Globify

Globify Issa Halili,
Founder & CEO of GLOBLIFY
+255782621022
(1)

GLOBIFY is a global digital media network, marketplace and platform that provides dynamic solutions and digital services based on programs and contents which inform, engage and entertain the world.

Globify Charity Yatoa Msaada kwa Watoto Yatima Katika Kituo Cha Islamic Yatima FoundationWadau wa Globify Charity, kwa m...
14/10/2024

Globify Charity Yatoa Msaada kwa Watoto Yatima Katika Kituo Cha Islamic Yatima Foundation

Wadau wa Globify Charity, kwa moyo wa upendo na mshik**ano, wametembelea kituo cha watoto yatima cha Islamic Yatima Foundation kilichopo Ilemela, Mwanza. Katika ziara hiyo, walikabidhi mahitaji muhimu kwa watoto hao, yakiwemo magodoro, vyandarua, vifaa vya shule, mahitaji ya vyakula na nguo.

Baada ya kutoa msaada, wadau walipata nafasi ya kutembelea Saanane National Park na kujionea vivutio mbalimbali vya kipekee vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ya kitalii.

Uongozi wa Globify Charity unatoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliowezesha mafanikio ya tukio hili kupitia michango ya fedha, vifaa, uhamasishaji, na ushiriki wa moja kwa moja katika safari hii ya matendo ya huruma na upendo kwa jamii. Pia, uongozi unatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa kituo kwa mapokezi na ushirikiano mzuri. Uongozi unawakaribisha wadau wengine kuungana na Globify ili kupata fursa za uelimishaji na ushiriki katika matukio ya kijamii.

Jiunge nasi kupitia https://chat.whatsapp.com/BiYVpSHVGt34tTA2eMQA3z

Let Love Connect Us.

Ulisoma na mtu gani maarufu!?
08/10/2024

Ulisoma na mtu gani maarufu!?




SHERIA 6 ZA KUFANIKIWA MAISHANI: 1. Tambua mshindani wako ni yule uliyekuwa jana2. Tengeneza pesa na wekeza kabla ya kul...
01/10/2024

SHERIA 6 ZA KUFANIKIWA MAISHANI:

1. Tambua mshindani wako ni yule uliyekuwa jana

2. Tengeneza pesa na wekeza kabla ya kula bata

3. Kwepa watu hasi, maisha ni mafupi

4. K**a usiposaka kile unachokitaka, hutakipata.

5. Ona kufeli k**a mwanzo tu, sio mwisho.

6. Tabia zetu ndizo huamua maisha yetu ya baadae.

GLOBIFY

"Haijalishi ni kiasi gani tunachotoa bali ni upendo kiasi gani tunaowekeza katika kutoa"Kila tendo jema ni sadaka . Toa,...
29/09/2024

"Haijalishi ni kiasi gani tunachotoa bali ni upendo kiasi gani tunaowekeza katika kutoa"

Kila tendo jema ni sadaka . Toa,penda,rudia,tenda wema,tabasamu na uonyeshe utofauti katika kutoa kwako

Jiunge nasi tukawape tabasamu watoto wenye uhitaji
https://whatsapp.com/channel/0029VaER90OEgGfVZhNXv00o/1336

GLOBIFY

MDAU TUAMBIE HAPA NI WAPI!?
24/07/2024

MDAU TUAMBIE HAPA NI WAPI!?





Mchana fulani wa kibabe,chagua sahani moja hapo twende sawa
22/07/2024

Mchana fulani wa kibabe,chagua sahani moja hapo twende sawa





Wakati Mwingine unaweza usione tumaini lolote mbele yako,machozi yatakuwa sehemu ya maisha yako. Kumbukumbu nzuri na za ...
06/06/2024

Wakati Mwingine unaweza usione tumaini lolote mbele yako,machozi yatakuwa sehemu ya maisha yako. Kumbukumbu nzuri na za kufurahisha za miaka ya nyuma utatamani zirudi tena.

Wakati mwingine maisha hayawezi kukupa unachotaka sio kwamba hustahili kupata,ni kwasababu inabidi ukose inabidi upitie mateso,inabidi uchekwe na watu ili upate kilichobora zaidi ya unachotaka.Kuna ushindi mbele yako Mungu amekuandalia ndiomaana bado upo hai,usichoke kusubiri usichoke kujaribu,usikate tamaa na kuishia njiani ENDELEA MBELE 💪

Globify inakutakia siku i njema na yenye furaha na baraka wewe na familia yako.





