📌 USIKOSE KUTAZAMA📌
🎬 BAMBO LA MTAA
📺 CLOUDS TV
🕤 3:30 USIKU
🗓️ALHAMISI, OKTOBA 03, 2024
#tcratz
#elimukwaumma
#nirahisisana
#klabuzakidijiti
#digitalclubs
#lesenikidijitali
#usalamamtandaoni
#mtandaonifursabakisalama
#bambolamtaa
KUNDO ASHUHUDIA MASHINE INAVYOVUNJA MIAMBA NA KUTOA MAJI NYAMIHANGA, BUHIGWE
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew ameshuhudia mashine inavyojaribu kuvunja miamba na kuweza kutoa maji katika kijiji cha Nyamihanga kilichopo Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma.
Kundo amesema dhamira ya Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji safi na salama.
Akiwa katika kijiji hicho Kundo amewatoa hofu wananchi kuwa katika mradi wa visima 900 vitachimbwa vyote na hakuna kijiji kitakosa maji, na katika wilaya ya Buhigwe visima vitano vitachimbwa.
"Kuna dhana ya baadhii ya watu wanaendelea kupotosha kuwa magari ya rais yanayochimba maji ni mabovu nitoe rai hawa ni wapotoshaji kwakuwa wanaona hahajafika kwao wanatafuta vikwazo,na sisi Kama Wizara ya Maji bado tunashughulikia yale maeneo ambayo yana uhaba zaidi na lengo ni kuhakikisha maeneo yote nchini yanapata huduma ya Maji"amesema Kundo
@engkundo
@wizarayamajitz
*"HADI JUNI 2024 DIRA ZA MALIPO YA MAJI KABLA ELFU 14,914 ZIMEFUNGWA" KUNDO*
*Dodoma- Bungeni*
WIZARA ya Maji imesema imeendelea na ufungaji wa dira za malipo kabla (Pre paid Water Meters) ambapo hadi kufikia mwezi Juni, 2024 jumla ya dira 14,914 zilikuwa zimefungwa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini pamoja na RUWASA.
Kati ya dira hizo, dira 11,861 zilifungwa kwa Mamlaka za Maji za Miji Mikuu ya Mikoa, dira 325 zilifungwa na Mamlaka za Miradi ya Kitaifa, dira 692 zilifungwa na Mamlaka za Maji za Miji Mikuu ya Wilaya, na dira 50 Mamlaka za Miji Midogo.
Hayo yamesemwa leo Septemba 6,2024 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la mbunge wa viti Maalum Dorothy Kilave, aliyeuliza Serikali ina mkakati gani wa kuweka Mita za Maji kama za LUKU ili kuwawezesha Wananchi kulipa bili za maji kulingana na matumizi.
Mhandisi Kundo amesema kwa upande wa vijjijni jumla ya dira 1,986 zilifungwa kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO).
"Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali inakamilisha uandaaji wa andiko Dhana (Concept Note) pamoja na Mpango Mkakati sambamba na kutengeneza mfumo wa ankara wa kuendesha dira za malipo ya kabla ifikapo Julai, 2025"
"Aidha, Serikali inaendelea kusimamia, kusisitiza na kuziwezesha Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira pamoja na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha zinaongeza kasi ya ufungaji wa dira za malipo kabla ili kuwawezesha wananchi kulipa ankara za maji kulingana na matumizi na kuboresha usimamizi wa mauzo na makusanyo" amesema Mhandisi Kundo
Mwisho
*SERIKALI YAJIDHATITI KUKARABATI SKIMU YA NYANGANGA KIGOMA*
KATIKA kutatua changamoto ya ukosefu wa Maji katika Kijiji cha Nyanganga Kata ya Kazuramimba iliyopo Mkoani Kigoma Serikali imesema itakarabati Skimu ya Nyanganga kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 ili kurejesha ufanisi wake wa kuhudumia wananchi wa kijiji hicho.
Hayo yamesemwa leo Septemba 4,2024 na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la mbunge wa Kigoma Kusini Nashoni Bidyanguze, aliyeuliza lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha Mradi wa Maji uliokwama kwa muda mrefu Kijiji cha Nyanganga Kata ya Kazuramimba iliyopo Kigoma.
