST (EOI) TO INVEST IN FUND'S LANDS.Cc:
19/09/2024

PUBLIC NOTICE: REQUEST FOR EXPRESSION OF INTEREST (EOI) TO INVEST IN FUND'S LANDS.

Cc:

Hii ni kubwa kuliko na haijawahi kutokea. Kwa mara ya kwanza industry ya Comedy inakwenda kuandika historia kwa kukusany...
19/09/2024

Hii ni kubwa kuliko na haijawahi kutokea. Kwa mara ya kwanza industry ya Comedy inakwenda kuandika historia kwa kukusanya watu 10,000 watakaokaa pamoja pale Leaders Club tarehe 5 Oktoba 2024.

A-list ya Comedians wako unaowakubali watakuwepo Oktoba 5. Wahi tiketi yako mapema.

"Maabara ya maji Mtwara ni miongoni mwa maabara 17 nchini ambayo Serikali inajenga kuhakikisha kwamba tunafuatilia hali ...
19/09/2024

"Maabara ya maji Mtwara ni miongoni mwa maabara 17 nchini ambayo Serikali inajenga kuhakikisha kwamba tunafuatilia hali ya ubora wa maji nchini ili kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania wanapata maji yaliyobora, safi na salama. Hivyo maabara ya maji Mtwara jukumu letu la kwanza ni kufuatilia vyanzo vyote vya maji kuhakikisha maji yanayosambazwa kwa wananchi yako salama kwa matumizi" - Mtaalamu wa Maabara, Chacha wanda marwa.





Kabla ya kuwa na hivi visima nane kulikuwa na visima viwili. Kipindi kile hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ngumu sana...
19/09/2024

Kabla ya kuwa na hivi visima nane kulikuwa na visima viwili. Kipindi kile hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ngumu sana k**a unavyojua population ya manispaa ya Lindi kulinganisha na Sensa ni 174,000 wananchi na ni 30% ndio walikuwa wanapata maji kwa kipindi kile.

Ndipo Mhe. Rais akaona kuna haja ya kupeleka mradi mkubwa kwenye manispaa ya Lindi na ndipo tukapata huu mradi mkubwa kutoka chanzo cha Ng'apa na tumechimba visima 8 ambavyo kwa pamoja pake yake vina uwezo wa kuzalisha maji lita milioni saba na laki tano kwa siku." - MD LUWASA ( Mamlaka na Maji safi na Usafi wa Mazingira Lindi)





"Kazi ya kuujenga mradi ni kazi moja, lakini kazi ngumu ni kuhakikisha chanzo kinakuwa endelevu na miundombinu inakuwa e...
19/09/2024

"Kazi ya kuujenga mradi ni kazi moja, lakini kazi ngumu ni kuhakikisha chanzo kinakuwa endelevu na miundombinu inakuwa endelevu.

Kwa kweli tunaishukuru Serikali kwa sasa imeanzisha mfumo mzuri wa baada ya kukamilisha mradi kinatengenezwa chombo cha watumiaji maji ambacho upatikanaji wake unaanzia kwenye jamii, kile kinakuwa na kazi ya kuhakikisha vile vyanzo vinaendelea kutunzwa na huduma inaendelea kupatikana." - Mhandisi Muhibu Lubasa - Meneja wa RUWASA mkoa wa Lindi.





"Kwa takwimu za Sensa ya 2022, mkoa wa Lindi una watu takribani zaidi ya watu 1,194,000 lakini sisi k**a RUWASA tunahudu...
19/09/2024

"Kwa takwimu za Sensa ya 2022, mkoa wa Lindi una watu takribani zaidi ya watu 1,194,000 lakini sisi k**a RUWASA tunahudumia watu takribani zaidi ya 900,000 kwenye vijiji 502 na maeneo mengine wanahudumiwa na Mamlaka ya maji.

Kazi yetu ni kuhakikisha mwananchi wa kijijini tunamfikishia huduma ya maji karibu hivyo kila tukiamka tunahakikisha namna ya kumfikishia mwananchi maji na tunajivunia maeneo mengi ya mkoa wa Lindi tofauti na kabla ya serikali ya awamu ya 6.

