𝗥𝗔𝗗𝗜 𝟮𝟰/𝟳

𝗥𝗔𝗗𝗜 𝟮𝟰/𝟳 Huu ni ukurasa unaojihusisha na habari za kimataifa katika nyanja ya siasa, biashara, sayansi na teknolojia pamoja na michezo.

Ni rasmi hivi sasa Jeshi la Iran linamiliki ndege za kivita za kisasa za Urusi zinazojulikana k**a SU-35By:Abdull Najad ...
29/01/2025

Ni rasmi hivi sasa Jeshi la Iran linamiliki ndege za kivita za kisasa za Urusi zinazojulikana k**a SU-35
By:Abdull Najad Faiq

Aliyekua waziri wa usalama wa Israel Ben Gvir:"Kurudi kaskazini mwa Gaza kwa raia wa Palestina kunaonesha kushinda kwa u...
28/01/2025

Aliyekua waziri wa usalama wa Israel Ben Gvir:"Kurudi kaskazini mwa Gaza kwa raia wa Palestina kunaonesha kushinda kwa upinzani dhidi ya Israel.
By:Abdull Najad Faiq

Wadukuzi wa Iran walivunja mifumo ya usalama ya tahadhari ya Israel katika shule za chekechea na shule kadhaa za Israeli...
28/01/2025

Wadukuzi wa Iran walivunja mifumo ya usalama ya tahadhari ya Israel katika shule za chekechea na shule kadhaa za Israeli na kutangaza ujumbe kwa Kiajemi kupitia vipaza sauti.
By:Abdull Najad Faiq

KUACHILIWA KWA MATEKA WA ISRAEL NA WAFUNGWA WA PALESTINA,NAKISI NA MANTIKI YAKENa:Abdull Najad FaiqAwali wa yote msingi ...
27/01/2025

KUACHILIWA KWA MATEKA WA ISRAEL NA WAFUNGWA WA PALESTINA,NAKISI NA MANTIKI YAKE
Na:Abdull Najad Faiq
Awali wa yote msingi wa makubaliano haya ni kuonesha kwamba kuna kitu hakipo sawa baina ya jami 2 hizi
Palestina na Israel ni jamii 2 tofauti,Palestina ikiwa ni jamii ya Waarabu yenye mchanganyiko wa Waumini wa dini ya Ukristo pamoja na Uislam,Israel ikiwa ni jamii ya Waumini wa dini ya Kiyahudi na kabila la Uyahudi

Kwa miaka nenda miaka rudi Serikali ya Israel imekua ikiwashikilia mateka na wafungwa raia wa Palestina wapatao 5000,wapo waliodumu magerezani kwa muda wa miaka 39 ila ajabu ya yote hakuna mtu wala mamlaka yoyote yenye nguvu duniani iliyowahi kemea wala kukosoa jambo hili,kanakwamba jela za Israel zilijengwa kwa ajili ya kuhifadhi raia wa Palestina pekee, ambao hawapo chini ya mamlaka za Israel
Hamas walipokuja kuwachukua wafungwa raia 200 wa Israel dunia nzima iliripuka,kanakwamba wao Hamas ndio wa kwanza kufanya hivyo

Hakika makubaliano hayo yamefichua kwamba kuna dhulma kubwa wanayo fanyiwa raia wa Palestina ndani ya magereza ya Israel,kinachofanya jicho lako lisione hilo ni ile imani uliyolishwa ama ni kutokana na kwamba wanaofanya uovu huo Israel ni jamii yenye pesa na ushawishi katika taifa kubwa kijeshi duniani la Marekani

Ni jambo la ajabu mno kuona kwamba mipaka baina ya Israel na Palestina ilisha amuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1967,Umoja wa Mataifa ambao ndio ulio wazawadia nchi ya Israel Wayahudi mwaka 1947 kutokana na madhila waliyokua wakiyapata katika ardhi za Ulaya hadi kupelekea Wayahudi wapatao milioni 6 kuuwawa na Hi**er
Marekani imesimamiwa kugawanywa kwa nchi ya Sudan pamoja na uhuru wa kisiwa cha Taiwan dhidi ya China cha ajabu leo Marekani baba wa demokrasia duniani anapatwa na kiwewe kusimamia uhuru wa Palestina kisa ipo dhidi ya mshirika wake ambae ni Israel

Ikiwa Wayahudi watakua na haki dhidi ya ardhi ya Palestina kwa mgongo wa Biblia kuliko jamii za Wakristo na Waislam wa Palestina basi watuambie Wayahudi je ni Mungu gani aliyewapa wao ardhi, je!ni Mungu huyu wao wanao muabudu Wayahudi ama ni Mungu yule anae abudiwa na Wakristo ikiwa wao ni wakweli?