"Skimu ya Maji ya Kijiji cha Nyanganga iliyopo Kata ya Kazuramimba Wilaya ya Uvinza ilijengwa mwaka 1994 kwa lengo la kuhudumia wananchi 4,378 kwa wakati huo,
"Kwa sasa mahitaji ya maji katika Kijiji hicho yameongezeka na kufikia lita 178,340 kwa Siku kutokana na ongezeko la watu kufikia 8,917 mwaka 2024 sambamba na kuchakaa kwa miundombinu ya maji ya
Skimu hiyo iliyodumu kwa takribani miaka 30 sasa"amesema Mhandisi Kundo
Mhandisi Kundo amesema kazi zinazotarajiwa kutekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ukarabati wa tanki lenye ujazo wa lita 150,000, ukarabati wa mtandao wa mabomba umbali wa kilometa 3.2 na ukarabati wa vituo 10 vya kuchotea maji.
Hata hivyo inaaelezwa kuwa kazi ya ukarabati wa Skimu hiyo inatarajiwa kuanza kufanyika mwezi Oktoba, 2024.
Mwisho
📌Msingi wa Uchumi wa Kidijiti unajengwa na maandalizi yanayohusisha matumizi chanya ya fursa zinazoletwa na TEHAMA.
📌Ewe mwanafunzi, tembelea digitalclubs.tz LEO kujiunga na klabu ya kidijiti uipendayo au kuanzisha klabu yako.
#tcratz #digitalclubs #klabuzakidijiti #digitaleconomy #uchumiwakidijiti #elimukwaumma
Mhe. Kigwangala na wananchi wa Nzega wamaamua kusema #NasimamanaSamia kwa mambo mazuri na mema ambayo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyafanya kwa Tanzania ikiwepo kudumisha amani, maridhiano, maelewano na kuijenga Tanzania. #Kaziiendelee
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mtandao ni fursa ya AJIRA , chagua FURSA.
#usalamamtandaoni #cybersafety #cybersecurity #tcratz #ajira #mtandaonifursabakisalama
Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
📌Karibu Tukuhudumie📌
📞 0800008272 Bure
📥 [email protected]
#ijuetcra #tcratz #kaziiendelee #hudumakwawateja
Tembelea mfumo wa Huduma za Mawasiliano kwa njia ya mtandao "Tanzanite Portal" kupitia https://tanzanite.tcra.go.tz ili kujisajili na kutuma maombi ya leseni au kuhuisha leseni iliyoisha muda wake.
#tcratz #tanzaniteportal #hudumazamawasiliano #lesenikidijitali
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari, akitoa huduma kwa watumiaji na wateja wa mawasiliano katika banda la TCRA, viwanja vya Dimani, Nyamanzi - Zanzibar. Maonesho yalianza rasmi tarehe 10 Januari, 2024 na kuzinduliwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
TCRA inakaribisha wadau wa sekta ya mawasiliano kutembelea banda letu kupata elimu kuhusu Sekta ya Mawasiliano.
Kaulimbiu: "Biashara Mtandao kwa Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji."
#tcratz #mapinduziday #digitaleconomy #uchumiwakidijiti #elimukwaumma
Usikose kufuatilia kipindi mbashara kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii, kufahamu zaidi kuhusu leseni mpya ya Utoaji wa huduma za Usalama Mtandaoni
🔴MBASHARA
📅: 22 DESEMBA, 2023
🕰: SAA 12 JIONI
📺: YouTube, Facebook & Instagram @tcra_tanzania
USIKOSE!🔥🔥
#lesenikidijitali #hapohapoulipo #tcratz #tanzaniteportal #usalamamtandaoni #cybersecurity
📌MAFANIKIO MAKUBWA MATANO (5) YA TANZANIA KWENYE MKUTANO MKUU WA ITUWRC23:📌
1. Kupata Obiti mpya ya Satelaiti nyuzi 16° Magharibi (W) itakayowezesha Huduma za Utangazaji.
2. Kupata masafa mapya yatakayowezesha huduma ya intaneti ya kasi (5G) na kuendelea, kuchagiza Uchumi wa Kidijiti.
3. Kulinda matumizi ya Televisheni za Kidijitali kwenye bendi ya UHF ambayo ni masafa ya huduma za utangazaji kupitia mitambo ya kusimikwa ardhini (DTT).
4. Kupata nafasi ya kuweka angani kilometa 20 hadi 50 kutoka Usawa wa Bahari vifaa vitakavyowezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti maeneo yote, hasa yasiyofikiwa.
5. Maeneo mapya ya utafiti ambayo yatawezesha kuboresha sekta ya mawasiliano hapa nchi.
#atu #tcratz #spectrum #masafa #ITUWRC #ITUWRC2023