FurahaFmtz

FurahaFmtz its a radio Station situated in Dar es salaam and Zanzibar
(1)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa Wilayani Lushoto mkoani Tanga akifungua kituo kipya cha p...
11/09/2024

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa Wilayani Lushoto mkoani Tanga akifungua kituo kipya cha polisi kilichojengwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 400 ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kufanya kazi kwa weledi huku wakiishi falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya maridhiano, mabadiliko, ustahimilivu na kujenga upya.

Pia Waziri Masauni amewakumbusha kuwa moja kati ya kazi kubwa za Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, hivyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa karibu na wananchi kutaifanya jamii iendelea kuongeza ushirikiano.

Mkataba ulioingiwa na Serikali ya Nchi ya Kenya kwa lengo la kukodishwa kwa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatt...
11/09/2024

Mkataba ulioingiwa na Serikali ya Nchi ya Kenya kwa lengo la kukodishwa kwa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa muda wa miaka 30 kwa kampuni ya India ya Andani group kwa lengo la kuupanua umesitiahwa na Mahak**a ya Juu nchini humo kwa muda

Kulingana na taarifa ya shirika la habari la kimataifa la Reuters limesema chama cha Mawakili nchini Kenya (LSK) pamoja na shirika la kutetea haki za binadamu la Kenya Human Rights Commission (KHRC) waliopeleka jambo hilo Mahak**ani kwa pamoja wameishawishi Mahak**a kwa kueleza kwamba Kenya inaweza kujipatia dola bilioni 1.85, zinazohitajika kukarabati uwanja huo jijini Nairobi bila msaada kutoka nje ya nchi, pia wamedai hatua hiyo inatishia ajira za watu na wala haina faida yoyote kwa walipa kodi wa Kenya

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) baada ya kuf...
10/09/2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya REGROW kwenye hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro imemuelekeza Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege Kikoboga katika Hifadhi ya Taifa Mikumi, Badr East Africa Enterprises Ltd. wenye gharama ya Sh. Bilioni 20.6 kuongeza kasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

"Tunawapongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika na inaonekana lakini msisitizo wetu ni muda, Mkandarasi amalize kazi kwa muda uliopangwa" amesisitiza Mhe. Mnzava.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesikitishwa na kitendo cha kuchelewa kukamilika kwa mradi huo huku akimtaka mkandarasi kukamilisha kwa wakati la sivyo sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.

Hata hivyo, Ujenzi huo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) ulianza Mei 12 mwaka 2023 na unatakiwa kukamilika Disemba 10 mwaka huu.

Siku chache nyuma mwanariadha Rebecca Cheptegei alifariki dunia kwa kumwagiwa mafuta ya petroli kisha kumchomwa moto na ...
10/09/2024

Siku chache nyuma mwanariadha Rebecca Cheptegei alifariki dunia kwa kumwagiwa mafuta ya petroli kisha kumchomwa moto na aliyekuwa mpenzi wake aitwae Dickson Ndiema, baada ya tukio hilo taarifa zimetolewa kuwa Dickson Ndiema nae ameaga dunia katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) alikokuwa amelazwa.

Polisi walithibitisha kuwa wawili hao wamekuwa na mzozo wa muda mrefu sana kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi ambacho Rebecca alikuwa akiishi.

Kwa upande wa Cheptegei yeye atazikwa Jumamosi nchini Uganda kwa heshima ya kijeshi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA), Said Mohamed amesema kuwa maandalizi ya mtihani wa kumaliza elimu...
10/09/2024

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA), Said Mohamed amesema kuwa maandalizi ya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi (PSLE) kesho Jumatano Septemba 11, 2024 yamekamilika ambapo Watahiniwa 1,230,780 wanatarajiwa kufanya mtihani huo

Mohamed amesema katika watahiniwa hao, 564,176 sawa na asilimia 45.84 ni wasichana na wavulana ni 666,604 sawa na asilimia 54.16.

“Kati ya watahiniwa 1,230,780 waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka 2024, watahiniwa 1,158,862 sawa na asilimia 94.16 watafanya mtihani wa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 71,918 sawa na asilimia 5.84 watafanya mtihani wa lugha ya kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia,"amesema katibu huyo.

Amesema watahiniwa wenye mahitaji maalumu waliosailiwa kufanya mtihani huo ni 4,583 kati yao 98 ni wasioona,1402 wenye uoni hafifu,1067 wenye uziwi, 486 wenye ulemavu wa akili na 1530 ni wenye ulemavu wa viungo.