Jiunge na channel yetu ya WhatsApp kwa kugusa kiungo hiki
https://whatsapp.com/channel/0029VaER90OEgGfVZhNXv00o

  YA LEOWakati mwingine unaweza kukatishwa tamaa kutokana na changamoto unazopitia,utatamani uache kuendelea na  safari ...
30/05/2024

YA LEO

Wakati mwingine unaweza kukatishwa tamaa kutokana na changamoto unazopitia,utatamani uache kuendelea na safari ya mafanikio yako. Kumbuka hata ndege hupaa angani licha ya upepo mkali,usikate tamaa endelea na safari.

inakutakia mchana mwema na wenye baraka kwako.






JIUNGE NA 'CHANNEL' YETU YA WHATSAPP KWA TAARIFA MBALIMBALI

Globify inaendelea kukupa nafasi ya kupata Taarifa na Elimu kwa ukaribu na urahisi zaidi kupitia Mtandao wa WhatsApp

Jiunge nasi kwa kubofya kiungo hiki

https://whatsapp.com/channel/0029VaER90OEgGfVZhNXv00o

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, ameweza kumaliza msimu wa 2023/2024 kwa mafanikio makubwa baada ya...
20/05/2024

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, ameweza kumaliza msimu wa 2023/2024 kwa mafanikio makubwa baada ya timu yake ya PAOK Thessaloniki kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ugiriki. Katika mechi ya mwisho iliyochezwa jana, PAOK ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Aris Salonika ugenini, na hivyo kufikisha pointi 80 ambazo zimewafanya kuwa kileleni mwa ligi.

Hii ilikuwa ni hatua muhimu kwa Samatta na timu yake, huku AEK Athens ikimaliza msimu katika nafasi ya pili. Mafanikio haya ni ushahidi wa mchango mkubwa wa Samatta kwenye timu na umahiri wake uwanjani, ambao umeonekana katika kipindi chote cha msimu.

Kwa ushindi huu, PAOK imeongeza taji lingine kwenye kabati lao la mataji na Samatta anaendelea kuimarisha nafasi yake k**a mmoja wa wachezaji bora kutoka Tanzania.






Tembelea channel yetu ya WhatsApp kwa kugusa kiungo hiki
https://whatsapp.com/channel/0029VaER90OEgGfVZhNXv00o

Anaitwa Yuen Wah muigizaji maarufu wa Hong Kong, huyu mwamba ndio mkuu wa kitengo cha roho mbaya au unaweza kumuita msag...
18/05/2024

Anaitwa Yuen Wah muigizaji maarufu wa Hong Kong, huyu mwamba ndio mkuu wa kitengo cha roho mbaya au unaweza kumuita msaga sumu mkuu. Achana na yule Bill Drago wa Marekani, hiki chuma ukikiona k**a mtu mmoja mwenye minyoo ila mapigo yake k**a watu buku.

Anafinya ile mbaya huyu sina haja ya kumuelezea sana mliotazama Eastern Condors mtakua mashahidi, aliwakamua mavi wababe wote kina Sammo Hang, Yuen Biao mpaka wakakubali mziki

Kwa msiomfahamu huyu pia ndio alicheza kwenye ile movie ya yule mama mvuta fegi mwenye balaa ya Kung Fu Hustle akiwa sambamba na yule mama

Huyu jamaa ndiye aliyefanya wanaume wembamba k**a mimi admin wenu wa page hii maarufu zaidi kwa sasa tz "Dunia Ina Mambo" tuogopeke na kuheshimika duniani

Alisababisha wanaume wembamba tusichukuliwe oya oya kwamba kumbe tunaweza kuwa na balaa zito. Kwa sasa amekuwa mzee ana miaka 73, kwenye maisha yake amecheza movie zaidi ya 160 k**a staa, bedui

HAYA NDIO MAKABILA 125 YA TANZANIA​ ​ANDIKA NAMBA YA KABILA LAKO​ UWAJUE NDUGUZO1. Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)2. Waakie...
18/05/2024

