Lusabara

Lusabara Tired of feeling lost in the marketing maze? Ready to unlock the power of strategic funnels?

The Sales Funnel Strategist and Digital Marketing Expert for Serious Creators, Small Business Owners, and Companies Who Want to Turn Their Facebook Profiles into Lead Generation Machines. I help small businesses, creators, and coaches ditch the overwhelm and ignite explosive growth through strategic funnel design and automation.

๐ˆ๐ฆ๐š๐ ๐ข๐ง๐ž:

โ†ณ Effortlessly capturing leads with high-converting funnel

s.
โ†ณ Nurturing those leads with automated email sequences.
โ†ณ Transforming clicks into customers on autopilot.
โ†ณ We craft beautiful, data-driven funnels that do the heavy lifting for you. Here's what you can expect:

โ†ณ ๐ˆ๐ง๐œ๐ซ๐ž๐š๐ฌ๐ž๐ ๐œ๐จ๐ง๐ฏ๐ž๐ซ๐ฌ๐ข๐จ๐ง๐ฌ: We obsess over optimizing your funnel for maximum results.
โ†ณ ๐’๐š๐ฏ๐ž๐ ๐ญ๐ข๐ฆ๐ž: Focus on what you do best while your funnels work for you 24/7.
โ†ณ ๐‘๐ž๐๐ฎ๐œ๐ž๐ ๐ฌ๐ญ๐ซ๐ž๐ฌ๐ฌ: Say goodbye to marketing headaches and hello to a streamlined system. Follow me for insights on:

โ†ณ ๐Œ๐š๐ซ๐ค๐ž๐ญ๐ข๐ง๐ : Direct response, sales funnels, and conversion optimization strategies.
โ†ณ ๐ƒ๐ž๐ฌ๐ข๐ ๐ง & ๐๐ซ๐š๐ง๐๐ข๐ง๐ : Crafting captivating visuals for both personal brands and SaaS.
โ†ณ ๐€๐ˆ ๐€๐ฎ๐ญ๐จ๐ฆ๐š๐ญ๐ข๐จ๐ง: Leveraging technology to streamline your marketing efforts. Click my name, hit follow, and get ready to watch your business take off!

92% ya wafanyabiashara hutumia maneno haya angalau mara moja kwa wiki...Na, nina uhakika, unatumia angalau mojawapo!Leo,...
14/04/2024

92% ya wafanyabiashara hutumia maneno haya angalau mara moja kwa wiki...

Na, nina uhakika, unatumia angalau mojawapo!

Leo, nitakushirikisha maneno 5 ambayo unapaswa kuepuka kabisa katika mauzo, pamoja na mbinu bora za kutumia badala yake.

1๏ธโƒฃ ๐—๐—ฒ, ๐˜„๐—ฒ๐˜„๐—ฒ ๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜†๐—ฒ ๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐˜†๐—ฒ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ฎ๐—บ๐˜‚๐˜‡๐—ถ?
Maneno haya yanaweza kuonekana k**a dharau kwa mteja, na yanaweza kumfanya ahisi k**a hajathaminiwa.

Badala yake, uliza kwa heshima: "๐‘ต๐’Š ๐’๐’‚๐’๐’Š ๐’Ž๐’˜๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’๐’† ๐’‚๐’•๐’‚๐’‰๐’–๐’”๐’Š๐’Œ๐’‚ ๐’Œ๐’‚๐’•๐’Š๐’Œ๐’‚ ๐’Ž๐’„๐’‰๐’‚๐’Œ๐’‚๐’•๐’ ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’‡๐’‚๐’๐’š๐’‚ ๐’–๐’‚๐’Ž๐’–๐’›๐’Š?"

Hii itakusaidia kujenga uhusiano na watu wote wanaohusika na ununuzi.

2๏ธโƒฃ ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ฎ๐—ต๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฐ๐—ต๐—ฒ๐—น๐—ฒ๐˜„๐—ฎ.
Kuomba msamaha kwa kuchelewa kunashusha hadhi yako na kuonyesha kutokuwa na mtaalamu.

Badala yake, shukuru mteja kwa uvumilivu wake na ueleze kwa ufupi sababu ya kuchelewa.

Kwa mfano, unaweza kusema, "๐‘จ๐’”๐’‚๐’๐’•๐’† ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’–๐’—๐’–๐’Ž๐’Š๐’๐’Š๐’—๐’– ๐’˜๐’‚๐’Œ๐’. ๐‘ต๐’Š๐’๐’Š๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’‚ ๐’Ž๐’Œ๐’–๐’•๐’‚๐’๐’ ๐’˜๐’‚ ๐’…๐’‰๐’‚๐’“๐’–๐’“๐’‚, ๐’๐’‚๐’Œ๐’Š๐’๐’Š ๐’๐’Š๐’Œ๐’ ๐’‰๐’‚๐’‘๐’‚ ๐’”๐’‚๐’”๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’Œ๐’–๐’”๐’‚๐’Š๐’…๐’Š๐’‚."

3๏ธโƒฃ ๐—ง๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—น๐—ถ๐—ผ ๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฎ ๐—ฝ๐—ฒ๐—ธ๐—ฒ๐—ฒ.
Maneno haya yanaweza kuonekana k**a ya kiburi na ya kujisifu, na yanaweza kumfanya mteja ahisi k**a hafai. Badala yake, zungumza kuhusu thamani unayoweza kuleta kwa mteja na jinsi unaweza kumsaidia kufikia malengo yake. Kwa mfano, unaweza kusema, "๐‘ต๐’Š๐’๐’‚ ๐’–๐’‰๐’‚๐’Œ๐’Š๐’Œ๐’‚ ๐’•๐’–๐’๐’‚๐’˜๐’†๐’›๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’Œ๐’–๐’”๐’‚๐’Š๐’…๐’Š๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’‡๐’Š๐’Œ๐’Š๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’๐’†๐’๐’ˆ๐’ ๐’š๐’‚๐’Œ๐’ ๐’š๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’–๐’›๐’ ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’๐’๐’ˆ๐’†๐’›๐’‚ ๐’–๐’‡๐’‚๐’๐’Š๐’”๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’‚๐’Ž๐’‘๐’†๐’๐’Š ๐’›๐’‚๐’Œ๐’ ๐’›๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’”๐’๐’Œ๐’.

