๐‡๐€๐ƒ๐ˆ๐“๐‡๐ˆ ๐™๐„๐“๐”

  • Home
  • Tanzania
  • Dar es Salaam
  • ๐‡๐€๐ƒ๐ˆ๐“๐‡๐ˆ ๐™๐„๐“๐”

๐‡๐€๐ƒ๐ˆ๐“๐‡๐ˆ ๐™๐„๐“๐” Kwa uhitaji wa stori za tamthilia wasiliana nasi;
(WSP) 0655 057 884.

๐”๐ฌ๐ข๐ค๐ฎ๐›๐š๐ฅ๐ข ๐ค๐ฎ๐ฉ๐ข๐ญ๐ฐ๐š ๐ง๐š ๐ฌ๐ข๐ฆ๐ฎ๐ฅ๐ข๐ณ๐ข ๐ณ๐ž๐ญ๐ฎ ๐ญ๐š๐ฆ๐ฎ.

28/11/2024

With Onefootball โ€“ I just earned their OneFootballers badge!

Alex alifeli kidato cha nne, aliugua nusu ya kufa, kibarua kikaota nyasi lakini hakukata tamaa unajua ni kwa nini! Aliku...
23/06/2024

Alex alifeli kidato cha nne, aliugua nusu ya kufa, kibarua kikaota nyasi lakini hakukata tamaa unajua ni kwa nini! Alikuwa na malengo, alikuwa na bidii na hakuwahi kukata tamaa, alifanya mtihani wa marudio kisha akafaulu vizuri!

โ€œMshika mbili moja humponyokaโ€ huu msemo hautumiki kila sehemu! Kuna sehemu ambayo ukiutumia utafeli vibaya sana, lakini baki nao kichwani ipo siku utakusaidia. Niliwahi kuwa mwanafunzi kwenye chuo kimoja nchini Tanzania, tulikuwa tunahudhuria lecture, semina na mijadala kwenye vikundi, tulikuwa na muda mwingi wa kusoma lakini pia muda mwingi wa kupumzika (kwa upande wangu ilikuwa hivyo, labda ni kutokana na nilichokuwa nakisomea) hapa likaniijia wazo la kufanya biashara!

Vijana wengi tunapata fursa lakini uoga wetu unatufanya tusiziamini fikra zetu hatimaye tunaishia kufeli na kuwa watumwa wa fikra za watu wengine!
Hivi ni kweli boom linasoma laki sita kasorobo kila baada ya miezi miwili alafu unasema haujui hela inaishaje! Umewahi kujiuliza kabla ya kuanza kuipata hiyo hela ulikuwa unatumia pesa kiasi gani au ndo zile โ€œPonda mali kifo chajaโ€ na kimekuja kweli, huna ajira na zile pesa pia hauna! Kwanini haukuishi maisha k**a ya Alex!

Alijiunga na elimu ya Juu baada ya kufaulu vizuri masomo ya A level, alipata mkopo akaugeuza kuwa fursa, unashangaa! Ndiyo, kutokana na stori za uhaba wa ajira alizokuwa anapiga na washkaji akaondoka na moja kichwani. Alipopata boom la kwanza alinunua desktop! Najua utajiuliza โ€œ Ya nini sasaโ€ we kaa hivyo hivyo!

Hicho kidogo ambacho unakiangalia na kukidharau, kuna mtu anakimezea mate na anatamani akipate! Safari huanza na hatua moja, unapoidharau elfu moja una wazimu! Kaa peke yako jioni ujaribu kuhesabu umetumia elfu moja ngapi kwa muda wa siku nzima kisha endelea na dharau zako. Wewe unabaki nyuma wenzako wanasonga mbele, unaishia kuilaumu serikali na ndugu zako hatimae unakumbwa na majukumu na hela huna! Unadandia kila fani na mtaji hauna, si ulikula kuku na vinyama uzembe, starehe na warembo mixer pombe kali, ukajiona fundi, chuo bata wewe, sherehe kali ya kuhitimu unakumbatia joho si ulifurahi sana, sasa ni muda wa kulia na hakuna wa kumlaumu ila ukiweza chagua pa kuzitupa lawama, hahahaha wala hatujali!

Muda haushikiki lakini ndicho kitu cha thamani kuliko vitu vyote! Unachokifanya leo ndicho kinachokupa furaha au huzuni kesho! Thamini kila sekunde namaanisha Usipoteze muda hasa kwenye mambo ambayo ni kipaumbele kwako. Wengi wamecheza na muda wakiamini bado wana nafasi kubwa lakini kumbe muda haujawahi kumsubiri mtu!

Boom la pili lilipotoka Alex alinunua Photocopy machine iliyotumika, alibaki akidaiwa kiasi kidogo sana, akaomba kushea chumba na muuza duka akamtafuta kijana akaanza kazi! Unashangaa? Hata farao alibaki anaduwaa hivyo hivyo wakati Musa anapasua bahari watu wakavuka ng'ambo!