Jamal Musiala ambaye ni Mchezaji wa Bayern Munich akizungumza na gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag, ameweka wazi kw...
10/09/2024

Jamal Musiala ambaye ni Mchezaji wa Bayern Munich akizungumza na gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag, ameweka wazi kwamba rafiki yake Joshua Zirkzee aliyejiunga na Manchester United akitokea Bologna alijaribu kumshawishi ajiunge na United katika dirisha lililopita la usajili ila akamkatalia

"Kila mara unataniana na marafiki mnapokuwa pamoja na hiyo inakuvutia pia kutaka kucheza nao timu moja, ni kweli aliwahi kuniambia kiutani na mimi nilimwambia Josh kwamba inafaa arejee Bayern."

"Nina furaha sana kuwa FC Bayern na ninaangalia zaidi malengo yetu k**a klabu na timu ya taifa pia, sifikirii sana kuhusu ni wapi nitacheza katika miaka mitano ijayo. Mambo yanaweza kubadilika haraka katika ulimwengu wa soka." amesema Musiala

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) akiwa ameambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratiu...
10/09/2024

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) akiwa ameambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi (Mb) wamekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K-FINCO), Dkt. Lee Eun Jae pamoja na Watendaji wakuu wa Makampuni Makubwa ya Ujenzi zaidi ya 30 ya Korea Kusini, leo tarehe 09 Septemba 2024 jijini Seoul, Korea Kusini.

Katika Mazungumzo yaliyofanyika katika nyakati tofauti, Waziri Bashungwa amewasilisha Mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kuwezesha Makandarasi Wazawa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo ameyakaribisha Makampuni ya Korea kufika nchini na kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara.

Bashungwa ametoa wito kwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya K-FINCO kuyawezesha Makampuni ya Ujenzi ya Korea kushirikiana na Makandarasi Wazawa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi nchini Tanzania ambayo yatawezesha Makandarasi Wazawa kujengewa uwezo na kupata ujuzi wa teknologia za ujenzi wa miundombinu.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K-FINCO), Dkt. Lee Eun Jae ameeleza kuwa Serikali ya Korea itaendelea kushirikiana na Tanzania ambapo tayari wameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kusaini hati za makubaliano na Wizara ya Ujenzi na Taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB.

Serikali ya nchini Uingereza na Wales imekuja na mpango wa kupunguza msongamano magerezani ambao umepanga kuwaachia zaid...
10/09/2024

Serikali ya nchini Uingereza na Wales imekuja na mpango wa kupunguza msongamano magerezani ambao umepanga kuwaachia zaidi ya wahalifu 1,700 kutoka gerezani mapema hii leo ili kupunguza huo msongamano.

Sera hiyo itawaruhusu wafungwa kuachiliwa baada ya kukamilisha 40% ya kifungo chao - badala ya 50% - katika jitihada za kuhakikisha vitanda 5,500 vinakuwa wazi.

Wafungwa waliopatikana na hatia ya makosa ya ngono, ugaidi, unyanyasaji wa nyumbani au baadhi ya makosa ya vurugu hawatakuwa sehemu ya mpango huo

Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya...
10/09/2024

Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mwanga, Askofu Chediel Sendoro.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Baba Askofu Chediel Elinaza Sendoro, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mwanga. Natoa pole kwa Mkuu wa KKKT Baba Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Maaskofu wote, waumini, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawaombea faraja kwa neno kutoka katika Biblia Takatifu Kitabu cha Waebrania 13:14; “Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.”

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina "

Askofu Sendoro alifariki Dunia usiku wa jana Jumatatu, Septemba 9, 2024 kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kisangiro, Wilaya ya Mwanga ambapo gari aina ya Toyota Prado alilokuwa akiendesha kugongana na lori.

Mapema leo kupitia mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za uzushi zikieleza kuwa Msanii maarufu wa Hip Hop nchini amba...
09/09/2024

Mapema leo kupitia mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za uzushi zikieleza kuwa Msanii maarufu wa Hip Hop nchini ambaye pia Mwanasiasa, Joseph Haule 'Profesa Jay' amefariki Dunia ila mwenyewe amekanusha taarifa hizo akizungumza na Moja ya chombo Cha habari nchini huku akisema yeye ni mzima wa afya njema na haumwi chochote.

