SINGIDA WAOMBA MABORESHO YA
UWANJA WA NDEGE WAKISHEREHEKEA UHURU
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego Amesema Uwekezaji Mkubwa unafanywa na Serikali Katika Sekta Mbalimbali Hasa ya Afya katika Mkoa wa Singida Unasadifu Maendeleo Makubwa yanayotokana na Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo yamefanyika Kimkoa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) RC Dendego Amesema Vifaa Tiba na Wataalamu Ambao wanaendelea Kutoa Huduma za Kitabibu kwa Wananchi Mkoa Singida ni Mafanikio Makubwa ambayo Kila Mwananchi Anapaswa Kujivunia Katika Maadhimisho Hayo.
Baadhi ya Viongozi walioshiriki katika Maadhimisho hayo wameiomba Serikali kuboresha Miundombinu ya Usafiri na Usafirishaji Hasa Uwanja wa Ndege ili kuchochea Maendeleo Mkoani Singida.
Cc @irundetz
#WasafiDigita
MWALIMU NYERERE ALIPOKEA UJUMBE WA KWENDA UMOJA WA MATAIFA AKIWA MPANDA
Leo Desemba 09 ni Maadhimishi ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, wazee mkoani Katavi wamesema kikao cha kwanza cha harakati za kupigania Uhuru kilifanyika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Akizungumzia historia hiyo wazee hao wamesema baada ya kikao hicho kufanyika mwalimu Nyerere na timu yake walipanda miti kama kumbukumbu ya kilichofanyika.
"Ilikufanya kumbukumbu ya mkutano wa kwanza walijenga hili boya na kumpanda hii miti miwili ya misufi, mwaka 1958-1959 Mwalimu Nyerere alikuja kutembelea Chama ndipo akatumiwa meseji telegram ikimtaka aende kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa,"
@official_bintihussein
#WasafiDigital
WATANZANIA WAHIMIZWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUWA NA TAIFA LENYE WATU WENYE AFYA NJEMA
Akizungumza Katibu tawala wa wilaya ya sumbawanga Gabriel Masinga kwenye maadhimisho ya miaka sitini na tatu ya uhuru( 63) wa Tanganyika yaliyofanyika katika wilaya ya sumbawanga vijijini amewahimiza wananchi kufanya mazoezi ili kujenga Taifa lenye afya na nguvu
Katika hatua nyingine masinga amewataka watanzania kuendelea kutunza mazingira ili kuondokana na majanga mbalimbali kama kukosekana kwa mvua, ukame na majangwa.
Kwa upande wao wadau wa mazingira wakala wa misitu Tanzania (TFS ) wilaya ya sumbawanga wametoa miche elfu moja (1000) ili kuunga mkono juhudi za serikali.
@risasiramadhankisumbul
#WasafiDigital
BIDEN: KUPINDULIWA KWA RAIS ASAD NI FURSA MUHIMU KWA KIZAZI CHA WATU WA SYRIA KUAMUA HATIMA YAO
🛑 Viongozi mbalimbali wa Dunia wameendelea kutoa hisia zao,baada ya waasi nchini Syria kutangaza kuuangusha utawala wa Bashar Al Assad na kumaliza miaka 50 ya utawala wa kiimla kutoka kwa familia ya kiongozi huyo.
🛑 Maelfu ya raia wa Korea Kusini wanaendelea kuandamana mbele ya Bunge la Seoul dhidi ya Rais Yoon Suk Yeol jana Jumapili siku moja baada ya rais huyo kukwepa kushtakiwa kwa tuhuma za sheria za kijeshi ambazo zimeikumba nchi hiyo.
🛑 Mtandao wa kundi la waokoaji wa kujitolea nchini Sudan umesema raia 28 wameuawa jana Jumapili wakati kituo cha mafuta kilichopo katika eneo la Khartoum chini ya udhibiti wa kundi la RSF kiliposhambuliwa kwa makombora.
Cc @irundetz
#YaliyomoDuniani
#WasafiDigital
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kati Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma Kwa mwezi huhudumia watoto 250 mpaka 400 wengi wao wakiwa ni ambao wamezaliwa kabla ya wakati.
Hayo yameelezwa na Daktari Bigwa wa Magonjwa ya watoto Hospitali hiyo Dkt. Julieth Kabengula wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya uongozi wa Hospitali hiyo kutembelea wodi ya watoto hao ikiwa ni kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara
Awali akizungumza na Wazazi wa Watoto hao ambao wanaendelea kupatiwa Huduma Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital hiyo ya BMH Prof. Abel Makubi ameitaka jamii kuachana na imani potofu ya kuwaficha watoto hao na kuwanyanyapaa Wazazi wanaojifungua watoto kabla ya wakati Kwa kuamini kuwa watoto hao ni mkosi
Mmoja ya Wazazi wanaendelea kupatiwa Huduma ya matibabu Cleopatra Wagira ameelezea namna ambavyo anapatiwa Huduma katika Hospitali hiyo lakini pia anavyojitahidi pia kumpatia joto Mtoto wake Kwa kukumbatia(kangaroo) ili aweze kukua Kwa haraka.