Kwa hakika mgogoro huu hauhusu udini bali unahusu haki na mamlaka baina ya jamii tajiri za Wayahudi pamoja na jamii maskini za Waarabu wa Palestina

Jamii za Wayahudi zimetapakaa sehem mbali mbali duniani,tena wakiwa hadi viongozi wakubwa ndani ya nchi ya Marekani pamoja na nchi za Ulaya lakini Wayahudi hao wanaishi katika nchi hizo kwa amani,wamewekeza na wala kamwe hawajawahi kuhamishwa wala kubaguliwa sasa kwanini leo iwe ni vurugu,manyanyaso pamoja na mauaji dhidi ya jamii ya Palestina wanayofanyiwa katika ardhi zao?

Ni ngumu kuishi na jamii za Wayahudi wa kizayuni ambao wanaamini ardhi yote ya Mashariki ya kati ni yao,hakika hata raia wote wa Palestina wahamishwe Misri na Jordan basi hapo mbeleni kutazuka mgogoro mpya baina ya Israel dhidi ya Misri,Syria,Jordan na baadae dhidi ya Iraq na Saud Arabia sababu katika nchi zote hizo kuna maeneo Serikali ya Israel inaamini ni yake,ikirejelea mpango wake wa "The great Israel" wa kuunda nchi kubwa ya Kiyahudi duniani,je!hamuoni kwamba Israel ndio tatizo?

Kwa wale wenye ajenda za kidini watambue kwamba Uislam upo karibu zaidi na dini ya Ukristo kuliko Uyahudi sababu Uislam haupingi kuhusu Yesu(Masihi Issa) ila unaamini kuwa Yesu alikua tu ni Nabii wa Mungu,ila dini ya Uyahudi haiamini chochote kuhusu Yesu bali inaamini Yesu alikua ni mtoto wa zinaa
Wayahudi wanaamini kupitia Nabii wao M***a ambae dini zote Uislam na Ukristo unamuamini kuhusu Unabii wa M***a,swali katika jamii hizi 3 ni ipi jamii korofi na iliyo kinyume zaidi?

Kuhitimika kubadilishana wafungwa baina ya Israel dhidi ya Hamas hakuwezi kutoa hakikisho la amani kwa raia wa Palestina,sababu Israel wana jeshi na kamwe hawazingatii sheria za kimataifa,mfano ilivyo sasa jeshi la Israel linafanya uharibifu wa miundombinu ya kiraia Ukingo wa Magharib wa Palestina ajabu utajiuliza je wanagombana na nani ikiwa wao na hasimu wao Hamas wametia sain ya kusitisha mapigano?

Suluhu pekee ya kupatikana kwa amani ya kudumu Mashariki ya kati ni kule Israel kuheshimu sheria za kimataifa pamoja na mipaka iliyowekwa na Umoja wa Mataifa na pili ni kuhakikisha Palestina inapata uhuru, k**a vile Israel ilivyo na haki ya kujilinda vile vile Palestina nao wana haki ya kujilinda dhidi ya maadui zao.

Kuanza kwa uvamizi pamoja na mauaji mapya ya Jeshi la Israel katika maeneo ya Palestina yanayozibitiwa huko Ukingo wa Ma...
24/01/2025

Kuanza kwa uvamizi pamoja na mauaji mapya ya Jeshi la Israel katika maeneo ya Palestina yanayozibitiwa huko Ukingo wa Magharib,baada ya usitishaji vita huko Gaza,Ukingo wa Magharib sehem ambapo hakuna utawala wa Hamas je hii imanaanisha tatizo la Palestina ni Hamas ama ni kukosa Uhuru wao?
NB: Wajuzi tujuzeni
By:Abdull Najad Faiq

Hati za ndani zilizopatikana na The Washington Post zinaonyesha ushirikiano kati ya Google na Wizara ya Ulinzi ya Israel...
22/01/2025