"Mimi niko salama kabisa na hapa nipo nyumbani kwangu nimetulia wala siumwi hata mafua. Naomba hizo habari za kifo kuhusu mimi zipuuzwe kabisa na watu waendelee kusapoti kazi zangu. Pia nawaomba mnisaidie kukanusha hili kwa mashabiki zangu, najua mna nguvu kubwa ya kunisaidia kwenye hili," amesema Profesa Jay.

“Mheshimiwa Masauni, wote tumesikia kauli ya Rais (Samia Suluhu Hassan) jana, lakini kauli ya Rais ambayo inaelekeza vyo...
09/09/2024

“Mheshimiwa Masauni, wote tumesikia kauli ya Rais (Samia Suluhu Hassan) jana, lakini kauli ya Rais ambayo inaelekeza vyombo vilevile ambavyo ndiyo watuhumiwa namba moja wakajichunguze wenyewe, tunaona hilo haliwezekani, hii nchi haitarekebika."

“Wewe k**a mwakilishi wa Rais katika msiba huu, mwambie Mheshimiwa Rais, rai ya waombolezaji katika msiba huu yeye pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuunda tume ya kijaji ya kimahak**a ambayo inaweza ikachunguza matukio yote haya na mengine mengi ambayo yamejificha,” amesema Mbowe

Hizo ni kauli za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe mkoani Tanga kwenye msiba wa aliyekuwa Kada wa chama hicho, Ali Kibao huku akimsihi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kumshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume ya kijaji kuchungua utekaji na mauaji nchini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni amesema kufuatia maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu mauaji ...
09/09/2024

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni amesema kufuatia maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu mauaji ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA, Ally Kibao serikali imeshaanza kufanyia kazi huku akiahidi wahusika wote kuchukuliwa hatua

"Niwahakikishie waombolezaji wote hususani familia k**a Serikali hatutaliacha liende hivi hivi maelezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yameshanza kutekelezwa na hatua zitachukuliwa kwa wale wote waliohusika. Natoe wito kwa watu wote waache kushutumu badala yake kwa mtu yoyote k**a ana kielelezo chochote kwa mtu kuhusika na jambo hili aweze kuwasilisha ili kusaidia kupata wahusika na hatua ziweze kuchukuliwa" amesema Waziri Masauni kwenye msiba wa Kibao

Ameandika Mwanasheria wa Yanga SC, Simon Patrick "Kanuni ya 41 (13) ya Kanuni za Ligi Kuu ya 2024/2025 inasema kuwa mche...
09/09/2024

Ameandika Mwanasheria wa Yanga SC, Simon Patrick

"Kanuni ya 41 (13) ya Kanuni za Ligi Kuu ya 2024/2025 inasema kuwa mchezaji atakayebainika kusaini mikataba na timu zaidi ya moja atafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka 1 hadi 3.

Kwenye ligi ya Cuba, kuna mchezaji mwenye mikataba miwili, na tayari ameshacheza mechi mbili za ligi.

Tathmini ya haraka inaonyesha kuwa pale kanuni zinapozigusa timu, wadau wengi hukubaliana kwamba ni njia sahihi ya kukuza soka letu, lakini zinapowagusa wachezaji, wadau hubadilika kuwa k**a walezi au wazazi, wakisisitiza matumizi ya busara kwa hoja kwamba maisha ya mchezaji ni mafupi.

NB: January na mimi nitasaini vilabu viwili alafu nitacheza timu nitakayoamua😎"

Kazi iliyotakiwa kufanyika ndani ya wiki moja ya ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Buhongwa jijini Mwanza ilitokiwa kukam...
09/09/2024

Kazi iliyotakiwa kufanyika ndani ya wiki moja ya ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Buhongwa jijini Mwanza ilitokiwa kukamilishwa mpaka Ijumaa, Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehakikisha inafanyika ndani ya siku moja kwa kuamua kuweka kambi na mafundi eneo la tukio mpaka saa sita usiku mradi wa dharula Buhongwa ulipokamilika na Maji rasmi yamefika Buhongwa Centre huku kazi itakayofuata ni kuunganisha kwa wananchi.

Awali Waziri Aweso ameshuhidia maunganisho ya bomba ya mwisho ya mradi wa Sahwa Buhongwa ambao unalenga kutatua changamoto katika maeneo ya Sahwa, Lwanhima na Buhongwa.