Cc: @carlosngonya
#WasafiDigital
OMO: 2025 HAPANA KURA YA SIKU MBILI ZANZIBAR
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Taifa, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ACT Wazalendo haitakubali Zanzibar kufanyika kura ya siku mbili.
Mheshimiwa Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo Jumatatu Disemba 09 2024, aliposhiriki akiwa Mgeni Rasmi, wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Vijana wa ACT-Wazalendo wa Mkoa wa Kati Kichama, huko katika Ukumbi wa Chama hicho, Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.
"Wajibu wetu ni kuilinda Katiba ya Zanzbar; kama ambavyo tuliahidi katika Kiapo, ili kupambania haki na kuwahudumia wananchi; hivyo tunaahidi 'Kura ya Mapema' haitojirudia Zanzibar".
Aidha Mheshimiwa Othman amesema Chama cha ACT Wazalendo siyo Wakala wa Ajira kama wafanyavyo vyama vyengine, bali dhima yake kuu ni kupigania haki na maslahi ya watu wote, bila ya ubaguzi. Amewahimiza Vijana kuacha kughilibiwa na kudanganywa, kwa kivuli cha kupewa ajira, na badala yake wasimame imara kutekeleza dhamira ya kuitafuta Zanzibar yenye Mamlaka Kamili.
Wakitoa salamu zao, Katibu wa Taifa wa Vijana, na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Mkoa wa Kichama wa Kati, wa Chama hicho, Ndugu Muhamed Khamis Busara, na Ndugu Suleiman Ali Seif, kwa nyakati tofauti wamesema kuwa, 2025 ni Mwaka wa Maamuzi na wa mabadiliko, ambapo vijana kwao ni wajibu kuwepo mstari wa mbele katika kulifanikisha hilo.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa Makongamano ya Ngome ya Vijana yanayoendelea, na yanayotarajiwa kufanyika Nchini kote, likibeba Kaulimbiu ya "Nafasi ya Vijana kuelekea Uchaguzi 2025 na Ukombozi wa Zanzibar"
Cc: @Baarakadon_
#WasafiDigital
HUDUMA ZA AFYA ZIMEIMARIKA TANGU TUPATE UHURU
Mkoa wa Shinyanga umeendelea kushuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya afya tangu Tanganyika ipate Uhuru mwaka 1961. Serikali, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imefanikiwa kuboresha miundombinu ya afya, kuongeza vituo vya kutolea huduma, na kuimarisha upatikanaji wa dawa na wataalamu wa afya, hali ambayo imeongeza ubora wa huduma kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania bara leo Disemba 09, 2024 yaliyofanyika kwenye kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wakizungumza na Wasafi Media wamesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma za afya kabla ya kupata uhuru ilikuwa si nzuri kutokana na ukosefu wa vituo vya afya na hospitali kwenye maeneo mengi hali iliyopelekea kutumia dawa za asili kwaajili ya matibabu huku wakina mama wajawazito wakipoteza maisha kwa kukosa huduma.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya imeendelea kuboresha huduma za afya tangu ilipopata uhuru.
"Kwa sasa huduma za afya kwenye mkoa wetu zimeboreshwa ambapo tuna Vituo vya afya 326, hospitali ngazi ya wilaya 9, zahanati 264 na kliniki 19, ukilinganisha na kabla ya kupata uhuru wa nchi yetu, zamani ili upate matibabu ni lazima uende kwa mganga wa kienyeji lakini kwa sasa huduma zote zinapatikana kila sehemu", amesema DC Mtatiro.
Cc: @officialkimoco
#WasafiDigital
ROYAL TOUR YAONGEZA IDADI YA WATALII HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA MAGAMBA || IDADI YA WATALII YAFIKA 5293 MWAKA 2024 KUTOKA 390 MWAKA 2021
Ikiwa imepita Miaka miwili ya Filamu ya Royal Tour iliyofanywa na Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Idadi ya Watalii katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Magamba imeendelea Kuongezeka hadi kufika watalii 5,293 mwaka 2024 kutoka watalii 390 kwa mwaka 2021.
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo kwenye Hifadhi ya Mazingira Asilia Magamba iliyohusisha Watalii kutembea kwa Miguu pamoja na Mbio za Baiskeli, Mkuu wa wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye amepongeza ubunifu huo kwani ambao unasaidia kuchochea ongezeko la Watalii na kutangaza Vivutio la Utalii.