4๏ธโƒฃ ๐—๐—ฒ, ๐˜‚๐—ป๐—ด๐—ฒ๐—ฝ๐—ฒ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ๐˜€๐—ถ?
Maneno haya yanaonekana ya kitoto na hayana ufanisi. Badala yake, tumia mbinu ya kufunga mkataba ki-makisio na muulize mteja kuhusu njia yake ya malipo. Kwa mfano, unaweza kusema,

๐‘ฑ๐’†, ๐’–๐’๐’ˆ๐’†๐’‘๐’†๐’๐’…๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’๐’Š๐’‘๐’‚ ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’๐’‹๐’Š๐’‚ ๐’š๐’‚ ๐’”๐’Š๐’Ž๐’– ๐’‚๐’– ๐’ƒ๐’†๐’๐’Œ๐’Š?

5๏ธโƒฃ ๐—ช๐—ฎ๐˜€๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐—ป๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐˜†๐—ฎ, ๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜€๐—ถ๐˜€๐—ถ.
Kusema vibaya kuhusu washindani wako sio tu unprofessional, lakini pia ni hatari. Inaweza kumfanya mteja ahisi k**a hauna uhakika na bidhaa au huduma zako.

Badala yake, zingatia faida za kipekee za kampuni yako na jinsi unavyoweza kumsaidia mteja kwa njia ambayo washindani wako hawawezi.

๐‘ด๐’˜๐’‚๐’„๐’‰๐’† ๐’Ž๐’•๐’†๐’‹๐’‚ ๐’‚๐’‚๐’Ž๐’–๐’† ๐’Ž๐’˜๐’†๐’๐’š๐’†๐’˜๐’† ๐’Œ๐’‚๐’Ž๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’๐’† ๐’๐’Š ๐’˜๐’‚๐’ƒ๐’‚๐’š๐’‚!

Umependa post hii?

Ninaposti ujumbe k**a huu kila siku ili kukusaidia kupata pesa nyingi zaidi mtandaoni!

Usikubali kukosa mbinu zangu zijazo, ni-follow na ushinde!

Mwaka huu wa 2024, jina la Bernard Arnault limekuwa likisikika kila mahali. Akiwa mtu tajiri zaidi duniani, hadithi yake...
13/04/2024

Mwaka huu wa 2024, jina la Bernard Arnault limekuwa likisikika kila mahali. Akiwa mtu tajiri zaidi duniani, hadithi yake ya mafanikio imewavutia wengi nikiwamo mimi binafsi.

K**a kawaida yangu nikashawishika kujua wasifu wake, aina ya biashara anazofanya, tabia yake, n.k.

Nimejifunza mambo kadhaa ambayo natamani ningalimbiwa nikiwa na miaka 20. Kwa wadogo zangu, tafadhali, msichulie poa. Yako mengi niliojifunza, hapa nitashirikisha machache.

Bernard amefikia kuwa mtu tajiri zaidi duniani kwa kuzingatia kabisa BIASHARA MOJA, akapata utajiri MKUBWA kisha kutumia utajiri huo kueneza biashara zake.

Ngoja nieleze:

Baba yake alikuwa mtu wa tabaka la kati na mmiliki wa kampuni ndogo ya Uhandisi - Ferret-Savinel.

Arnault alihitimu kutoka moja ya shule bora ya Uhandisi nchini Ufaransa mwaka 1971 na mara moja akaanza kufanya kazi katika kampuni ya baba yake ambayo ilikuwa inafanya vizuri 'kiasi'.

Kampuni hiyo ilikuwa na idara 2 - ujenzi wa viwanda na milki kuu (Real Estate).

Baada ya miaka 3 ya kufanya kazi kwa baba yake, alimshawishi baba yake kuuza idara ya ujenzi wa viwanda kwa Quillery na kutumia pesa hizo kuingia kikamilifu katika Milki Kuu (KULENGA, a.k.a FOCUS).

Baada ya uuzaji huo, Ferret-Savinel ilibadilisha jina lake, kuwa Ferinel, ikalenga soko la milki kuu, na ikaanza kuongeza miradi yake.

Aliweka nguvu zake zote katika BIASHARA MOJA hiyo akifanya kazi mchana na usiku kutoka 1971 hadi 1984 (miaka 13) na kuikuza kutoka kampuni inayohangaika kuwa biashara yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja.

Sasa ana utajiri na connections na anaweza kueneza biashara zake.

Wakati yote haya yakiendelea, kampuni ya anasa (wamiliki wa Dior), Boussac Saint-Frรจres ilikaribia kufirisika na serikali ya Ufaransa ilikuwa ikimtafuta mtu wa kuichukua... Arnault aliona fursa hiyo, akanunua kampuni nyingine ya anasa na kutumia kampuni hiyo kushinda zabuni na kuchukua Boussac.

Boussac ilikuwa na idara 5:

โ†’ Gazeti (L'Aurore)
โ†’ Rejareja (Conforama)
โ†’ Anasa (Dior)
โ†’ Supermarket (Le Bon Marchรฉ)
โ†’ Kiwanda cha Napkin (Peaudouce)
โ†’ Kiwanda cha nguo
โ†’ Kiwanda cha kuunganisha nguo
โ†’ Kiwanda cha karatasi
โ†’ nk pamoja na usafirishaji na chakula/kilimo.

Unajua kitu cha kwanza Arnault alichofanya alipochukua uongozi?

Aliuza karibu mali yote ya kampuni, akabaki na Christian Dior tu (KULENGA)

Kulenga huku kulifanya Boussac kutoka katika ufilisi hadi kutengeneza faida ya dola milioni 112 kwenye mtiririko wa mapato ya dola bilioni 1.9 katika miaka 3.