2021 upatikanaji wa maji ulikuwa wastani wa 28% lakini sasa hivi tuko 72%" - Mhandisi Muhibu Lubasa - Meneja wa RUWASA mkoa wa Lindi.





"Lengo kubwa la Rais Samia Suluhu Hassan ni kumtua mama ndoo kichwani na aliianza kampeni hii tangu akiwa Makamu wa Rais...
19/09/2024

"Lengo kubwa la Rais Samia Suluhu Hassan ni kumtua mama ndoo kichwani na aliianza kampeni hii tangu akiwa Makamu wa Rais. Lakini tukumbuke pale tu ambapo aliingia kwenye Urais alikwenda kuzungumza na wabunge bungeni na akazungumza vitu vingi sana kwenye sekta mbalimbali lakini kwenye sekta ya maji alimsimamisha Mhe. Aweso na akatoa kauli moja tata kidogo alisema ukinizingua nitakuzingua na alisema hilo kwenye sekta ya maji tu kwa sababu anajua maji ni uhai na adhma ya wizara ya Maji na ya Mhe. Rais ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji safi na salama, bora na yenye kutosheleza" - DC Lindi, Victoria Mwanziva.





"Kuanzia Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Lindi Manispaa imepata zaidi ya Bilioni 52.9 kwa ajili ya ...
19/09/2024

"Kuanzia Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Lindi Manispaa imepata zaidi ya Bilioni 52.9 kwa ajili ya mradi wa maji pekee.

Na mradi wetu mkubwa unaitwa mradi wa ng'apa ambao huu peke yake umegharimu bilioni 33." - DC Lindi, Victoria Mwanziva





"Ruangwa ina tarafa 3, kata 22, vijiji 90 na kijiographia Ruangwa imezungukwa na miamba tuna madini ya graphite na dhaha...
19/09/2024

"Ruangwa ina tarafa 3, kata 22, vijiji 90 na kijiographia Ruangwa imezungukwa na miamba tuna madini ya graphite na dhahabu na chuma kwa asili maji yake yanakuwa mbali sana na ya chumvi sana.

Kwa muda ambao nimekuwepo niseme ukweli ambao hauna mjadala kuna wakati alikuja mwanasiasa alikuwa na mawazo yaleyale akasema unaona watu wanateseka maji hamna watu wakamwambia uongoo kwa sababu ukweli wanaujua" - DC Ruangwa Hassan Ngoma


"Suala la maji ni jambo ambalo mwanadamu yoyote anahitaji na namna ya kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana ni ka...
19/09/2024

"Suala la maji ni jambo ambalo mwanadamu yoyote anahitaji na namna ya kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana ni kazi ngumu na inahitaji uwekezaji mkubwa." - DC Ruangwa - Hassan Ngoma.


19/09/2024

CLOUDS 360

"Kilichosababisha mauaji ya Kimbari ya Rwanda ni redio na kauli za chuki. Tunachokumbushana ni wajibu k**a chombo cha ha...
18/09/2024

"Kilichosababisha mauaji ya Kimbari ya Rwanda ni redio na kauli za chuki. Tunachokumbushana ni wajibu k**a chombo cha habari kwenye kudumisha mshik**ano na amani katika jamii"- (), Mkurugenzi Mtendaji - The African Leadership Initiative For Impact-alii Africa


"Tarehe 6, October ni Siku ya Utindio wa Ubongo Duniani itakuwa ni siku ya Jumapili. Tutafanya workshop pamoja na semina...
18/09/2024

"Tarehe 6, October ni Siku ya Utindio wa Ubongo Duniani itakuwa ni siku ya Jumapili. Tutafanya workshop pamoja na semina. Tutajumuika na akina mama au wazazi, walezi 300 ambao watapata elimu jinsi ya kumlea mtoto wake mwenye tatizo hilo. Tukio litafanyika pale Genesis International Schools (Oysterbay)"- Tayana S Tibenda () •