Hati za ndani zilizopatikana na The Washington Post zinaonyesha ushirikiano kati ya Google na Wizara ya Ulinzi ya Israeli na IDF wakati wa vita huko Gaza, ambavyo vilianza mara tu baada ya Oktoba 7, 2023.
Hati hizo zinaonyesha jinsi kampuni hiyo ilivyoruhusu ufikiaji wa teknolojia zake za hali ya juu za kijasusi kwa vikosi vya usalama, kinyume na taarifa zake kwa umma kujaribu kujitenga na matumizi ya kijeshi ya teknolojia yake kwa Jeshi la Israel
By:Abdull Najad Faiq

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Jewish Power kimetangaza kuwa kinaiacha serikali ya Israel kwa kupinga makub...
21/01/2025

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Jewish Power kimetangaza kuwa kinaiacha serikali ya Israel kwa kupinga makubaliano ya kusitisha mapigano, na kumwacha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akiwa amesalia na wabunge wachache.

Waziri wa usalama wa taifa Itamar Ben-Gvir, pamoja na Yitzhak Wasserlauf na Amichai Eliyahu, wamewasilisha barua zao za kujiuzulu leo ​​asubuhi.

Ben-Gvir kwa muda mrefu amekuwa mpinzani mkubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano, na ameshinikiza Israel kuendelea na operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Hamas huko Gaza.

Akimwandikia Netanyahu kutangaza kujiuzulu, Ben-Gvir alisema hatafanya kazi ya kupindua serikali, lakini akataja makubaliano ya kusitisha mapigano kuwa "ushindi kamili kwa ugaidi".
By:Abdull Najad Faiq

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuondoa kizuizi cha utawala wa Biden juu ya usambazaji wa mabomu ya pauni 2,00...
21/01/2025

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuondoa kizuizi cha utawala wa Biden juu ya usambazaji wa mabomu ya pauni 2,000 kwa Israeli katika siku zake za kwanza ofisini, Walla News iliripoti Jumatatu, ikinukuu mahojiano na mjumbe wa Israeli huko Washington

Utawala wa Biden uliwahi kuzuia leseni ya usambazaji wa bomu hayo kwa Israel kutokana na hofu yao dhidi ya uharibifu uliokua ukiendelezwa na Jeshi la IDF huko Gaza .
By:Abdull Najad Faiq

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu alifuta vikwazo vilivyowekwa na utawala wa zamani wa Biden dhidi ya makun...
21/01/2025

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu alifuta vikwazo vilivyowekwa na utawala wa zamani wa Biden dhidi ya makundi ya walowezi wa mrengo wa kulia wa Israel na watu binafsi wanaotuhumiwa kuhusika na ghasia dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, tovuti mpya ya White House ilisema. Tovuti hiyo ilisema Trump alibatilisha Amri ya Utendaji 14115 iliyotolewa Februari 1, 2024, ambayo iliidhinisha kuwekwa kwa baadhi ya vikwazo "kwa Watu Wanaodhoofisha Amani,
By:Abdull Najad Faiq

Kulingana na ripoti ya Inspekta Jenerali wa Pentagon, serikali ya Marekani imetoa msaada wa zaidi ya dola bilioni 182 kw...
21/01/2025

Kulingana na ripoti ya Inspekta Jenerali wa Pentagon, serikali ya Marekani imetoa msaada wa zaidi ya dola bilioni 182 kwa kufikia Desemba 2024, wakati mishahara ya wazima moto wa Marekani katika jimbo la California haijaongezeka kwa miongo minne na Kulingana na ABC News, ripoti, serikali ya Marekani imepeleka wafungwa elfu moja kuzima moto huo.
By:Abdull Najad Faiq

Jeshi la Israel IDF limeanza tena kuk**ata mateka raia wa Palestina katika eneo la West Bank masiku machache baada ya ku...
21/01/2025

Jeshi la Israel IDF limeanza tena kuk**ata mateka raia wa Palestina katika eneo la West Bank masiku machache baada ya kuanza kwa utekelezaji wa kubadilishana wafungwa baina ya Israel na Hamas.
By:Abdull Najad Faiq

MIZANI HURU YA HAKI BAINA YA ISRAEL NA PALESTINANa:Abdull Najad FaiqHakika kila binaadam mwenye imani na akili timam, ku...
20/01/2025

MIZANI HURU YA HAKI BAINA YA ISRAEL NA PALESTINA
Na:Abdull Najad Faiq
Hakika kila binaadam mwenye imani na akili timam, kupata uzima na maisha yaliyo mazuri ndio lake tumainio
Ikiwa Serikali ya Israel na Hamas zimeingia katika mkataba wa kusitisha vita,jambo ambalo limeibua furaha na vifijo kwa wapendwa wa pande zote 2 ambao ndugu,jamaa,vipenzi na watoto wao walikua wakizuiliwa vizuizini huko Gaza pamoja na Israel, basi je! Pande zote hizi mbili zinahitaji nini zaidi ya amani na utulivu kwa wananchi wa?