Mara baada ya bomba la mwisho kuunganishwa saa 4.15 usiku alielekea katika kituo cha kusukuma maji Sahwa ili kuwasha pump ya maji kwa lengo la kusafisha bomba hilo.

Bila kupoteza muda Usiku huo huo Waziri Aweso amewakabidhi Wenyeviti wa Serikali za Mitaa za Sahwa chini na Semba mabomba kwa ajili ya kusogeza maji katika maeneo yao.

Mradi huu una gharama ya Tshs. Milioni 864.81 unatarajiwa kunufaisha wakazi wa mitaa ya Sahwa ya chini, Sahwa ya juu, Buhongwa mashariki, Buhongwa magharibi, Buhongwa centre na Maliza.

Nchini Nigeria watu 48 na Ng'ombe 50 wamefariki Dunia baada ya lori la mafuta kugongana na gari lingine lililokuwa limeb...
09/09/2024

Nchini Nigeria watu 48 na Ng'ombe 50 wamefariki Dunia baada ya lori la mafuta kugongana na gari lingine lililokuwa limebeba wasafiri na ng'ombe, Kaskazini mwa Nigeria hali iliyosababisha Lori hilo kulipuka na kuleta moto Mkubwa eneo hilo.

Kulingana na taarifa ya Shirika la Usimamizi wa Dharura la Jimbo la Niger nchini Nigeria imeeleza kuwa magari mengine kadhaa yalihusika katika ajali hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Sekre...
08/09/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Sekretariet ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho Ali Mohamed Kibao.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.” ameandika Rais Samia Suluhu

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa Tamasha la 'Azimio la Kizimkazi' ambalo limetumika kuhamasisha matum...
08/09/2024

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa Tamasha la 'Azimio la Kizimkazi' ambalo limetumika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia likihusisha Mamalishe na Babalishe Jijini Dar es Salaam amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

"Kiongozi aina ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ana maono ya nishati safi ya kupikia hapatikani mara zote, hatokei mara zote hivyo tuna wajibu wa kumuunga mkono katika ajenda hii ambayo faida zake ni nyingi kiafya, kimazingira, kiuchumi na kijamii." Amesema Kapinga.

Ameeleza kuwa, Rais Dkt. Samia anathamini watanzania wote bila kujali hali zao na ndio maana ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia inagusa makundi yote ya Wananchi hivyo nao wana wajibu kumuunga mkono katika kuiletea Tanzania maendeleo.

Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa wiki ijayo ndio atamaliza program yake ya Pre season na ndio ataanza kuanga...
08/09/2024

Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa wiki ijayo ndio atamaliza program yake ya Pre season na ndio ataanza kuangalia maendeleo ya timu yake

“Wiki ijayo tunaenda kumaliza rasmi wiki sita za Pre Season yetu, hapo tutakuwa rasmi tumekamilisha kuweza kumudu dakika zote 90 kisha ndipo tuanze kuikamilisha rasmi ile timu tunayoitaka kwakuwa kuna baadhi ya Wachezaji walijiunga kwa kuchelewa". Amesema Kocha Fadlu

Hamasa ya wananchi wa Ngorongoro kuhama eneo hilo inazidi kuongezeka ambapo leo tarehe 7 Septemba, 2024 jumla ya kaya 58...
07/09/2024

Hamasa ya wananchi wa Ngorongoro kuhama eneo hilo inazidi kuongezeka ambapo leo tarehe 7 Septemba, 2024 jumla ya kaya 58 zenye wananchi 228 na mifugo 350 wamehama katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine waliyochagua

Meneja mradi wa kuhamisha wananchi wa Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu Flora Assey ameeleza kuwa, kati ya kaya 58 zilizohama leo, kaya 30 zenye watu 151 na mifugo 235 zinahamia Kijiji cha Msomera, Kaya 28 zenye watu 78 na mifugo 115 zinakwenda maeneo mengine waliyochagua katika wilaya za Monduli Mkoani Arusha, Meatu mkoani Simiyu na Simanjiro katika mkoa wa Manyara.

Amebainisha kuwa tangu zoezi la kuhamisha wananchi kwa hiari lilivyoanza mwezi Juni 2022 hadi kufikia leo Septemba 7, 2024 Jumla ya kaya 1,627 zenye watu 9,778 na mifugo 40,051 zimeshahama ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro.