Haba na haba hujaza kibaba, hii methali ichukue itakusaidia. Wakati wewe unalialia na una simu ya laki mkononi, kuna mtu anahitaji shilingi elfu hamsini tu aanze biashara. Ndoto za kutengeneza mtaji wa mamilioni ndipo uanze biashara zimewapotezea wengi muda. Unakesha ukiandaa mikeka ya milioni mia kwa shilingi mia tano, ngosha, tambua kuwa si wote wanashinda, na ikitokea mtu kashinda hiyo inakuwa ni habari! Utapoteza bando, utanunua odds, utastake hela kubwa lakini matokeo hautaambulia chochote. K**ari imewaumiza wengi, imeua ndoto za vijana wengi, mtu anapoteza kiasi cha pesa ambacho hajawahi kukimiliki kwa wakati mmoja, si wanataka mpunga mwingi, badala ya kuupata, inasikitisha sana!

Tutaendelea....

SIMULIZI:KIVULI CHANGUMWANDISHI: K. WambiaMAWASILIANO (WSP) 0655057884Sehemu ya 01.Wakati huo nimekaa chini nikiwa nimek...
22/06/2024

SIMULIZI:KIVULI CHANGU
MWANDISHI: K. Wambia
MAWASILIANO (WSP) 0655057884

Sehemu ya 01.

Wakati huo nimekaa chini nikiwa nimekunja miguu, kichwani nimebeba bakuli pana jeupe ambalo limezungushiwa kitambaa chekundu chenye mafundo meusi. Mbele yangu wamesimama wanawake wawili ambao wamenigeuzia mgongo wakiwa wameinamisha vichwa. Wamevalia kanzu nyeusi na vilemba vyekundu. Mmoja amebeba chungu kilichovikwa shanga na vitu vyenye mwonekano wa kobe mdogo. Mwingine ameshikilia bakuli dogo na mkono wa kushoto umeshikilia mti wenye mwonekano wa mkongojo japo yeye haonekani kuwa mzee. Ni usiku sana na ni pori kubwa lakini tulipokuwa ni sehemu yenye uwazi k**a kiwanja cha mita ishirini za mraba.

Nyuma yangu alipita ndege kisha akatua kwenye bega la mwanamke aliyekuwa upande wa kushoto mbele yangu, kisha nikaona moshi unafuka kutoka kwenye bakuli dogo alilokuwa ameshikilia yule wa kulia kisha ghafla nikastaajabu mtu mrefu amesimama mbele yangu, ikawa kichwa changu kinakaribia kabisa kuigusa kanzu yake! niliogopa sana, nikajisemea mwisho wa maisha yangu ndo umefika!
Aliinua mikono yake Akatamka maneno ambayo siwezi kuyakumbuka lakini kufumba na kufumbua, watoto wachanga wawili ambao vitovu vyao havijakatika wakawa wamekaa kwenye viganja vya mikono yake iliyotapakaa damu! Aliinamisha kichwa kisha nikawaona wale wanawake wawili wanamsogelea kinyumenyume.

Ni kipindi ambacho nilikuwa nalala na mama kwa kuwa baba alikuwa safarini. Pia ni kwa sababu nyumba ilikuwa kubwa na wakati mwingine mle ndani palikuwa pakisikika sauti za kuogofya usiku wa manane kutoka kwenye chumba ambacho baba alikataa tusikifungue. Huwezi kuamini
pale kitandani nilikuwepo, ni mimi huyu huyu lakini tofauti ni kuwa niko hapa na niko pia pale!

Mwili wangu kitandani unaonekana umelala chali, sigeuki wala kutikisika labda k**a mtu angenitikisa. Mama amejilaza kwa pembeni, yuko kwenye njozi hawezi kuamka. Nakitazama kile kitanda kwa huruma machozi yakiwa yanabubujika mashavuni nikashindwa kuyazuia, niliwaza sana nisijue la kufanya. Nikiwa bado nimesimama pale kwenye kizio cha nyuzi tisini ndani ya chumba cha mama, unatokea mwanga mkali ukiwa umeambatana na upepo, kisha bila kujua kipi kilicho tokea nikajikuta nipo kwenye mji mkubwa uliojaa watu! kilichonishangaza zaidi ni kuwa watu wengi ninaowafahamu ambao walishakufa wako huku, yupo Mustafa ambaye alikuwa fundi ujenzi ananiangalia sana machoni, kisha nikaona machozi yanamdondoka, amebeba jiwe kubwa sana! jasho linamtiririka mithili ya chupa ya maji iliyogandishwa! Namuona babu akisukumwa ili awapishe matingo ambao wamebeba magogo mazito, anaomba maji hakuna anayemjali, kuna binti mmoja nimemsahau jina, yuko uchi akimbembeleza mtoto mdogo wa miaka k**a miwili hivi, nakumbuka huyu binti alifariki yeye na mtoto mchanga wakati wa kujifungua, ni miaka miwili imepita, niliogopa sana! Kule kuna shughuli za kila aina! Nilitembezwa kila sehemu.

