“Hatuweki matangazo yetu kwenye TV STATIONS kwakuwa wateja wetu hawaangalii TV “
Ni wapi wewe huwezi weka tangazo lako kwakuwa watu wako hawaangalii?
Sasa wacha nikupe faida za vitu kama hivi, assume wewe ni content creator, na uko mji Fulani na unatakiwa kupata baadhi ya shots za kuongezea kwenye video yako unayo shoot kwenye huo mji, sasa hizi ndo B-ROLL overlays kwenye video yako.
ila kama unataka ku fake tu kuwa uko mji Fulani - wala sikuzuiii
Unatafuta idea ya biashara simple na yenye mtaji Mdogo?
Sajili ofisi Kisha chukua vijana wafunze kuhudumia ofisi Kisha watafutie uniform nzuri Kisha anza kutupostia mitandoani na kuanza omba kazi kwenye ofisi kadhaa kuhusu kuleta wafanya usafi mara 2,3,4 kWa wiki Kisha patana hela na kıla ofisi wawe wanalipa kiwango fulani cha fedha na wewe utakuwa unalipa basic salary ndogo Ila unakuwa unamwongezea hela pindi mteja akija
Na muda mwingine na wewe Fanya kazi pia
NB: najua kuna ofisi Kama hizi na watoa huduma kama hawa Ila mko down kujitangaza ongeza speed
Business Goal ni kuweka Maisha ya watu katika njia nyepesi, tunanunua magari ili kufika kWa wepesi, tunanunua mavazi ili kujistiri, nyumba ili kuwa salama, insurances ili Kuwa na tahadhari Juu ya yajayo
Unajua biashara Yako iwe na nini?
PREMIUM goals yaani
Watu wananunua nguo kujistiri, premium goal ni wanunue kuongeza STATUS
wanunue magari kufika kWa wepesi, WANUNUE ILI KUJISIKIA SLAAMA UTULIVU NA UPEKEE
Wanunue nyumba ili kupata makazi WANUNUE NYUMBA ILI KUISHI KWA AMANI NA UHURU NA USALAMA
Hakikisha malengo yako ya biashara yako yanakuwa EXTRA ORDINARY
Usiwe Mtu wa kawaida kawaida twende kwenye mambo EXTRA
HEBU NAMBIE JAMBO EXTRA KWAKO ILI WATU WAJUE WEWE SIO MFANYA BIASHARA WA KAWAIDA WEWE NI EXTRA
Kuwa Juu Namba 1 sio sawa na Kuwa namba Moja kithamani, branding lazima ujue hili,
Ni sawa na kusema, Kuwa na followers Wengi sio guarantee ya Kuwa mauzo Makubwa sana, so
Brand Za magari mfano ambazo ni Kubwa Duniani ni
1 - @volkswagen
2- @toyota
Ila brand Zenye thamani kubwa duniani ni
@devel_sixteen
@we_are_covert
So kuna thamani na ukubwa kwenye branding inaangaliwa thamani zaidi Ndo maana huoni ma brand makubwa mfano handbags, simu nk kutajwa kama brand kubwa ki mauzo ila ni brand kubwa ki THAMANI
So brand kubwa maana yake ni?
Kwenye BIASHARA ya ubunifu wowote lazima kuwe na uhakika wa mambo mawili muhimu sana
1 - STORY YA HICHO KILICHOBUNIWA!?
2 - KIMEBUNIWA KWA AJILI YA NANI!?
Kila muda ukitengeneza product mpya ipe story hiyo BIDHAA, story kuhusu nani ame inspire kuunda hiyo, jambo gani limeku inspire na je situation Gani imeku inspire kuunda hiyo BIDHAA, ni kitu gani mtu akivaa hiyo BIDHAA akikiona ata resonate na hiyo story
Hapa unaweza hata kushona nguo kutokana na waalimu au manesi au madereva au askari au viongozi au wasanii kwahiyo story ya BIDHAA ukasema imekuwa inspired na hao, wasanii au waalimu au ma dokta nk
Kisha alama gani mtu akivaa atajua story, weka style ya mifuko ya kidokta au mix rangi ku inspire wasanii au weka kombat like kama askari au weka style kama ya kimwalimu mwalimu, ili mtu akivaa anajiona NA YEYE NI MWALIMU AU DOKTA AU ASKARI (hisia)
Hebu mtu mmoja wa fashion aje aseme is this not DEMURE AND MINDFUL? 🤣
KILA MMOJA ANAWEZA KUWA INFLUENCER ILA NI WACHACHE WANAWEZA KUWA CONTENT CREATORS
Why?
CONTENT CREATORS LAZIMA AWE NA
Niche!