(Maono yalikuwa kujenga chapa kubwa zaidi ya anasa duniani na kwa hivyo wakati biashara ya milki kuu ilikuwa ikimvuruga kutoka kwa chapa ya anasa, baadaye aliiuza biashara ya milki kuu kwa CGE ambao waliibadilisha jina kuwa Nexity)

Ili kufikia ndoto yake ya chapa ya anasa, aliwekeza pesa taslimu ya dola bilioni 2.2 kununua 43% ya LVMH (Louis Vuitton/Moรซt Hennessy) kwa kufanya kazi na Alain Chevalier, Mkurugenzi Mtendaji wa Moรซt Hennessy, na Henry Racamier, rais wa Louis Vuitton. Baadaye alimfukuza Henry Racamier na kuchukua uongozi.

Leo anaendesha kampuni kubwa zaidi ya bidhaa za anasa duniani, ikiwa na zaidi ya chapa 75 zikiwa chini ya mwavuli wake.

VTY, hakuna katika chapa hizi 75 zilijengwa upya na yeye. Hizo ni chapa 75 zilizojengwa na wengine waliozingatia JAMBO MOJA na kulijenga kuwa kubwa vya kutosha kununuliwa na Arnault.

Mfano Claude Moรซt ambaye alitumia maisha yake katika kujenga kitu kimoja - chapa ya Moet zaidi ya miaka 280 iliyopita. Na Christian Dior ambaye alitumia maisha yake katika kujenga chapa moja miaka mingi kabla ya Arnault kuzaliwa.

Mbinu ya "Ku-FOCUS" na Mafanikio:

Mafanikio ya Arnault yanatokana na mbinu yake ya "Ku-FOCUS". Alielewa kuwa ili kufanikiwa, ni lazima aelekeze nguvu na rasilimali zake kwenye biashara moja na kuikuza hadi kiwango cha juu kabla ya kueneza uwekezaji wake. Hii ilimwezesha kuunda chapa zenye nguvu k**a vile Louis Vuitton, Dior, na Givenchy, ambazo zimekuwa alama za kifahari duniani kote.

Bw. Bernard Arnault anatupa somo gani?

Kuna masomo mengi muhimu tunayoweza kujifunza kutoka kwa maisha ya Bernard Arnault. Mojawapo ya muhimu zaidi ni umuhimu wa "Ku-FOCUS". Ili kufikia malengo yako, ni lazima uelekeze nguvu zako kwenye jambo moja na ujitahidi kulifanya vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Arnault pia anatuonyesha thamani ya uvumilivu na uvumilivu. Alichukua muda mrefu kujenga himaya yake ya biashara, na hakukata tamaa hata alipokumbana na changamoto.

Nahitimisha:

Bernard Arnault ni mfano wa kuvutia wa mtu aliyefikia mafanikio makubwa kwa bidii, kujitolea, na maono. Mbinu yake ya "Ku-FOCUS" ni ya thamani kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa viwango vyote. Ingawa baadhi ya watu wanaweza kumkosoa kwa mbinu zake za ukali za biashara, hakuna shaka kuwa ameacha alama yake isiyofutika kwenye tasnia ya bidhaa za anasa.

Hadithi ya Arnault inatukumbusha kuwa tuna uwezo wa kufikia chochote tunachotaka tukielekeza nguvu zetu na kujiamini kuwa tunaweza kufanikiwa. Tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa mbinu yake ya "Ku-FOCUS", uvumilivu, na kuazimia.

P.S: Unapokuwa na mayai machache tu, unapaswa kuyaweka kwenye kapu moja na hilo kapu likishakuzalishia mayai mengi, hapo ndipo unapoweza kuyatawanya.

I rest my case ๐Ÿ˜„

Kuna vijana wanaotangaza huduma ya kufuta madeni ya akaunti hizi, wakidai kuwa wanaweza kukusaidia kuepuka kulipa gharam...
12/04/2024

Kuna vijana wanaotangaza huduma ya kufuta madeni ya akaunti hizi, wakidai kuwa wanaweza kukusaidia kuepuka kulipa gharama za matangazo. ๐—›๐˜‚๐˜‚ ๐—ป๐—ถ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ฝ๐—ฒ๐—น๐—ถ!

Pengine nitoa ufafanuzi wa mfumo wa malipo wa Facebook kwa ufupi:

โ†ณ Kila akaunti, hata yako binafsi, inayotangaza au kuongeza machapisho, hupewa akaunti ya matangazo ("Ad Account") na Facebook.

โ†ณ Akaunti hii ya matangazo ni ya kibinafsi ("Personal Ad Account") na kumbukumbu za malipo yote ya matangazo huhifadhiwa hapa.

Mbinu Wanayotumia Hawa Ninaowaita Matapeli

1๏ธโƒฃ Wataunda akaunti ya biashara ya Facebook ("Facebook Business Manager") kwa ajili yako.
2๏ธโƒฃ Watakutengenezea "Ad Account" mpya, tofauti na ile ya kibinafsi.
โ—๏ธKumbuka akaunti hii mpya haina deni lolote la awali.
3๏ธโƒฃWataunganisha kurasa zako za Facebook na Instagram na akaunti hii mpya ya matangazo.

Hatari za Kutumia Mbinu Hii:

โ›”๏ธ Facebook haitasauhau deni la akaunti yako ya awali.
โ›”๏ธ Malipo wataendelea kujaribu kukata malipo yao kutoka akaunti yako ya awali.

Na hii inaweza kusababisha:

๐Ÿšซ Kufungiwa akaunti ya matangazo ("Ad Account") moja kwa moja au adhabu ya muda mfupi.
๐Ÿšซ Kufungiwa akaunti yako ya Facebook.
๐Ÿšซ Kufungiwa kurasa zako za biashara za Facebook na Instagram.
๐Ÿšซ Kufungiwa akaunti yako ya biashara ya Facebook ("Facebook Business Manager").

Unayopaswa Kuzingatia K**a Mfanyabiashara:

โœ… Mtandao ni sehemu muhimu ya biashara yako, k**a vile kodi ya pango au duka lako.
โœ… Kulipa deni ni muhimu, hata k**a matangazo hayakuleta faida ya moja kwa moja.

Nini cha Kufanya Unapodaiwa:

๐Ÿ“› Wasiliana na Facebook moja kwa moja kwa usaidizi.
๐Ÿ“› Lipa deni lako haraka iwezekanavyo.
๐Ÿ“› Epuka kujihusisha na watu wasiowaaminifu wanaotoa huduma za kufuta madeni.

