
01/02/2025
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema urafiki kati ya CCM na Prosperity Party, chama tawala cha Ethiopia, ni hatua muhimu katika kuboresha na kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili, pamoja na watu wake.
Dk Nchimbi amesema ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Ethiopia umebebwa kwenye misingi imara ya itikadi za kisiasa iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo mbili, akitoa wito uongozi wa kizazi cha sasa unawajibika kuimarisha zaidi kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi ya wananchi wa pande zote.
Amesema hayo alipokuwa akitoa salamu za CCM kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha PP, uliofanyika mjini Addis Ababa, jana Ijumaa Januari 31, 2025, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini Ethiopia.
“Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, tunawapongeza sana wenzetu wa Prosperity Party, chini ya uongozi wa Rais wa chama, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
“Uongozi wake madhubuti umekuwa mojawapo ya chachu na nguzo imara kw