Wakati tukiwa tunamalizia matembezi mjini pale, niliona aina fulani ya kidani, ni k**a kile ambacho kimening'inizwa mbele ya mlango ambao baba alitukataza tusiufungue! Nikapigwa na butwaa lakini sikutaka mtu yeyote ahisi badiliko! Kichwani mwangu maswali yakaanza kupishana, au labda baba naye...! Mara nikasikia sauti sikioni mwangu โ€œole wakoโ€ nikaogopa sana maana ile sauti ilikuwa nzito na sikumuona mtu.

Tulipolivuka geti nilijikuta nimeurudia mwili wangu ambao upo kitandani. Nikiwa kwenye hali ya mshangao, ni maswali mengi najiuliza na mengi ni yenye utata mkubwa lakini sikuwa na papara, sikumwambia mtu k**a nilivyokatazwa na ile sauti lakini woga ulitamalaki, ila sikurudi nyuma! awamu hii lengo langu ni mpaka nijue kwenye kile chumba kuna nini! Nikiwa kitandani nimelala, nasikia sauti za watu zaidi ya mmoja zikisemezana dirishani kwetu, nikamwamsha mama lakini alikuwa amelala, nikasogea ili nione nini kinachoendelea, ile tu nasogea, taa zikazima! nikahisi k**a kitu kimepita karibu kabisa na uso wangu lakini sikukiona, upesi nikarudi kitandani! โ€œ...hii ni nyumba gani haiishi matatizo?โ€ nilijiuliza huku woga umetanda mithili ya mtoto mchanga kwenye maji ya baridi.

Asubuhi ilipofika tukaamka. sikumsimulia mtu, niliondoka nyumbani kuelekea bandarini ambako ndiko nilikuwa nafanya kibarua, nikasimamisha tax nikapanda...! Wakati tunaendelea na safari mbele yetu kulikuwa na gari aina ya Volkswagen ndogo iliyozeeka, kioo kimoja kimepasuka kidogo, ningeweza kujiuliza liliweza vipi kuwapita askari wa usalama barabarani likiwa na hali ile lakini sikufanya hivyo! Nikiwa nalishangaa gari ghafla likasimama, na kwakuwa dereva hakuonesha ishara yoyote magari haya mawili yakawa yamegongana!

Akatoka ndani ya gari mwanamke mrembo sana, nikimtazama ni k**a sura yake inanijia kichwani lakini sikumbuki nilimuona wapi nikapotezea! Wakazungumza na dereva wa taksi niliyoipanda kisha akaondoka. Kwakuwa nilikuwa nimekaribia kufika bandarini sikuhitaji tena usafiri mwingine ikabidi nitembee kwa mguu. Wakati nakatiza barabara nikamuona mwanamke mwingine ameketi chini ya mnazi, ni sehemu ya wazi sana, namkumbuka pia, nilivomtazama akapotea! nilishtuka sana, nikatembea upesi hadi bandarini.

โ€œMama alisema huu ufunguo ni wa baba ila hajui unafungua nini!โ€ ninajisemea kimoyonimoyoni nikiwa peke yangu chumbani kwa akina mama โ€œhuenda ni wa pale mlangoniโ€ Nikauchukua! nikatoka upesi kuelekea kwenye mlango wa chumba ambacho tulikatazwa tusikifungue! Nilivyoukaribia mlango nikaona uko tofauti na nilivyouzoea, hakuna kufuli na ni k**a kuna mtu mle ndani! Nikarudi nyuma taratibu nikiwa najizuia vishindo visisikike, nikiwa sijafika mbali nikamuona baba anatoka, nikastuka kidogo baba akawa amehisi kitu, akaniita, Anifa... bh, bbhe baba!! Unatoka wapi? Natoka huwani baba!! Hapana, chumbani kwangu!, Wakati huo nimeshikilia ufunguo ambao sitaki baba auone! Mbona una hofu? aya sawa, mi naondoka mama yako akirudi mwambie nilikuwa hapa! โ€œnimwambie alikuwa hapa!!โ€ nikashindwa kuelewa kabisa, anaonekana hayuko sawa, why!! anyway! Sawa baba! Nikaitikia akaondoka.

โ€œ...au niingie! lakini sidhani kuwa huu ndio ufunguo sahihi wa pale mlangoni maana wenyewe baba anao! au nijaribu tu huenda ukawa ndio wenyewe!โ€

Itaendelea.....

TUNAANZIA WAPI.Kila kiumbe Duniani huangaika kutafuta jinsi ya kuendelea kuishi, japo kwa upande wa binadamu tumegawanyi...
05/06/2024

TUNAANZIA WAPI.

Kila kiumbe Duniani huangaika kutafuta jinsi ya kuendelea kuishi, japo kwa upande wa binadamu tumegawanyika. Wapo wanaoangaikia kuishi na wapo wanaoangaikia kuishi vizuri. Maisha mazuri yamekuwa ni ndoto ya kila kijana katika karne hii.
Maisha siyo tu kuwa ni fumbo bali ni fumbo ambalo mfumbuaji ni wewe mwenyewe. Tofauti na zamani, leo ni wewe mwenyewe unayeamua uwe mtu wa aina gani. Utofauti uliopo katika maamuzi ndio huzaa UTAJIRI na UMASIKINI!