P.S: Share ujumbe huu ili kuwasaidia wafanyabiashara wengine kuhusu utapeli huu.

Karibu wote ambao wamefanikiwa katika biashara na kuvuka kiwango cha mauzo ya dola milioni 1, wanakiri kwamba kufikia le...
11/04/2024

Karibu wote ambao wamefanikiwa katika biashara na kuvuka kiwango cha mauzo ya dola milioni 1, wanakiri kwamba kufikia lengo hilo kunaweza kuchukua miaka 10 au hata 20. Lakini mara tu unapofanikiwa kufikia hiyo, una uwezo wa kuzalisha kiwango kikubwa zaidi ndani ya mwaka mmoja.

Hii inatufundisha nini?

Inaonyesha kwamba mafanikio katika biashara yanahitaji zaidi ya juhudi na maarifa. Mtazamo na ujuzi ni muhimu sana. Haijalishi unafanya nini au kiwango cha elimu ulichonacho, bali ni jinsi unavyoiona biashara na jinsi unavyojenga njia yako ya kufikia malengo.

Kwa mfanyabiashara k**a wewe, ambaye ujuzi na mtazamo vimewezesha kutengeneza $1 milioni, ni muhimu kuwa na mpango wa mauzo uliothabiti.

Kwa mfano, ikiwa unauza bidhaa kwa bei ya dola 1,000, unahitaji kuuza bidhaa 1,000 tu ili kufikia kiwango cha dola milioni 1 katika mapato. Mara nyingi, unahitaji kuzidisha hilo mara mbili ili kupata faida.

Ingawa inaweza kuonekana k**a idadi kubwa, fikiria kwamba kampuni kubwa k**a Apple iliuza iPhones milioni 240 mwaka jana pekee. Pia, watumiaji milioni 112 wa Apple pia wanalipa kila mwezi kwa ajili ya kifurushi cha Apple Music na watumiaji milioni 44 wa Apple wanalipa kila mwezi kwa ajili ya kifurushi cha Apple TV.

Na jambo la kuvutia zaidi, wamefanya hivyo kwa kuzalisha faida kubwa. Kwa mwaka jana wa 2023 walitengeneza faida ya dola bilioni 97. (Hii sio jumla ya mapato bali ni faida yao halisi baada ya matumizi na kodi zote).

Hii inaonyesha kuwa tatizo sio pesa au bei, bali ni jinsi unavyojenga thamani na jinsi unavyowafikia wateja wako. Mauzo 1,000 yanaweza kukufikisha kwenye dola milioni 1. Lakini hata mauzo chini ya hiyo yanaweza kukusaidia kufikia mafanikio ya kifedha, hasa k**a lengo lako si kujenga kampuni kubwa sana.

Jambo muhimu: Wateja wananunua kulingana na thamani wanayoona. Ilibidi nijifunze hili kwa miaka mingi. Ni jukumu lako kuhakikisha kuwa bidhaa au huduma unayotoa ina thamani isiyopingika kwa wateja wako.

P.S: Unapobuni bidhaa au huduma, fikiria jinsi ya kuifanya iwe ya thamani isiyopingika kwa watu unaowalenga.

P.S.S: Mafanikio ya kibiashara yanahitaji zaidi ya juhudi na maarifa. Inahitaji mtazamo sahihi na mpango wa mauzo uliothibitishwa.

Jifunze jinsi ya kuunda mpango wa mauzo unaofaa kwa biashara yako na jinsi ya kuhakikisha kuwa bidhaa au huduma yako ina thamani isiyopingika kwa wateja wako.

Fuata akaunti hii kwa maelezo zaidi!

Nyakua mbinu yangu ya mauzo ndani ya sekunde 30Linapokuja suala la kuuza mtandaoni, ninalenga:90% kutoa thamani bila mal...
11/04/2024

Nyakua mbinu yangu ya mauzo ndani ya sekunde 30

Linapokuja suala la kuuza mtandaoni, ninalenga:
90% kutoa thamani bila malipo
10% kutoa suluhisho la malipo ya thamani ya juu.

Katika machapisho, natumia muundo wa mauzo ufuatao:
1. Kuvutia.
2. Tena, kuvutia.
3. Mara nyingine tena, kuvutia.
4. Onyesha tatizo.
5. Onyesha gharama ya kutolitatua tatizo.
6. Toa suluhisho la sehemu yenye thamani.
7. Tumia wito wa kuchukua hatua kwa watu wanaotaka nitatue hilo kwa ajili yao.

96% ya watengenezaji mahudhui mtandaoni huishia kukosa uvumilivu wa kuendelea kutengeneza machapisho yanayovutia wateja watarajiwa.

Mwanzoni, wanaanza kwa kasi na shauku. Lakini baada ya miezi michache, wanaanza kukata tamaa na kuacha.

Kwa nini?

Kwa sababu hawatumii mbinu sahihi ya kuunda machapisho.

Hapa ndipo kanuni ya 3F inapoingia:

โœ… Feel: Anza kwa kuamsha hisia za msomaji kwa kushiriki hadithi ya kibinafsi au mfano unaohusiana na tatizo.
โœ… Felt: Eleza jinsi wewe au wateja wako walivyokabiliwa na tatizo hilo na jinsi lilivyowaathiri.
โœ… Found: Toa suluhisho la tatizo hilo, ukionyesha jinsi livyowasaidia wewe au wateja wako kufanikiwa.

Mfano wa Matumizi ya Kanuni ya 3F:

โ†’ Feel: Nilianza safari yangu k**a mtengenezaji maudhui mtandaoni nikiwa na shauku kubwa. Nilitaka kusaidia watu na kubadilisha maisha yao kwa maarifa yangu.

โ†’ Felt: Lakini baada ya miezi michache, nilianza kukata tamaa. Nilikuwa nikipata wateja wachache sana na mauzo yangu yalikuwa ya chini.

โ†’ Found: Nilipogundua kanuni ya 3F, kila kitu kilibadilika. Nilianza kuunda machapisho yenye kuvutia zaidi na yenye ushawishi, na idadi ya wateja wangu watarajiwa ikaongezeka sana.