Historia inaonesha ni ngumu kupatikana utulivu baina ya Israel na Palestina,wale walio wadini huwa wanatoa hoja kwamba Wayahudi walipewa ardhi ya Palestina na Mungu hivyo wana haki kuiporoa ardhi yote ya Mashariki ya kati kinguvu pasina kuangalia sheria za kimataifa,basi na tuupime mgogoro huu katika mizani ya haki na uhuru ili tuupate ukweli wa mambo

Katika ulimwengu wa kimataifa unatoa haki kwa kila mtu kuamini na kuabudu chochote kile ndiomaana hakuna mdahalo utaoweza kufanywa katika ulimwengu huu na watu wote duniani tukakubaliana kwa pamoja kwamba dini fulani ndio dini ya kweli na ya haki

Walio wadini wanatuambia kwamba Wayahudi walipewa ardhi ya Palestina na Mungu, ila zimeshapita karne na tawala nyingi wakiwemo Warumi na Ottoman Empire ambao waliwahi kuitawala ardhi ya Palestina pamoja na maeneo mengine ya Ulaya na Arabuni

Wayahudi wanao unda Serikali ya Israel hawakuwahi na wala hawamuani Yesu hadi sasa,Wayahudi wana kitabu chao kinachoitwa Tora,Wayahudi hawaiamini Biblia sasa iweje leo kitabu ambacho Wayahudi wasicho kiamini leo iwe ni rejea ya ushahidi wao ili kuwafukuza Wapalestina na kuchukua ardhi zao kinguvu?
Ukiacha hilo Ukristo umegawanyika madhehebu chungu nzima na kila dhehebu linatofautiana Biblia yake swali je! Hivi ni nani atakae tupa uthibitisho usio na shaka kwamba Wayahudi hawakuchakachua Biblia ili kujipendelea?
Je! Waisrael walio zungumziwa katika Biblia ndio hawa Wayahudi wa leo na ni kwanini Wasiwe wafuasi wa dini ya Kikristo badala yake waabudu katika imani ya Uyahudi?,imani ambayo ibada zake ni tofauti na ibada za kikristo?
Je!kati yangu mimi na wewe ni nani mdini?

Kwa hakika inawezekana kabisa jamii za Waarabu wa Palestina pamoja na jamii za Wayahudi wa Israel kuweza kuishi jirani na kwa amani,kilichopo ni kurejea katika mipaka iliyo amuliwa na Umoja wa Mataifa 1947 kwamba ardhi ya Palestina inapaswa kuundwa mataifa mawili huru,Taifa la Kiyahudi ambalo litamiliki ardhi kwa 55% na Taifa la Waarabu wa Palestina ambao watamiliki 45% ya ardhi ambayo hapo nyuma ilikua katika miliki ya Ottoman Empire baadae ikawa chini ya umiliki wa England

Ikiwa tutatumia mizani huru ya haki basi tutajua kwamba hakuna haki ya Serikali ya Israel kuwashikilia wafungwa raia wa Palestina wapatao 10,000 ambao hawaishi ndani ya ardhi ya Israel
Ardhi ya Palestina ambayo walipewa 45% na Umoja wa mataifa hivi sasa imebakia 23% pekee,Je!ikiwa wewe ni mkweli na mpenda haki siku raia wa Palestina wakiamua kusimama katika mipaka yao waliyopewa na Umoja wa Mataifa je!ni nani sasa watakua wenye makosa baina yao na Wayahudi wa Israel?