K**a kijana mwenye mtaji mzuri wa UMRI, unadhani ni kundi lipi ambalo linakufaa kati ya hayo mawili? Najua wengi tunapenda UTAJIRI (wengine bila kujishughulisha!). Najua kuna mtu amejaribu kutafuta na sasa anakata tamaa โ€œWakati ambao wewe unafikiria kukata tamaa ndio huohuo wakati ambao unamruhusu mtu mwingine aendeleeโ€ MUHINDI ATAKUFUNGULIA DUKA.

Twende taratibu;
โ™ฆVitu gani umevipa kipaumbele?
Huenda umeweka kipaumbele kwenye vitu ambavyo kimsingi haviwezi kukusukuma uende mbele. Vipaumbele vyako ndio msingi wa maendeleo yako ukiachilia mbali MTAJI. Ngosha amewekeza kwenye k**ari, kila la kheri mk**aria!!

โ™ฆRatiba zako zimekaa vipi?
Kwenye masaa 24 unafanya kazi masaa mangapi? Wastani wa kukaa kazini kwa uhakika ni masaa nane tu. Lakini je tunayatumia vilivyo haya masaa manane? Au na stori za mpira humohumo, siasa, majungu na umbea kuhusu mambo yasiyokuhusu?

โ™ฆUna marafiki wa aina gani?
Ule msemo wa ndege wafananao huruka pamoja una maana kubwa sana. Aina ya marafiki tulionao husadifu tabia zetu, matendo yetu na mara nyingi hupanga mstakabali wetu kiuchumi. Ni vigumu sana kufanikiwa ikiwa umezungukwa na marafiki wasio wachapa kazi na wenye kupenda starehe.

โ™ฆ Je kazi unayoifanya unaipenda?
Wakati mwingine tunajikuta tunafanya kazi ilimradi tu mahitaji muhimu yapatikane lakini uhalisia ni kuwa hatuzipendi kazi hizo hivyo tunakosa ubunifu na mipango kuhusu uendeshaji au utekelezaji wa majukumu katika kazi hizo.

Nimewahi kukutana na kesi mbalimbali za vijana katika biashara, hasa wale wa migahawa na maduka ya rejareja, wengi walikuwa na haya;

1. Biashara yangu haikui.
Unafahamu ni kwanini biashara yako haikui? Mzani umekaaje baina ya kinachoingia na kinachotoka, au ndo zile nimeuza sana leo lazima nile pilau nyama, sahau kuhusu kukua kwa biashhara, iko hivi, kwa kawaida duka la mangi faida yake ghafi ni 10% mpaka 20% yani ukiuza sh 100000 faida inaelea kati ya sh 10000 mpaka 20000(hiyo siyo yako yote) toa hesabu ya pango, leseni, Kodi ya TRA, usafirishaji kisha utakayobaki nayo ndiyo halali yako kwa siku hiyo na mbaya zaidi k**a huachi akiba basi ndo usahau kabisa kuhusu kukua kwa biashara yako. We kula pilau kukuUtazeekea dukkani!

2. Wateja wanazidi kupungua!
Wakati mwingine unaweza kuwa na kila kitu dukani lakini ukashangaa watu kwako hawaji k**a inavyotakiwa, ukiwa na ufinyu wa fikra unaweza kufikiria kuwa kuna mtu anakulogea biashara, si unajua nyie mangosha na imani hizo (nyie ni watani zangu) utafeli! Jitathmini, kauli zako kwa wateja wako, tabia zako ( vijana wengi wanapenda kutongozatongoza na stori za mapenzi mapenzi) si wote wanapenda stori hizo na mara nyingi wazazi huwazuia mabinti zao kwenda kwenye mazingira ya aina hiyo. Kugeuza duka kuwa kijiwe cha stori, hii nimeielezea vizuri kwenye kitabu cha OKOA BIASHARA YANGU. Bei zako zikoje? Unaweza kulegeza bei kidogo, ila angalia isiathiri mzunguko wako wa biashara, wateja wengi wanapenda bei ndogo, pangilia vizuri bidhaa zako, muonekano mzuri na rahisi kwa mteja, ikiwezekana bidhaa za kupima ziwekwe mbele ya duka( mara nyingi tunatumia mabeseni kuweka bidhaa k**a mchele, maharage, kunde, kande, karanga, unga nk) na bei ziandikwe kwenye vikaratasi vigumu kisha vichomekwe juu ya bidhaa.

3. Nikopeshe imezidi.
Kukopesha ni njia nzuri ya kuwavuta wateja lakini pia ni njia nzuri mno ya kuiangamiza biashara. Mkopaji mzuri ni yule anaerejesha kwa wakati, kuna wale wakopaji ambao akichukua bidhaa anahama kijiwe mpaka atakapopata hela ya kurejesha, mwingine anakopa na harejeshi, mwingine anakopa anakaa siku kadhaa anakuja kukopa tena, unajua nini, ukikataa inakuwa uadui kisha anakuhama. Kuwa mjanja kuwaelewa wateja wako, anaefaa kukopeshwa ni yule tu ambae anarejesha kwa wakati. Kumbuka pia kuwa mara nyingi bidhaa isiyotoka haraka ndiyo hukopeshwa.