Kila ifikapo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Septemba Dunia huadhimisha Siku ya NDEVU DUNIANI hivyo leo ndiyo siku yenyeweIk...
07/09/2024

Kila ifikapo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Septemba Dunia huadhimisha Siku ya NDEVU DUNIANI hivyo leo ndiyo siku yenyewe

Ikiwa leo ni SIKU YA NDEVU DUNIANI tutajie rafiki ako mmoja ambaye hana NDEVU.

Kwamujibu wa Jarida la  ambalo limemtangaza  Nyota wa Muziki wa Pop kuwa mmoja ya Mabilionea wadogo duniani mwenye utaji...
07/09/2024

Kwamujibu wa Jarida la ambalo limemtangaza Nyota wa Muziki wa Pop kuwa mmoja ya Mabilionea wadogo duniani mwenye utajiri wa Dola Bilioni 1.3.

Utajiri wake unatajwa kuwa umechagizwa zaidi na ujasiriamali wake unatokana na chapa yake ya urembo ambayo aliizindua mwaka 2019 inayojishughulisha na kila aina ya vipodozi,

Pia kazi yake ya muziki, majukumu yake ya uigizaji, mali zake za ardhi, ubia wa chapa, na mikataba mingine vimechangia kumuongezea Wafuasi ambao walimsindikiza kwenye ubilionea huo mpaka sasa kwani Selena ni mtu wa tatu anayefuatiliwa zaidi duniani kwenye Mtandao wa Instagram nyuma ya Mwanasoka Christiano Ronaldo, ambaye ana wafuasi milioni 639 huku Messi, akiwa na wafuasi milioni 505. anafuatia Selena mwenye wafuasi milioni 424.

VIJANA WA TANZANIA KIPO CHA KUJIFUNZA HAPO??

06/09/2024

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert Siwa ametoa taarifa inayoeleza kuwa watu 12 wamefariki dunia huku watu 33 wakiwa wamejuruhiwa katika ajali ya basi lenye namba za usajili T.282 CXT aina ya Yutong lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Tabora kupitia Wilaya ya Chunya baada ya kuacha njia na kugonga gema na kisha kupinduka.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa Bungeni jijini Dodoma wakati wa kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge ameitaka Wizara ya ...
06/09/2024

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa Bungeni jijini Dodoma wakati wa kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge ameitaka Wizara ya Uchukuzi iendelee kulisimamia kwa karibu Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuhakikisha huduma za treni ya SGR zinaimarishwa

Majaliwa amesema kuwa Desemba 31, 2023, Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza kuanza uendeshaji wa reli ya SGR kwa kipande cha Dar es Salaam - Dodoma ifikapo mwezi Julai, 2024.

“Naomba kulitaarifu bunge lako tukufu kuwa, safari za treni ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam - Morogoro zilianza tarehe 14 Juni 2024 na tarehe 25 Julai 2024 uendeshaji wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ulianza,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema Agosti 10, 2024 , Rais Samia Suluhu Hassan alizindua utoaji wa huduma za reli ya kisasa ya SGR kutoka jiji la Dar es salaam kupitia Mkoa wa Morogoro hadi Dodoma.

Amesema treni hiyo inaendelea kutoa huduma kwa wananchi na imechangia kuimarisha sekta ya usafirishaji. “Kipekee ninaomba kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia maono yake na kwa kweli anaahidi, anatekeleza, Kazi Iendelee”.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC amesema kuwa wapo kwenye mchakato wa kuanzisha tawi maalum kwa ajili ya mabi...
06/09/2024

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC amesema kuwa wapo kwenye mchakato wa kuanzisha tawi maalum kwa ajili ya mabinti tu

“Tunakwenda kuanzisha tawi lingine maalum kwa ajili ya mabinti tu (Umri 18-30), tutaliita YANGA DIVAZ, hapa tupo kwenye mchakato wa kutafuta nani atakuwa M/Kiti wa hili tawi tuanze usajili. msimu huu hakuna kupoa” amesema Ali Kamwe

06/09/2024

Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla akizungumza kwenye Mkutano na Wananchi wa Longido na kuwaasa wananchi jamii ya wafugaji kutopata hofu kutoka kwa watu ambao wanatumika lakini waendelee kumuamini Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wetu kwani anawapenda sana .