"Watoto wa mtindio wa Ubongo wametengwa hawana sauti. Mtoto mwenye ulemavu huo mama wakati anajifungua akipata matatizo ...
18/09/2024

"Watoto wa mtindio wa Ubongo wametengwa hawana sauti. Mtoto mwenye ulemavu huo mama wakati anajifungua akipata matatizo kuna wengine wanazaliwa hivyo hivyo"

"Utindio wa Ubongo ni tofauti na Usonji. Mtoto wangu yupo kwenye wheel chair Saa 24, unambeba unamuweka kitandani analala. Familia ya baba yake imesimama na Mimi kuanzia siku ya kwanza mpaka kesho.

"Nina uwezo wa kukaa hapa mpaka sasa hivi kwa sababu najua yupo na bibi yake. Na yupo na mtu ambaye anaweza kumuangalia. Nina uwezo na kuwa na jukumu la kuzunguka Tanzania nzima kwa sababu najua mtoto wangu yupo salama"- Tayana S Tibenda () •


"Asante yangu kubwa ni kwa CMG na Asante yangu kubwa ya pili ni Afya Check chini ya Dk. Isaac Maro na ndio maana nipo ha...
18/09/2024

"Asante yangu kubwa ni kwa CMG na Asante yangu kubwa ya pili ni Afya Check chini ya Dk. Isaac Maro na ndio maana nipo hapa.

"Mimi ni mama mwenye mtoto wa miaka 16. Mtoto wangu ana ulemavu wa ubongo 'Mtindio wa Ubongo'. Miaka yangu 16 ya malezi yake k**a mzazi na mama, nimepitia changamoto nyingi sana na bado nitaendelea kuzipitia kwa sababu kijana wangu bado anaendelea kukua na mengine ya kesho siyajui.

"Nilichukua initiative kwenye safari yake ya malezi kwamba ninaomba niwe Balozi wa kuwa sauti yake na watoto wenzake"- Tayana S Tibenda () •


Mwaka 2022/23 Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Kibondo ilitenga zaidi ya Shilingi Bilioni 1.49 kwa ajili ya ujenzi wa ta...
18/09/2024

Mwaka 2022/23 Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Kibondo ilitenga zaidi ya Shilingi Bilioni 1.49 kwa ajili ya ujenzi wa tanki la maji la ujazo wa lita 1,500,000 ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 95.

Utekelezaji wa mradi huo unaolenga kutatua changamoto ya maji wilayani Kibondo na kuwawezesha wananchi kuboresha maisha yao kijamii na kiuchumi

Akizungumza leo Septemba 18, 2024 wilayani Kibondo mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa tanki hilo, Dkt. Biteko amesema mradi huo wa maji unaojengwa na wataalam kwa kuwashirikisha vijana wa Kitanzania utasaidia kuounguza mgao na kuongeza muda wa upatikanaji wa maji kwa siku huku akiwataka wananchi wa Kigoma kulinda vyanzo vya maji.

“Awali maji yalikuwa machache na yenye tope kwa sababu ya kutokuwa na chujio, nataka niwaombe mnavyo vyanzo vya maji mvilinde, mkikata miti hovyo na kuchoma mashamba itasababisha ukame licha ya kuwa na tanki hili mvilinde vyanzo vya maji ili tupate maji kwa muda mrefu,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt. Biteko ametaja faida za mradi huo kuwa ni kuboresha huduma ya maji kwa kuongeza saa za upatikanaji maji kutoka saa nne hadi 12 kwa siku

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amewataka wananchi wa Kigoma kushik**ana na kujiepusha na migogoro na badala yake washirikiane ili kuendelea kujiletea maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya uendelezaji wa miradi na miundombinu ya maendeleo Mkoani Kigoma.

18/09/2024

Jumla ya Tsh bilioni 67 zimezalishwa na wakulima wa Tumbaku katika Halmashauri ya Manispaa ya Ushetu kutoka katika bero 204,329.10 ambayo ni sawa na Kilogramu milioni 10 zilizozalishwa na wakulima hao.