4. Nimeshindwa kurejesha mkopo.
Mikopo ipo ya aina nyingi; kuna mikopo ya kibenki na ile ya kwenye vikundi vya upatu. Mikopo midogomidogo ni pasua kichwa na urejeshaji wake ni mgumu kupindukia. K**a biashara yako ipo tu vizuri ni vema kuukuza mtaji kulikoni kudumbukia kwenye shimo la madeni.

Kwa leo naishia hapa, tukutane kwa ajili ya mwendelezo.

SEHEMU YA 03.Sadiki alipoteza fahamu palepale. Mashambulizi yalikuwa makali sana, kumbuka Kizito anagalagala chini k**a ...
13/05/2024

SEHEMU YA 03.

Sadiki alipoteza fahamu palepale. Mashambulizi yalikuwa makali sana, kumbuka Kizito anagalagala chini k**a chatu baada ya kupigwa risasi mbili, moja kwenye paja na nyingine begani. Kibonge anafanya mashambulizi akiwa peke yake huku akimuhamasisha kizito ambaye anarusha viazi akiwa amelala chini. Sadiki anazinduka, hapajapoa anakutana na mashambulizi makali, anajibanza chini ya mti anavua bullet proof jacket na kugundua kuwa risasi haikupenya bali msukumo wake ndio ulioush*tua mwili, si unajua Sadiki ni muogamuoga! Kwa haraka anasimama na kuungana na Kibonge ambaye anaelekea kuelemewa, โ€œKufa kiume, usiwe mwoga, pambana, okoa maisha yako na ya taifa zimaโ€ alisikika kibonge ambaye ameshikilia AK 47 ikimimina risasi k**a njugu.

Akiwa nje, Zainabu anasikia minong'ono ndani, ni minong'ono inayoashiria kuna jambo linaendelea chumbani kwa dada yake โ€œ... lakini si nilisikia kuwa shemeji Kizito ameenda kwenye oparesheni ya taifa ya kijeshi, imekuwaje yuko ndani?!โ€ Zainabu alijiuliza bila kupata majibu! Ikabidi awaache, ikapita dakika tatu hivi Zikasikika sauti za miguno isiyo ya kawaida, oh, hapana, usifanye hivyoo, niache kwanza...aaah, wewe mtaariiim... Hapo Zainabu akaelewa kiutu uzima kuwa yanayoendelea humo siyo ya kawaida akaacha mzigo wake mlangoni akaenda kukaa kwenye veranda. Akiwa pale chini aliwaza akaamua kwenda tena pale mlangoni akasikia sauti za kimahaba zinazidi, akagonga mlango kwa nguvu zaidi, wakati huu anaita kwa sauti โ€œDada, dada, fungua mlangoโ€ kimya kikatawala, kumbe mda huo Mtalimbo ameshavaa nguo zake na yuko nyuma ya mlango! Zuwena akafungua mlango lakini tofauti na ilivyokuwa kawaida, hakuonesha furaha ya ujio wa mdogo wake, alimtazama kwa hofu sana, Zainabu hakujali akapita chumbani kwa dada yake akakaa kitandani. โ€œDada, kwani humu ndani mnaishi wangapi?โ€ โ€œwewe ni karani wa sensa? Zuwena alijibu kwa dharau kisha akatoka nje! Hakuwa na habari kuwa Mwenzie Mtalimbo amejibanza nyuma ya mlango kwa hofu! Zainabu akatoa kicheko cha kejeli kisha akavua nguo akapanda kwenye kitanda cha dadake! Akiwa pale kitandani anatizama chini anaona simu ndogo ya batani ikiwa inachomoza nyuma ya mlango lakini hakujali akaendelea kujipumzisha! Kutokana na uchovu aliokuwa nao akataka aufunge mlango ili asibugudhiwe.

โ€œ...Siamini k**a nimewadondosha wote, tena k**a wewe ...tututututtt!โ€ akajisemea Kibonge huku akiumiminia risasi mwili wa askari hasimu aliyemjeruhi Kizito. Wakati anageuka nyuma akasikia โ€œ...inamaaaโ€ sauti ya kizito ilisikika ikiashiria kuna shambulio. Ni risasi iliyomkosa Kibonge ikiruka usawa wa nyuzi thelathini na tano na kuutoboa mti, kabla hajavuta tena trigger akakutana uso kwa uso na risasi ya kichwa kutoka ndani ya silaha aliyokuwa ameishikilia Kizito, โ€œ...kwisha habari yakoโ€ alisema Kizito ambaye anaonekana mwenye furaha baada ya kufanikiwa kuuokoa uhai wa rafiki yake. Kibonge anamfuata Kizito na kumkumbatia, wanaongozana huku Kizito akiwa anachechemea โ€œ...kaka ingenipata hiyo ungenisahau kabisaโ€ alisema Kibonge huku akiisonta risasi iliyotoboa mti baada ya kumkosa. Sadiki anawafuata akinyata kutokea kwenye kichaka ambako alienda kujificha baada ya mapambano kuwa makali, โ€œ...Sadiki ulikuwa wapi? ...nilikuwa nawavizia maadui, wapi? Kabla hajajibu akapewa mizigo abebe โ€œ...jamani nilizimiaโ€ yani sadiki ni mzembe mzembe. Wakati wanatembea Kizito akatoa picha ya mkewe Zuwena, anaifuta kwa dole gumba kisha anairudisha kwenye mfuko wa kushoto wa kombati, anashika mfuko wa kulia anatoa picha ya Daudi mwanae mkubwa kisha anatengana na wenzake, anaibusu kisha anairudisha pahala pake. Ulikuwa mwendo mrefu na sasa wanaelekea kuungana na kikosi kikubwa.

