02/01/2025
🚨 KLABU ya Yanga inasemekana inaelekea kukamilisha usajili mmoja mkubwa ambao inatarajia kuutangaza hivi karibuni na kushtua nchi, huku taarifa zikisema imeingilia kati dili la Simba la kumwania straika anayeongoza kwa mabao mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, Elvis Rupia.
Awali Simba ilitajwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Kenya na tayari mazungumzo yalishaanza baina ya pande hizo.
Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe, alisema kipindi hiki cha dirisha dogo Yanga inafanya usajili wa kuboresha kikosi chake na wanamalizia vitu vichache tu ili kuweza kumtangaza mmoja wa wachezaji ambaye atakuwa gumzo kwenye usajili kipindi hiki.
Hata hivyo, habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa ilikuwa kwenye harakati za mwisho kupata saini ya Rupia na ndio wanatarajia kumtangaza wakati wowote kuanzia sasa akitokea Singida Black Stars.
Follow