
07/06/2023
ALIYETOBOLEWA JICHO NA MMEWE AFUNGUKA, INASIKITISHA AISEE 😭😭
"Naitwa Jackline Nkonyi, tukio lilinitokea tarehe 23, usiku mida ya saa tano usiku, Mume wangu alinipigia simu akasema uko wapi, nikasema kwasababu nipo nyumbani hamna shida hata akinipigia nipo nyumbani, sasa tumekaa na ndugu zangu waliokuja kunisalimia imefika saa tatu inaenda saa nne, ndugu zangu wakaniambia sisi muda umeenda tunaondoka nikawambia basi haina shida, walivyoondoka nikaenda nikafunga geti nikajiandaa kwenda kulala"
"Nikawa bado sijalala lakini niko chumbani, kidogo nikasikia honi getini na hapo tayari ilikuwa saa tano usiku, basi kuna mtoto wake wa kiume tunaishi nae akaenda akamfungulia, mimi nikakaa sebreni namsubiri, alipoingia hakunisemesha kitu akaniacha nimesimama akanipita akaenda chumbani, mimi nikawa namfata huko chumbani"
"Ile namfata na yeye anatoka, yani hamna kusemeshana wala nini akatoka na mimi akanitupa kwenye kochi hapohapo akaanza kuniambia nitakuuwa, malay* wewe akawa anaongea maneno mengi na kunipiga, nikawa siwezi tena kujitetea ameshanipiga nimezidiwa, yani nikawa sielewi mimi naona tu mateke, mangumi, mkanda yani sielewi"
"Akamaliza akachukua (Plaizi) akaniambia fungua mdomo, nikamwambia nisamehe kwani unataka kuning'oa meno? akaniambia fungua yani leo nakung'oa yote, akafanikiwa alitoa lile jino jamani likatoka damu zikawa zinanitoka, akamaliza pale akaendelea na mikanda mgongoni, alivyomaliza akasema ngoja nikupeleke kwenu mbw* wewe ukafie huko"
"Akanibeba mimi na mtoto wangu wa kiume ambaye sio wa kwake ni wa kwangu, akasema nenda na mtoto wako, akatubeba vizuri kwenye gari akafika hapa akampigia mama yangu simu akamwambia 'toka nje mchukue mtoto wako' mama yangu alivyofungua mlango akapewa mwili wangu akanisukumia kwake kisha akawasha gari akaondoka zake"
"Tatizo ni kwamba ana wivu sana, hataki hata niende popote, hataki hata nije hapa nyumbani kwetu, hataki ndugu, hataki niwe na marafiki, yani hataki kitu chochote sasa wakati mwingine mimi nashindwa sasa mimi ni binadamu nitaachaje kuongea na ndugu zangu, na hajawahi kunifumania ni wivu tu anahisi kuna vitu namfanyia labda namdanganya au namchiti"
" Kabla ya hapo tulikuwa tuna ugomvi wa kwenye simu mkubwa tu, nilikuwa namwambia bwana mbona hutaki kuja nyumbani na upo tu hapo Moshi (kwa miezi mitatu alikuwa hajakanyaga nyumbani) basi nikimwambia anakasirika, nikimwambia basi njoo hata wikiendi anasema nina mambo mengi yani tulikuwa hatuko sawa"
"Siku moja tulipishana kidogo akawa ananiambia usinitishie-tishie nina uwezo wa kuchukua mwanamke yoyote na nikazaa nae hata watoto 20 usinibabaishe we kaa hukohuko, na Moshi kuna mwanamke wake, mimi sijafunga nae ndoa lakini naishi nae na nimezaa nae watoto wawili wakike na wa kiume na alinikuta tayari nina watoto wangu, tukakubaliana tutaishi tu ndio tukazaa hao watoto wawili"
"Sasa hivi naona na jicho moja, nikipona nitaendelea na maisha yangu, mimi naiachia tu Serikali wafanye kazi yao kisheria, kusema ukweli alikuwa ananiua ni Mungu tu ameniokoa".
Hata hivyo cha kusitaajabisha ni kwamba Mwanaume huyo ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Arusha, anaitwa Isaac Mnyagi.