Wakati anaushika mlango aufunge akashangaa auhami, akageuka kutazama nyuma ya mlango, mamaaah! kuna mtu! mimi ni shemeji yako, nyamaza nikwambie vizuri, wakati huo akiwa anauvuta mlango ambao zainabu analazimisha kuufunga kwa nje, vuta nikuvute akafanikiwa kuponyoka, akakimbilia chumbani kwake. โ€œangeniitia mwizi sijui ingekuwaje...inabidi niachane na haya mambo lasivyo nitakufaโ€ alijisemea Mtalimbo wakati huo akichungulia kwenye upenyo wa mlango kuona nini kinaendelea huko nje. โ€œMasikini shemeji angelikuwepo hii pimbi ingegeuka mboga, yani dada anawaleta mpaka ndani, kumbe ndiyo maana alikuwa ananijibu vibaya, nimeshausoma mchezo! Ata hivyo nisiwe mbea, kila mtu ajali mambo yakeโ€ mara anamuona Izdori ambaye anatokeza uwani akamuita โ€œ Izdori mwanangu โ€œnaamโ€ nimekumisi sana, Daudi yuko wapi โ€œshuleniโ€ njoo โ€œayaโ€ mbona umechafuka sana โ€œtulikuwa tunacheza na akina Nurdini kule barabaraniโ€ usiwe unacheza barabarani kuna magari na pikipiki zitawagonga. Aya twende nikakupe tende tamu niliwabebeeni โ€œahsante mamdogoโ€ wakati huo Zuwena akiwa anatoka sokoni anapishana na Mtalimbo ambaye anaonekana mwenye hofu sana โ€œwapi tenaโ€ โ€œshhhhhh! mdogo wako atasikia, amenifuma chumbani kwako, nimekimbia ila nilikuwa nimeficha uso, nimejikwaa nimechanika kucha, niangalizie ufunguo wangu humo chumbani mwako, mimi naenda kuchukua dawa hapa dukaniโ€

Siipendi hii rangi...ni k**a boksa ya Mtal...Shhhh! Akikusikia, tena nitakusema kwa mama...walikuwa na mama, wapi, chumbani..nilichungulia kwenye pazia, mama alikuwa uchi, Mtalimbo akavua akabaki na boksa ya rangi k**a hii, alilala k**a baba alivyokuwa analala, niliogopa nikakimbia! Namchukia mama, sijui baba atarudi lini! Usihofu atarudi, ila usimwambie mtu jambo hili... Uhalisia ni kwamba Daudi ni mkubwa hivyo anaelewa madhara yake, japo anasononeka lakini hana namna zaidi ya kumzuia mdogowe asiseme kitu.
Kwani mama yuko wapi, yuko ndani na mamdogo, njoo nikunong'oneze....!

(Fuatilia Sehemu ya 4 wiki ijayo)



09/04/2024
Tunatangaza ujio wa simulizi kali ambayo itafunika simulizi zote ambazo umewahi kuzisikiliza. Kaa mkao wa kula.
04/01/2024

Tunatangaza ujio wa simulizi kali ambayo itafunika simulizi zote ambazo umewahi kuzisikiliza. Kaa mkao wa kula.

SIMULIZI: JINO BOVUMTUNZI: Kelvin WambiaMAWASILIANO (WSP): +255 628 364 931SEHEMU YA 01.Kuna wakati akili husimama haifa...
13/12/2023

SIMULIZI: JINO BOVU
MTUNZI: Kelvin Wambia
MAWASILIANO (WSP):
+255 628 364 931
SEHEMU YA 01.

Kuna wakati akili husimama haifanyi kazi yake!......mapigo ya moyo huenda kasi, hasira, chozi la damu, mkuki moyoni na bunduki mkononi magazine imejaa risasi na huwezi kufanya chochote!.... JINO BOVU! Safiri nami kwenye simulizi kali yenye visa tele vya usaliti, mapenzi, vita, visasi na majuto.