Amesema Matembezi katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Magamba yanasaidia kujiepusha na Magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza, Kutengeneza furaha na wageni mbalimbali pamoja za zaidi wananchi kufahamu Utalii uliopo katika Hifadhi ya Mazingira Magamba
Kwa Upande wake Mhifadhi Mkuu wa Mazingira Asilia Magamba PCO. Christoganus Vyokuta amesema hifadhi hiyo inapatikana katika Wilaya za Lushoto na Korogwe yenye ukubwa wa Hekta 9283.9 na urefu wa mpaka wa KM 82 ambapo madhumuni ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo ni kutunza na kuendeleza Bionawai, kuendeleza udongo na uhifadhi wa vyanzo vya maji, kuendeleza utalii Ikolojia na kupunguza kasi ya matumizi hasi ya Rasilimali za Misitu
Cc @official_calvinbeda
#WasafiDigital
MIAKA 63 YA UHURU: "TUMEPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO, TUENDELEE KUWAENZI WAPIGANIA UHURU"
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Jawadu Mohamed amesema kuwa Taifa limeendelea katika Nyanya mbalimbali ndani ya Kipindi Cha miaka 63 ya uhuru huku akiwaasa Wananchi kuendelea kudumisha amani na mshikamano pamoja na kuwaenzi wapigania uhuru.
Jawadu ameyasema hayo leo Denver 9, 2024 wakati akihojiwa na Wasafi Media kuhusu miaka ya 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara
Jawadu amesema kuwa pamoja na Changamoto zilizopo lakini angalau kiwango Cha Watanzania wanaomiliki mali Kiko juu ukilinganisha na miaka iliyopita
Ndg. Jawadu ameongeza Kwa kusema kuwa ujinga bado upo na haujaisha na Kuna vita kubwa ya kuangamiza ujinga lakini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ya kuelimisha watu ili kuwaondoa katika ujinga
Aidha Ndg. Jawadu amesema kuwa Serikali imefanya mageuzi makubwa katika Huduma katika Sekta ya Afya Kwa kujenga majengo mbalimbali ya Huduma za Afya na ununuzi wa vifaa tiba
Cc: @carlosngonya
#WasafiDigital
WATALII WALIOPATA AJALI ZANZIBAR WASAFIRISHWA KWA NDEGE MAALUM NA ZIC
Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) kupitia huduma mpya ya Bima ya Wageni limepokea ndege maalum iliyokuja kwa ajili ya kusafirisha majeruhi wa ajali ya barabarani iliyotokea mwezi uliopita, ambao walikuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Lumumba.
Ndege hiyo ya kampuni ya AOM Air Ambulance iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume hapo juzi saa tano usiku, na kuondoka siku ya jana saa sita mchana ikiwa na wagonjwa hao wawili kuelekea nchini Hungary ambako wanakwenda kuungana na ndugu, jamaa na marafiki.
Aidha, gharama zote za kukodi ndege hiyo maalum pamoja na matibabu yote zimelipwa na bima ya lazima ya wageni wanaoingia Zanzibar ambayo wageni hao walikuwa nayo wakati wa ajali.
cc: @rashidbattashy
#WasafiDigital
MIAKA 63 YA UHURU, WATANZANIA WAASWA KUWA NA MIOYO YA KUJITOLEA KULIENDELEZA TAIFA
Katika maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika, Watanzania wameaswa kuwa na mioyo ya kujitolea pamoja na uzalendo na kushiriki kikamilifu katika juhudi za kulijenga na kuliendeleza taifa.
Akihutubia Desemba 8, 2024 katika kongamano la miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara sherehe za uhuru lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu Muhonda, Wilayani Mvomero, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndg. @saidnguya amewahimiza wananchi kuenzi uhuru walioupata kwa kujituma, kushirikiana, na kuchangia maendeleo ya nchi katika sekta zote.
"...utapewa unachopewa lakini lazima tutangulize moyo wa kujitolea ndiyo silaha ya maendeleo yetu..." amesisitiza Ndg. Nguya.
Akinukuu maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa mwaka 1988 wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tabora, Mwl. Nyerere alisisitiza kuwa "kama tunataka kupata maendeleo ya haraka ni lazima kama nchi tujenge mioyo ya kujitolea".
Aidha, Katibu Tawala huyo amewataka vijana, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini, kutumia fursa zilizopo kujenga taifa lao kwa moyo wa kujitolea, ubunifu, na uzalendo, huku akisisitiza kuwa roho ya kujitolea ni urithi unaopaswa kudumu kwa vizazi vyote.
Sherehe za uhuru mwaka huu 2024 zinatawaliwa na kaulimbiu inayosema "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu"
Cc: @Barakadon_
#WasafiDigital