Matokeo:
Kwa kutumia mbinu hii ya mauzo ya 90/10 na mfumo wa mauzo wa machapisho, nimeweza kupata wateja wengi na kuongeza mauzo yangu kwa kiasi kikubwa.

Wito wa Kuchukua Hatua:
Je, uko tayari kuanza kutumia mbinu hii ya mauzo yenye ufanisi?

Anza leo kwa:

โœ… Kufuata kanuni ya 3F katika machapisho yako.
โœ… Kutoa thamani ya bure kwa wateja watarajiwa.
โœ… Kuwauliza wateja watarajiwa kuchukua hatua.

Teknolojia Nyuma ya ChatGPT Siyo Mpya!Teknolojia inayotumika kuendesha ChatGPT na programu nyingine nyingi za AI (Akili ...
10/04/2024

Teknolojia Nyuma ya ChatGPT Siyo Mpya!

Teknolojia inayotumika kuendesha ChatGPT na programu nyingine nyingi za AI (Akili Mnemba au Akili Unde) siyo mpya kabisa. Imekuwepo tangu kabla ya mwaka 2020.

Lakini, tulikuwa tumefungwa kwa sababu tulihitaji vitu viwili: data nyingi na mashine zenye uwezo wa hali ya juu.

Kisha, tukapata bahati nzuri na vyote viwili (data na mashine) na bam! GPT (ChatGPT) ilizaliwa, ikatuonyesha jinsi AI inaweza kuwa nzuri kweli. Lakini, ili kuzidi kuboresha uwezo wa AI, tulihitaji kitu chenye nguvu zaidi.

Na hii ndiyo habari njema: Nvidia imetoa chipu yenye uwezo mkubwa sana inayoitwa Blackwell ambayo imebadilisha kabisa mchezo linapokuja suala la machine, ikiwa na transista bilioni 208, ni mara 30 zaidi ya nguvu ya kawaida na ni nafuu mara 25 kuliko ile iliyokuwepo awali.

Nyakati za kusisimua zinakuja!

Pembeni: Ili kuelewa jinsi tumepiga hatua kubwa, fikiria hivi: redio ya mwanzo ilikuwa na transista karibu 9 tu, wakati iPhone ya kwanza ilikuwa na transista milioni 19โ€ฆ na sasa tuna macshine yenye transista bilioni 208 kwenye chipu moja.

Ugunduzi wa kyomputa hii, ni muhimu sana katika kufungua uwezo wa teknolojia ya kisasa na inatufungulia zama mpya za akili undi -AI.

Hata hivyo, wakati tunafurahia uvumbuzi huu, kwa upande mwingine inabua wasi wasi na maswali mengi miongoni mwa watu. Moja ya wasi wasi huo inatokana na uwezo wa AI jinsi inanvyotatua changamoto korofi ndani ya muda mfupi.

Wengi wanahoji, Je, AI itachukua kazi nyingi na kuwaacha watoto wetu bila ajira?

Hii ni swali linalowasumbua wazazi na walimu. Haina tofauti na hofu iliyoibuka wakati wa kuingia kwa calculators. Lakini, hebu tufanye tafakari kidogo kuhusu ukweli usiopingika: licha ya calculators, mafanikio ya binadamu katika sayansi na teknolojia yamefika viwango vipya.

AI, k**a ilivyo kwa calculators, itaendelea kuimarika. Kadri AI inavyosonga mbele, inatuwezesha kufikia viwango vya juu zaidi vya uwezo wa binadamu. Inakuwa kichocheo cha ukuaji, chombo kinachoongeza uwezo wetu badala ya kuupunguza.

Tukiangalia takwimu: AI tayari imeshabadilisha tasnia mbalimbali, kuanzia afya hadi usafiri, na kuwezesha mafanikio na uvumbuzi ambao hapo awali ulikuwa hauyumkiniki. Imefungua milango ya uvumbuzi mpya, ikitusaidia kutatua matatizo magumu na kupata suluhu kwa haraka zaidi kuliko hapo awali.

Kwangu sioni sababu ya kuwa na hofu kwamba AI itawafanya watoto wetu kuwa wajinga (dumb). Tujiandae kuukubali uwezekano wa kusisimua uliopo mbele yetu. Kadri AI inavyokua, itanoa akili zetu, itapanua uwezo wetu, na kuchochea ubunifu wetu.

Na kwa taarifa yako, utafiti uliofanywa na Forbes kupitia Dell Technologies & Institute of the future, umeonyesha kuwa 85% ya kazi zitakazokuwepo mwaka 2030 zitakuwa kazi mpya ambazo hazijawahi kutokea hapo awali.

Moja kati ya hizo kazi ni 'Prompt Engineer,' inayosadikika kuwa na kiwango cha juu cha mishahara kinachokadiriwa kuwa ni dola 360,000 kwa mwaka.

Kuhusu yajayo...

โ†ณ Je, unajua kuwa soko la AI linatarajiwa kufikia dola trilioni 150 ifikapo 2030? Hiyo ni sawa na Pato la Taifa la Marekani!

โ†ณ Zaidi ya kazi milioni 133 zitazalishwa na AI ifikapo 2030, na hii itasababisha ukuaji wa uchumi wa kimataifa.

โ†ณ AI itaokoa maisha milioni 36 kwa mwaka ifikapo 2030 kwa kusaidia kugundua magonjwa mapema na kuboresha matibabu.

P.S: Pengine nikuulize... Je, utafurahia kufanya kazi na mifumo ya AI k**a mimi?

Wakati ujao upo karibu!

Siku chache zilizopita, nimegundua ukweli fulani mgumu ambao umetikisa hisia na ufahamu wangu kuhusu ujasiriamali.Mmojaw...
09/04/2024

Siku chache zilizopita, nimegundua ukweli fulani mgumu ambao umetikisa hisia na ufahamu wangu kuhusu ujasiriamali.

Mmojawapo ni huu:

Vyanzo vingi vya mapato ni njia ya KUWEZA KUDUMISHA utajiri wako, sio njia ya KUPATA utajiri. Ili kupata mafanikio makubwa, unahitaji KULENGA (FOCUS).

Elon Musk ni mfano mzuri wa hili.

Ngoja nieleze.