Tunapaswa tuangalie na tupime kila kitu katika mizani ya haki ikiwa tutasimama katika udini kamwe hatuwezi kupata suluhisho la hili
Hem fikiria Wakoloni waliligawa Bara la Afrika katika mipaka ambayo leo tunatumia na tunajivunia kiasi kwamba baadhi ya makabila yakajikuta yakiwa nchi 2 tofauti,hem fikiria Wamasai wa Kenya wakiamua kurudi Tanzania leo kuja kudai ardhi za mababu zao na asili zao je Tanzania itakalika na kuwa na amani?
Fikiria Black Amerika waliopo U.S.A wakiamua kurudi Afrika katika ardhi za asili na mababu zao je!dunia itakua ni sehem salama ya kukalika?
Fikiria kuhusu maeneo waliyokua wakimiliki dola kubwa zilizopita k**a Roman na Ottoman leo hii wakitaka kuyarudisha je!itakuaje
Je!Tanzania tunaweza kurudi tena katika tawala za kichifu zenye kuongoza vijiji na zenye mamlaka kamili k**a ilivyokua awali?

Kamwe hutoweza kuyajibu hayo maswali ikiwa wewe sio mtu wa haki na amani

Gaza hata ikiwa Hamas wataondoka ila mgogoro hauwezi kuisha sababu Serikali ya Kiyahudi ya Israel haiwezi kuwatendea haki raia wa Palestina,suluhisho ni kwa Palestina kuachiwa huru wajiongoze namna wanavyotaka wao wenyewe k**a mataifa kwengine

Kuingiliwa kwa uhuru wa Ukrain kujiunga na NATO dhidi ya Urusi kumepelekea vita baina yao wawili sembuse Israel kuidhibiti Gaza kwa kila kitu kuanzia ardhi,anga hadi bahari unategemea itasababisha nini k**a sio vurugu na uasi?.

KUSHINDWA KIVITA KIMALENGO KWA ISRAEL DHIDI YA HAMAS no:2Na:Abdull Najad FaiqNiendelee kwa kutoa ufafanuzi zaid,watu wan...
19/01/2025

KUSHINDWA KIVITA KIMALENGO KWA ISRAEL DHIDI YA HAMAS no:2
Na:Abdull Najad Faiq
Niendelee kwa kutoa ufafanuzi zaid,watu wanatakiwa watambue kwamba Gaza hakukuwa na vita bali kulikua na mauji ya holela ya makusudi na k**a utakua ulifuatilia vyombo vya habari utagundua kwamba mauaji yaliyokua yakifanywa na jeshi la Israel yaliwalenga pia wale wanaotoa misaada ya kibinaadam kwa raia wa Gaza,iliwahi kutokezea wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu raia wa Marekani,Ufaransa na Uingereza waliuwawa na mashambulizi ya jeshi la IDF kiasi kwamba ikapelekea kuibuka kwa sitofaham baina ya Israel pamoja na washirika wake
Sio hivyo tu idadi ya waandishi wa habari wa Palestina wanaokadiriwa 200 pia waliuwawa kupitia mashambulizi ya Jeshi la Israel,miundombinu ya kiraia pamoja maeneo ya kambi za wakimbizi nazo pia hazikuachwa salama katika gharika hiyo

Kuna watu ni wajinga sana na hata ukitumia miaka 100 kamwe hutoweza kuwafuta ujinga wao
Miongoni mwao ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya vita pamoja mauaji ya raia,mfano ukiiangalia vita vya Urusi na Ukrain kulikua na shutma kwamba Jeshi la Ukrain linawatumia raia k**a ngao ya kivita lakini kamwe hatukuwahi kuona hadi leo Urusi kulisambaratisha jengo lolote la ngorofa hata 3 la kirai huko Ukrain
Lakini haya yamefanyika ndani ya ardhi ya Gaza,hivi ni nani angeamini kwamba jengo la ghorofa 11 linaweza kudidimia lote chini ya ardhi na kubakia vifusi vitupu baada tu ya kuangushiwa bomu moja?
Nadhani watu wanaojaribu kuzima haki kwa hoja za udini wao ndio wadini

Nawaambia tena malengo ya Israel kivita kamwe hayajatimia na wala hayawezi kutimia
~Israel inahitaji kuwahamisha raia wote wa Gaza ama nusu yake ili kujenga makaazi ya raia wake Walowezi wa kiyahudi
~Israel inahitaji kuona kwamba Hamas hawatawali tena ndani ya Gaza wala hawapati nguvu zozote za kijeshi
~Israel inatamani kulikalia eneo lote la Gaza kijeshi na kulizibiti k**a ilivyokua kabla ya kujiondoa mwaka 2005,lakini kinacho kwamisha malengo yote hayo ni kule Jeshi la IDF kushindwa kuwagomboa mateka wao wote na kwa wale wachache walioweza kuwagomboa walihitaji msaada wa makomandoo wa Marekani sambamba na kufanya shambulizi kubwa lililo pelekea kuuwawa kwa mateka wao wengine walio wengi kuliko mateka walio wagomboa
Hakika huku ndipo kufeli kivita,licha ya mauaji makubwa yaliyofanywa na jeshi la Israel lakini nguvu kamwe imeshindwa kuwa suluhisho la kuwapata mateka badala ya njia ya mazungumzo ama diplomasia ambayo hapo mwanzo waliikataa