Usihofu nitarudi salama! Ni maneno yaliyojaa faraja yakitoka kinywani mwa Mtumbuka kijana mwenye umri wa miaka 27 akielekea kwenye mission kubwa ya kitaifa, safari hii ni kuitetea hadhi ya nchi yake, amevalia kijeshi, anakabidhiwa kofia na mkewe mwenye watoto wawili wa kiume, anaonesha uso uliojaa huzuni, anamkumbatia mmewe machozi yakibubujika asiwe na la kufanya zaidi ya kumuachia na kumpungia mkono akimtakia kheri. Kizito alimshika bega yule mwanae mkubwa Daudi akainama akamnon'goneza jambo na wakaonekana wote wakitabasamu, kisha akamshika kichwani yule mdogo aitwaye Isdori akapiga hatua kadhaa mbele akatoa sigara mfukoni na kiberiti akaiwasha akawapungia mkono akiashiria kuwaaga, haina namna, ni suala la kitaifa.

Safari ya kuelekea kwenye uwanja wa vita inaanza, wakiwa kwenye gari Kizito anaonekana akitafakari jambo kisha anazima moto kwenye kipande cha sigara ambacho kinaonekana kuelekea kuisha... ghafla mlio mkubwa unaoziba masikio unasikika, moshi mweusi uliozungukwa na vumbi jingi unaonekana ukipaa angani, vilio kila kona, njiani kumetapakaa watu na wanyama wa kila aina, vinyonga na mwendo wa maringo ni wakati wa amani tu, hapa hata twiga asingetikisa shingo, tausi walinywea k**a khanga wa mwituni, hakuna kung'atana, mbwa walikuwa wapole k**a mbuzi jike hata kubweka hawabweki, hakuna kuhubiri wala kuswalisha, hakuna sadaka wala zaka, kila mtu ananena na roho yake! Ama kweli hakuna mbadala wa amani!
Gari alilokuwa amepanda kizito lilikaribia kwenye uwanja wa vita, kila aliyekuwa ndani ya lile gari aliamriwa kuhakiki silaha zake za kujilinda na za mapigano, mara moja Kwa haraka kila mmoja anakuchukua nafasi, kimyakimya mgawanyiko unafanyika na kila askari anaelekea alikoelekezwa na kapteni. Kizito anakumbuka kuwa amesahau kipisi cha sigara alichokizima wakati anaingia ndani ya gari, ile anageuka nyuma, gari linawaka moto! ...tunashambuliwa!

Nyumbani kwa kizito hakuna furaha k**a zamani, Zuwena ambaye ni mke wake Kizito anaonekana mpweke mithili ya njiwa aliyefiwa mume, โ€œ...lakini atarudi tu k**a alivyosemaโ€ alijisemea taratibu akielekea kwenye meza ya kulia chakula ambako tayari Daudi na Isdori wameshaanza kula โ€œ...mama mbona wewe hauli?โ€ aliuliza Isdori huku aking'ata kipande cha nyama,...kuleni kwanza mimi nitakula badae...โ€œShauri yakoโ€ alisikika Daudi ambaye yuko bize na kipande cha mfupa wenye nyama ngumu. Nyumbani kwa akina Daudi kulikuwepo na wapangaji watatu, mmoja anaitwa Ashura muuza genge, yeye hurudi mida ya saa tatu usiku, hana mume, baada ya kuachana na mmewe aliamua kupanga chumba kwa akina Daudi, mwingine anaitwa Jimmy, huyu ni fundi gereji, huwa anawahi kufunga maana kazi zake mara nyingi ni za mchana na mara chache hufanya kazi usiku, mara moja moja huwa anasafiri kikazi nje ya mkoa, ana familia ya mke na mtoto mmoja lakini familia yake inaishi nje ya mkoa, wa mwisho ni Mtalimbo, huyu ni Muhitimu wa chuo kikuu lakini hajapata ajira, amejiajiri k**a afisa usafirishaji (bodaboda), hajaoa na huwa halali nyumbani mara kwa mara.

Ni asubuhi imefikia, mtalimbo ananusa kikwapa ili kuona k**a anaweza kwenda kazini kwa mara nyingine bila kuoga, mara Zuwena anamuona, ooh! Masikini kaka wa watu, kumbe anatingwa na kazi kiasi kwamba hapati hata mda wa kuoga! Leo nitampelekea maji bafuni! Anaonesha kuridhika Mtalimbo, anaweka ufunguo ili kuwasha pikipiki lakini anagundua kuna mtu alikuwa akimchungulia kwa kificho, โ€œ...huyu atakuwa ni mama Daudi maana hakuna anayebaki hapa tofauti na yeyeโ€ alijisemea mtarimbo huku akiachana na zoezi la kuwasha pikipiki na kurejea ndani! Ah! Ni wewe mama D! Nilihisi mwizi! โ€œ...hapana ni mimi, ila weka ratiba zako vizuri, mwanaume unatakiwa uwe smart!โ€ ...k**a Kizito mmeo? alidakia Mtarimbo akakatishwa na Mama D ambae anaonekana kuyachukia matamshi ya Mtarimbo, โ€œ...sasa mpaka umtaje, huyo yuko mbali kwa sasa, jiongeze!โ€