Alikuwa akigonga codes (kuandika mfumo) kila usiku kwenye bidhaa/biashara MOJA iliyojulikana k**a Zip2 na kuifanya kuwa kubwa sana hadi waliweza kufunga mkataba na The New York Times na Chicago Tribune. Alifanya kazi kwa bidii kwenye biashara hiyo MOJA tu (hakuna kitu kingine) kutoka 1995 hadi 1999 na kuiuza kwa Compaq kwa dola milioni 307. Elon alipokea dola milioni 22 kwa hisa zake za asilimia 7 akiwa na umri wa miaka 28.

Mwaka huo huo (1999) alianzisha biashara yake ya pili: x /dot com, kampuni ya huduma za kifedha na malipo ya barua pepe ambayo baadaye iliunganishwa na continuity kuunda paypal. Alilenga kwenye biashara hiyo MOJA kwa mwaka mmoja uliofuata.

Sasa sikia hili: Mnamo Oktoba wa mwaka huo alifunga huduma zingine za kifedha za paypal ili kulenga tu kwenye malipo (KULENGA).

Ali-LENGA kwenye biashara hiyo MOJA (x/paypal) hadi alipoiuzia ebay kwa dola bilioni 1.5 mwaka 2002. (Alipokea dola milioni 175.8 kwa hisa zake za asilimia 11) akiwa na umri wa miaka 31.

Kwa sasa tayari ana utajiri na hivyo ameanza kupanua uwekezaji wake:

โ†ณ Alianzisha SpaceX mwezi Mei 2002 (na dola milioni 100 za pesa zake) na KULENGA Spacex pekee kwa miaka 2
โ†ณ Aliwekeza katika Tesla mwaka 2004
โ†ณ Aliwekeza katika Solarcity mwaka 2006 (baadaye aliinunua kwa zaidi ya dola bilioni 2 mwaka 2016)
โ†ณ Alikua bilionea mwaka 2012
โ†ณ Alikuwa mbia wa OpenAI mwaka 2015 na alitoa zaidi ya dola milioni 100
โ†ณ Ni mbia wa Neuralink mwaka 2016 (na dola milioni 100 za pesa zake)
โ†ณ Alianzisha The Boring Company mwaka 2017
โ†ณ Alinunua twitter kwa dola bilioni 44 mwaka 2022

Hitimisho: Alipata utajiri kwa KULENGA kwenye MOJA kisha akaendelea kuwa tajiri kwa kueneza uwekezaji wake.

Hii ndiyo mifumo sawa kwa WAJASIRIAMALI wengi waliofanikiwa katika kiwango cha kimataifa. Wanaweka nguvu zao zote kwenye kitu kimoja, wanatengeneza utajiri mkubwa na kisha kutumia utajiri huo kueneza uwekezaji wao.

Unapokuwa na mayai machache tu, unapaswa kuyaweka kwenye kikapu kimoja na kuwa na hicho kikapu kikuzalie mayai zaidi ili uweze kutotolesha kuku wengine wa kukupa mayai mengi zaidi.

Vipi katika mazingara yetu ya kiafrika na hususani Tanzania... Je, dhana hii inafanya kazi? NDIYO.

Nimesikiliza Mo Dewji katika moja ya mahojiano yake yaliyorushwa Feb 27, 2024 akisema kwamba, ni vigumu kufanikiwa Africa Mashariki kwa kuitegemea biashara moja k**a ilivyo ilivyo kwa nchi za ulaya na Marekani.

Je, yuko sahihi? NDIYO yuko sahihi 100%

Lakini pamoja na kwamba ushari wake ni yakinifu, bado hatupaswi kuukumbatia kwa upofu. Inabidi turudi nyuma, tuchimbe msingi wa maoni yake umeegemezwa wapi.

Katika Instagram LIVE, aliyoifanya usiku wa tarehe 7 April 2024 alisema kwamba biashara yao ilianzishwa na bibi yake, ikaendelezwa na baba yake, na yeye amepokea kijiti hicho kutoka kwake.

Biashara anayoisimamia sasa, ni ya kizazi cha tatu toka ianzishwe. Swali la msingi kujiuliza ni Je, mwanzilishi wa hiyo biashara alianza kwa kuitawanya? Jibu ni HAPANA. Wa pili (baba yake) aliyepokea kijiti, Je aliitawanya? Pengine ALIWEKA MISINGI, maana yupo katika orodha ya walionunua mashamba na viwanda wakati ule raisi Mkapa wa ubinafsishaji.

Kwa upande wake Mo Dewji, ameipokea ile biashara tayari ikiwa na msingi imara na akaipeleka mbali zaidi. Na ameahidi ataipeleka IPO na kisha kustaafu k**a mkurenzi mtendaji. Successor wake ataifikisha wapi? Mimi na wewe hatujuhi. Hata hivyo haituhusu๐Ÿ˜…

Ngoja tuzungumzie yanayotuhusu. Hasa mimi na wewe ambao hatujapokea kijiti cha aina yoyote kutoka kwa watangulizi wetu. K**a umebahatika wakakupeleka shule, pia mshukuru Mungu. Wengine hatuna hizo report cards za shule.

Kwa mazingira yetu ya Kitanzania, hatuwezi kuwa k**a Elon. Hilo tusahau ๐Ÿฅฒ

Akiwa anazungumzia hali ya elimu na siasa katika kipindi cha mahojiano na Salama kilichorushwa Mar 13, 2023, Prof Anna Tibaijuka alihibua hoja ya msingi iliyomuacha Salama katika kicheko...

Aliuliza, "Hivi huyu Mark Zuckerberg angelikuwa m-Tanzania, tungempa leseni ya kuendesha Facebook?"

Majibu unayo mwenyewe๐Ÿ˜‚

Nasi yafaa kujiuliza, inawezekanaje kuvuka hapa... ukaanzisha biashara ambayo uzao wako watairithi na kuiendeleza mbele? Uzingatie mambo gani kuchagua biashara hiyo kwa mazingira yetu ya sasa? Inabidi uwe mtu wa aina/mwenye tabia gani? Biashara hizo zinahitaji uwe na rasirimali gani? n.k

Kujibu maswali haya kunahitaji maktaba nzima. Lakini jibu la haraka linaweza kuwa... Anza SASA. Anza na RASIRIMALI hizo ulizo-nazo. Kwa UELEWA na UMRI huo huo ulio-nao.