HAYA NDIO MAKABILA 125 YA TANZANIA​ ​ANDIKA NAMBA YA KABILA LAKO​ UWAJUE NDUGUZO

1. Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
2. Waakiek
3. Wameru
4. Waassa
5. Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang’ati)
6. Wabembe
7. Wabena
8. Wabende
9. Wabondei
10. Wabungu (au Wawungu)
11. Waburunge
12. Wachagga(admin wenu wa page hii maarufu zaidi kwa sasa tz "Dunia Ina Mambo" pia ni mangi wa old moshi kidia)
13. Wadatoga
14. Wadhaiso
15. Wadigo
16. Wadoe
17. Wafipa
18. Wagogo
19. Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
20. Wagweno
21. Waha (watan zangu wakopeshaji vyombo hawa)
22. Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na Watindiga)
23. Wahangaza
24. Wahaya
25. Wahehe
26. Waikizu
27. Waikoma
28. Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
29. Waisanzu
30. Wajiji
31. Wajita
32. Wakabwa
33. Wakaguru
34. Wakahe
35. Wakami
36. Wakara (pia wanaitwa Waregi)
37. Wakerewe
38. Wakimbu
39. Wakinga
40. Wakisankasa
41. Wakisi
42. Wakonongo
43. Wakuria
44. Wakutu
45. Wakw’adza
46. Wakwavi
47. Wakwaya
48. Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
49. Wakwifa
50. Walambya
51. Waluguru
52. Waluo
53. Wamaasai
54. Wanyantuzu
55. Wamagoma
56. Wamakonde
57. Wamakua (au Wamakhuwa)
58. Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
59. Wamalila
60. Wamambwe
61. Wamanda
62. Wamatengo
63. Wamatumbi
64. Wamaviha
65. Wambugwe
66. Wambunga
67. Wamosiro
68. Wampoto
69. Wamwanga
70. Wamwera
71. Wandali
72. Wandamba
73. Wandendeule
74. Wandengereko
75. Wandonde
76. Wangasa
77. Wangindo
78. Wangoni
79. Wangulu
80. Wangurimi (au Wangoreme)
81. Wanilamba (au Wanyiramba)
82. Wanindi
83. Wanyakyusa
84. Wanyambo
85. Wanyamwanga
86. Wanyamwezi
87. Wanyanyembe
88. Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
89. Wanyiha
90. Wapangwa
91. Wapare (pia wanaitwa Wasu)
92. Wapimbwe
93. Wapogolo
94. Warangi (au Walangi)
95. Warufiji
96. Warungi
97. Warungu (au Walungu)
98. Warungwa
99. Warwa
100. Wasafwa
101. Wasagara
102. Wasandawe
103. Wasangu
104. Wasegeju
105. Wasambaa
106. Washubi
107. Wasizaki
108. Wasuba
109. Wasukuma
110. Wasumbwa
111. Wamanyema
112. Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
113. Watongwe
114. Watumbuka
115. Wavidunda
116. Wavinza
117. Wawanda
118. Wawanji
119. Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
120. Wayao
121. Wazanaki
122. Wazaramo
123. Wazigula
124. Wazinza
125. Wazyoba

Wewe ni kabila lipi hapo?


Follow channel yetu ya WhatsApp kwa kugusa kiungo hiko https://whatsapp.com/channel/0029VaER90OEgGfVZhNXv00o

MDAU UNAIKUMBUKA HII MOVIE!?ITAJE
15/05/2024

MDAU UNAIKUMBUKA HII MOVIE!?ITAJE




KING XABI ALONSO Kipindi anaichukua Bayer Leverkusen Mwaka 2022 katikati ya Msimu aliikuta ipo nafasi ya 2 kutoka Mwisho...
11/05/2024

KING XABI ALONSO

Kipindi anaichukua Bayer Leverkusen Mwaka 2022 katikati ya Msimu aliikuta ipo nafasi ya 2 kutoka Mwisho kwenye Msimamo wa Ligi kuu ya Nchini Ujerumani (Bundesliga).

Hadi sasa Xabi Alonso na jeshi lake hawajapoteza Michezo 49 Mfululizo , Bayer Leverkusen imefunga mabao 136 kwenye michezo 49 pekee na hizo ni Takwimu za Mashindano yote .

Wamechukua Bundesliga , Wapo fainali DFB POKAL, Wapo Fainali kwenye Europa league na pia wamebakiza Michezo minne pekee ili wamalizae Msimu huu wa 23 /24 bila ya Kupoteza .

Bundesliga Michezo -2
Europa league Mchezo - 1
DFB POKAL -Mchezo -1

What a Manager





Ukitoa kaki 5 kwenye mshahara wako utabaki na shilingi ngapi!?tunasoma comment yako.
08/05/2024

Ukitoa kaki 5 kwenye mshahara wako utabaki na shilingi ngapi!?tunasoma comment yako.





Baadhi ya wanasoka maarufu Afrika wanaoshiriki BundesligaWanasoka wa Afrika wanazidi kupamba ligi kuu ya soka nchini Uje...
29/04/2024

Baadhi ya wanasoka maarufu Afrika wanaoshiriki Bundesliga

Wanasoka wa Afrika wanazidi kupamba ligi kuu ya soka nchini Ujerumani, Bundesliga baada ya kuchezea ligi hiyo kwa miongo kadhaa tangu Ibrahim Sunday wa Ghana alipo weka historia kwa kuwa mwafrika wa kwanza kucheza katika ligi hiyo, akiiwakilisha Werder Bremen mnamo Juni 1976.

Bara la Afrika linazidi kuwasilisha wachezaji mahiri uwanjani huku majina maarufu katika historia ya soka la Afrika yakizidi kuhamia ligi hiyo na kuonyesha vipaji vyao katika Bundesliga.





Address

Masaki
Dar Es Salaam
14110

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Globify posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Globify:

Videos

Share


Other Broadcasting & media production in Dar es Salaam

Show All