Timu ya Real Madrid inatajwa kuwa imepanga kumsajili kiungo wa Manchester City na Hispania Rodri kwenye dirisha lijalo l...
06/09/2024

Timu ya Real Madrid inatajwa kuwa imepanga kumsajili kiungo wa Manchester City na Hispania Rodri kwenye dirisha lijalo la usajili

Kiwango cha Rodri alichoonesha msimu uliopita kimewavutia mabosi wengi ingawa Madrid ndio wanapewa kipaumbele kukamilisha dili Hilo.

Mkataba wake na Man City unamalizika mwaka 2027 na mpaka sasa bado hajasaini mkataba mpya

Mchezaji Cristiano Ronaldo ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno amefanikiwa kufunga goli moja hii leo kwenye mche...
05/09/2024

Mchezaji Cristiano Ronaldo ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno amefanikiwa kufunga goli moja hii leo kwenye mchezo dhidi ya Croatia na kumfanya afikishe magoli 900 tangu aanze maisha ya kucheza soka la ushindani.

Mwamba huyu ndoto yake ni kufunga magoli 1000. Je ataweza kufanikisha hilo na sasa ana miaka 39?

Mchezaji Victor Osimhen baada ya kutangazwa k**a mchezaji mpya wa Galatasara ya Uturuki na kuhama katika timu yake ya Na...
05/09/2024

Mchezaji Victor Osimhen baada ya kutangazwa k**a mchezaji mpya wa Galatasara ya Uturuki na kuhama katika timu yake ya Napoli, inaelezwa kuwa ni k**a ameondoka na kijiji chake katika timu hiyo kwani ndani ya masaa 47 Napoli imepoteza zaidi ya wafuasi milioni 1.2 kwenye akaunti yao ya Instagram

Wakati Napoli ikiwa kwenye kilio hicho ila upande wa Klabu ya Galatasaray ni neema kwani imepata wafuasi wapya zaidi ya milioni 2 kwenye akaunti yao Instagram ndani ya saa 48 baada ya kumsajili Osimhen.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa J...
05/09/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika katika ukumbi wa The Great Hall of the People Jijini Beijing nchini China tarehe 05 Septemba, 2024.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime kupitia taarifa aliyoitoa Septemba 04,2024 ameeleza kuwa Jeshi hilo linawashiki...
05/09/2024

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime kupitia taarifa aliyoitoa Septemba 04,2024 ameeleza kuwa Jeshi hilo linawashikilia Mtila Ausi maarufu k**a Shehe Mtila ambaye ni mganga wa kienyeji, Omary Abdallah na Amini Sanga kufuatia vifo vya wafanyabiashara wawili mkoani Ruvuma ambao ni Raymond Hyera na Riziki Mohamed waliofika kwa mganga huyo kwa lengo la kuwezesha Biashara zao kufanya vizuri .

"Agosti 3, 2024 katika Kituo cha Polisi Songea Mkoa wa Ruvuma, zilipokelewa taarifa za kupotea kwa wanyabiashara wawili toka Julai 31, 2024.

"Wafanyabiashara hao walitajwa na ndugu waliofika kituoni kutoa taarifa kuwa ni Raymond Hyera jina maarufu Ray (25) mkazi wa eneo la Msamala, Manispaa ya Songea na Riziki Mohamed (30) mkazi wa eneo la Mjimwema, Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.

"Baada ya uchunguzi na mahojiano, mganga na wenzake walikiri wafanyabiashara hao kufika nyumbani kwao wakiambatana na mfanyabiashara mwenzao aitwaye Amini Sanga kwa lengo la kupata dawa za kuwawezesha biashara zao kufanya vizuri zaidi.

"Waliwanywesha maji ambayo yaliwafanya walegee na kupelekea kupoteza maisha, baada ya kufariki, waliwachukua na kwenda kuwazika katika pori la Mdinguli, Kijji cha Mtangashari, Tunduru kisha kuchukua fedha walizokuwa nazo shilingi milioni ishirini na kugawana.

"Septemba 3, 2024, Mtila Ausi na Omary Abdallah waliwaongoza Polisi hadi walipowazika wafanyabiashara hao, ufukuaji ulifanyika na miili ya wafanyabiashara hao ilikutwa, uchunguzi unaendelea kukamilishwa ukiwepo wa kisayansi ili taratibu nyingine zifuate." Imeeleza taarifa ya polisi

Address

Kiko Street, Mikocheni
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FurahaFmtz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to FurahaFmtz:

Videos

Share

Category



You may also like