Ndiyo... moto utakuwakia! Familia inaweza kulala njaa, unaweza kufukuzwa nyumba kwa sababu ya kukosa kodi... lakini INAKUPASA. Hakuna mwingine yeyote, na hakuna kungoja kesho. Bibi yake na Mo Dewji hakujua kwamba mjuu wake ataifikisha hapa ilipo sasa na kuajiri zaidi ya watu 28,000.

Hakikisha biashara yako ni ile inayoweza kurithishwa na kuendelezwa na wengine. Isiwe biashara ya utaalam ambayo usipokuwepo, hakuna wa kutumia muhuri au vyeti vyako.
Jambo la kutia moyo ni kwamba, ukielekeza nguvu zako zote kwenye kitu kimoja badala ya vitu vitatu, uwezekano wa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa huongezeka.

Hilo ndo jambo ambalo mimi binafsi nimejifunza na nikawiwa kukushirikisha.

Tafuta hicho kitu kimoja na uwekeze nguvu zako zote.

P.S: Katika kumalizia, ningependa unisaidie kujibu walau moja ya maswali yafutayo...

โ†’ Je, unakubaliana na ushauri wa kulenga biashara moja?
โ†’ Ni biashara gani unayofikiri inaweza kurithishwa kwa vizazi vijavyo?
โ†’ Ni changamoto gani zinazowakabili wajasiriamali vijana nchini Tanzania?
โ†’ Ni ushauri gani ungependa kuwapa wajasiriamali wanaoanza?
โ†’ Ni wazo gani la biashara ambalo UMELENGA na unalifanyia kazi sasa kwa ajili ya vizazi vijavyo?

P.S.S: Ningependa kusikia kutoka kwako kwenye comment hapa chini.

RedBull ni kampuni ya masoko, sio mzalishazaji wa vinywaji vya kusisimua!Mapato ya 2023: Dola bilioni 11Inatawala: 43% y...
08/04/2024

RedBull ni kampuni ya masoko, sio mzalishazaji wa vinywaji vya kusisimua!

Mapato ya 2023: Dola bilioni 11
Inatawala: 43% ya soko la vinywaji vya kusisimua duniani

Je, wanazalisha bidhaa wenyewe? Hapana.

Ingawa waliuza zaidi ya makopo (pieces) bilioni 12 mwaka jana, hawajazalisha hata kopo moja kati ya hayo. Kampuni ya ki-Austria ndio inashughulikia uzalishaji wote, ikiwaruhusu Red Bull kusimamia na kushughulika na MASOKO ikiwa ni pamoja kujenga chapa (brand) tunayoipenda sote.

Sasa tuitizame Monster, kampuni ya pili kwa ukubwa wa vinywaji vya kusisimua. Wao hutengeneza vinywaji vyao wenyewe lakini bado hawawezi kuishinda Red Bull. (Wateja, wingi wa mauzo, au faida).

Na zaidi ya hayo, Microsoft ina injini ya utafutaji (search engine) lakini Apple inatengeneza pesa nyingi zaidi kutoka kwa biashara ya injini za utafutaji kuliko Microsoft, hata hawana injini yao wenyewe! (Google huilipa Apple dola bilioni 15 kila mwaka ili kubaki kuwa chaguo namba moja katika injini ya utafutaji kwenye iOS).

Tunajifunza nini? Sio lazima utengeneze bidhaa ili kufanikiwa. Unachohitaji ni kupata njia nzuri ya kuingia kwenye mchezo, k**a vile ushirikiano na masoko ya watu wengine.

Jambo muhimu zaidi katika kujenga biashara au niche yoyote, SI BIDHAA, bali ni kujenga (audience) WAFUASI wanaokujua, wanakupenda na wanakuamini!

Na kwa nyakati zetu hizi, shukrani kwa AI... mtu yeyote mahali popote duniani anaweza kujenga wafuasi wanaopenda kile unachofanya. Unatapaswa kufanya ni kujifunza ni kwa kwa jinsi gani...

Maswali ya msingi kujiuliza, ni Je...

โ†ณ Nini muhimu zaidi: bidhaa au wafuasi?
โ†ณ Unawezaje kujenga wafuasi kwa biashara yako?
โ†ณ AI inaweza kukusaidia vipi kujenga wafuasi?

Tutayaangazia haya kwenye machapisho yajayo.

P.S: Niandikie maoni yako kuhusu mada hii!

Watu hawanunui uanachama wa gym.โ†’ Wanataka kupendeza na kuwa na ujasiri (hasa kwa wale wasiojihamini).Watu hawanunui iPh...
05/04/2024

Watu hawanunui uanachama wa gym.
โ†’ Wanataka kupendeza na kuwa na ujasiri (hasa kwa wale wasiojihamini).

Watu hawanunui iPhone.
โ†’ Wanataka kuonekana wamefanikiwa.

Watu hawanunui nguo.
โ†’ Wananunua mwonekano mzuri.

Hapa ndipo ninapotaka kukuelekeza:

Fikiria hivi:

Uanachama wa gym. Sio mashine ya kukimbilia (treadmill) wala vifaa vya vingine vya gym ambayo watu wanataka, bali ni hisia ya afya na kujiamini. ๐Ÿ’ช

Simu aina ya iPhone. Sio viwango vya kiteknolojia, ni ile hali ya kujiona umefanikiwa na unaendana na wakati. ๐Ÿ“ฑ

Nguo. Sio kitambaa tu wala mtindo wa mshono, bali mvuto wa kuonekana mtanashati. ๐Ÿ”ฅ

โŒ Acha kuuza vitu.
โœ… Anza kuuza hisia.

P.S. Utangazaji bora ni ule unaozingatia jinsi bidhaa au huduma yako inavyomfanya mteja wako AJISIKIE.