Ikiwa kuyasema haya unaniita mimi mdini basi tuambie wewe usie mdini ni sababu gani inayo ifanya Israel kuchukua kinguvu maeneo ya Palestina pamoja na maeneo ya kule Syria ilhali Umoja wa Mataifa tayari ulishachora mipaka ya kila mmoja na uliamua yawepo mataifa mawili huru lile la Israel pamoja na taifa la Palestina ambayo yatakua yanaishi jirani?

Hakika kuna tofauti kubwa sana kati ya haki na uonevu,mtu huyu anaeshangiria mauji yanayofanywa na Wazayuni wa Israel kwa kisingizio kwamba ardhi ile wamepewa na Mungu ndie huyu huyu anae itukana Serikali kwa kuwaondoa Wamasai katika mbuga za wanyama ilhali wao Wamasai walipewa ardhi ile na Serikali waishi kwa muda je!iweje sasa leo iwe ni halali Wapalestina watolewe katika ardhi za mababu zao kwa kisingizio kwamba ardhi ile kuna jamii fulani wamepewa na Mungu,Mungu ambae wao wenyewe Wayahudi hawamuamini?
Hakika hili linatafikirisha kwa kila aliye na mazingatio

Sisi sote tunajua kwamba vita ni vibaya na madhara yake yanawaathir zaid wanawake,watu wazima na watoto lakini kutokana na uchu wa ardhi pamoja na roho mbaya ya kikatili waliyonayo viongozi wa Israel dhidi ya Wapalestina kamwe hawawezi kuwa radhi wawaache Wapalestina waishi kwa amani katika ardhi zao,na hiki ndicho kilichopo

Ikiwa bado unafikiri mateka ndio sababu ya uharibifu pamoja na mauji yanayofanywa na jeshi la Israel huko Gaza basi na tujiulize je kipi wanatakiwa wafanye Wapalestina wapatao elfu10 waliochukuliwa katika ardhi yao ya Gaza na kufanywa wafungwa katika magereza ya Israel?
Je!ni ipi tofauti kati ya mfungwa wa kipalestina na mateka wa kiyahudi wa Israel ikiwa wote wanadhulumiwa?

Ulimwengu unapaswa upimwe katika mizani ya haki,vita vimeonesha na kuthibitisha kwamba haviwezi kuibua mshindi aliye kamili lazima pande zote zipate hasara ,Israel nao wamepoteza askari wao wasiopungua 1000 Gaza pekeyake na zaidi ya 4000 kubaki majeruhi na walemavu,hakika mama na ndugu wa askari wa vijana hawa ndio wanao umia na sio wewe Myahudi wa kwampalange unaekula ugali kwa mlenda nyumbani kwako kwa raha kabisa

Israel imeshindwa kivita kwa kushindwa kutimiza malengo yake huko Gaza na ndiomaana wanatafuta kila sababu kupitia support pamoja na nguvu kubwa ya Marekani waweze kuviendeleza tena hivi vita baada ya kupatiwa wafungwa wao

Daima mwenye kushindwa huwa na hasira na asiye kubali hitimisho la mpambano.

Bbc wametoa habari hii,kuna Wayahudi wa Buza kwampalange jana niliwaandikia makala kuhusu kushindwa kwa Israel kivita dh...
19/01/2025

Bbc wametoa habari hii,kuna Wayahudi wa Buza kwampalange jana niliwaandikia makala kuhusu kushindwa kwa Israel kivita dhidi ya Hamas ila wakanibishia someni sasa, mimi daima huwa sikurupuki naandika vitu vya ukweli mtupu inahitaji uwe na akili ndipo uweze kuchanganua ukweli uliopo,laasivyo k**a akili zako ni za kushikiwa utabakia mbumbumbu maisha.
By:Abdull Najad Faiq