Niche ni eneo rasmi la maudhui yake, yaani yanahusu nini, haiwezi kuwa kitu chochote Ila kuhusu jambo fulani muhimu tu! Ndio maana content creator wengi unaona wanakuwa na idadi wastank ya watu kwakuwa yeye huwa hapost kila kitu Bali vitu vichache na hii hufanya watu wachache kuendelea ku fuatilia na hao watu wachache wakofuatilia wanafuatilia kweli hawana masihara
ILA
INFLUENCER
Yeye hana eneo rasmi, Leo anaweza kupost mahusiano yake, kesho akanza kuwa Mshauri wa biashara kesho kutwa akaanza post vituko mtandaoni kesho kutwa akapost kichambo kesho kutwa akapost kingine
Yaani hana kitu maalumu na sana sana hawa utakuta kWa sababu ya mambo hayo wanakuwa na idadi kubwaaaaa ya watu kumfuatilia kwakuwa ana mada nyingi anapost (hata connection hawakawii kupost hawa)
Sasa ukitaka kuwa tumia utaelewa yupi ni yupi na nani ni nani?
Mfano wa content creator
@ossegrecasinare - PHOTOGRAPH
@fahad_fuad - WILDLIFE PHOTOGRAPH
@dikobymonalisa - FOODS NA MANYAM NYAM
@doreenandy - LIFESTYLE
@djdorex - LIFESTYLE AND BEAUTY
Na mwanangu @_kisherscloset -
Na pia kuna Ambao ni content creator plus influencer yaani anaweza fanya vyote mara moja
Please tag wengine
Ila umeelewa?
Wezi wa mitandao ni taaasisi kabisa na ukiwa hujui unachotaka unaweza jikuta unafaidisha taasisi hizo kila siku
Kuna wafanya biashara wengi sana wanaweza kukubali kuwa wamepoteza pesa nyingi sana either kWa WATU ambao ni matapeli au WATU ambao wamewadanganya BIDHAA walizokuwa wanataka nk
Kuwa makini mitandaoni, tamaa yako huwa ndo hasara yako, na dezo unazotaka ndo unapokamatiwa hapo
Tag mwenzio apate somo pia
MADHARA YA KUTOKUWA NA TABIA YA KUJIFUNZA KWAKO WEWE MFANYA BIASHARA
1 - KUHISI HUNA UWEZO WA KUZALISHA MAUDHUI YAKO MWENYEWE BILA KUTEGEMEA MTU
2 - KUHISI KILA MTU ANAYEFANYA BIASHARA AU HATA ANAANZA HUWA ANASHINDANA NA WEWE
3 - KUWA NYUMA KITAARIFA
4- KUKATIA TAMAA JITIHADA NDOGO
5- KUANZA KUJENGA UVIVU
6- KUANZA KUJIJIBU MAJIBU HATA YASIYO YA KWELI KUCHWANi
Nk
@topratedreignstore hongera kwa kazi nzuri na jitihada binafsi
Let’s all win
Kipindi umekosa Ubunifu kwenye BIASHARA YAKO tu, Ndipo kipindi utaanza kuona kama biashara hailipi tena, na utaanza ona
Labda jina la biashara sio
Labda eneo nililipo sio
Labda BIDHAA sio
Labda bei kubwa
Labda numerogwa 🤣
Labda watu wananiripoti
Naniiii achana na haya yote, WEKEZA KWENYE UBUNIFU İLİ USIANZE KUHISI VITU AMBAVYO HAVIPO
Mmeuliza nimejibu, now hizo hapo ni steps za ku rusha tangazo upande wa @tiktok kWa wale wapenzi wa PAID GROWTH!
Kuna sheria zile zile kama ilivyo hapa @instagram sheria za matumizi brands personal attributes nk hivyo uwe makini, jifunze kwanzza
So kama una swali drop kWa comment hapo chini
Mtandao ni sehemu nzuri san kwa maisha ya sasa ila ni sehemu moja ya hatari sana kama hautakuwa makini na vitu unavyoangalia na watu unaowaangalia
Maisha ha mtandao ni mazuri san na ma rahisi sana isikufanye ukaanza kukufuru na kujidharau mwisho wa siku ukaharibu maisha yako mwenyewe
Kuwa salama, hii ni kumbusho kwako na kwa mwenzako.
Stay safe
Usije sema kaka zako hatukukwambia, kasome mistari ya hiyo nyimbo kisha elewa chanzo cha maradhi yako..
Nimekutana na wafanya biashara kibao wakiwa na stress juu ya logo iweje Ila kila mmoja anaamini kama nauza nguo basi wazo la haraka ni mtu aonekane ameva nguo, au mdoli wa nguo
Başı Leo nikuongezee maarifa juu ya logo, LOGO NI ALAMA ZA UMILIKI AU UTAMBUZI İLA SİSİ HUWA TUNAWAZA utambuzi wa huduma zetu tu Ila sio kweli utambuzi ni zaiid ya huduma na BIDHAA Bali utambuzi ni mpaka mmiliki wa ile alama
Kwahiyo tunapofikiria logo usifikirie BIDHAA na huduma yako tu ila fikiria wewe mmiliki pia kwakuwa inakuwakilisha na inakuzungumza pia
So logo sio lazima ibebe huduma tu Bali zaidi ya huduma au BIDHAA zako, fikiria zaidi ya huduma yako zaidi ya BIDHAA zako
Kisha changanya zote pamoja kisha jenga alama itakayodumu na hiyo itakuwa LoGo nzuri na bora zaidi
Umepata somo?