Nyakua Mbinu Yangu ya Mauzo Ndani ya Sekunde 30Linapokuja suala la kuuza mtandaoni, ninalenga:90% kutoa kila kitu bure10...
04/04/2024

Nyakua Mbinu Yangu ya Mauzo Ndani ya Sekunde 30

Linapokuja suala la kuuza mtandaoni, ninalenga:

90% kutoa kila kitu bure
10% kutoa thamani ya juu zaidi.

Linapokuja suala la machapisho, natumia muundo wa mauzo ufuatao:

1. Kuvutia.
2. Tena, kuvutia.
3. Mara nyingine tena, kuvutia.
4. Onyesha tatizo.
5. Onyesha gharama ya kutolitatua tatizo.
6. Toa suluhisho la sehemu yenye thamani.
7. Tumia wito wa kuchukua hatua kwa watu wanaotaka nitatue hilo kwa ajili yao.

Mfano wa kunakili:

96% ya wachapishaji mahudhui mtandaoni hupata shida ya kuwa na mwendelezo wa kuvutia wateja watarajiwaโ€ฆ

Mwezi wa kwanza, wanafanya vizuri.

Miezi inayofuata ni majanga.

K**a hujajipanga vizuri, unaweza kuishia kupata msongo wa mawazo na hata kwa familiaโ€ฆ

โ˜๏ธ Katika chapisho kwa kutumia kanuni ya 3F, yaani Feel, Felt, Found. Tumia hiyo kanuni katika mtindo wa simulizi na hakikisha unazingatia suluhisho linalowezekana kwa tatizo husika.

Kwa ujumla, unaweza kutumia mbinu hii kuzalisha wateja watarajiwa wengi

P.S. Mbinu hii ni rahisi kutekelezeka na unaweza kuanza kuutumia leo.

Pengine huu ni mojawapo ya UONGO mkubwa uliyowahi kuambiwa kuhusu kufanya biashara mtandaoni..."Unahitaji idadi kubwa ya...
03/04/2024

Pengine huu ni mojawapo ya UONGO mkubwa uliyowahi kuambiwa kuhusu kufanya biashara mtandaoni...

"Unahitaji idadi kubwa ya wafuasi ili kutengeza kipato mtandaoni."

Si kweli.

Unahitaji wafuasi SAHIHI na,

Ujuzi SAHIHI!

K**a una wafuasi wanaokaribia 1000, unakuwa na nafasi kubwa ya kuwa na wafuatiliaji wote hawa wanaotazama na kusoma mahudhui yako.

Wanaokupa umakini wao.

Unahitaji nini?

Unahitaji tu kuwa na uwezo wa kubadilisha umakini huo kwenda katika hatua nyingine, yaani kuwafanya wachukue HATUA unayokusudia.

Hapo ndipo UCHAWI ulipo.

HATUA? Bila shaka unajiuliza...

Hapa simaanishi comment, like wala share. Kwa taarifa yako, zaidi ya asilimia 90% ya wateja halisi huwa hawana muda huo.

Inapotokea hatua KUSUDIWA imechukuliwa, hapo ndipo unapojiongezea nafasi ya kutengeneza hela.

Ili uweze kupata wateja zaidi mtandaoni, unahitaji kujenga au kuwa na ujuzi wa aina 5 muhimu:

โ†’ Mauzo.
โ†’ Masoko.
โ†’ Kuandika Nakala za Matangazo.
โ†’ Kujenga Mfumo wa Mauzo.
โ†’ Kujenga Jumuiya.

P.S. Hapa kuna siri ya kutengeneza kipato mtandaoni:

โ†ณ Si idadi ya wafuasi, bali ni ubora wa wafuasi.
โ†ณ Si idadi ya likes na shares, bali ni idadi ya mauzo.

Boresha ujuzi huo kila siku na utakuwa na wateja.

P.S.S: Tayari una ujuzi huo? Ikiwa HAPANA, Unachukua hatua gani kuongeza ujuzi huo? Nijulishe kupitia comment hapa chini.

K**a mfanyabiashara, unajua umuhimu wa mawasiliano yenye ufanisi. Kuchapisha mahudhui mtandaoni ni zana yenye nguvu ya k...
02/04/2024

K**a mfanyabiashara, unajua umuhimu wa mawasiliano yenye ufanisi. Kuchapisha mahudhui mtandaoni ni zana yenye nguvu ya kukuza biashara yako, kuunganishwa na wateja, na kujenga mamlaka (authority) katika tasnia yako. Lakini kwa baadhi, kuandika mtandaoni kunaonekana kuwa changamoto, hasa k**a huna uzoefu.

Ni kawaidia kusikia "Ni vigumu sana," wanasema. "Sina ujuzi wa kutosha." "Sitajua wapi kuanzia."

Ikiwa nawe upo katika kundi hili, usiwe na wasiwasi!

Kwa kufuata vidokezo hivi rahisi, unaweza kuanza kuunda maudhui ya kuvutia na yenye ushawishi ambayo yatasaidia kufikia malengo yako ya biashara.

Unachohitaji kufanya ni:

โ†’ Kuwa msaada kwa msomaji wako
โ†’ Tatua tatizo la "kweli" kwa ajili yao
โ†’ Changia maoni na mitazamo yako kwa uaminifu
โ†’ Andika kwa ufupi na uweze kueleweka

Unachotakiwa ni kuepuka makosa haya ambayo naona wafanyabiashara wengi hufanya wanapoandika mtandaoni.

Epuka...

โ†’ Machapisho yasiyo na maana "halisi"
โ†’ Kuandika vitu vinavyochanganya ambavyo ni vigumu kusoma
โ†’ Kutoa maoni ambayo sio yako mwenyewe
โ†’ Kutumia lugha ngumu ambayo ni ngumu kueleweka

Njia rahisi ndio njia sahihi.

P.S: Uandishi mtandaoni ni mchakato unaoendelea. Kadiri unavyoandika zaidi, ndivyo utakavyoboresha ujuzi wako. Kwa hivyo usiogope kuanza! Jaribu vidokezo hivi leo na uone jinsi unavyoweza kuboresha ujuzi wako.

P.S.S Ni ipi tafsri yako juu ya "Uandishi mzuri" unaopaswa kuchapisha? Nipe maoni yako hapa chini.

Address

DERM Plaza
Dar Es Salaam
14107

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lusabara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Lusabara:

Share