(Gazeti la Times of Israel jan 18/2025).Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema Jumamosi kuwa limefanya maandalizi yote muhim...
19/01/2025

(Gazeti la Times of Israel jan 18/2025).Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema Jumamosi kuwa limefanya maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kusitisha mapigano na Hamas huko Gaza, ambayo yalipangwa kuanza saa 8:30 asubuhi Jumapili. Jeshi pia lilisema liko katika tahadhari kubwa kwa hali mbalimbali ambazo zinaweza kutokea wakati usitishaji mapigano unaanza na walikuwa tayari "mara moja" kurejea kwenye mapigano ikiwa mapatano hayo yatasambaratika wakati wowote. Katika taarifa, IDF ilisema imeanza "kutekeleza taratibu za utendakazi" ambazo makubaliano yanaelekeza, ikimaanisha uondoaji wa wanajeshi wa IDF kutoka maeneo yenye watu wengi ndani ya Gaza hadi maeneo fulani ambayo yamekubaliwa. Siku moja, Kamandi ya Kusini itafanya kazi ya kupeleka tena wanajeshi ndani ya Ukanda wa Gaza, na kujiondoa katika maeneo ya mijini na kuwaweka kwenye njia ambazo zilikubaliwa kati ya Israel na Hamas. Idadi kubwa ya vikosi vitakuwa vinazunguka wakati wa usiku na saa za asubuhi, IDF ilisema.
By:Abdull Najad Faiq

TEL AVIV/CAIRO, Jan 18 (Reuters) - Israel iliidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi la wanamgambo wa Pales...
19/01/2025

TEL AVIV/CAIRO, Jan 18 (Reuters) - Israel iliidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas siku ya Jumamosi ambayo yanahusisha kuwaachilia mateka katika Ukanda wa Gaza, na vikosi vya Israel vilifanya mashambulizi mapya katika eneo hilo kabla ya kuanza kwa makubaliano hayo siku ya Jumapili. Makubaliano hayo ya awamu tatu yanatazamiwa kusitisha vita vilivyodumu kwa miezi 15 kati ya Israel na watawala wa Gaza Hamas ambayo yameliangamiza kabisa Ukanda wa Gaza, kuua makumi ya maelfu ya Wapalestina na kuyumbisha Mashariki ya Kati.
Vita hivyo vilichochewa na shambulio la Hamas Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israeli ambapo watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 250 kuchukuliwa mateka, kulingana na hesabu za Israeli. Zaidi ya wanajeshi 400 wa Israel wameuawa katika mapigano huko Gaza tangu wakati huo. Baraza la mawaziri la Israel liliridhia makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yanalenga kusitisha mapigano na kuona kuachiliwa kwa makumi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas ili kuwalipa Wapalestina wengi waliofungwa jela nchini Israel. Hatua yake ya kwanza itachukua wiki sita.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema kuwa Israel bado inasubiri orodha ya watu waliotekwa nyara kuachiliwa na ina haki ya kuanzisha tena vita, ikiungwa mkono na Marekani, iwapo hatua ya pili ya usitishaji vita itatoweka. "Ikiwa lazima turudi kwenye mapigano tutafanya hivyo kwa njia mpya, zenye nguvu," Netanyahu alisema katika taarifa yake ya video. Huko Gaza, ndege za kivita za Israel zimeendeleza mashambulizi tangu makubaliano hayo yalipokubaliwa, na kushambulia eneo hilo siku ya Jumamosi.
By:Abdull Najad Faiq
NB:Leo nimekuja na chanzo cha habari anaeweza akaitafute,kuna mijitu ni migumu kuelewa kuwa Wazayuni wa Israel kinacho wauma ni kufeli kwao kuichukua Gaza pamoja na kuitokomeza Hamas,Serikali ya Israel wao na haki pamoja na amani ya ulimwengu ni vitu viwili tofauti

KUSHINDWA KIVITA KWA ISRAEL DHIDI YA HAMAS KATIKA MJENGEKO WA KIMALENGONa:Abdull Najad FaiqDaima dhamira ndiyo inayo amu...
18/01/2025

KUSHINDWA KIVITA KWA ISRAEL DHIDI YA HAMAS KATIKA MJENGEKO WA KIMALENGO
Na:Abdull Najad Faiq
Daima dhamira ndiyo inayo amua hatma ya mtu,kufanikiwa ama kufeli kwa mtu yeyote kunategemea ni ipi ilikua haswa dhamira yake na kwa kiwango gani ameweza kuitimiza,je amepata zaidi ama amepoteza?
Naam na hivi ndivyo ninavyoweza kuianza makala yangu

