Bibi yake Merysiana Melkzedeck, amefunguka kuwashukuru watanzania kwa jumla waliokuwa wakiwaombea kwa ajili ya kumpata mtoto Merysiana akiwa salama.
Mtoto huyo alipatikana jana, Januari 24, 2025 na kukabidhiwa kwa familia yake.
Video kamili ipo Youtube, Global TV!
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Treyzah, amefunguka kuhusu aina ya menejimenti anayoihitaji kupitia mazungumzo ya simu kwenye kipindi cha Funky Friday cha 255 Global Radio. Akizungumza kwa njia ya simu, Treyzah alisema anahitaji menejimenti itakayoweza kuwekeza na kutoa pesa nyingi ili kuendeleza kazi yake ya muziki na kufikia malengo yake makubwa.
Video kamili ipo YouTube ya Global TV.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Tanzania inazalisha umeme megawati 3,410 zaidi ya mahitaji ya kawaida ikilinganishwa matumizi ya megawati 1, 880 ambapo kwa sasa wameanza kujenga miundombinu ili kusafirisha umeme kutoka bwawa la Mwalimu Nyerere kwenda nchi ya Kenya na Zambia.
Msigwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika hifadhi ya Mikumi na kuongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya kusambaza umeme ndani ya nchi ili kuondoa kukatika umeme.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers #msigwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Kikosi maalum cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi kinaendelea na operesheni ya kuwatafuta na kuwaokoa wavuvi katika Ziwa Rukwa ambapo kufikia leo Januari 25, 2025 saa tisa mchana, miili ya wavuvi 8 imeopolewa.
Bashungwa akiwa ameambata na Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede kutoa pole kwa wananchi wa Nankanga, ameeleza kuwa kufuatia upepo mkali uliotokea mnamo Januari 23, 2025 na kuwakuta wavuvi 550 wakiwa katika shughuli zao ambapo jitihada za awali zilifanikiwa kuwaokoa wavuvi 540 wakiwa salama.
“Kwa taarifa tulizozipata sasa, pamoja na jitihada nzuri za mafanikio tuliyopata ya kuokoa ndugu zetu 540 ambao tumewaokoa kutoa ziwani kutokana na takwimu tulizokuwa nazo jana, lakini bahati mbaya kwa taarifa nilizo nazo sasa kutoka kwa wanaonendelea ukoaji ziwani tumewapoteza ndugu zetu saba” ameeleza Bashungwa saa sita mchana.
Bashungwa ameeleza zoezi za ukoaji linaendelea likiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga ambaye anatumia helkopta kuwasiliana vikosi maalum vya uokoaji ambao wanashirikiana na wananchi ambao wana jumla ya vyombo 19.
Bashungwa ametoa wito kwa wananchi kufuatilia na kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa sababu Rais, Dkt. Samia ameiwezesha mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa na vifaa vya kisasa vinavyotoa taarifa za uhakika kwa wakati.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga ameeleza kuwa Oparesheni ya Ukoaji inaendelea vizuri kwa kuhakikisha wavuvi wote waliokuwa ziwani wanapatikana wakiwa hai au kupata miili yao.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Babu wa mtoto Merysiana Melkzedeck, amefunguka kuhusu namna alivyokuwa akimtafuta mjukuu wake katika maeneo ya vichakani kwa kufyeka nyasi pamoja na sehemu zenye mashimo.
Mtoto huyo alipatikana jana, Januari 24, 2025 na kukabidhiwa kwa familia yake.
Video kamili ipo Youtube, Global TV!
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Msanii wa muziki wa BongoFleva nchini, Tryezah ameeleza kupitia kipindi cha Funky Friday kuwa kuna baadhi ya wasanii wanapaswa kupunguza kiki ili kuweza kuwa kioo katika jamii nzima.
Video kamili ipo YouTube ya Global TV
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amedai kuwa katuni ya mchoraji maarufu na mtangazaji, Masoud Kipanya iliyosambaa mitandaoni ni 'dongo' kwa wapinzani wao, Simba kwa sababu inasomeka T5 ikiwa ni ukumbusho wa mabao matano ambayo Yanga iliwafunga Simba.
Nini maoni yako? Weka comment yako 👇
Bonanza la Bunge linatarajiwa kufanyika Februari Mosi, 2025 jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge zilizopo Posta jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza ambaye pia ni Mbunge wa Makete, Festo Sanga amesema kuwa bonanza hilo litajumuisha wabunge wa Bunge la Tanzania ambao pia ni mashabiki wa timu za Simba na Yanga.
Pia amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuimarisha uhusiano kati ya wabunge na taasisi nyingine.
Video kamili ipo YouTube ya Global TV
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji nchini, Undare Mtaki @undareymtaky kutoka National Arts Auction, anatarajiwa kupiga mnada wa picha ya kuchorwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan, tarehe 8 Februari 2025 katika Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam.
Mtaki @undareymtaky ni mmoja wa vijana waliofaidika na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kufungua fursa kwa vijana wenye vipaji, hususan katika sekta ya sanaa, na kuwapa masoko ya kazi zao ndani na nje ya nchi.
Video kamili ipo YouTube ya Global TV
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Chamata Association Tanzania imeandaa kongamano la Samia na Miradi lenye lengo la kuwakutanisha wadau na wananchi kumpongeza na kusheherekea tarehe ya kuzaliwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katibu wa Chamata Peter Christopher amebainisha kuwa wadau mbalimbali watakuwepo kujadili maendeleo ambapo Kongamano hilo litafanyika siku ya kesho jumapili tarehe 26, januari mwaka 2025 katika ukumbi City Center Hall, Soko la Magomeni jijini Dar es Salaam.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
Msanii maarufu wa uchekeshaji wa jukwaani (Stand-Up Comedy) kutoka kambi ya Watubaki, Kipotoshi, amempongeza kwa dhati staa mwenzake kutoka kambi ya Cheka Tu, Leonardo, kwa uwezo wake mkubwa wa uandishi wa vichekesho.
Akizungumza kuhusu Leonardo, Kipotoshi alisema:
"Leonardo ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuandika. Anafikiri sana nje ya boksi, na kwa kweli hilo ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa ananizidi."
Kuhusu tuzo za Tanzania Comedy Awards ambazo zinatarajiwa kutolewa Februari 14 mwaka huu, Kipotoshi aliongeza:
"Tuzo hizi zitatusaidia kupewa heshima tunayostahili na pia kufungua milango ya taasisi kubwa kuwekeza kwetu bila hofu."
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
#Globaltv #globaltvupdates #globaltvonline #255globalradio #globalpublishers
#TanzaniaComedyAwards #StandUpComedy #Watubaki #ChekaTu