Hayo yameelezwa leo Septemba 18, 2024 na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani alipokuwa akizungumza na wakulima wa halmashauri hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Waziri wa Kilimo, Hussein Muhamed Bashe.

Aidha, Cherehani alieleza licha ya kazi kubwa inayofanyika bado mzigo wa madeni umekuwa kwa wakulima, hivyo aliiomba wizara kusaidia wakulima kuondokana na madeni hayo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Umefanya mengi kwenye korosho, umefanya mengi kwenye Pamba, umefanya mengi kwenye chai fanya tena kwenye chai fanya jingine kwenye tumvaku mzigo wa miti wakashughulikie wanunuzi wa tumbaku kwa gharama zao sio kwa gharama za wakulima,” amesema Cherehani.

.

S/O
18/09/2024

S/O

Zile kashikashi zote wanazokutana nazo mabinti na wakina mama wa Kimwera, Wamachinga, Wamatumbi na Wangido wakati wa kuf...
18/09/2024

Zile kashikashi zote wanazokutana nazo mabinti na wakina mama wa Kimwera, Wamachinga, Wamatumbi na Wangido wakati wa kufuata maji visimani hazijawahi kuwapendeza wakazi wa Lindi, adhma ni kuzigeuza historia na inaelezwa kuwa tayari harakati za kumtua mama ndoo kichwani zimeshaanza, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa maji na maji kuwa mwa mwa mwa, harakati hizi zimefikia katika kiwango gani ? ndicho kilichoileta timu ya taifa katika kazi maalumu mkoani hapa kesho kuanzia 12:30 mpaka 4:00 za asubuhi live on .

Wananchi wa Mtwara wilaya ya Tandahimba wamshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Sul...
18/09/2024

Wananchi wa Mtwara wilaya ya Tandahimba wamshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogezea Huduma za kibingwa na Bingwa Bobezi karibu na kuwawezesha kutosafiri umbali mrefu kufuata Huduma.

Shukrani hizo zimetolewa leo na baadhi ya Wananchi walio jitokeza kupata Huduma kwa madaktari bingwa wa Rais Samia walioweka kambi ya siku Sita katika halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara.

Miongoni mwa wakazi waliofika katika Hospitali ya Mji Nanyamba, ni Mohammed Issa (29) ambaye amempongeza Rais Samia kwa hatua ya kuwafikia wananchi wa ngazi ya msingi ukizingatia wao kipato chao ni cha chini na Huduma hizi za kibingwa na bingwa bobezi ili waweze kuzipata ilikuwa wasafiri umbali wa mwendo mrefu na kutumia gharama kubwa kufata Huduma hizo.

“Hakika kambi hii ya ujio wa Madaktari Bingwa wa Mama Samia kutufikia katika maeneo yetu ni ishara tosha ya utendaji mzuri na uwajibikaji wa kiongozi wetu kwa wananchi wake ili kuhakikisha tunakuwa na afya bora kwajaili ya kuendelea kulitumikia taifa kwa shughuli za utafutaji wa maendeleo”, ameeleza Ndugu Issa.

Kwa upande wake Bwana Hamisi Malela Mnandaje (47) mkazi wa Wilaya ya Tandahimba ametoa wito kwa wananchi wenzake kuhakikisha wanakata bima ya afya mara baada ya mauzo ya zao la korosho ili kuwa na uwakika wa matibabu kwani serikali chini ya uongozi wa Rais Samia umefanya uwekezaji mkubwa katika sekya ya afya ikiwemo kuhakikisha madaktari bingwa na bingwa Bobezi wanafika katika ngazi ya msingi na wananchi waweze kupata Huduma hizo katika maeneo yeo.

NEWS FLASH HEADLINES•     Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Mke wa Mtoto wa Mfalme wa Uingereza,Iku...
18/09/2024

NEWS FLASH HEADLINES

•     Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Mke wa Mtoto wa Mfalme wa Uingereza,Ikulu Jijini Dar es Salaam.