Kushindwa kwa Israel kunaanzia kwa kupoteza sifa yake ya kidiplomasia Ulimwenguni kutokana na kuingia kashfa kubwa ya kufanya uhalifu wa kivita kupitia mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza
Hakika hii sio fedheha kwa taifa la Israel pekee,taifa ambalo watu wake wanajinasibihisha na utukufu kutoka kwa Mungu wa haki na mpenda amani bali ni fedheha pia na ni aibu kwa Serikali ya Marekani ambayo kwa miaka mingi imejipambanua kwamba ndie mtetezi wa haki za watu pamoja na demokrasia ya Ulimwengu,silaha zake hazikufanya mauaji ya kutisha pekee bali zilimpa kiburi mshirika wake Israel kuweza kuminya hata haki muhim za raia wa Gaza kuweza kupata chakula,maji safi pamoja na madawa hivyo kutumia njaa k**a silaha ya kivita,kitendo ambacho kamwe hakikubaliki katika Ulimwengu wa kimataifa

Kushindwa kwengine kwa Israel kunatokana na kushindwa kufikia malengo ya kauli yao kwamba hawato kubali kusitisha vita dhidi ya Hamas hadi wahakikishe kwamba Hamas wamesambaratishwa na kamwe hawatoweza kuwa tishio tena,ila tumeendelea kusikia Israel wakilalama kwamba Hamas inajipanga upya tena na kurudi maeneo ambayo kulingana na Israel ni kwamba yalikua tayari yamesha safishwa kivita na jeshi la IDF

Bado Israel imeshindwa kuidhibiti kikamilifu Gaza na kulingana na mkataba wa kusitisha vita,Jeshi la IDF litalazimika kujiondoa katika maeneo ya Gaza ambayo yalikua tayari katika miliki yao

Kushindwa kwengine kunako jitokeza ni kule kufeli kwa mpango wa Israel kuwahamisha raia wa Gaza kwa lazima katika maeneo yao kwani kupitia mkataba walio ingia kuna kipengele cha raia wa Palestina kurudi katika maeneo yao kikamilifu na pia kuruhusu misaada ya kibinaadam iingie ndani ya Gaza pasina vikwazo

Pia Israel italazimika kusitisha mpango wake wa ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi katik ardhi ya Gaza,hilli litakua ni pigo kubwa kwa Serikali ya mrengo wa kulia ya Israel,ambayo daima imekua ikiota kuhusu kunyakua zaid maeneo ya ardhi ya Palestina,ikumbukwe ardhi ndiyo kiu isiyokauka ya raia wa Israel na ndio sababu ya mgogoro huu wote pamoja na uvamizi unaofanywa na jeshi la IDF katika maeneo mengine mfano huko Syria

Swali la kujiuliza je usitishaji huu wa vita utakua ni wa kudumu ama ni swala la muda tu?

Kwa hakika Serikali ya mrengo wa kulia ya Israel itatafuta kila njia za kuibua vita na migogoro mashariki ya kati,lengo likiwa ni kunyakua ardhi zaid kupitia msaada usio yumba wa Trump,kutulia na kupatikana kwa amani mashariki ya kati kutategemea na nia ya dhati ya Trump ya kuto hitaji kuingiza Marekani katika vita yoyote duniani,ikumbukwe Iran bado haijalipiza kisasi chake dhidi ya Israel
Hivi sasa Iran itakua inasoma ramani na matendo ya Rais mpya wa Marekani Trump dhidi ya kuiuunga mkono kivita Israel dhidi ya washirika wake Iran wanaojulikana k**a "Mhimili wa Upinzani".

Iran na Urusi kuingia makubaliano ya kuondosha vikwazo baina yao katika mnyororo mzima wa usafirishaji wa mazao ya chaku...
17/01/2025

Iran na Urusi kuingia makubaliano ya kuondosha vikwazo baina yao katika mnyororo mzima wa usafirishaji wa mazao ya chakula.
By:Abdull Najad Faiq

Address

Masaki
Dar Es Salaam

Telephone

+255743184044

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when 𝗥𝗔𝗗𝗜 𝟮𝟰/𝟳 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to 𝗥𝗔𝗗𝗜 𝟮𝟰/𝟳:

Videos

Share