Vita imechachamaa, makombora yanarindima kila kona, hakuna kupumua, kikosi cha akina Kizito kinakatiza bondeni kwenye majani marefu na maji-kwa miguu maana ndiyo njia salama ili kutokea upande wa pili, Kibonge ambaye ni rafiki wa karibu wa Kizito amebeba silaha begani anatokwa jasho kila sehemu, jua ni kali sana unaweza kuchomea muhindi ukaiva. โ€œ...hili tope linanikumbusha kipindi tunapalilia mpunga kwenye shamba la baba baada ya shule yetu kufungwaโ€ alisikika kibonge ambaye alionekana kuchoshwa na safari ndani ya maji yenye tope jeusi. Shule yenu ilifungwa! Kwa nini? Aliuliza Sadiki ambaye anafuata kwa taratibu nyuma ya Kibonge, Mauaji! โ€œunasema..โ€ Ndiyo, aliuawa mwalimu, hii ni baada ya mfululizo wa walimu kufariki shuleni hapo ikabidi shule ifungwe, hatukuruhusiwa kupokelewa na shule nyingine yoyote, kwahiyo tukaishia kukaa nyumbani! ...du! Miezi sita, nilihenyeka topeni kupalilia mpunga, sikuwa na namna! Ghafla Kizito ambaye alikuwa ametangulia mbele akasimama, walipokaribia akawaonyesha ishara ya hatari akiashiria kuwa amekanyaga bomu na hawezi kubandua mguu!

Aaah! Mke wa mtu sumu, mimi nina kisu, mwenzangu ana bunduki! Uoga wako ndo unaokuponza, ona mpaka sasa hujaoa! Mama D, sijataka tu kuoa lakini sifa za kuwa na mke zote ninazo! Alijigamba Mtarimbo Zote zipi? Zuwena aliuliza kwa kejeli โ€œTuone k**a kweli unazo!โ€ Alisema huku akimsogelea Mtarimbo, akaelekeza mkono wake chini ya kitovu cha Mtarimbo akamgusa....wakati huo Mtarimbo ambaye siyo mzoefu wa masuala ya mahusiano ametoa macho mithili ya korongo anaenyongwa, alisikika akisema kwa sauti ya chini, usishike huko! Jamaa ni mtarimbo kweli k**a lilivyo jina lake, Ooh! Wow! Kumbe kweli, sasa kwanini hujaoa na mti wote huu ghafla mlango ukasukumwa na kufunguliwa, Zuwena...!!
(Fuatilia sehemu ya pili)
https://whatsapp.com/channel/0029VaBncmT4CrfiUFXoZE45

12/12/2023

Maisha ni MRADI ambao mtekelezaji ni wewe mwenyewe. Imewachukua wengi nusu ya maisha yao kulitambua hili!

Kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kukupotezea mwelekeo katika maisha yako:1. Matumizi mabaya ya teknolojia: Kuwa mwathir...
14/10/2023

Kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kukupotezea mwelekeo katika maisha yako:

1. Matumizi mabaya ya teknolojia: Kuwa mwathirika wa matumizi mabaya ya teknolojia k**a vile kuwa watumwa wa mitandao ya kijamii, michezo ya kubahatisha, au kutumia muda mwingi sana kwenye kompyuta au simu ya mkononi yanaweza kukupotezea muda na nguvu zako ambazo ungeweza kuzielekeza katika malengo yako.

2. Kukosa malengo na dira: Kukosa malengo na dira maishani kunaweza kukufanya ukose lengo la kuelekea na hivyo kujikuta unafanya vitu kwa nasibu tu. Ni muhimu kuweka malengo yako na kuanza kuweka mikakati ya kufikia malengo hayo.

3. Kukosa nidhamu ya matumizi ya fedha: Kutokuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha kunaweza kukufanya utumie pesa vibaya na hivyo kukupotezea mwelekeo katika maisha yako. Ni muhimu kujifunza kuhusu usimamizi wa fedha na kuweka mipango ya bajeti ili kuwa na udhibiti mzuri wa matumizi yako ya fedha.

4. Kujiingiza katika ulevi na madawa ya kulevya: Kuingia kwenye tabia ya ulevi au utumiaji wa madawa ya kulevya kunaweza kukusababishia matatizo mengi katika maisha yako. Inaweza kukupotezea mwelekeo na kukuletea athari kubwa kwa afya yako na maisha yako kwa ujumla.

5. Kukosa msaada wa kifedha na kijamii: Kukosa msaada wa kifedha na kijamii kunaweza kukufanya uhisi kutokuwa na matumaini na kukosa hamasa ya kuendelea na malengo yako. Ni muhimu kujenga mtandao wa msaada ambao unaweza kukusaidia kufikia malengo yako na kukupa nguvu ya kuendelea.

Ni muhimu kuwa makini na mambo haya ili kuweza kuepuka kupoteza mwelekeo katika maisha.

14/10/2023

Wazungu; Hey sir, you dropped your money.
Mbongo; ๐Ÿ‘€๐Ÿฅพ
๐Ÿ˜‚

14/10/2023

Amemwagiwa maji ya moto akiiba.

14/10/2023

Tafuta pesa chali yangu. Pesa haina mbadala.

Address

Kwa Limboa
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ๐‡๐€๐ƒ๐ˆ๐“๐‡๐ˆ ๐™๐„๐“๐” posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share