
06/02/2025
FOUNTAIN GATE FOOTBALL CLUB WALIFANYA UZEMBE.
Simba sports club waliwahi kufanya hivyo wakati wanacheza na Azam football club pale Songea, walipokutana na Young Africans sports club wachezaji wa Yanga ilikua kila ikitokea faulo kwanza wanashika mpira mkononi mpaka mwamuzi aweke ukuta.
Simba sports club toka kipindi cha kwanza walikua hawampi nafasi mwamuzi Abel William toka Arusha ya kufanya maamuzi yake baada ya faulo kutokea kuna muda ilitokea faulo Abel William akatoa njano wakati anataka kuandika ili kuweka kumbukumbu zake Simba wakaanza haraka sana.
Nini walitakiwa kufanya Fountain Gate football club..?
Baada ya faulo kutokea alitakiwa mchezaji mmoja akasimame mbele ya mpira eneo la faulo ili kumfanya mwamuzi Abel William awaamuru wakapange ukuta wao lakini hawakufanya hivyo Simba wakaanza haraka k**a kawaida yao na kuwaadhibu kirahisi sana.
Mwamuzi Abel William aliwahi kuvurunda katika mchezo wa Lipuli na Ruvu Shooting msimu wa 2020 ikapelekea Afisa habari wa wakati huo Masau Bwire akalalamika sana siku hiyo.
Kuna namna wachezaji mnapaswa kuwa wajanja mnapokutana na timu ambayo wachezaji wake ni wajanja wajanja sana.
Cosmasy William Choga | Sport STAR TV