·       Taasisi za serikali kuongoza katika ukwepaji wa malipo ya kodi

·        Kiongozi Mkuu wa Chama cha  ADC Taifa,ataka wananchi kujiandikisha ili kupata haki ya kushiriki uchaguzi kwa kumchagua kiongozi wanaemtaka.

·       Hezbollah yasema italipiza kisasi dhidi ya Israel baada ya shambulio la vifaa vya mawasiliano.

ndie mwenye dhamana ya jioni za Radio ya Watu kuanzia 12:00 đź•›

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema miradi ya kimkakati inayoendeshwa ...
18/09/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema miradi ya kimkakati inayoendeshwa Zanzibar inahitaji kuzingatia wakati katika utekelezaji wake ili kuleta tija kwa Taifa

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipokutana na Ujumbe wa watendaji kutoka Kituo cha Nishati cha Oman uliofika kuelezea hatua za miradi wanayoisimamia hapa Zanzibar ukiwemo miradi ya Maji, Nishati na ukarabati wa Mji Mkongwe ambao ni urithi wa dunia.

Rais Dk. Mwinyi ameuhakikishia ujumbe huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itawapa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha miradi hiyo aliyoielezea kuwa na umuhimu mkubwa kwa Uchumi wa Zanzibar, maendeleo na ustawi wa wananchi wake.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo hicho, Abdallah Humaid Al Ma’amary alisema, moja ya maboresho ya Mji Mkongwe ni kuufanya kuwa mji wa kisasa (Smart City) bila kuharibu uhalisia wa mji huo na kuzingatia vigezo na miongozo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuwa ni urithi wa dunia na kielelezo muhimu cha historia ya Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Princess Sophie (Duche...
18/09/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) kwenye kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 18 Septemba, 2024.

Ni Tayana tena amerudi tena na safari hii anakutana uso kwa Uso na makachero wa Taifa kujadili masuala muhimu ya Kitaifa...
18/09/2024

Ni Tayana tena amerudi tena na safari hii anakutana uso kwa Uso na makachero wa Taifa kujadili masuala muhimu ya Kitaifa

Ikumbatie kuanzia 1:30


Ukipata nafasi ya kuandika mistari “verse” kuhusu Amani utaandika ujumbe wa aina gani?Makachero wa Taifa Leo wana Launch...
18/09/2024

Ukipata nafasi ya kuandika mistari “verse” kuhusu Amani utaandika ujumbe wa aina gani?

Makachero wa Taifa Leo wana Launch Wimbo wa Amani wenye chorus na Verse 1 tu inaitwa Verse ya amani.

Kwenye verse hiyo kachana vibaya mno halafu kapita na Sauti ya nyuma (back vocal) kisha kaumiza mbaya kwenye Chorus.


Punguzo la bei limenoga... na limenoga tena.Furahia young zee na   ukiwa na code ya kibeach beach ⛱️ tukitia na punguzo ...
18/09/2024

Punguzo la bei limenoga... na limenoga tena.
Furahia young zee na ukiwa na code ya kibeach beach ⛱️ tukitia na punguzo la bei kwa juu, na sio beach code tu, hadi viatu, vifaa, na vingine vingi.
Harakisha, ofa hizi hazitadumu kwa muda mrefu!

—————————
Piga simu đź“ž +255 692 558 888
đź“Ť Mayfair Plaza, Mikocheni

  | .Maisha marefu na mafanikio zaidi tunakutakia
18/09/2024

| .
Maisha marefu na mafanikio zaidi tunakutakia

27/09/2024 Venue: Little theater 🎭Ticket: 50k kwa 100k all on  Piga: 067 908 6100Cc:
18/09/2024

27/09/2024
Venue: Little theater 🎭
Ticket: 50k kwa 100k all on
Piga: 067 908 6100

Cc:

Address

Https://www. Facebook. Com/images/places/map/red-pin. Png
Dar Es Salaam
00255

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222781445

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Clouds TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Clouds TV:

Videos

Share

Nearby media companies


Other Media/News Companies in Dar es Salaam

Show All